Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Zomba ,
Naona mlishazoea kuobsfucate. Ritz alisema Arafat alikutana na Moshe Dayan Camp David. All I said there was no such meeting. Wewe ukaleta za Menachem Begina kukutana na Anwar Sadat. Where does Arafat come in here? Is Sadat Arafat? Is Egyptian peace treaty equal to Moshe Dayan meeting with Arafat at Camp David? Come on? Mbona Ritz mwenyewe amekaa kimya baada ya kutambua aliboronga? Come on!

Hayo niliyokuwekea rangi nyekundu ni maandiko yako au si yako?

quote_icon.png
By Jasusi
Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.
 
Unatafuta pakutokea? kwi kwi kwi teh teh teh.

Kuna mwingine atakuja kesho kwa mkwala mzito na maneno yake sasa umefika wakati wa kumuumbua huyu Mohamed Said.

Halafu anaweka maswali ya chekechea anaondoka.

Huyu yeye anajifanya mwakilishi wa members wa JF.
 
Mohamed,
What is the point? Hata kama kuna mtu ameunga mkono hoja yako kuwa Nyerere alikuwa hajulikani wakati huo, lakini ukweli ni kwamba alipouchukua uongozi wa TANU alifanya kazi ambayo hata wazee wako hawakuweza kuifikia--kuisambaza TANU kwenye pembe au kona zote za Tanganyika. Ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu cha Judith Listowell:
" In the north of Tanganyika, Nyerere made a great impression. Lucy Lameck, the first woman to become a junior minister in Tanganyika, was present when he addressed her tribe, the Chagga:
I had met Julius in Dar-es-Salaam in 1953 [Lucy told the author]. Long before that I had felt that, in order to be effective in a hospital, or a school, or an office, I had to turn to politics. To obtain equal treatment was part of a much larger problem, the problem of existence under a colonial government... At this time we Chaggs had a paramount Chief called Tom Marealle, an arrogant man who made life very difficult for all of us who did not approve of his politics. When Twining offered me a scholarship to England, Marealle turned it down. I would rather not tell you why. I have never cried so much in my life. By then TANU was in existence and I pinned all my hope on it.
In October 1954 Julius Nyerere came to Moshi and held meetings. At one of them I enrolled my father, my mother, my aunt and my two sisters. Soon after that I was elected representative of the district. On his return from the Trusteeship Council meeting, Julius came north again and held two meetings: one in Machame and the other in Moshi. I went to both and witnessed the marvellous effect he had on my people. Now we TANU enthusiasts began to campaign in earnest.....We told people about the need for education and how little the British had done about it. We talked about the land shortage, and the injustice of having large areas not permitted to be used. We told them that Tanganyika was our country and that we were going to run it in our way. We told them that TANU, headed by Julius, would lead us to independence."

Hiyo ndiyo kazi aliyoifanya Julius Nyerere mbali na wazee wako kuanzisha TAA. Hiyo ndiyo sababu Julius Nyerere stands above the rest, including above your Gerezani TANU founders. Kesho nitawaletea kisha cha Austin Shaba na jinsi alivyomsaidia Nyerere katika Southern Highlands. Taking the baton from your Gerezani wazee, Nyerere became a trailblazer spreading the fires of independence in all corners of Tanzania.
J,

Ni kweli alivyosema Listowel lakini si kweli tupu karuka baadhi ya mambo.
Ngoja nikuonjeshe hapa siasa za TANU zilivyokuwa Kilimanjaro.

Ila napenda tu kukufahamisha wengi wakipata huwa wanapata maradhi
ya kusahau.

Mzee Yusuf Ngozi ndiye aliyemtia Lucy Lameck katika siasa.
Inasikitisha sana kuwa Mzee Yusuf Ngozi hadi leo mchango wake haujathaminiwa.

Na alifanya makubwa.

Nyerere asingeweza kazi hii peke yake kuna wengi waliomsaidia huko mikoani.
Hao wote nimekutananao na ninaweza Insha Allah kuweka taarifa zao hapa jamvini.

Inasikitisha kuwa hata yeye alipokuwa anatajika peke yake katika historia ya uhuru
wa Tanganyika hakujisikia vibaya.

Mimi nimefanya mahojianonae na nimemweleza vizuri katika kitabu changu ''Uamuzi
wa Busara,'' Abantu Publications Dar es Salaam 2007.

Mtoto wake mkubwa alinitafuta na kunishukuru sana na kunizawadia picha ya baba
yake katika ujana akiwa katika siasa.

Moja ya matatizo ya kitabu cha Listowel ni kuwa utafiti wake
ulikwenda haraka haraka na akikutana na ''high society'' kama
alivyokuwa yeye mwenyewe.

Kabla hajaolewa na Listowel ambae alikuwa kutoka ''upper class''
huyu mama alikuwa mtu wa ''show business.''

Mumewe alikuwa balozi wa Uingereza Ghana.

Nakuwekea siasa za Moshi kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'':

Joseph Kimalando na Japhet Kirilo walikuwa wajumbe toka Jimbo la Kaskazini katika ule mkutano mkuu wa 1954 wa kuunda TANU.[

Kumbukumbu za wakoloni zinamuonyesha Kimalando kama mtu aliyejihusisha na siasa za African Association alipokuwa akifanya kazi mjini Dar es Salaam katika miaka ya 1930.

Kimalando akiwa mzee mwanaharakati, aliheshimiwa sana na vijana waliokuwa makao makuu kama vile kwa John Rupia.

Kimalando alikataa kusajili TANU Moshi.

Kimalando alikuwa mwanasiasa mkongwe toka enzi ya African Association katika miaka ya 1930, akishiriki siasa za wakati ule huku akifanya kazi Tanganyika Railways.

Aliporudi Moshi sasa akiwa mtu mzima, aliajiriwa katika ofisi ya wakili mwenye asili ya Kiasia.

Inawezekana kabisa fikra za umri wake mkubwa baada ya kustaafu na kazi yake hii mpya ilimuweka katika hali ambayo haikumwezesha kukijenga TANU ili kudai uhuru wa Tanganyika.

Aliwazia hali yake ya baadaye zaidi kuliko siasa. Kwa ajili hii Kimalando alishindwa kukisajili TANU Moshi kama chama cha siasa.

Hii ilikuwa pigo kubwa kwa kuwa Kimalando alikuwa hodari wa kuandika Kiingereza na kwa wakati ule ilidhaniwa kuwa kujua lugha hiyo kwa fasaha ni muhimu katika kuendesha mambo ya siasa na serikali.

Wakati sehemu nyingine zikihamasika na harakati za kudai uhuru Moshi ilikuwa katika usingizi.

Uongozi wa TANU Arusha, chini ya Japhet Kirilo ulikuja Moshi pamoja na Rajab Chamshama na Robert Otieno kuja kuchunguza kwa nini TANU ilikuwa inachelewa kusajiliwa Moshi.

Viongozi hawa waliitisha mkutano wa uchaguzi Welfare Centre ambao ulihudhuriwa na watu takriban ishirini na wa tano, mmoja wao akiwa Yusuf Ngozi.

Mkutano ule ulimchagua Mzee Yusuf Ngozi kuwa mwenyekiti wa kwanza wa tawi la TANU Moshi mjini.

Taratibu Kimalando akawekwa pembeni.

Katika halmashauri ya kwanza ya tawi lile alikuwapo msichana mdogo wa miaka ishirini na minne, Lucy Lameck ambae baadaye alikuja kuwa waziri katika serikali ya wananchi.

Inasemekana miongoni mwa matawi yote ya TANU nchini Tanganyika, tawi pekee lililoungwa mkono na wanawake na wao kuwa ndiyo nguvu kuu ya chama, lilikuwa tawi la TANU la Moshi mjini.

Nguvu kuu ya TANU ilikuwa wanawake waliokuwa wakiuza mbege, pombe maarufu ya kienyeji huko Kilimanjaro.

Uuzaji wa pombe huko Kilimanjaro ilikuwa ni kazi ya wanawake tu, wanaume hawakujishughulisha nayo.

Mkuu wa kilabu cha pombe alikuwa mwanamke mmoja wa Kimasai, Mama Binti Maalim.

Ingawa mume wa Binti Maalim, Jumbe Mohamed, alikuwa mtumishi wa serikali, na kwa hiyo alijitenga na siasa, hili halikumzuia mke wake, Binti Maalim kuwa mwanachama na mwanaharakati wa TANU.

Binti Maalim alihakikisha kwamba kila mwanamke aliyekuwa akifanya biashara mahali pale alikuwa mwanachama wa TANU na alikuwa akitoa sehemu katika kipato chake kusaidia harakati za kudai uhuru.

Wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU walikuwa wale akina mama wauza pombe waliohamasishwa kujiunga na chama na Mama Binti Maalim.

Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari yake ya pili ya Nyerere Kilimanjaro.

Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi la TANU Moshi.

Joseph Kilamalando aliogopa kuitumikia TANU lakini alijiona amesalimika kuifanyia kazi United Tanganyika Party (UTP), chama cha Wazungu kilichoundwa kuipinga TANU.

Kimalando alikuwa katibu wa UTP Moshi, na Mohamed ''Kishikio'' Badi mwenyekiti wake.

Mzee Yusuf Ngozi aliwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTP hadi ikafa.

Wanawake wale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi ofisi ya TANU.

Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vya kisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya kadi za UTP na kumpelekea rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwa hawakitaki chama chake cha vibaraka.
 
Ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu cha Judith Listowell:

Kwanini usitumegee kutoka kitabu cha kivukoni? na ingekuwa raha zaidi ungesema "ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu (changu)".
 
Kwanini usitumegee kutoka kitabu cha kivukoni? na ingekuwa raha zaidi ungesema "ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu (changu)".

Zomba,

Ni hivi kwa hakika kwa hadhi ya Jasusi si mtu wa maskhara ni mtu makini.

Kwa kumleta Listowel alikuwa na yakini na kwa nia njema kuongeza taarifa
katika mnakasha sote tufaidike.

Ila hakujuwa kuwa katika hali tafiti zilipofikia kuhusu historia ya uhuru wa
Tanganyika mengi mapya yamepatikana.

Unajua Listowel kaja Tanganyika 1962.

Bahati mbaya kaja wakati tu Abdu na Nyerere wameshaghitafiana kuhusu
historia ya TANU.

Waliokuwa wanahojiwa na Listowel walikuwa wanajua kuwa ukienda kinyume
na historia kama alivyotaka Nyerere iwe...

Kwa hiyo akawa Listowel analishwa kile kilichokuwa kinapendeza masikioni kwa
Nyerere.

Hapo ndipo kulipokuwa na matatizo makubwa.

Historia ya TANU ni ile ile Listowel kaieleza na mimi nimeieleza kama nilivyopokea
kwa wazee wangu.

Jasusi hawezi kuleta ukurasa kutoka Kivukoni.
Jasusi ni mjuzi na akimjua vyema marehemu Abdu Sykes ni mzee wake.
 
WC.

Umesema kweli.
Hayo yote wamefanya wazee wangu.

Nakubali na wewe yako mengi unayajua ambayo mimi
siyajui.

Kitu kimoja umenikumbusha mbali.

Hakika dunia yangu ilikuwa Kipata na New Street na
gramafoni niliyokuwa nikisikiliza nyimbo za Salum Abdallah
na Septet Habanero ya Cuba.

Nje ya hapo labda nikipanda basi la gorofa la DMT.

Nilichojifunza, ila nakili kwamba, mwanzoni nilimuona mwanazuoni Mohamed ni mdini na anaipotosha history ya Tanganyika. Lakini kadini, nilivyokuwa nafuatilia, nimejifunza Mohamed ni mwanazuoni hasa.
Mimi si mshabiki wa malumbano ya dini, lakini mzee mohamed amwchambua historia kwa undani sana, amewaelimisha wengi sana...
Mods hii thread kama ingewapendeza, mngeiweka kwenye sticky category. Humu kuna mambo mengi sana ya ki historia ambayo wanazuoni wanaweza kujifunza.
Pia, Mods mngefanya utaratibu wa kumuomba Mzee Mohamed, ili mfanye nae "exclusive interview" kuhusu historia ya tanzania kwa ujumla. wazee kama hawa wamebaki wachache sana...
 
Interview tena? Huyu si mzee wa 'nipe nikupe' kama mwenyewe anavyosema. Sema wapange ili Mohamed Said aje awasimulie simulizi. Msome vizuri mzee wetu utaelewa nina maana gani!
 
Interview tena? Huyu si mzee wa 'nipe nikupe' kama mwenyewe anavyosema. Sema wapange ili Mohamed Said aje awasimulie simulizi. Msome vizuri mzee wetu utaelewa nina maana gani!

Sweke34,

Ndipo ulipoangukia huko?
Sasa umekuwa mchezea pembeni?
 
Tatizo jingine la Uislam ni kuficha kwa saana mapungufu ya DINI hii na yale ya Mtume Mohamad( S.A.W). Hamtatoka mlipo. Endeleeni kuyahamishia matatizo haya kungine au kuyafutika kwenye busati. Hayatatulika!

Ukitaka kujua Mwalimu hakuwa na mchezo katika kusimamia KATIBA na SHERIA za NCHI, OK, rafiki yake mkubwa ni mfano mzuri sana. Jakaya wetu kamgwaya Lowasa!

Punguza jazba, hapa unapewa ukweli, hiyo ndio sifa moja ya Waislaam.

Naona povu linakutoka, punguza munkar kidogo ili uweze kupata darsa la historia ya Waislaam waliopigania Uhuru.

Tatizo lako ni Uislaam, Waislaam, Historia ya Tanganyika, au unayosomeshwa na Maalim Mohamed Said? Maana naona mara huku mara kule, unakuwa kama kadondo? Hutulii ukachuma ilm?

Raha ya mnakasha utulie, usipopaelewa unauliza, usipokubali unapakataa na wewe unaleta unayo ona ndio sawa, sasa ukiwa unahaha kila upande unakuwa hueleweki.

Kunywa maji kidogo, tulizana nusu saa, fikiria, ujuwe tatizo ni lipi katika hayo niliyokuuliza? Ukishalijuwa, njoo uendelee. Ukiwa na jazba mwishowe unashindwa ku "reason". Usiwe na wasi, inshaAllah Mohamed Said yupo, Ritz yupo, The big show yupo na wenzako wapo. Tutapeana tu ilm taratiiiibu.

Huoni mwenzako Yericko Nyerere alivyo tulizana, ujuwe anajifikiria, ajue tatizo ni nini haswa!
 
Nilichojifunza, ila nakili kwamba, mwanzoni nilimuona mwanazuoni Mohamed ni mdini na anaipotosha history ya Tanganyika. Lakini kadini, nilivyokuwa nafuatilia, nimejifunza Mohamed ni mwanazuoni hasa.
Mimi si mshabiki wa malumbano ya dini, lakini mzee mohamed amwchambua historia kwa undani sana, amewaelimisha wengi sana...
Mods hii thread kama ingewapendeza, mngeiweka kwenye sticky category. Humu kuna mambo mengi sana ya ki historia ambayo wanazuoni wanaweza kujifunza.
Pia, Mods mngefanya utaratibu wa kumuomba Mzee Mohamed, ili mfanye nae "exclusive interview" kuhusu historia ya tanzania kwa ujumla. wazee kama hawa wamebaki wachache sana...

Wazo lako zuri sana na nnakuunga mkono, nawaomba magwiji wa interview wa JF kina Mwali, AshaDii, na wengineo watutayarishie hiyo interview. Natumai wataitikia huu mwito na kutuandalia ukumbi.
 
Maalim Mohamed Said niruhusu nimwambie Nguruvi3;

Haya, ukisimama tena katafute lingine la kuzuwa hilo umesambaratishwa kwa kulambwa moja ya kichwa, moja ya mbavu.
Ama kweli, Zomba mtu aulizwe swali halafu ajinukuu! wewe unaona ilm hiyo! real
Anyway, nilichotaka kukumbusha ni kuwa ukijibu post zangu usi quote napata notification zako nisizohitaji kujua kama umefanya chochote kuhusu hoja zangu. Please nisaidie kwa hili.

Halafu huu mnakasha hukuwepo umeanzia mwisho basi kila wakati unaandika hata kisicho na tija.
Sheikh Zomba, hivi hujiulizi kwanini watu hawakujibu! just think about that.

Mbona Mohamed alisharambaratika siku nyingi! kwani hujui ''mimi sijibu kila kitu'' au ''hilo sina ujuzi nalo'' pia ''tusiongelee hilo tuliache kwanza'' na sasa ''mimi nakwenda Capetown, nina vitabu cambridge na Yemeni university''.

Muulize hoja ya namba za mitihani imeishia wapi kama si hapa JF! siku hizi kimya wala hataki kuisikia.
Anyway, tutaendelea kusoma historia ya Tandamti, kidongo chekundu, kipata na Narung'ombe.
Ikija ya Tanganyika tutamwambia , Dear Mzee this is anachronism! Hell no! Tanganyika is more than Gerezani.

Basi sheikh Zomba wajulie hali nyumbani na inshallah tutaendelea kukusoma bila kukujibu maana kiwango chako ni cha kuosmwa tu kwa mwenye nafasi ya ziada.

Masalaam sheikh wangu
 
MM,

Ikiwa wewe unaona Nyerere alikuwa maarufu Dar es Salaam hakuna shida.
Tusivutane na jambo dogo kama hilo.

Tuachie kuwa alikuwa mashuhuri na wote akina Shariff Attas, Tatu biti Mzee,
Abdu Sykes, Sheikh Hassan bin Amir na wengine wote wakimjua na hakukuwa
na haja yoyote ya yeye kutambulishwa kwa wanamji.

Na hii inaeleza ule wepesi wa yeye kuasisi TANU na katika miezi 10 tu akenda
UNO, New York.

Huyu ni mwanamji mtu maarufu.

Wasaa, fedha, umaarufu alikuwanao ndiyo maana alipofika Dar tu kaanzisha chama
cha siasa na kapata wanachama wengi.

Ndiyo maana hapakuwa na sababu ya kumtaja Abdu Sykes na nduguze katika historia
ya TANU ya Kivukoni kwa kuwa mambo yote Nyerere kafanya kwa nguvu zake mwenyewe.

Nyerere alikuwa maarufu.
Hakuwa muhitaji kwa yeyote yule katika wenyeji wa Dar es Salaam.

Jaribio lako la kejeli ni dhaifu na linasikitisha; inahitaji ujifunze kidogo kuandika sarcasm. Hakuna mtu yeyote aliyedai Nyerere alikuwa maarufu katika jiji la Dar; ukinisoma vizuri - kitu ambacho nina mashaka unaweza kukifanya - hoja yangu ilikuwa ndogo tu. Nyerere kutokujulikana Dar hakukuwa tatizo kwake na wazee wako kutomkujua Nyerere haina maana Nyerere alikuwa siyo maarufu. Tayari umeambiwa alipoenda kusoma Uingereza alikuwa ni Mtanganyika wa pili kwenda kusoma Uingereza na wa kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Edinburg! Hiyo ilikuwa katikati ya miaka ya 40.

Waingereza ndio walikuwa wanatawala Tanganyika; katika Tanganyika yote wakati Nyerere anamaliza shahada yake ya pili alikuwa ni Mtanzania wa kwanza kupata shahada ya pili Uingereza. Halafu unawaambia watu kwua hakuwa maarufu! Kweli katika kada ya wasomi Dar-es-Salaam hakuna aliyesikia juu ya Mtanganyika huyo wa kwanza ambaye amesoma Uingereza? Ukisoma kitabu chako wewe mwenyewe unaashiria kuwa Nyerere alipokuja Dar sifa zake zilikuwa tayari zimetangaa.

Umaarufu wa Nyerere haukuja baada ya kuja Dar 1953; ulimtangulia muda mrefu kabla. Wazee wa Uswahilini labda hawakuwahi kusikia lakini watoto wao kina Mwapachu, Dossa na wenzao walishamsikia Nyerere! Na ni wao walitambua wanamhitaji na walitambua wanahitaji kuwatambulisha wazee wao kwake. Na Nyerere akiwa mtu aliyelelewa na wazee na aliyekuwa na marafiki Waislamu tangu utoto - kabla hajawa Mkatoliki - aliwaamini wazee hao, aliwaheshimu na kwa kweli aliwapenda na wao walimpenda. Hadi mwaka 1965 angalau unatusimulia jinsi wazee wako walivyokuwa na mapenzi naye licha ya kuwa tayari kikundi cha waasi kilishang'olewa mwaka 1963. Hadi anakufa mwaka 1999 wazee wa Dar walikuwa na mapenzi naye, walimlilia, na kwa kweli kabisa wanamkumbuka kwa haiba kubwa ukiondoa wale waliokwua na udini tangu 1958 ambao hawakuwa tayari kuona Mkristu anapata nafasi ya umaarufu Dar.

Hawa watoto wao ndio leo wameanzisha mashambulizi yale yale dhidi ya Nyerere kama baba zao walivyofanya miaka ya 1950. Na bila ya shaka katika hawa wewe umekuwa mfalme wao.
 
Ama kweli, Zomba mtu aulizwe swali halafu ajinukuu! wewe unaona ilm hiyo! real
Anyway, nilichotaka kukumbusha ni kuwa ukijibu post zangu usi quote napata notification zako nisizohitaji kujua kama umefanya chochote kuhusu hoja zangu. Please nisaidie kwa hili.

Halafu huu mnakasha hukuwepo umeanzia mwisho basi kila wakati unaandika hata kisicho na tija.
Sheikh Zomba, hivi hujiulizi kwanini watu hawakujibu! just think about that.

Mbona Mohamed alisharambaratika siku nyingi! kwani hujui ''mimi sijibu kila kitu'' au ''hilo sina ujuzi nalo'' pia ''tusiongelee hilo tuliache kwanza'' na sasa ''mimi nakwenda Capetown, nina vitabu cambridge na Yemeni university''.

Muulize hoja ya namba za mitihani imeishia wapi kama si hapa JF! siku hizi kimya wala hataki kuisikia.
Anyway, tutaendelea kusoma historia ya Tandamti, kidongo chekundu, kipata na Narung'ombe.
Ikija ya Tanganyika tutamwambia , Dear Mzee this is anachronism! Hell no! Tanganyika is more than Gerezani.

Basi sheikh Zomba wajulie hali nyumbani na inshallah tutaendelea kukusoma bila kukujibu maana kiwango chako ni cha kuosmwa tu kwa mwenye nafasi ya ziada.

Masalaam sheikh wangu

Unakwenda kuja na ile ya nani hii? Unajifanya hukuona "kaniki" ? Ile ilikuwa nzito. Nilijuwa utaingia mitini ilikuwa nzito sana kwako.
 
Jaribio lako la kejeli ni dhaifu na linasikitisha; inahitaji ujifunze kidogo kuandika sarcasm. Hakuna mtu yeyote aliyedai Nyerere alikuwa maarufu katika jiji la Dar; ukinisoma vizuri - kitu ambacho nina mashaka unaweza kukifanya - hoja yangu ilikuwa ndogo tu. Nyerere kutokujulikana Dar hakukuwa tatizo kwake na wazee wako kutomkujua Nyerere haina maana Nyerere alikuwa siyo maarufu. Tayari umeambiwa alipoenda kusoma Uingereza alikuwa ni Mtanganyika wa pili kwenda kusoma Uingereza na wa kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Edinburg! Hiyo ilikuwa katikati ya miaka ya 40.

Waingereza ndio walikuwa wanatawala Tanganyika; katika Tanganyika yote wakati Nyerere anamaliza shahada yake ya pili alikuwa ni Mtanzania wa kwanza kupata shahada ya pili Uingereza. Halafu unawaambia watu kwua hakuwa maarufu! Kweli katika kada ya wasomi Dar-es-Salaam hakuna aliyesikia juu ya Mtanganyika huyo wa kwanza ambaye amesoma Uingereza? Ukisoma kitabu chako wewe mwenyewe unaashiria kuwa Nyerere alipokuja Dar sifa zake zilikuwa tayari zimetangaa.

Umaarufu wa Nyerere haukuja baada ya kuja Dar 1953; ulimtangulia muda mrefu kabla. Wazee wa Uswahilini labda hawakuwahi kusikia lakini watoto wao kina Mwapachu, Dossa na wenzao walishamsikia Nyerere! Na ni wao walitambua wanamhitaji na walitambua wanahitaji kuwatambulisha wazee wao kwake. Na Nyerere akiwa mtu aliyelelewa na wazee na aliyekuwa na marafiki Waislamu tangu utoto - kabla hajawa Mkatoliki - aliwaamini wazee hao, aliwaheshimu na kwa kweli aliwapenda na wao walimpenda. Hadi mwaka 1965 angalau unatusimulia jinsi wazee wako walivyokuwa na mapenzi naye licha ya kuwa tayari kikundi cha waasi kilishang'olewa mwaka 1963. Hadi anakufa mwaka 1999 wazee wa Dar walikuwa na mapenzi naye, walimlilia, na kwa kweli kabisa wanamkumbuka kwa haiba kubwa ukiondoa wale waliokwua na udini tangu 1958 ambao hawakuwa tayari kuona Mkristu anapata nafasi ya umaarufu Dar.

Hawa watoto wao ndio leo wameanzisha mashambulizi yale yale dhidi ya Nyerere kama baba zao walivyofanya miaka ya 1950. Na bila ya shaka katika hawa wewe umekuwa mfalme wao.

Unauliza wewe unajijibu wewe, Mohamed Said kishakwambia alikuwa maarufu sana. Mimi naongezea, umaarufu wake ndio ulimfikisha kwa Alwatan Sykes. Au nalo ni kejeli?

Naona umerudi kivingine.
 
Uuzaji wa pombe huko Kilimanjaro ilikuwa ni kazi ya wanawake tu, wanaume hawakujishughulisha nayo.

Mkuu wa kilabu cha pombe alikuwa mwanamke mmoja wa Kimasai, Mama Binti Maalim.

Humtambulisi kama mwanamke wa Kiislamu... kwanini?

Ingawa mume wa Binti Maalim, Jumbe Mohamed, alikuwa mtumishi wa serikali, na kwa hiyo alijitenga na siasa, hili halikumzuia mke wake, Binti Maalim kuwa mwanachama na mwanaharakati wa TANU.

Binti Maalim alihakikisha kwamba kila mwanamke aliyekuwa akifanya biashara mahali pale alikuwa mwanachama wa TANU na alikuwa akitoa sehemu katika kipato chake kusaidia harakati za kudai uhuru.

Huyu mama wa Kiislamu inaonekana alitoa mchango mkubwa kama wa Mshume Kiyeta lakini hata jina la mtaa halipo; maskini wa Mungu.

Wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU walikuwa wale akina mama wauza pombe waliohamasishwa kujiunga na chama na Mama Binti Maalim.
Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari yake ya pili ya Nyerere Kilimanjaro.

Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi la TANU Moshi.

Joseph Kilamalando aliogopa kuitumikia TANU lakini alijiona amesalimika kuifanyia kazi United Tanganyika Party (UTP), chama cha Wazungu kilichoundwa kuipinga TANU.

Kimalando alikuwa katibu wa UTP Moshi, na Mohamed ''Kishikio'' Badi mwenyekiti wake.

Mzee Yusuf Ngozi aliwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTP hadi ikafa.

Wanawake wale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi ofisi ya TANU.

Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vya kisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya kadi za UTP na kumpelekea rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwa hawakitaki chama chake cha vibaraka.

Duh; kumbe nilidhani wamesahauliwa Waislamu tu; kumbe wapo na wauza pombe waliotoa mchango mkubwa katika kuijenga TANU. Inabidi hawa nao wakumbukwe isije kuwa Nyerere alikuwa na jambo dhidi ya kinamama wauza pombe.
 
Hayo niliyokuwekea rangi nyekundu ni maandiko yako au si yako?

Zomba,
Mbona unataka kukuza jambo dogo? Ritz alizungumzia mkutano wa Camp David baina ya Arafat na Moshe Dayan. Haukuwepo. Mkutano uliokuwepo Camp David enzi za Menachem Begin ni baina ya Begin na Sadat. That is all what I was telling Ritz. Begin hawezi kugeuka kuwa Moshe Dayan, na Sadat hawezi kugeuka kuwa Arafat. Capice?
 
Back
Top Bottom