Punguza jazba, hapa unapewa ukweli, hiyo ndio sifa moja ya Waislaam.
Naona povu linakutoka, punguza munkar kidogo ili uweze kupata darsa la historia ya Waislaam waliopigania Uhuru.
Tatizo lako ni Uislaam, Waislaam, Historia ya Tanganyika, au unayosomeshwa na Maalim Mohamed Said? Maana naona mara huku mara kule, unakuwa kama kadondo? Hutulii ukachuma ilm?
Raha ya mnakasha utulie, usipopaelewa unauliza, usipokubali unapakataa na wewe unaleta unayo ona ndio sawa, sasa ukiwa unahaha kila upande unakuwa hueleweki.
Kunywa maji kidogo, tulizana nusu saa, fikiria, ujuwe tatizo ni lipi katika hayo niliyokuuliza? Ukishalijuwa, njoo uendelee. Ukiwa na jazba mwishowe unashindwa ku "reason". Usiwe na wasi, inshaAllah Mohamed Said yupo, Ritz yupo, The big show yupo na wenzako wapo. Tutapeana tu ilm taratiiiibu.
Huoni mwenzako
Yericko Nyerere alivyo tulizana, ujuwe anajifikiria, ajue tatizo ni nini haswa!