Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

sasa si tulikubaliana tena hakuna kejeli za namna hii? sijawahi kusema unayoandika ni ngano... unless wewe mwenyewe unaamini hivyo. Swali langu kwa kweli ni genuine. Nani alishinda baina ya hawa wawili na ilikuwa ni katika mazingira gani?

Wewe mwenyewe unaziita habari za Mohamed Said ni simulizi za hadithi hadithi. Leo tena unapinda mgongo unataka darsa. Achana na hizo ngano muulize Yericko Nyerere na Mag3, wajuvi wa historia ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
MM, Mimi siwezi nikabishana na wewe kuhusu mwanzo wa African Association 1929 na kuja kufikia kuundwa kwa TANU 1954. Hapa siwezi kubishana na wewe kwa kuwa wewe unajenga hoja kwa jambo moja au mawili au kuzidi kidogo. Mimi huko kuundwa kwa TANU wazee wangu wamekuishi maisha yao kuanzia 1929 hadi 1954 walipounda TANU. Katika maisha yao hayo ya siasa nimeandika kitabu chenye kurasa takriban 400. Vipi katika hali kama hii nijiingize katika mjadala na wewe? Mtu ambae hukuwajua wazee wangu mpaka pale nilopowaeleza katika kitabu changu? Endelea na kejeli lakini historia hii ya wazee wangu ipo na kama unapenda kuamini kuwa Nyerere kaja Dar es Salaam na fikra ya kuunda TANU na akafanikiwa kuiunda peke yake ni sawa kwangu.

Pole mzee mwezangu; tatizo la msingi hapa ni kuwa hubishani na mimi hata kidogo. Ninaijua historia ya Tanganyika kwa kiasi kikubwa sana kuliko historia ya wazee wa Dar. Katika hilo la wazee wa Kiislamu wa Dar sidhani kama kuna mtu anakupita. Lakini kwenye historia ya Tanganyika nzima tunaweza kuzungumza hadi mtondogoo. Lakini hili hapa wala sikuwa nakukejeli au kudharau mchango wa wazee wetu.

Miye naipenda historia sana na nimeisoma vizuri tu na ninaendelea kujifunza. Wewe ulisema ulimwambia mwalimu wako chuuoni kuwa ni Abdul Sykes aliyeanzisha TANU na yeye akapigwa na mshangao. Sasa hilo ni dai (claim). In argumentation sir, once you make a claim you need to give evidence of it to make it valid. You just don't make a claim and leave it hanging there na watu wapokee tu.

Vinginevyo you need to learn qualifying claims - don't give generalized claims which can me misconstrued as attempts at deception. Labda niulize swali ambalo jibu lake siyo simulizi refu na unaruhusiwa kuqualify: Unaamini Abdul Sykes ndiye aliyeanzisha TANU?

Jibu ni 'ndiyo' au 'hapana' au ukipenda unaweza kuqualify statement yako ya awali na itakuwa vyema tu.
 
WC,

Mimi nakusihi kitu kimoja.
Lete maswali uniulize hivi tutakwenda vyema na utafaidika na jamvi.

Usinijie na sura kuwa wewe ni mjuzi wa historia hii.

Sitazungumza TANU na ASP baada ya 1977 sina ujuzi mkubwa wa
vyama hivyo.

Nitazungumza kuhusu African Association (AA) na TAA.
Mwaka 1948 AA ilibadili jina na kuwa Tanganyika African Association.

Katiba haikubadilishwa katika kubadili jina.

Kutokana na haya maswali yako najua kuwa huijui historia ya uhuru
wa Tanganyika.
Unaongopa mzee Mohamed. hakuna KATIBA ulioiona wala kuisoma. Ulijuaje katiba haikubadilishwa? Historia ya TANU na TANGANYIKA nisioifahamu ni hii yenye DINI za watu.
 
sasa si tulikubaliana tena hakuna kejeli za namna hii? sijawahi kusema unayoandika ni ngano... unless wewe mwenyewe unaamini hivyo. Swali langu kwa kweli ni genuine. Nani alishinda baina ya hawa wawili na ilikuwa ni katika mazingira gani?

Ilikuwa uchaguzi wa 1962 Bagamoyo.

Ile usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi Sheikh Mohamed Ramia
alifanya maulidi makubwa uwanjani kwake kama ilivyo kawaida.

Ilipofika usiku wa manane maulid yamepamba moto Sheikh Ramia
akiwa katika mavazi yake rasmi ya ukhalifa wa Tariqa Quadiriyya
akapanda katika membar kuwahutubia murid wake na wana TANU
kuhusu uchaguzi kati ya Dossa na Mtemvu.

Siwezi kurudia maneno aliyosema sheikh...
Ule ulikuwa wakati mwingine.
 
Mohamed Said,samahani kwa kwenda personal,hivyo mbali ya royalities unazopata kwa vitabu vyako viwili/vitatu, what else do you do for a living???
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli anachotoa ni simulizi ambapo ndani yake kuna utamu na ukweli.. na manjonjo..
Ukishaandika au ukisema kitu kwa kuegemea DINI au KABILA utapata wafuasi wa dini yako au kabila yako! Siamini watu kama Ritz, zomba, hawajaona kasoro, dosari, uongo wowote kwenye historia ya Mzee Mohamed. Watakuwa hawazitendei haki nyoyo na nafsi zao!

Sisi tunaomkosoa Mzee Mohamed hatupingi kila kitu alichokiandika. Tunapinga UDINI wake na udini anaowapakazia wazee wake na Mwalimu. Mchango wa kuanzisha TANU na kudai uhuru wa Tanganyika wa wazee wake hawa ulianzia Kipata na kuishia New Street. Mwalimu ndie aliyekwenda bara. Mwalimu ndie aliyekwenda UNO. Wazee wake hawa walitafuta nauli, wengine wakamhifadhi majumbani mwao. Wengine wakampelekea chakula Magomeni. Wengine wakamfanyia tambiko.
 
Last edited by a moderator:
Kama ni malumbano ya hoja na facts za uhakika,basi Mohamed Said kawafisha kifo kibaya sana,
Yan amefafanua kwa kila mwenye akili zake timamu hawezi kuona wapi kwenye uchochezi zaid ya kuelezwa kwa uhalisia ulivyo,
Kawafisha kifo kibaya sana cha hoja na ushahid wazi wazi kama hiki..

View attachment 82154
Tatizo ndiyo lipo hapo. Hata kichaa anajiona ana akili timamu. Hata mtu aliyeshikiwa akili anajiona ana akili timamu. Haya mambo inabidi uzifungue fikra zako na siyo kuyapokea tu na kuyaamini kama maandiko matakatifu.
 
tambo nyiingi!
ungeandika nawe kitabu
cha historia ya uhuru wa tanganyika
Kinachokushinda nini?
hujui historia ya tanganyika
post zako zinathibitisha humu
kazi yako humu ni kuuliza na kupinga basi!
huna chochote ulicholeta kusaidia historia ya tanganyika
kuandika hadithi unaweza lakini si historia ya kweli ya tanganyika

Pole mzee mwezangu; tatizo la msingi hapa ni kuwa hubishani na mimi hata kidogo. Ninaijua historia ya Tanganyika kwa kiasi kikubwa sana kuliko historia ya wazee wa Dar. Katika hilo la wazee wa Kiislamu wa Dar sidhani kama kuna mtu anakupita. Lakini kwenye historia ya Tanganyika nzima tunaweza kuzungumza hadi mtondogoo. Lakini hili hapa wala sikuwa nakukejeli au kudharau mchango wa wazee wetu.

Miye naipenda historia sana na nimeisoma vizuri tu na ninaendelea kujifunza. Wewe ulisema ulimwambia mwalimu wako chuuoni kuwa ni Abdul Sykes aliyeanzisha TANU na yeye akapigwa na mshangao. Sasa hilo ni dai (claim). In argumentation sir, once you make a claim you need to give evidence of it to make it valid. You just don't make a claim and leave it hanging there na watu wapokee tu.

Vinginevyo you need to learn qualifying claims - don't give generalized claims which can me misconstrued as attempts at deception. Labda niulize swali ambalo jibu lake siyo simulizi refu na unaruhusiwa kuqualify: Unaamini Abdul Sykes ndiye aliyeanzisha TANU?

Jibu ni 'ndiyo' au 'hapana' au ukipenda unaweza kuqualify statement yako ya awali na itakuwa vyema tu.
 
Hakika kupitia huu uzi Watanzania wengi wamejifunza mengi sana ambayo hawakuwai kuyasikia popote isipokuwa hapa JF Home of Great Thinkers.

Pamoja na watu kutofautiana misimamo pamoja na mitazamo lakini bado kuna elimu kubwa inapatakina.

Mpaka sasa hivi huu uzi umechangiwa na watu 4,192 na kusomwa na watu 42,445 huu umati ni sawa na umati unaojaza uwanja wa Liverpool, Anfleld capacity 45,276.

Huu munakasha upo kama grafic unapanda unashuka.
 
Ukishaandika au ukisema kitu kwa kuegemea DINI au KABILA utapata wafuasi wa dini yako au kabila yako! Siamini watu kama Ritz, zomba, hawajaona kasoro, dosari, uongo wowote kwenye historia ya Mzee Mohamed. Watakuwa hawazitendei haki nyoyo na nafsi zao!

Sisi tunaomkosoa Mzee Mohamed hatupingi kila kitu alichokiandika. Tunapinga UDINI wake na udini anaowapakazia wazee wake na Mwalimu. Mchango wa kuanzisha TANU na kudai uhuru wa Tanganyika wa wazee wake hawa ulianzia Kipata na kuishia New Street. Mwalimu ndie aliyekwenda bara. Mwalimu ndie aliyekwenda UNO. Wazee wake hawa walitafuta nauli, wengine wakamhifadhi majumbani mwao. Wengine wakampelekea chakula Magomeni. Wengine wakamfanyia tambiko.
WildCard,

Hivi umeshajiuliza kwa nini wewe Mwanakiji, Nguruvi, Mag3, Sweke, na Wakiristo wengine kwa nini mnawaponda wazee wa Kiislam na kumsifia Nyerere kwa kila kitu mnasukumwa na nini kama siyo Ukiristu.

Bahati nzuri tunajuana kwa maandiko yetu labda hayo maneno uwambie mtu mgeni JF.
 
Last edited by a moderator:
Kuna elimu kubwa sana kwenye huu mjadala.

ila kuwa makini kuna "histohisia" na "ngano" uwe mwerevu wa kupembua mambo; mwezako nilishatekwa kupitia hicho kitabu na upembuzi wa radio imaani mnamo tarehe 14/10/12 ila nashukuru Mungu mnakasha umenipa ilmu kubwa
 
Mwanahistoria Shekh Mohamed Said, kaka naomba unijuze kuhusu mgogoro kati ya Al marhum Shekh Kassim bin Jumaa aliyekuwa Imamu wa Msikiti maarufu wa Mtoro Dar na Serikali hususan John Malecela! Jee, Shekh Kassim ana uhusiano wowote na harakati za kupigania uhuru?

Na jee, Almarhum Shekh Mohamed Ali Al Burhi aliyekuwa katibu Mkuu wa Bakwata nini kilisababisha ajiuzulu Ukatibu Mkuu? na Kuna Mtu aliyeitwa Adam Nasibu kiongozi mkubwa Bakwata! huyu Mzee yuko hai au ameshatangulia? na Jee, Al marhum Tewa Saidi Tewa alifariki lini? maana mara ya mwisho kumuona Mpigania uhuru huyu ilikuwa mwaka 1991 ktk ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu dar ktk harakati za kuleta mabadiliko Bakwata!

Jee, Mohamed, ktk vitabu vyako umewakumbuka wapigania uhuru wetu wa huku Moshi kama akina Mzee Yusuf Olotu, Osman Farah, Mariam baiskeli, Mama Halima Selengia (bado yu hai), Liwali Musa Mwinyijanga na wengine? hawa Wazee ni watu muhimu sana hasa kwa huku Moshi walishiriki kikamilifu ktk kuchangishana fedha Misikitini na fedha hizo kupewa Tanu ili ijiimarishe! lakini wote wamesahaulika na hakuna mtu anaewakumbuka hata kwa dua!
 
Kila binadamu kwenye kichwa chake kuna part kwenye ubongo inaitwa Weight Skills unapima mambo kabla hujakubaliana nayo.

Hakuna wa kumshikia akili mwenzake nadhani umenipata.

Spike Lee.
 
WildCard,

Hivi umeshajiuliza kwa nini wewe Mwanakiji, Nguruvi, Mag3, Sweke, na Wakiristo wengine kwa nini mnawaponda wazee wa Kiislam na kumsifia Nyerere kwa kila kitu mnasukumwa na nini kama siyo Ukiristu.

Bahati nzuri tunajuana kwa maandiko yetu labda hayo maneno uwambie mtu mgeni JF.
Hakuna mzee wa Kiislam anayepondwa humu. Infact, baadhi yetu tunajaribu kuwaepusha na UDINI wa Mzee Mohamed anaowapakazia. Wazee wenye UDINI walikuwepo. Wengi wao walijiunga na AMNUT ilipoanzishwa.

Mwalimu hakuwa MDINI. Ndio maana hakupata taabu kujiunga na TAA ya Kariakoo iliyokuwa na Waislam watupu na kuipatia sura ya KITAIFA zaidi.
 
Tatizo ndiyo lipo hapo. Hata kichaa anajiona ana akili timamu. Hata mtu aliyeshikiwa akili anajiona ana akili timamu. Haya mambo inabidi uzifungue fikra zako na siyo kuyapokea tu na kuyaamini kama maandiko matakatifu.

Hata ukiniita kichaa na sina akili timamu ni juu yako,
Lakini nimeamini na hakuna wa kunirudisha tena kwenye upotofu,nawewe amini hicho unachokiamini ndugu yangu..
 
zubeda
Adam Nassib amefariki muda mrefu
Moja ya nyumba zake ipo magomeni mtaa wa ifunda
Mwanahistoria Shekh Mohamed Said, kaka naomba unijuze kuhusu mgogoro kati ya Al marhum Shekh Kassim bin Jumaa aliyekuwa Imamu wa Msikiti maarufu wa Mtoro Dar na Serikali hususan John Malecela! Jee, Shekh Kassim ana uhusiano wowote na harakati za kupigania uhuru?

Na jee, Almarhum Shekh Mohamed Ali Al Burhi aliyekuwa katibu Mkuu wa Bakwata nini kilisababisha ajiuzulu Ukatibu Mkuu? na Kuna Mtu aliyeitwa Adam Nasibu kiongozi mkubwa Bakwata! huyu Mzee yuko hai au ameshatangulia? na Jee, Al marhum Tewa Saidi Tewa alifariki lini? maana mara ya mwisho kumuona Mpigania uhuru huyu ilikuwa mwaka 1991 ktk ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu dar ktk harakati za kuleta mabadiliko Bakwata!

Jee, Mohamed, ktk vitabu vyako umewakumbuka wapigania uhuru wetu wa huku Moshi kama akina Mzee Yusuf Olotu, Osman Farah, Mariam baiskeli, Mama Halima Selengia (bado yu hai), Liwali Musa Mwinyijanga na wengine? hawa Wazee ni watu muhimu sana hasa kwa huku Moshi walishiriki kikamilifu ktk kuchangishana fedha Misikitini na fedha hizo kupewa Tanu ili ijiimarishe! lakini wote wamesahaulika na hakuna mtu anaewakumbuka hata kwa dua!
 
Last edited by a moderator:
Unaongopa mzee Mohamed. hakuna KATIBA ulioiona wala kuisoma. Ulijuaje katiba haikubadilishwa? Historia ya TANU na TANGANYIKA nisioifahamu ni hii yenye DINI za watu.

WC,

Sina sababu ya kusema uongo.

Umeniliza swali nami nimekujibu
kadri ya uelewa wangu.
 
Hakuna mzee wa Kiislam anayepondwa humu. Infact, baadhi yetu tunajaribu kuwaepusha na UDINI wa Mzee Mohamed anaowapakazia. Wazee wenye UDINI walikuwepo. Wengi wao walijiunga na AMNUT ilipoanzishwa.

Mwalimu hakuwa MDINI. Ndio maana hakupata taabu kujiunga na TAA ya Kariakoo iliyokuwa na Waislam watupu na kuipatia sura ya KITAIFA zaidi.
Wewe uwezi kuona sababu wewe na wenzako ndiyo mnaponda, wewe Uislam hujui ndiyo maana unasema mwanamke wa kiislam akiolewa na mkiristu au mwanaume wa kiislam akioa mwanamke wa kiristu wewe unamuta muislam safi ndiyo maana hata kejeli na dhihaka dhidi ya uislam na waislam huwezi kuziona.
 
TANU imeanzishwa na WATANGANYIKA wengi. Wale wazee 17 akiwemo Abdu na Mwalimu walitusaidia kuiasisi bila kutumwa na DINI zao.

WC,

Usemalo wewe leo mimi nimeandika miaka mingi.

Tatizo ni kuwa ili uielewe historia ya TANU hapo New Street
watu wa karibu sana wawezao kukupa taarifa na nyaraka ni
akina Sykes.

Hebu soma hapo kutoka ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...'':

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Among the TANU founding members, it is only those from the headquarters who could give a correct account of the formation of the Party.

These are: John Rupia, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Julius Nyerere, Dome Budohi, Abdulwahid and Ally Sykes.

The two Sykes brothers, Abdulwahid and Ally, have a family connection in the African Association, their father Kleist Sykes having been founder Secretary of the Association in 1929.

The Sykes files make very interesting reading for any researcher in the political history of colonial Tanganyika. These records contain information on Nyerere's early political career and it is surprising that when Party historians were researching, these records, which have so much information about Nyerere, and the party itself, were not consulted.

No member of the family, including Ally and Abbas Sykes, the two surviving members of the three Sykes brothers, were interviewed.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] In the late 1960s, when John Iliffe from Cambridge University, then at the Department of History, University of Dar es Salaam, began his research on Tanzania's history he obtained a lot of information on the African Association from one of his students, Aisha Daisy Sykes, Abdulwahid's daughter.

Although Daisy informed Iliffe that it was her father who provided her with additional primary information articulated in her history seminar papers on Tanzania, it is very strange that Iliffe, interested as he was in the modern history of Tanzania, did not bother to meet Abdulwahid.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Iliffe, however, realising the potential in the Sykes' records encouraged Daisy to write a biography of her grandfather, Kleist Sykes[1] which she did.

When Abdulwahid died in 1968, Daisy, encouraged by the success of her previous work, wanted to work on the biography of her late father.

Daisy was fired by the passion to write after realising that history had been unfair to her father and it was time she put the record straight.

Daisy had in her possession Abdulwahid's files and diaries. Iliffe, for reasons probably unknown to Daisy at that time, discouraged her from writing on the grounds that the timing was inappropriate, and that the subject should be given time.

There was no doubt in Iliffe's mind that Abdulwahid was a reliable source of information on TANU and its history; and any work on his life history would have been a great contribution to the political history of Tanzania. Following Iliffe's negative response Abdulwahid's biography was never to be written by her daughter.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[1] Daisy Sykes Buruku, ‘The Townsman: Kleist Sykes', in Iliffe (ed) Modern Tanzanians, Nairobi, 1973, pp.
95-114.

Back
Top Bottom