Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mimi nisiyejua kusoma sawa sawa naona kuna conflicting information. Nyerere alikuwa na akina Mwapachu Makerere, bila shaka Makererian wengine kama akina Kyaruzi walimfahamu pia.
Alikuwa katibu wa AA tawi muhimu sana la Tabora.

Alipelekwa kwa Sykes na Kasella Bantu. Nyerere alihudhuria mkutano wa AA iliyozaa TAA.
Hivi mtu akisema hafahamiki na yeyote kuna ukweli hapo! Mwenyezi mungu anazidi kutuwekea wazi yale yaliyofichwa na yasiyosemwa. Mwenyezi anazidi kuthibitisha ushahidi wetu kuhusu udini. Hapa Mohame anamnukuu Abdul Sykes aliyesema ''kwa ajili ya masilahi ya waafrika na yale ya jumuiya ya waafrika KWA UJUMLA''. Abdul Sykes, mwanaharakati na kiongozi mzalendo hakusema kwa ajili ya Waislam kama Mohamed anavyopotosha umma.

Mohamed amesema Waislam ndio walioongoza mapambano, hata kama aliji contradict kwa kuingiza majina ya akina Rupia, Mhando n.k. bado Abdul Syke anamsuta kuwa kazi hiyo haikufanywa kwa masilahi ya Waislam bali Waafrika kwa ujumla.
Hoja ya udini imetoka wapi?
 
Hii ''kukiri'' unakusudia kitu gani?
Kweli sijaziona wala haikunipitia kuzitafuta.
Ulijuaje kwamba katiba ya TANU ilinakiliwa kutoka katiba ya chama cha Nkrumah na kwamba ilibadilishwa tu majina pale pa Ghana iliandikwa Tanganyika?
 

Sadakta Bwana Mohammed! Allah aendelee kuipa nguvu YAKINI yako. Insha Allah uzidi kutuelimisha. Kitabu chako cha Abdulwahid sykes nimekipamba sebuleni pangu na nakupa Ahadi kuwa mwanangu sasa yupo nursery anasoma A, B, C, D..lakini akikuwa na yeye nitampa akisome!
 

... mwandishi amekuwa akiulizwa maswali mengi na watu mbalimbali kuhusu
ukweli ya yale aliyokuwa akiyaandika katika mchango wa Abdulwahid katika
uhuru wa Tanganyika.

Wasiwasi huu umekuwapo lau kama mwandishi amefanyarejea nyingi na za
kutosha kutoka magazeti ya zamani, vitabu,majarida na kumbukumbu zingine
za wakati wa ukoloni. Juu ya wasiwasi wote uliokuwapo hakuthubutu kujitokeza
yeyote kupinga yake mwandishi aliyoandika kuhusu historia ya Abdulwahid katika
TANU na uhuru wa Tanganyika.

Hata mwanahistoria wa CCM hakunyanyua kalamu yake. Hali hii ya CCM kuikataa
historia yake na wakati huo huo ikidai kuwa haijaweza kuihifadhi historia yake inatoa
mvuto fulani kwa watafiti kutaka kujua kulikoni. Ukweli wa kuwa CCM imeandika historia
yake lakini hapo hapo imeonekana upo upungufu mkubwa unaweka wazi suala la utafiti
ufanywe na watafiti huru ili ukweli upate kujitokeza.

Somo la historia ya uhuru wa Tanganyika bado lipo wazi kwa utafiti zaidi.
 

Asante sana mkuu!

Sasa waelewa wa mambo tukisema kuwa huyu mzee ni mchochezi wapo binadamu wanaoibuka kuja umtetea kwa jasho na damu.
 
Two different ideas are as good as parallel lines they will never met cuz mmoja ana discuss objectively mwingine ana discuss religiously,anyway ndio uhuru wa kutoa maoni huo na kuzungumza kile unachokiamini.
 

K,

Insha Allah.
Mungu atukuzie.

Amin.
 
Asante sana mkuu!

Sasa waelewa wa mambo tukisema kuwa huyu mzee ni mchochezi wapo binadamu wanaoibuka kuja umtetea kwa jasho na damu.

Yericko,

Ngoja nikufunze adabu.

Kwa kuniita mzee tayari ushafuzu kuwa una heshima na umeniheshimu
kwa uzee wangu.

Ukisema ''Huyu Mzee.''
Umetukana.

Sasa ile staha ulioonyesha awali inaondoka tunakuwa sawa.
Inawezekana kwa makuzi ya kwenu hili si hadhir kwako.

Ungesema mathalan ''Mzee ni mchochezi'' ungepatia.
Ondoa ''Huyu.''

Lakini sikulaumu haya mambo ya adabu na akhlak za mazungumzo nadhani
ziko mbali na nyie zinahitaji mfunzwe.
 
Sasa wewe kama msomi hukuona umhimu wa kujiridhisha kwa kuisoma katiba hiyo mwenyewe badala ya kumuamini Tewa moja kwa moja na kutuletea sisi simulizi hiyo?

Wala.

Nimesoma mswada wake huo ulinitosha unaitwa ''Probe Into the History of Islam in Tanzania.''
 
Wala.

Nimesoma mswada wake huo ulinitosha unaitwa ''Probe Into the History of Islam in Tanzania.''
Sijakuelewa, mswada wake nani?Tewa? kwa hiyo uandishi wako pamoja na majigambo yako yote ni wa "hear say" tu!
 

Naona mnaumizwa kwa kuambiwa kuwa Nyerere hakuwa anafahamika Dar es Salaam.

Ngoja nikuambie.
Abdu hakuwa anamjua Nyerere kabla ya siku ile alipoletwa kwake na Kasella Bantu.

Ikiwa aliokuwa anajulikana na wenzake wa Makerere bado kwa mji wa Dar es Salaam
Nyerere alikuwa mgeni hajulikani.

Baba yangu alikuwa maarufu sana Dar es Salaam katika circle za vijana wenzake na
kamjua Nyerere nyumbani kwa Abdu Sykes.

Shariff Attas mtu maarufu Dar es Salaam hakuwa anamjua Nyerere hadi alipomuona anakuja
ofisini kwa Abdu Sykes Kariakoo Market.

Mzee Mshume mtu maarufu Dar es Salaam hakumjua Nyerere hadi alipojulishwa na Abdu pale sokoni.

Sheikh Hassan bin Amir hakumjua Nyerere hadi alipopelekwa kwake na Abdu na Dossa.

Sheikh Mohamed Ramia hakuwa anamjua Nyerere hadi alipoletwa kwake na Idd Tosiri na
Idd Faiz Mafongo.

Waliokuwa wanamjua Nyerere ni hao hao jamaa waliotoka pamoja sehemu za bara.
Kwa Dar es Salaam alikuwa ni mgeni.

Kwani cha ajabu nini?

Ugeni si kitu cha kukionea aibu.

Mengine sina haja ya kujibu.
 
Sijakuelewa, mswada wake nani?Tewa? kwa hiyo uandishi wako pamoja na majigambo yako yote ni wa "hear say" tu!

G,

Haswa wala hujakosea.

Nikiwauliza naandika.

Mswada ni wa Tewa.

Kujigamba si kwa kuandika.
Kujigamba ni kule hawa waliofanya haya ni wazee wangu.
 
Nadhani umefika wakati mwafaka wa kumuumbua huyu mchochezi anayetumia kalamu yake kupandikiza chuki baina ya jamii ya Watanzania bila kutambua athari za hizi juhudi zake. Mohamed Said ni mtu hatari aliyeweza kuwarubuni na kuwateka wengi wenye uelewa finyu kwa kivuli cha dini, mfano hai unapatikana humu...wapo waamini wake ambao kwa upofu wao wameshindwa kabisa kuzitambua hila zake huyu mchochezi. Hapa chini ninampa maswali machache mapya ambayo natumaini yatawafumbua macho waliofunikwa na wingu zito na kushindwa kabisa kumwona huyu mchochezi kwa rangi yake;


  1. African Association (AA) kama ilivyo chimbuko lake ni nini, iliasisiwa lini, na nani na kwa malengo yapi?
  2. Kwa nini baadaye ilibidi jina hili libadilike na kujulikana kama TAA?
  3. Je ilikuwa lazima mtu awe mkaazi wa Dar es Salaam ili aweze kuwa Kiongozi wa TAA?
  4. Mawasiliano ya kwanza kabisa kati ya Mwalimu Nyerere na wazee wako wa Gerezani yalifanyika lini?
  5. Hayo mawasiliano yalianzishwa na nani, Mwalimu Nyerere au wazee wako wa Gerezani?
  6. Nani alifanya "approach" ya kwanza kumfikia (kumtembelea) mwingine...Mwalimu Nyerere au wazee wako wa Gerezani.
  7. Je kuna mikutano yoyote ilifanyika nyumbani kwa Mwalimu Nyerere akiwa Pugu? Kama ilifanyika ni ipiilikuwa ajenda kuu?
  8. Mkutano wa TAA wa October, 1953 ulifanyika katika nyumba iliyokuwa New Street, Dar es Salaam...hii nyumba ilikuwa ya nani, ilijengwa na nani na kwa malengo gani?
  9. Katika kubuni jina TANU, pendekezo la kwanza lilikuwa TAU (kumbuka Kenya tayari walikuwa na KAU)...je ni nani alipendekeza neno "National" liongezwe na kwa sababu zipi?
 
G,

Haswa wala hujakosea.

Nikiwauliza naandika.

Mswada ni wa Tewa.

Kujigamba si kwa kuandika.
Kujigamba ni kule hawa waliofanya haya ni wazee wangu.
Asante sana mzee Mohamed Saidi kwa kuongea ukweli wako kwamba huku wahi kuziona wala kuzisoma katiba za TAA na TANU, na kwmba masimulizi yako yote nikutoka kwa wazee wako tu na hasa mzee Tewa, na hata kama mzee Tewa aliongea hisia zake tu wewe kwako ni "historical facts" ambazo sisi wanahistoria wasomi ni lazima tukubaliane bila ubishi. Tukibisha hatuwatendei haki hawa mashujaa la si hivyo basi na sisi tuandike historia za mizee yetu ambayo haikuwa na mchango wowote!
 

G,

Ulichosisitiza ni sawa kabisa.
Nadhani sasa tumeelewana.

Sasa kuanzia hapa tusonge mbele.


a
 

Mag3,

Nadhani unaelewa sana kuwa huwa sijibu kila post.
 
Hapo unajisikiaje? Roho inatamani kuona Founder wa TANU ni Abdu Sykes?

Hapana.

Nimeeleza kuasisiwa kwa TANU katika kitabu na
hapa jamvini.

Wengi wamefaidika kwa yale ambayo hayakuwa
hadhir.

Khiyari ni yao kuamua kati ya ile historia rasmi
ya Kivukoni na hii yangu nani mkweli?
 
Bw Said wewe hujanipata mimi kabisa; sina tatizo na uandishi wako hata kidogo wala kuandika kwa kutumia mwanga wa Uislamu. Nilikuwa namjibu huyu kijana ambaye ameona miye kukuuliza kuhusu dini ya Kina Kleist na wazee wao kuwa ni udini. Hoja nzima ya kwako ya kitabu na kazi zako imejengwa kwenye dini kwa hiyo ni vizuri mtu akasoma hivyo na kufanya hivyo wala siyo udini ni uamuzi tu umeuchukua. Sasa na wasomaji nao wana haki ya kuulizia maswali ya dini kwa kadiri yanavyojitokeza katika uandishi wako sivyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…