Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed:Sheikh Hassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye mufti wa Tanganyika na aliwakilisha Waislam ambao hasa ndiyo waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo wa Dar es Salaam na vitongoji vyake. John Rupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wa chama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza alijulikana kwa misimamo mikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere, Dk. Kyaruzi akiwa mmojawapo
Mimi nisiyejua kusoma sawa sawa naona kuna conflicting information.
Mohamed: Hiki ni kitu kikinishughulisha sana. Jambo hili likishighulisha sana fikra zangu kwa kujiuliza mbona Kyaruzi anamruka Abdulwahid Sykes katika historia yao ya uongozi wa TAA mwaka wa 1950 na kumwingiza Nyerere ilhali Nyerere wakati ule hakuwa anafahamika na yeyote katika duru za siasa za Tanganyika? Nikawa nashangaa nikijiuliza kwani Dk. Kyaruzi hajui kuwa Nyerere aliingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953? Nilikuwa nikijifariji kwa kusema kuwa haya ndiyo matatizo ya historia ya uhuru wa Tanganyika
Nyerere alikuwa na akina Mwapachu Makerere, bila shaka Makererian wengine kama akina Kyaruzi walimfahamu pia.
Alikuwa katibu wa AA tawi muhimu sana la Tabora.

Alipelekwa kwa Sykes na Kasella Bantu. Nyerere alihudhuria mkutano wa AA iliyozaa TAA.
Hivi mtu akisema hafahamiki na yeyote kuna ukweli hapo!
Mohamed: Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo. Katika taarifa yake ya TAA ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika: "Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba."
Mwenyezi mungu anazidi kutuwekea wazi yale yaliyofichwa na yasiyosemwa. Mwenyezi anazidi kuthibitisha ushahidi wetu kuhusu udini. Hapa Mohame anamnukuu Abdul Sykes aliyesema ''kwa ajili ya masilahi ya waafrika na yale ya jumuiya ya waafrika KWA UJUMLA''. Abdul Sykes, mwanaharakati na kiongozi mzalendo hakusema kwa ajili ya Waislam kama Mohamed anavyopotosha umma.

Mohamed amesema Waislam ndio walioongoza mapambano, hata kama aliji contradict kwa kuingiza majina ya akina Rupia, Mhando n.k. bado Abdul Syke anamsuta kuwa kazi hiyo haikufanywa kwa masilahi ya Waislam bali Waafrika kwa ujumla.
Hoja ya udini imetoka wapi?
 
Hii ''kukiri'' unakusudia kitu gani?
Kweli sijaziona wala haikunipitia kuzitafuta.
Ulijuaje kwamba katiba ya TANU ilinakiliwa kutoka katiba ya chama cha Nkrumah na kwamba ilibadilishwa tu majina pale pa Ghana iliandikwa Tanganyika?
 
MM,

Sijui vipi unapata tabu na mimi.

Kwangu mimi nikizungumza dini namuona Allah.
Nikuzungumzia Waislam namzungumza Allah.

Kwangu mimi hiki si kitu cha kuona aibu.
Kwangu mimi Uislam ni kitu adhim.

Na katika kitabu changu nilitaka kuanza na
Bismillah Rahman Rahim...

Publisher akasema haifai.
Tulivutana sana katika hilo.

Baada ya kukueleza haya bado utakuwa na tabu kunifahamu?

Sadakta Bwana Mohammed! Allah aendelee kuipa nguvu YAKINI yako. Insha Allah uzidi kutuelimisha. Kitabu chako cha Abdulwahid sykes nimekipamba sebuleni pangu na nakupa Ahadi kuwa mwanangu sasa yupo nursery anasoma A, B, C, D..lakini akikuwa na yeye nitampa akisome!
 
Ahsante kwa hili. Bwana Mohamed Said kajibu wengi. Na wengine wakimtukana naye akiwajibu kistaarabu kama mtoto wa kiungwana aliyepewa malezi mema na wazazi wake. Kukhitilafiana katika mas'ala si jambo geni. Hao wanaomwandama kwa matusi hawajaleta mada zao. Bwana Mohamed Said kaandika vitabu na references chungu mzima kwa msomaji mwenyewe kufanya utafiti wake mwenyewe. "Mohamed Said amefungua mlango wa kufanya utafiti katika masuala hayo yote." Haya nayanukuu kutoka katika kitabu chake "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968) Historia ilyofichwa Kuhusu Harakati za Waislamu Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza Katika Tanganyika" lakini badala ya ndugu zetu wengine kufanya huo utafiti wao wanaanza kuvurumisha matusi.

Nadhani topic ya mjadala huu badala ya kuwa "UCHOCHEZI WA MOHAMED SAID" ingelikuwa "CHANGAMOTO YA MOHAMED SAID YA KUFANYA UTAFITI"

... mwandishi amekuwa akiulizwa maswali mengi na watu mbalimbali kuhusu
ukweli ya yale aliyokuwa akiyaandika katika mchango wa Abdulwahid katika
uhuru wa Tanganyika.

Wasiwasi huu umekuwapo lau kama mwandishi amefanyarejea nyingi na za
kutosha kutoka magazeti ya zamani, vitabu,majarida na kumbukumbu zingine
za wakati wa ukoloni. Juu ya wasiwasi wote uliokuwapo hakuthubutu kujitokeza
yeyote kupinga yake mwandishi aliyoandika kuhusu historia ya Abdulwahid katika
TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hata mwanahistoria wa CCM hakunyanyua kalamu yake. Hali hii ya CCM kuikataa
historia yake na wakati huo huo ikidai kuwa haijaweza kuihifadhi historia yake inatoa
mvuto fulani kwa watafiti kutaka kujua kulikoni. Ukweli wa kuwa CCM imeandika historia
yake lakini hapo hapo imeonekana upo upungufu mkubwa unaweka wazi suala la utafiti
ufanywe na watafiti huru ili ukweli upate kujitokeza.

Somo la historia ya uhuru wa Tanganyika bado lipo wazi kwa utafiti zaidi.
 
Mimi nisiyejua kusoma sawa sawa naona kuna conflicting information.Nyerere alikuwa na akina Mwapachu Makerere, bila shaka Makererian wengine kama akina Kyaruzi walimfahamu pia.
Alikuwa katibu wa AA tawi muhimu sana la Tabora.

Alipelekwa kwa Sykes na Kasella Bantu. Nyerere alihudhuria mkutano wa AA iliyozaa TAA.
Hivi mtu akisema hafahamiki na yeyote kuna ukweli hapo!Mwenyezi mungu anazidi kutuwekea wazi yale yaliyofichwa na yasiyosemwa. Mwenyezi anazidi kuthibitisha ushahidi wetu kuhusu udini. Hapa Mohame anamnukuu Abdul Sykes aliyesema ''kwa ajili ya masilahi ya waafrika na yale ya jumuiya ya waafrika KWA UJUMLA''. Abdul Sykes, mwanaharakati na kiongozi mzalendo hakusema kwa ajili ya Waislam kama Mohamed anavyopotosha umma.

Mohamed amesema Waislam ndio walioongoza mapambano, hata kama aliji contradict kwa kuingiza majina ya akina Rupia, Mhando n.k. bado Abdul Syke anamsuta kuwa kazi hiyo haikufanywa kwa masilahi ya Waislam bali Waafrika kwa ujumla.
Hoja ya udini imetoka wapi?

Asante sana mkuu!

Sasa waelewa wa mambo tukisema kuwa huyu mzee ni mchochezi wapo binadamu wanaoibuka kuja umtetea kwa jasho na damu.
 
Two different ideas are as good as parallel lines they will never met cuz mmoja ana discuss objectively mwingine ana discuss religiously,anyway ndio uhuru wa kutoa maoni huo na kuzungumza kile unachokiamini.
 
Sadakta Bwana Mohammed! Allah aendelee kuipa nguvu YAKINI yako. Insha Allah uzidi kutuelimisha. Kitabu chako cha Abdulwahid sykes nimekipamba sebuleni pangu na nakupa Ahadi kuwa mwanangu sasa yupo nursery anasoma A, B, C, D..lakini akikuwa na yeye nitampa akisome!

K,

Insha Allah.
Mungu atukuzie.

Amin.
 
Asante sana mkuu!

Sasa waelewa wa mambo tukisema kuwa huyu mzee ni mchochezi wapo binadamu wanaoibuka kuja umtetea kwa jasho na damu.

Yericko,

Ngoja nikufunze adabu.

Kwa kuniita mzee tayari ushafuzu kuwa una heshima na umeniheshimu
kwa uzee wangu.

Ukisema ''Huyu Mzee.''
Umetukana.

Sasa ile staha ulioonyesha awali inaondoka tunakuwa sawa.
Inawezekana kwa makuzi ya kwenu hili si hadhir kwako.

Ungesema mathalan ''Mzee ni mchochezi'' ungepatia.
Ondoa ''Huyu.''

Lakini sikulaumu haya mambo ya adabu na akhlak za mazungumzo nadhani
ziko mbali na nyie zinahitaji mfunzwe.
 
Sasa wewe kama msomi hukuona umhimu wa kujiridhisha kwa kuisoma katiba hiyo mwenyewe badala ya kumuamini Tewa moja kwa moja na kutuletea sisi simulizi hiyo?

Wala.

Nimesoma mswada wake huo ulinitosha unaitwa ''Probe Into the History of Islam in Tanzania.''
 
Wala.

Nimesoma mswada wake huo ulinitosha unaitwa ''Probe Into the History of Islam in Tanzania.''
Sijakuelewa, mswada wake nani?Tewa? kwa hiyo uandishi wako pamoja na majigambo yako yote ni wa "hear say" tu!
 
Mimi nisiyejua kusoma sawa sawa naona kuna conflicting information.Nyerere alikuwa na akina Mwapachu Makerere, bila shaka Makererian wengine kama akina Kyaruzi walimfahamu pia.
Alikuwa katibu wa AA tawi muhimu sana la Tabora.

Alipelekwa kwa Sykes na Kasella Bantu. Nyerere alihudhuria mkutano wa AA iliyozaa TAA.
Hivi mtu akisema hafahamiki na yeyote kuna ukweli hapo!Mwenyezi mungu anazidi kutuwekea wazi yale yaliyofichwa na yasiyosemwa. Mwenyezi anazidi kuthibitisha ushahidi wetu kuhusu udini. Hapa Mohame anamnukuu Abdul Sykes aliyesema ''kwa ajili ya masilahi ya waafrika na yale ya jumuiya ya waafrika KWA UJUMLA''. Abdul Sykes, mwanaharakati na kiongozi mzalendo hakusema kwa ajili ya Waislam kama Mohamed anavyopotosha umma.

Mohamed amesema Waislam ndio walioongoza mapambano, hata kama aliji contradict kwa kuingiza majina ya akina Rupia, Mhando n.k. bado Abdul Syke anamsuta kuwa kazi hiyo haikufanywa kwa masilahi ya Waislam bali Waafrika kwa ujumla.
Hoja ya udini imetoka wapi?

Naona mnaumizwa kwa kuambiwa kuwa Nyerere hakuwa anafahamika Dar es Salaam.

Ngoja nikuambie.
Abdu hakuwa anamjua Nyerere kabla ya siku ile alipoletwa kwake na Kasella Bantu.

Ikiwa aliokuwa anajulikana na wenzake wa Makerere bado kwa mji wa Dar es Salaam
Nyerere alikuwa mgeni hajulikani.

Baba yangu alikuwa maarufu sana Dar es Salaam katika circle za vijana wenzake na
kamjua Nyerere nyumbani kwa Abdu Sykes.

Shariff Attas mtu maarufu Dar es Salaam hakuwa anamjua Nyerere hadi alipomuona anakuja
ofisini kwa Abdu Sykes Kariakoo Market.

Mzee Mshume mtu maarufu Dar es Salaam hakumjua Nyerere hadi alipojulishwa na Abdu pale sokoni.

Sheikh Hassan bin Amir hakumjua Nyerere hadi alipopelekwa kwake na Abdu na Dossa.

Sheikh Mohamed Ramia hakuwa anamjua Nyerere hadi alipoletwa kwake na Idd Tosiri na
Idd Faiz Mafongo.

Waliokuwa wanamjua Nyerere ni hao hao jamaa waliotoka pamoja sehemu za bara.
Kwa Dar es Salaam alikuwa ni mgeni.

Kwani cha ajabu nini?

Ugeni si kitu cha kukionea aibu.

Mengine sina haja ya kujibu.
 
Sijakuelewa, mswada wake nani?Tewa? kwa hiyo uandishi wako pamoja na majigambo yako yote ni wa "hear say" tu!

G,

Haswa wala hujakosea.

Nikiwauliza naandika.

Mswada ni wa Tewa.

Kujigamba si kwa kuandika.
Kujigamba ni kule hawa waliofanya haya ni wazee wangu.
 
Nadhani umefika wakati mwafaka wa kumuumbua huyu mchochezi anayetumia kalamu yake kupandikiza chuki baina ya jamii ya Watanzania bila kutambua athari za hizi juhudi zake. Mohamed Said ni mtu hatari aliyeweza kuwarubuni na kuwateka wengi wenye uelewa finyu kwa kivuli cha dini, mfano hai unapatikana humu...wapo waamini wake ambao kwa upofu wao wameshindwa kabisa kuzitambua hila zake huyu mchochezi. Hapa chini ninampa maswali machache mapya ambayo natumaini yatawafumbua macho waliofunikwa na wingu zito na kushindwa kabisa kumwona huyu mchochezi kwa rangi yake;

  1. African Association (AA) kama ilivyo chimbuko lake ni nini, iliasisiwa lini, na nani na kwa malengo yapi?
  2. Kwa nini baadaye ilibidi jina hili libadilike na kujulikana kama TAA?
  3. Je ilikuwa lazima mtu awe mkaazi wa Dar es Salaam ili aweze kuwa Kiongozi wa TAA?
  4. Mawasiliano ya kwanza kabisa kati ya Mwalimu Nyerere na wazee wako wa Gerezani yalifanyika lini?
  5. Hayo mawasiliano yalianzishwa na nani, Mwalimu Nyerere au wazee wako wa Gerezani?
  6. Nani alifanya "approach" ya kwanza kumfikia (kumtembelea) mwingine...Mwalimu Nyerere au wazee wako wa Gerezani.
  7. Je kuna mikutano yoyote ilifanyika nyumbani kwa Mwalimu Nyerere akiwa Pugu? Kama ilifanyika ni ipiilikuwa ajenda kuu?
  8. Mkutano wa TAA wa October, 1953 ulifanyika katika nyumba iliyokuwa New Street, Dar es Salaam...hii nyumba ilikuwa ya nani, ilijengwa na nani na kwa malengo gani?
  9. Katika kubuni jina TANU, pendekezo la kwanza lilikuwa TAU (kumbuka Kenya tayari walikuwa na KAU)...je ni nani alipendekeza neno "National" liongezwe na kwa sababu zipi?
 
G,

Haswa wala hujakosea.

Nikiwauliza naandika.

Mswada ni wa Tewa.

Kujigamba si kwa kuandika.
Kujigamba ni kule hawa waliofanya haya ni wazee wangu.
Asante sana mzee Mohamed Saidi kwa kuongea ukweli wako kwamba huku wahi kuziona wala kuzisoma katiba za TAA na TANU, na kwmba masimulizi yako yote nikutoka kwa wazee wako tu na hasa mzee Tewa, na hata kama mzee Tewa aliongea hisia zake tu wewe kwako ni "historical facts" ambazo sisi wanahistoria wasomi ni lazima tukubaliane bila ubishi. Tukibisha hatuwatendei haki hawa mashujaa la si hivyo basi na sisi tuandike historia za mizee yetu ambayo haikuwa na mchango wowote!
 
Ulichosisitiza ni sawa kabisa.
Nadhani sasa tumeelewana.

Sasa kuanzia hapa tusonge mbele.

a
 
Nadhani umefika wakati mwafaka wa kumuumbua huyu mchochezi anayetumia kalamu yake kupandikiza chuki baina ya jamii ya Watanzania bila kutambua athari za hizi juhudi zake. Mohamed Said ni mtu hatari aliyeweza kuwarubuni na kuwateka wengi wenye uelewa finyu kwa kivuli cha dini, mfano hai unapatikana humu...wapo waamini wake ambao kwa upofu wao wameshindwa kabisa kuzitambua hila zake huyu mchochezi. Hapa chini ninampa maswali machache mapya ambayo natumaini yatawafumbua macho waliofunikwa na wingu zito na kushindwa kabisa kumwona huyu mchochezi kwa rangi yake;

  1. African Association (AA) kama ilivyo chimbuko lake ni nini, iliasisiwa lini, na nani na kwa malengo yapi?
  2. Kwa nini baadaye ilibidi jina hili libadilike na kujulikana kama TAA?
  3. Je ilikuwa lazima mtu awe mkaazi wa Dar es Salaam ili aweze kuwa Kiongozi wa TAA?
  4. Mawasiliano ya kwanza kabisa kati ya Mwalimu Nyerere na wazee wako wa Gerezani yalifanyika lini?
  5. Hayo mawasiliano yalianzishwa na nani, Mwalimu Nyerere au wazee wako wa Gerezani?
  6. Nani alifanya "approach" ya kwanza kumfikia (kumtembelea) mwingine...Mwalimu Nyerere au wazee wako wa Gerezani.
  7. Je kuna mikutano yoyote ilifanyika nyumbani kwa Mwalimu Nyerere akiwa Pugu? Kama ilifanyika ni ipiilikuwa ajenda kuu?
  8. Mkutano wa TAA wa October, 1953 ulifanyika katika nyumba iliyokuwa New Street, Dar es Salaam...hii nyumba ilikuwa ya nani, ilijengwa na nani na kwa malengo gani?
  9. Katika kubuni jina TANU, pendekezo la kwanza lilikuwa TAU (kumbuka Kenya tayari walikuwa na KAU)...je ni nani alipendekeza neno "National" liongezwe na kwa sababu zipi?

Mag3,

Nadhani unaelewa sana kuwa huwa sijibu kila post.
 
Hapo unajisikiaje? Roho inatamani kuona Founder wa TANU ni Abdu Sykes?

Hapana.

Nimeeleza kuasisiwa kwa TANU katika kitabu na
hapa jamvini.

Wengi wamefaidika kwa yale ambayo hayakuwa
hadhir.

Khiyari ni yao kuamua kati ya ile historia rasmi
ya Kivukoni na hii yangu nani mkweli?
 
MM,

Sijui vipi unapata tabu na mimi.

Kwangu mimi nikizungumza dini namuona Allah.
Nikuzungumzia Waislam namzungumza Allah.

Kwangu mimi hiki si kitu cha kuona aibu.
Kwangu mimi Uislam ni kitu adhim.

Na katika kitabu changu nilitaka kuanza na
Bismillah Rahman Rahim...

Publisher akasema haifai.
Tulivutana sana katika hilo.

Baada ya kukueleza haya bado utakuwa na tabu kunifahamu?
Bw Said wewe hujanipata mimi kabisa; sina tatizo na uandishi wako hata kidogo wala kuandika kwa kutumia mwanga wa Uislamu. Nilikuwa namjibu huyu kijana ambaye ameona miye kukuuliza kuhusu dini ya Kina Kleist na wazee wao kuwa ni udini. Hoja nzima ya kwako ya kitabu na kazi zako imejengwa kwenye dini kwa hiyo ni vizuri mtu akasoma hivyo na kufanya hivyo wala siyo udini ni uamuzi tu umeuchukua. Sasa na wasomaji nao wana haki ya kuulizia maswali ya dini kwa kadiri yanavyojitokeza katika uandishi wako sivyo?
 
Back
Top Bottom