Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jaribu kutumia kidogo hizo chembe za Ubongo juu ya mabega yako; hoja nzima ya Mohammed Said iko kwenye dini. Sijui hata kama unajua kichwa cha habari cha kitabu chake cha Sykes kinaitwa nini. Huwezi kuzungumzia hoja za Said bila kuzungumzia dini na kuzungumzia dini siyo udini. Kwa taarifa kitabu kinaitwa:
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDUL WAHID SYKES (1924 -1968)
Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said
Said hakuandika historia ya wazee wa Dar-es-Salaam au wa Gerezani walioshirki katika harakati za Uhuru; msisitizo wake uko kwenye "Waislamu" na ndio maana swali langu ni muhimu sana katika kuangalia historia hiyo.
TUNATOA POLE KWA WADAU WOTE KUFATIA KIFO DOKTA VEDASTO KYARUZI ALIYEBUNI JINA LA TANZANIA NA ALIWAHI KUWA RAIS WA TAA. MIAKA YA 50.
Mdau Erick akimlisha keki dokta Kyaruzi wakati wa uhai wake.
MAKALA YA MDAU UPENDO ERICK BAADA YA KIPO CHA DOKTA KYARUZI
Si watanzania wengi sana wa kizazi cha miongo baada ya Uhuru wanaomfahamu au wamesikia habari za Dokta Vedasto Mzungu Kyaruzi, Mtanzania Mzalendo na Mwanamapinduzi, Msomi wa awali wa kiwango cha Udaktari wa Binadamu ndani ya Tanganyika. Nafasi ya wengi kumjua Dokta Kyaruzi imepotea kutokana na kuwa na Taifa lisilo na misingi mizuri ya kutambua michango na kuona ufahari juu ya uzalendo wa watu wake.
Ninamshukuru Mungu kwa kunipa nafasi ya kuwa karibu na Dokta Kyaruzi. Amekuwa rafiki na mlezi wangu; akiningoza vema jinsi ya kukua kitaaluma, kuishi na watu, makundi na jamii mbalimbali. Nakumbuka wakati wa hafla ya kunipongeza kwa kuhitimu Shahada ya Kwanza, Dokta aliniusia kwa msisitizo kwamba; Waafrika wengi wanadhani kuhitimu masomo ndo mwisho wa elimu katika fani husika. Kwake kuhitimu kulimaanisha mwanzo mpya wa kusoma fani kiundani zaidi, kujisajiri katika Journals, Periodicals, na Newsletters ili kuhakikisha anakwenda sambamba na kukua kwa maarifa katika tasnia yake. Ndipo alipopata kunijulisha maana ya neno "Practitioner" linalowekwa mbele ya vyeo vya Madaktari, Wahasibu, Wanasheria na fani zingine huko kwenye nchi zilizoendelea.
Pia, daima Daktari hakuacha kuniusia juu ya siasa na nafasi ilipotokea alinikutanisha na wanasiasa wakongwe mmoja wapo akiwa ni marehemu Abdulnoor Suleiman. Siku zote aliniambia na kunikanya kuwa, kama nia ya mtu kujiunga na siasa ni kujilimbikizia mali basi mtu huyo amekosea njia maishani. Katika ushiriki wake kwenye siasa, alithamini sana haki iliyompa mtu uhuru maishani kuliko mali ambayo ingemkosesha amani na heshima kwenye jamii. Mara kwa mara alisema; mtu akigonga mlango wa nyumba yake usiku wa manane atajua ama ni jirani kapata shida au kuna mtu anataka maelezo kapotea njia. Hawezi kuogopa kama wanasiasa wa siku hizi walafi ambao likiwatokea haraka uhisi "mambo yameharibika". Mbele ya nyumba yake mara nyingi alijipumzisha Mbeba-Mkaa, Mlevi aitwaye Rostamali. Dokta alipenda kumtumia Rostamali kama mfano wa watu wasiokuwa na hofu juu ya maisha yao. Wanaopata pesa yao kihalali kwa kusota, wakaitumia wapendavyo na kisha kuishi kwa amani wakilala nje bila kumhofia mtu yeyote na hata mdudu kama mbu naye asiwadhuru! Katika mfano huu alipenda kuhitimisha kwa kuniuliza, ni mwanasiasa gani (huu ulikinukiliwa enzi za Mkapa lakini bado una uhai) anaishi nyumba isiyo na geti kubwa, uzio wa umeme, walinzi wenye silaha, mbwa wakali na Je, ana amani kuliko mimi au Rostamali?
Kulingana na kumbukumbu ya masimulizi mbalimbali, Dokta Kyaruzi ni miongoni mwa Watanganyika watatu wa kwanza kabisa kupata dalaja la Udaktari wa Binadamu. Na wa kwanza alitoka ukoo wa Kichifu pale Gera-Ishozi, Bukoba. Dokta Kyaruzi alikuwa miongoni mwa Maktaba zinazotembea. Ni mmoja wa watu waliomfahamu Mwl. J.K Nyerere fika tuliokuwa tumebaki nao. Kwa mara ya Kwanza Dokta walikutana na Mwl. Nyerere Tabora mwaka 1939 wakati Dokta akisoma St. Mary (Kwa sasa Milambo Sec. School) na Mwl. naye alikuwa akisoma Tabora School (Sasa Tabora Sec. School). Walibahatika kuwa wote tena katika masomo ya Elimu ya Juu huko Makerere-Uganda. Na kwa pamoja walishiriki siasa za ukombozi kupitia tawi la TAA Chuo Kikuu cha Makerere, Dokta akiwa kama Katibu wa Tawi. Waliporejea nchini kila moja alikwenda kwanza kutumikia fani aliyosomea huku akijipanga vema kushiriki siasa za ukombozi. Dokta Kyaruzi alikwenda kufanya kazi Kingolwira wakati Mwl alikwenda kufundisha Tabora Boys. Baadaye hisia za ki-harakati ziliwarejesha Dar es Salaam na kuwakutanisha tena katika uongozi wa juu wa TAA huku Dokta Kyaruzi akikwea mpaka Uenyekiti wa chama mwaka 1949. Kama TAA ndiyo ilizaa TANU na TANU ikarithiwa na CCM basi utashangaa mbona Muasisi huyu hakuvuma na wala hukusikia habari zake kama usikiavyo habari za kina Sykes, Bibi Titi, n.k. Hili nakuachia uchunguze mwenyewe! Miongoni mwa wanasiasa ambao Daktari amekufa akiwakumbuka kwa kumkumbuka au kuthamini harakati zake ni Prof. Mark James Mwandosya. Mwaka 2005 wakati Prof. Mwandosya akiwa Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi alifunga safari kwenda kumsalimu Daktari. Baada ya mazungumzo, Prof. Mwandosya alimwachia Daktari zawadi ya simu ya mkononi aina ya NOKIA. Ni jambo ambalo hakulisahau mpaka uhai unamtoka.
Baada ya uhuru, Mwalimu J.K Nyerere alimteua Dokta Kyaruzi kuwa Mwakilishi wa Kwanza wa Tanganyika huru kwenye Umoja wa Mataifa, NY-Marekani. Kutokana na uhaba wa wasomi baadaye Mwl alimuhitaji na hivyo Dokta Kyaruzi alirejea nchini na kuwa Msaidizi wa Mwl-Ikulu. Kulitokea uchonganishi kati ya wasaidizi wa Mwl uliojikita katika majungu ya madaraka. Na Mwl kwa kutolichunguza vema akafanya uamuzi wa kumrejesha Dokta Kyaruzi kufanya kazi kwenye taaluma yake. Hivyo Dokta Kyaruzi alipangiwa kuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kazi ambayo aliripoti mara moja na kuitenda kwa moyo wake wote mpaka kustaafu utumishi wa umma. Aliporejea nyumbani Bukoba baada ya kustaafu alianzisha Zahanati iliyoangaliana uso kwa uso na duka la Nyegera Waitu. Kulingana na ugwiji aliokuwa nao katika masuala ya wanawake (Gynecology) huduma yake ilivuta watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi na hata toka nchi jirani. Kipindi ziwa Rwelu (viktoria) likiwa ndo njia kuu ya usafiri kati ya Kagera na mikoa mingine, hakuna meli ingefika asubuhi bila kuwa na wagonjwa wanaokuja kupata huduma kwa Dokta Kyaruzi. Pamoja na huduma yake hii lakini pia aliendelea kutoa mchango wa Elimu, Uzoefu na Maarifa yake kupitia majukwaa mbalimbali. Lakini ushiriki wake katika harakati za kisisasa ulikomea katika uandishi wa makala kwenye gazeti la Rai. Dokta amekuwa mjumbe na baadaye Mwenyekiti wa Bodi la Hospitali ya Mkoa wa Kagera kwa muda. Na katika kipindi chake mabadiliko makubwa katika miundombinu, rasilimali watu na huduma yaliweza kufanyika.
Hata katika umri wake wa mauti (miaka 91), Dokta ni mtu aliyeishi kwa kanuni na malengo. Siku yake iligawanywa kikanuni na haikubadilika iwe jua, umande ama mvua. Siku yake daima ilianza kwa kuhudhuria misa ya asubuhi. Baada ya misa hurudi nyumbani kupata kifungua kinywa na kujiandaa kwenda kazini. Saa saba alipata mlo wa mchana na kupumzika kwa saa na kisha kwenda kazini. Jioni alipenda kumpleleka mbwa wake ziwani na aliporejea alikaa bustanini kupata kikombe cha kahawa. Baada ya mazungumzo na mgeni ama kama muda wa sala ungefika angali bado na wageni, basi angeomba udhuru na kwenda kusali na aliporejea alifikia mezani kwa mlo wa usiku. Mara baada ya chakula iwe cha mchana au usiku, Dokta asingeweza kuhimili nguvu ya usingizi hivyo kila baada ya mlo tendo lililofuatia lilikuwa ni kupumzika.
Dokta Kyaruzi alijaliwa uzao wa watoto wane (4). Miongoni mwao, wawili (Patrick na Christina) aliwapata kwenye ndoa ya kwanza na Mama wa Kiganda. Mama huyu walifahamiana wakati Dokta akisoma Makerere. Patrick alisomea urubani na Tina ni mtaalamu wa kushona mavazi aliyebokea. Mama Patrick alifariki kwa saratani zaidi ya miaka 35 iliyopita. Baada ya msiba huu Patrick na Tina ambao hawakuwa wakiishi Tanzania waligundua msongo uliompata Baba yao. Walibaini kuwa iwapo msongo usingetafutiwa njia mbadala mapema, basi ungempelekea Baba yao mauti mapema zaidi. Hivyo kwa pamoja wakamsihi Dokta aoe mwanamke mwingine. Huu ulikuwa ni wakati mgumu mwingine kwa Dokta Kyaruzi kuufanyia maamuzi. Baada ya kitambo Dokta Kyaruzi aliafiki kufunga ndoa na mke ambaye amepata kuzaa naye watoto wawili; wa kike (Adela-Ngonzi) na wa kiume ( Edween-Shubi)-Ni wiki chache tu Dokta Kyaruzi alikuwa amepata mjuu kupitia Adela ambaye kwa bahati mbaya sana mauti yamemkuta kabla ya kumtia machoni. Pia mjukuu wa Dokta aitwaye- John Patrick Kyaruzi, aishiye nje wiki jana tu ndo alikuwa amekata tiketi ya kuja Tanzania mwishoni wa mwezi kumsalimu Babu yake! Huzuni iliyoje?
Katika ndoa ya pili Dokta Kyaruzi hakudumu kabla ya kupata jaribu lingine kubwa. Wakati ndoa inaanza kurejesha furaha na utulivu katika maisha yake, Patrick (mwanae mkubwa) aliyekuwa rubani wa ndege Marekani alipata ajali angani na ndege kuteketea. Kilichoshuhudiwa na kuzikwa ni majivu! Ukifuatilia vema maisha ya familia ya Dokta Kyaruzi utaduwaha kubaini mlolongo wa ajali za ndege na hasara zake katika mali na watu wa familia.
Katika maisha yake yote pamoja na utitiri wa fursa alizokuwa nazo, Dokta Kyaruzi alimiliki nyumba mbili tu; moja Kyaka-Mutukula na nyingine Miembeni-uwanja wa ndege, Bukoba. Nyumba ya Kyaka ilitunguliwa na ndege wakati wa vita ya Kagera na ile ya miembeni iliunguzwa upande kwenye ile ajali ya ndege ya Jeshi ya mwaka 1997. Wale mtakaokumbuka, pamoja na nyumba kuungua upande, Dokta Kyaruzi alipoteza magari yake mawili (Toyota Stout na Jeep) papo hapo. Pia vifaa vya Zahanati yake ambayo alikuwa ameihamishia nyumbani viliharibika na kupelekea huduma kufungwa. Hizi ajali na matokeo yake huniumiza sana hadi leo. Hata mara zote Dokta Kyaruzi alipokuwa akizirejea katika masimulizi, zimekuwa zikiniacha na simanzi kubwa. Kiufupi, HAKUNA FIDIA YOYOTE ALIYOPEWA Dokta Kyaruzi katika ajali hizi! Si kwa sababu yoyote ile ya msingi bali ni kutokana na ukiritimba na rushwa ambazo yeye hakuwa tayari kuafikiana nazo. Katika upanuzi wa uwanja wa ndege uliofanyika hivi karibuni, Dokta Kyaruzi alitakiwa kubomoa na kuondoka toka nyumba hii ya Miembeni. Kwa tabia yake ya kupenda kutenda na kutendewa haki alimanusura anyimwe hata kile kiduchu cha fidia aliyopewa. Mpaka pale Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi alipoingilia kati.
Ndugu na Jamaa tunamlilia mpendwa wetu Dokta Kyaruzi. Na kwa tabia ninahakika na viongozi wa Serikali-Kitaifa nao sasa watanakshi salamu na hotuba zao. Binafsi hisia zangu zinahama haraka kutoka kwenye huzuni na kujawa na furaha na amani ya moyo. Ni kwa kuwa imani yangu inanituma kuamini kuwa Dokta Kyaruzi hakufa bali ametwaliwa kwenye makazi ya kudumu akafurahie milele kifuani mwa Ibrahim baada ya kuyashinda majaribu makuu ya ulimwengu huu. Siku zote nimeyatathmini maisha ya Dokta Kyaruzi kwa kuyamithilisha na miasha ya Ayubu mtumishi wa Mungu. Naamini hata katika kulifanya simulizi langu kuwa fupi kadri niwezavyo bado umeweza kung'amua mateso na majaribu aliyopitia Dokta Vedasto Kyaruzi.
Hapo kwenye blue kazi ya Mohamed Said.
Mwandishi analalamika nani atawakumbuka kuandika historia ya waliopotezwa.
Mkuu WC, umemeliza kazi!Sasa Mzee wangu Mohamed, hivi vyeo unavyotaja wazee wako wamewahi kuvishika vilitokana na nini kama sio KATIBA hizo? Au walikuwa wanagawana vyeo na madaraka haya kama njugu au vikombe vya kahawa? Na haya ya ku-copy na ku-paste toka kwenye katiba ya Nkrumah uliyaona wapi au na yenyewe ulisimuliwa na wazee wako?
Dosari nyingine kubwa ya simulizi zako hizi ni hii ya kutozihusisha KATIBA hizi. Mzee Ally Sykes bado yupo. Tuombee kwake. Atakuwa nazo document hizi muhimu. Inawezekana wewe kuna mambo yanakusuta mle.
DAIMA udini huendekezwa na watu wenye mawazo ya kimaskini, watu hawataki kwenda shule, tazama matokeo ya form 2 shule za kiislam zilivyofeli mawka huu, sasa hawa ndo wakija kukua wanaanza kusema nyerere mchawi kawaonea, hivi mmeona shule za wakatoliki wameshika kumi bora kwa 50% pia mmeona na majina ya watoto hao kumi bora ni ya KIKRISTU. Hii inaakisi kwamba hata form 4, 6 na elimu ya juu, itakuwa hivyohivyo, mtalaumu nyerer weeee na umaskini wa MALI na maazo vitawatafuna mpaka KABURINI
K,
Nadhani umefaidika na majibu yangu.
wewe lazima katika"before life" ulikuwa sangomaKatuwacha wote hatuna njaa wala uchu na mali zote hizo, isipokuwa aliwaacha wazungu tu pale Williamson Diamond wajichotee. Na mabenki aliyotuwachia yalikuwa yana utajiri mkubwa wa ajabu na ya kimataifa. Na akaliwacha kanisa katoliki linahodhi ardhi kubwa zaidi Tanzania baada ya Serikali, au sio? Na nyadhifa zote Serikalini zimeshikiliwa na wakatoliki kwa asilimia 80 na zaidi au sio?
Na mpaka anaachia madaraka msaidizi wake mahsusi (personal secretary) ni mzungu, huyo ndio Nyerere.
![]()
Kumekucha...Mohamed Said, hebu tupe kisa cha huyu Sheikh.
[TABLE="class: infobox vcard, width: 22"]
[TR]
[TH="colspan: 2, align: center"]Kenya African National Union[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="class: logo, colspan: 2, align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"][/TH]
[TD="class: agent"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"][/TH]
[TD="class: agent"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Founder[/TH]
[TD="class: agent"]James Gichuru
Oginga Odinga
Tom Mboya[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Founded[/TH]
[TD]1960
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: infobox vcard, width: 22"]
[TR]
[TH="colspan: 2, align: center"]African National Congress[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="class: logo, colspan: 2, align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"][/TH]
[TD="class: agent"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"][/TH]
[TD="class: agent"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Founder[/TH]
[TD="class: agent"]JohDube,
Pixley ka Isaka Seme,
Sol Plaatje
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"][/TH]
[TD="class: agent"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"][/TH]
[TD="class: agent"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Founded[/TH]
[TD]8 January 1912[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: infobox vcard, width: 22"]
[TR]
[TH="colspan: 2, align: center"]Tanganyika African National Union[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="class: logo, colspan: 2, align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Leader[/TH]
[TD="class: agent"]Julius Nyerere[/TD]
[/TR]
[TR]
[TH="align: left"]Founded[/TH]
[TD]July 1954[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Si kweli! vitendo vyako vipo wazi.
...unatafuta pa kutokea! kwanza ulimdandia mwanasiasa kijana wa chama tawala ili akupe mdahalo, akakushtikia na kukutosa, sasa unaona njia ya kutokea ni kupitia Mohamed Said.
Kama Mohamed Said atakujibu basi itakuwa amekufanyia hisani sana, vizuri kawalete Maaskofu waje hapa na majina yao kamili (kama Mohamed Said anavyojiamini na jina lake kamili) ili waingie mdahalo na Mohamed Said, si wewe Yericko.
Hapo unajisikiaje? Roho inatamani kuona Founder wa TANU ni Abdu Sykes?
Hello am an honest caring good looking young girl
Hata waziri/naibu wa elimu/wakurugenzi wote baraza la mitihani/necta/watungaji/wasahihishaji mitihani wote wangekuwa ni waislam, bado waislam mngeendelea kulalama kuna mfumo kristo. Mkristo hana sababu ya kulalamikia NECTA ukizingatia mitihani ipo pale karibu mwaka mzima baada ya kusahihishwa...kama umeonewa ni suala la kuappeal tu...
We tapeli wa kinigeria umeibukia hapa? Humpati mtu hapa kakojoe ipumzishe.
Kwabahati mbaya kwako nikuwa hujui kuwa wanaukombozi wote wanaenziwa na serikali na sie tuaminio katika historia ya kweli tunawajua.La Hasha, nadhani nafasi ya Founders isingetosha ndiyo manaa pakaandikwa Leader kinyume na hizo za mbele kuandikwa founders. Hapana shaka Mwalimu alikuwa leader na si hapo tu aliendelea kuwa Leader kama rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mpaka alipoamua kwa khiari yake kung'atuka mwaka 1985.
Aidha roho inatamani au haitamani hili jambo jengine. La muhimu ni kwamba wazee wetu wote waliotoa mchango katika kututoa katika ukoloni wakumbukwe bila ya KUBAGUA na hao kwa uchache tu wakiwemo Sheikh Suleiman Takadir, Mwalimu Julius Nyerere, Sheikh Hassan bin Amir, John Rupia, Dosa Aziz, Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamed, Bilal Rehan Waikela, Saadani Abdu Kandoro, Kasella Bantu, Na wengine wengi!
MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA
Kwabahati mbaya kwako nikuwa hujui kuwa wanaukombozi wote wanaenziwa na serikali na sie tuaminio katika historia ya kweli tunawajua.
Ndugu yangu utaibiwa wewe, huyo ni mpigaji wa kinigeria wa mitandaoni ameni pm kwa meseji ya wizi kkama demu, lakini hapa anajigeuza kama dumeBwana Yericko tafadhali ondosha jina la muheshimiwa baada ya Yericko. Kwa sababu ya mstari huu tu umetuonesha ni mtu wa aina gani kwa maneno yako. Tafadhali fanya hili kwa heshima ya mwenye jina hilo
mzee Mohamed Saidi, ni kweli unakiri kwamba hukuwahi kuziona na kuzisoma katiba za TAA na TANU? na bado unajiita umeandika historia ya mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika "objectively"!