Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mwanakijiji, as Barney Frank would put it..."trying to have a conversation with some people would be like trying to argue with a dining room table". The goal posts are slowly being moved...na sasa tumefika kwa Binti Maalim muuza pombe wa Moshi. Ngano zaendelea kumwagwa, and the blind and faithful are swallowing it hook, line and sinker...wonders will never cease!
 
Ninachompendea Mohamed anajua kila kilichopita na huo ndio uandishi.
Kufanya uchunguzi na kujua chanzo chake.
Kama mama alikua muuza pombe na alikua anahamasisha wanawake wenzake kujiunga kwenye Tanu kuna matatizo gani?
Tungejuaje kwamba kuna mama wa kimasai muuza pombe alihamasisha wenzake kuiweka Tanu huko Moshi kwenye chart?

Mwanakijiji alikua hayajui hayo yeye anabahatisha tu.
Mambo mengi hayajui
 

D,

Elimu yote ipo katika utafiti.

Ukifanya utafiti unakutana na mambo hata akili yako peke
yake isingeweza kufikiri.

Nilipokuwa mwanafunzi nikimsikia mwalimu wangu anasomesha
''Nationalism in Tanzania'' anasema mambo mengi sana kinyume
ya ufahamu wangu nikihoji.

Akinisaili namweleza kama nilivyopokea kutoka kwa wazee wangu
akawa ''sceptic.''

Haamini.

Siku alipochoka nilipomwambia kuwa TANU kaanzisha Abdu Sykes.
Alipata mshtuko.

Uso wake kwa hakika ulisawajika na nikamuongezea kuwa haya
mambo ya TANU mipango inafanyika baba yangu yupo anaona
ingawa yeye hakuwa mshiriki katika siasa lakini Abdu rafiki yake
wakiongea mengi sana na Abdu ndiye aliyemjulisha Nyerere kwa
baba yangu.

Nikamgusia na Sheikh Hassan bin Amir na uhusiano wake na Nyerere.

Mwalimu kachoka, kahema akasema ''Mohamed tumekusikia na
tuendelee na ''topic'' yetu.''

Lakini nilimuona kuwa kapata mshtuko la ile ''confidence'' na vijembe
vya ''Waswahili wanywa kahawa vibarazani'' vikaanza kupungua.

Sishangai kuwa mtu kama Mag3 kuona mchango wa Mama biti Maalim
ni ngano.

Usichokijua usiku wa kiza.
Anachohitajika yeye kufanya ni kufanya utafiti tu basi.

Ukweli utamdhihirikia.
 
Siku alipochoka nilipomwambia kuwa TANU kaanzisha Abdu Sykes.
Alipata mshtuko.

sasa si ulimdanganya kwanini asishtuke hata mimi ningepaliwa kama nilikuwa nakula; Abdu Sykes hakuanzisha TANU. Ukweli unaujua na kila mtu aliyechukua dakika chache kujifunza historia ya TANU atakuwa anaujua. Historia haibadiliki.

Tukikuuliza Abdu Sykes alianzisha TANU lini utaanza kuruka kimanga kama tetere mmanga...
 

Mwanakijiji,

Nimekusoma.

Nashukuru ujumbe umefika ingawa kwa hakika niliutuma kwa ''sarcasm.''
Niliona hii ndiyo njia nyepesi ya kufikisha ujumbe wangu.

Hapakuwa na uasi dhidi ya Nyerere hicho kitu unakifikiri wewe tu kichwani
mwako.

Lakini kama unapenda kuamini hivyo hakuna wa kukuzuia.
Una haki ya kuamini chochote upendacho.
 

MM,

Hilo la Abdu Sykes kaanzisha TANU lini linishinde mimi?

Mbona hilo nililisema hadharani nje ya darasa la Chuo Kikuu Cha
Dar es Salaam mwaka 1988 katika Africa Events toleo la March/
April.

Toleo lote lilikusanywa likatolewa katika ''circulation.''
Niruke kama ''tetere mmanga...'' kwa lipi?

Hakika historia haibadiliki.

Umeona Kivukoni College and company walijitahidi kuibadilisha.
Je, tujiulize.

Yamepatikana mafanikio yoyote katika jitihada hizo?

Turudi kwa Abdu Sykes na TANU.
Itabidi urudi kwanza kwa baba yake alipoasisi African Association.

Je ungependa tufungue uzi mpya tuanze mnakasha mpya?
 

Nguruvi,

Wala usipate shida sina haja ya kukujibu kwa hiyo jihesabu
ushasalimika na post zangu.
 

Mzee Mwanakijiji,

Unaweza kuwa na hoja nzuri tena zenye mashiko lakini kutokana na kejeli zako dhidi ya hawa wazee wazalendo waliopigania uhuru kuwaita "wazee wa uswahilini" watu wakaidharau michango yako.

Bahati mbaya hawa wazee wa uswahilini hawana jema lolote kwako.

Pitia hotuba ya Nyerere hapo juu yeye mwenyewe kawaelezea hao wazee wa uswahilini walivyokuwa na msaada kwake kuna kipindi alikuwa peke yake waliyobaki wote walikuwa hao wazee wa uswahilini.

Watendee haki hao wa wazee wa uswahili hata kama wamefanya jambo zuri dogo kama punye ya mchele.
 
Last edited by a moderator:

Zomba,

Kweli hivi Yericko mbona kapotea?
Yericko ananichangamsha sana.

Kama kuna mtu ana taarifa zake atujuvye.
Nimepooza sahib wangu hayupo barazani.
 

Tofauti yako wewe na Mohamed Said yeye anasomesha na anakuja na data za tafiti wewe unakuja na maneno matupu.

Mohamed Said kwenu hata afanyaje hamuwezi kukubali chochote kutoka kwake.

Mohamed Said yeye anawaangalia hawa wafuatiliaji huu uzi zaidi ya watu 40,000 ndiyo muhimu kwake.
 

Nani aliyeitisha kikao cha TAA na kukiongoza na hatimaye kufikia uamuzi wa kuua TAA na kuanzisha TANU?
 
Mzee Mwanakijiji,

Unaweza kuwa na hoja nzuri tena zenye mashiko lakini kutokana na kejeli zako dhidi ya hawa wazee wazalendo waliopigania uhuru kuwaita "wazee wa uswahilini" watu wakaidharau michango yako.

Ooh no; wala sikutumia kejeli hapo nilisema kiukweli kwani "uswahilini" kwa maana hiyo wala siyo kejeli hata mzee Said hapa atakubali.

Bahati mbaya hawa wazee wa uswahilini hawana jema lolote kwako.

Inaonekana kabisa huelewi wengine tunazungumzia nini. Hawa wazee wana mema mengi kabisa wala sina tatizo hata moja na wao na tena kama utakuwa umenisoma miye nimekuwa mtu wa kwanza kuitisha Tume ya Historia Iundwe ili ikusanye michango yao na kuhiifadhi; siyo kwa wazee wa Dar tu bali wale wote waliochangia katika harakati za Uhuru.




Ritz huelewi kabisa ndugu yangu. Mimi hawa ni wazee wangu pia. Nawaheshimu na Mungu akinijalia kuandika kitu juu yao nitakiandika na kuwapa nafasi yao sahihi katikahistoria. Sitowabagua kama anavyofanya Mwalimu wenu hapa. Inabidi wewe utambue pia kuwa hawa ni wazee wetu na miongoni mwao ni Nyerere pia. Kwa Said Nyerere siyo mzee wake lakini wazee wake wangemuona Nyerere jamaa yao kabisa na ndugu wa kula, kufa na kuzikana. Unachokisema jaribu kukihamishia kwa Nyerere - hata jema moja humpi Baba wa Taifa?
 

Mimi tena sielewi kinachozungumzwa hapa haa haaa haa...

Ndiyo utetezi wako huu bahati nzuri watu wanakusoma unatumia neno hao "wazee wako wa uswahilini" ili nalo linaitaji kuwa na PhD kutambua kama hizo ni kejeli na dhiaka dhidi ya hao wazee.

Hayo mengine unayaongea tu lakini nafsi yako inakusuta.
 

Nimekusoma mara nyingi siku hizi mbili tatu unazungumza kama unajua hisia na mawazo yangu. Unajua ninachoamini moyoni na sasa unajua ninavyojisikia. Ukisoma vizuri hapo juu utaona tena niemandika kwa heshima zote ili kuwakwepa watu kama wewe wanaosoma haraka haraka. NImesema "Wazee wa Uswahilini"... sijui kama ulinotice nimetumia na herufi kubwa.

Usipende kujihisi victim sana... utakosa elimu bure..
 

Leo umemuelewa, ulimjuwa kabla ya Mohamed Said kumleta humu?
 
Mohamed Said,

Nikiwa napita Magomeni pale mtaa wa Ifunda kuna nyumba moja imepambwa na kuandikwa makumbusho ya Nyerere.

Unaweza kutupa historia yake.
 
Last edited by a moderator:

Maandiko yako ni haya hapa "Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin" tazama tofauti na ulivyoandika sasa, nime bold.

Kwanza uliandika "Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin" halafu sasa unaandika "Mkutano uliokuwepo Camp David enzi za Menachem Begin ni baina ya Begin na Sadat"

Maandiko yako mwenyewe unayaruka? si useme ulikosea tu? usione vibaya, hakuna asiyekosea isipokuwa muumba wetu tu.

Humu tunapata ilm tu kwa njia ya kubadilishana maandiko na picha.
 
Mohamed umesoma hiyo quotation vizuri au umehamaki? Nilikuwa namjibu Zomba

Unajuwa huna la kujibu unatafuta pakutokea ukaona ni kwa Zomba, hata ukijibadili kama kinyonga haisaidii kitu.

Mie uzi uleule tu, mpaka ukweli uwaingie, mkiukubali mkiukataa hiyo ni shauri yenu, kinachotakiwa muujuwe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…