zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Mohamed, TAA kama political party ulishawahi kuona katiba yake?
Unatafuta pakutokea? kwi kwi kwi teh teh teh.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mohamed, TAA kama political party ulishawahi kuona katiba yake?
Watch tower
Zomba ,
Naona mlishazoea kuobsfucate. Ritz alisema Arafat alikutana na Moshe Dayan Camp David. All I said there was no such meeting. Wewe ukaleta za Menachem Begina kukutana na Anwar Sadat. Where does Arafat come in here? Is Sadat Arafat? Is Egyptian peace treaty equal to Moshe Dayan meeting with Arafat at Camp David? Come on? Mbona Ritz mwenyewe amekaa kimya baada ya kutambua aliboronga? Come on!
Unatafuta pakutokea? kwi kwi kwi teh teh teh.
J,Mohamed,
What is the point? Hata kama kuna mtu ameunga mkono hoja yako kuwa Nyerere alikuwa hajulikani wakati huo, lakini ukweli ni kwamba alipouchukua uongozi wa TANU alifanya kazi ambayo hata wazee wako hawakuweza kuifikia--kuisambaza TANU kwenye pembe au kona zote za Tanganyika. Ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu cha Judith Listowell:
" In the north of Tanganyika, Nyerere made a great impression. Lucy Lameck, the first woman to become a junior minister in Tanganyika, was present when he addressed her tribe, the Chagga:
I had met Julius in Dar-es-Salaam in 1953 [Lucy told the author]. Long before that I had felt that, in order to be effective in a hospital, or a school, or an office, I had to turn to politics. To obtain equal treatment was part of a much larger problem, the problem of existence under a colonial government... At this time we Chaggs had a paramount Chief called Tom Marealle, an arrogant man who made life very difficult for all of us who did not approve of his politics. When Twining offered me a scholarship to England, Marealle turned it down. I would rather not tell you why. I have never cried so much in my life. By then TANU was in existence and I pinned all my hope on it.
In October 1954 Julius Nyerere came to Moshi and held meetings. At one of them I enrolled my father, my mother, my aunt and my two sisters. Soon after that I was elected representative of the district. On his return from the Trusteeship Council meeting, Julius came north again and held two meetings: one in Machame and the other in Moshi. I went to both and witnessed the marvellous effect he had on my people. Now we TANU enthusiasts began to campaign in earnest.....We told people about the need for education and how little the British had done about it. We talked about the land shortage, and the injustice of having large areas not permitted to be used. We told them that Tanganyika was our country and that we were going to run it in our way. We told them that TANU, headed by Julius, would lead us to independence."
Hiyo ndiyo kazi aliyoifanya Julius Nyerere mbali na wazee wako kuanzisha TAA. Hiyo ndiyo sababu Julius Nyerere stands above the rest, including above your Gerezani TANU founders. Kesho nitawaletea kisha cha Austin Shaba na jinsi alivyomsaidia Nyerere katika Southern Highlands. Taking the baton from your Gerezani wazee, Nyerere became a trailblazer spreading the fires of independence in all corners of Tanzania.
Ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu cha Judith Listowell:
Kwanini usitumegee kutoka kitabu cha kivukoni? na ingekuwa raha zaidi ungesema "ngoja na mimi niwamegee kipande kutoka kitabu (changu)".
WC.
Umesema kweli.
Hayo yote wamefanya wazee wangu.
Nakubali na wewe yako mengi unayajua ambayo mimi
siyajui.
Kitu kimoja umenikumbusha mbali.
Hakika dunia yangu ilikuwa Kipata na New Street na
gramafoni niliyokuwa nikisikiliza nyimbo za Salum Abdallah
na Septet Habanero ya Cuba.
Nje ya hapo labda nikipanda basi la gorofa la DMT.
Interview tena? Huyu si mzee wa 'nipe nikupe' kama mwenyewe anavyosema. Sema wapange ili Mohamed Said aje awasimulie simulizi. Msome vizuri mzee wetu utaelewa nina maana gani!Nilichojifunza, ila nakili kwamba, mwanzoni nilimuona mwanazuoni Mohamed ni mdini na anaipotosha history ya Tanganyika. Lakini kadini, nilivyokuwa nafuatilia, nimejifunza Mohamed ni mwanazuoni hasa.
Mimi si mshabiki wa malumbano ya dini, lakini mzee mohamed amwchambua historia kwa undani sana, amewaelimisha wengi sana...
Mods hii thread kama ingewapendeza, mngeiweka kwenye sticky category. Humu kuna mambo mengi sana ya ki historia ambayo wanazuoni wanaweza kujifunza.
Pia, Mods mngefanya utaratibu wa kumuomba Mzee Mohamed, ili mfanye nae "exclusive interview" kuhusu historia ya tanzania kwa ujumla. wazee kama hawa wamebaki wachache sana...
Interview tena? Huyu si mzee wa 'nipe nikupe' kama mwenyewe anavyosema. Sema wapange ili Mohamed Said aje awasimulie simulizi. Msome vizuri mzee wetu utaelewa nina maana gani!
Tatizo jingine la Uislam ni kuficha kwa saana mapungufu ya DINI hii na yale ya Mtume Mohamad( S.A.W). Hamtatoka mlipo. Endeleeni kuyahamishia matatizo haya kungine au kuyafutika kwenye busati. Hayatatulika!
Ukitaka kujua Mwalimu hakuwa na mchezo katika kusimamia KATIBA na SHERIA za NCHI, OK, rafiki yake mkubwa ni mfano mzuri sana. Jakaya wetu kamgwaya Lowasa!
Nilichojifunza, ila nakili kwamba, mwanzoni nilimuona mwanazuoni Mohamed ni mdini na anaipotosha history ya Tanganyika. Lakini kadini, nilivyokuwa nafuatilia, nimejifunza Mohamed ni mwanazuoni hasa.
Mimi si mshabiki wa malumbano ya dini, lakini mzee mohamed amwchambua historia kwa undani sana, amewaelimisha wengi sana...
Mods hii thread kama ingewapendeza, mngeiweka kwenye sticky category. Humu kuna mambo mengi sana ya ki historia ambayo wanazuoni wanaweza kujifunza.
Pia, Mods mngefanya utaratibu wa kumuomba Mzee Mohamed, ili mfanye nae "exclusive interview" kuhusu historia ya tanzania kwa ujumla. wazee kama hawa wamebaki wachache sana...
Ama kweli, Zomba mtu aulizwe swali halafu ajinukuu! wewe unaona ilm hiyo! realMaalim Mohamed Said niruhusu nimwambie Nguruvi3;
Haya, ukisimama tena katafute lingine la kuzuwa hilo umesambaratishwa kwa kulambwa moja ya kichwa, moja ya mbavu.
MM,
Ikiwa wewe unaona Nyerere alikuwa maarufu Dar es Salaam hakuna shida.
Tusivutane na jambo dogo kama hilo.
Tuachie kuwa alikuwa mashuhuri na wote akina Shariff Attas, Tatu biti Mzee,
Abdu Sykes, Sheikh Hassan bin Amir na wengine wote wakimjua na hakukuwa
na haja yoyote ya yeye kutambulishwa kwa wanamji.
Na hii inaeleza ule wepesi wa yeye kuasisi TANU na katika miezi 10 tu akenda
UNO, New York.
Huyu ni mwanamji mtu maarufu.
Wasaa, fedha, umaarufu alikuwanao ndiyo maana alipofika Dar tu kaanzisha chama
cha siasa na kapata wanachama wengi.
Ndiyo maana hapakuwa na sababu ya kumtaja Abdu Sykes na nduguze katika historia
ya TANU ya Kivukoni kwa kuwa mambo yote Nyerere kafanya kwa nguvu zake mwenyewe.
Nyerere alikuwa maarufu.
Hakuwa muhitaji kwa yeyote yule katika wenyeji wa Dar es Salaam.
Ama kweli, Zomba mtu aulizwe swali halafu ajinukuu! wewe unaona ilm hiyo! real
Anyway, nilichotaka kukumbusha ni kuwa ukijibu post zangu usi quote napata notification zako nisizohitaji kujua kama umefanya chochote kuhusu hoja zangu. Please nisaidie kwa hili.
Halafu huu mnakasha hukuwepo umeanzia mwisho basi kila wakati unaandika hata kisicho na tija.
Sheikh Zomba, hivi hujiulizi kwanini watu hawakujibu! just think about that.
Mbona Mohamed alisharambaratika siku nyingi! kwani hujui ''mimi sijibu kila kitu'' au ''hilo sina ujuzi nalo'' pia ''tusiongelee hilo tuliache kwanza'' na sasa ''mimi nakwenda Capetown, nina vitabu cambridge na Yemeni university''.
Muulize hoja ya namba za mitihani imeishia wapi kama si hapa JF! siku hizi kimya wala hataki kuisikia.
Anyway, tutaendelea kusoma historia ya Tandamti, kidongo chekundu, kipata na Narung'ombe.
Ikija ya Tanganyika tutamwambia , Dear Mzee this is anachronism! Hell no! Tanganyika is more than Gerezani.
Basi sheikh Zomba wajulie hali nyumbani na inshallah tutaendelea kukusoma bila kukujibu maana kiwango chako ni cha kuosmwa tu kwa mwenye nafasi ya ziada.
Masalaam sheikh wangu
Jaribio lako la kejeli ni dhaifu na linasikitisha; inahitaji ujifunze kidogo kuandika sarcasm. Hakuna mtu yeyote aliyedai Nyerere alikuwa maarufu katika jiji la Dar; ukinisoma vizuri - kitu ambacho nina mashaka unaweza kukifanya - hoja yangu ilikuwa ndogo tu. Nyerere kutokujulikana Dar hakukuwa tatizo kwake na wazee wako kutomkujua Nyerere haina maana Nyerere alikuwa siyo maarufu. Tayari umeambiwa alipoenda kusoma Uingereza alikuwa ni Mtanganyika wa pili kwenda kusoma Uingereza na wa kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Edinburg! Hiyo ilikuwa katikati ya miaka ya 40.
Waingereza ndio walikuwa wanatawala Tanganyika; katika Tanganyika yote wakati Nyerere anamaliza shahada yake ya pili alikuwa ni Mtanzania wa kwanza kupata shahada ya pili Uingereza. Halafu unawaambia watu kwua hakuwa maarufu! Kweli katika kada ya wasomi Dar-es-Salaam hakuna aliyesikia juu ya Mtanganyika huyo wa kwanza ambaye amesoma Uingereza? Ukisoma kitabu chako wewe mwenyewe unaashiria kuwa Nyerere alipokuja Dar sifa zake zilikuwa tayari zimetangaa.
Umaarufu wa Nyerere haukuja baada ya kuja Dar 1953; ulimtangulia muda mrefu kabla. Wazee wa Uswahilini labda hawakuwahi kusikia lakini watoto wao kina Mwapachu, Dossa na wenzao walishamsikia Nyerere! Na ni wao walitambua wanamhitaji na walitambua wanahitaji kuwatambulisha wazee wao kwake. Na Nyerere akiwa mtu aliyelelewa na wazee na aliyekuwa na marafiki Waislamu tangu utoto - kabla hajawa Mkatoliki - aliwaamini wazee hao, aliwaheshimu na kwa kweli aliwapenda na wao walimpenda. Hadi mwaka 1965 angalau unatusimulia jinsi wazee wako walivyokuwa na mapenzi naye licha ya kuwa tayari kikundi cha waasi kilishang'olewa mwaka 1963. Hadi anakufa mwaka 1999 wazee wa Dar walikuwa na mapenzi naye, walimlilia, na kwa kweli kabisa wanamkumbuka kwa haiba kubwa ukiondoa wale waliokwua na udini tangu 1958 ambao hawakuwa tayari kuona Mkristu anapata nafasi ya umaarufu Dar.
Hawa watoto wao ndio leo wameanzisha mashambulizi yale yale dhidi ya Nyerere kama baba zao walivyofanya miaka ya 1950. Na bila ya shaka katika hawa wewe umekuwa mfalme wao.
Uuzaji wa pombe huko Kilimanjaro ilikuwa ni kazi ya wanawake tu, wanaume hawakujishughulisha nayo.
Mkuu wa kilabu cha pombe alikuwa mwanamke mmoja wa Kimasai, Mama Binti Maalim.
Ingawa mume wa Binti Maalim, Jumbe Mohamed, alikuwa mtumishi wa serikali, na kwa hiyo alijitenga na siasa, hili halikumzuia mke wake, Binti Maalim kuwa mwanachama na mwanaharakati wa TANU.
Binti Maalim alihakikisha kwamba kila mwanamke aliyekuwa akifanya biashara mahali pale alikuwa mwanachama wa TANU na alikuwa akitoa sehemu katika kipato chake kusaidia harakati za kudai uhuru.
Wanachama wa mwanzo kujiunga na TANU walikuwa wale akina mama wauza pombe waliohamasishwa kujiunga na chama na Mama Binti Maalim.
Nafasi ya wanawake katika harakati mjini Moshi inaweza kuonekana katika katika safari yake ya pili ya Nyerere Kilimanjaro.
Katika safari hiyo Nyerere alifikia nyumbani kwa Bibi Halima Selengia aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya tawi la TANU Moshi.
Joseph Kilamalando aliogopa kuitumikia TANU lakini alijiona amesalimika kuifanyia kazi United Tanganyika Party (UTP), chama cha Wazungu kilichoundwa kuipinga TANU.
Kimalando alikuwa katibu wa UTP Moshi, na Mohamed ''Kishikio'' Badi mwenyekiti wake.
Mzee Yusuf Ngozi aliwahamasisha wanawake wa Moshi chini ya Mama bint Maalim kuipiga vita UTP hadi ikafa.
Wanawake wale walikuwa wakizikusanya kadi za UTP na kumpelekea Mzee Yusuf Ngozi ofisi ya TANU.
Yeye kama njia ya kuwakatisha tamaa na kuwapiga vita vya kisaikolojia UTP, alikuwa akichukua marundo kwa marundo ya kadi za UTP na kumpelekea rais wake Mohamed Badi kumhakikishia kuwa wananchi walikuwa hawakitaki chama chake cha vibaraka.
Hayo niliyokuwekea rangi nyekundu ni maandiko yako au si yako?