sasa si tulikubaliana tena hakuna kejeli za namna hii? sijawahi kusema unayoandika ni ngano... unless wewe mwenyewe unaamini hivyo. Swali langu kwa kweli ni genuine. Nani alishinda baina ya hawa wawili na ilikuwa ni katika mazingira gani?
MM, Mimi siwezi nikabishana na wewe kuhusu mwanzo wa African Association 1929 na kuja kufikia kuundwa kwa TANU 1954. Hapa siwezi kubishana na wewe kwa kuwa wewe unajenga hoja kwa jambo moja au mawili au kuzidi kidogo. Mimi huko kuundwa kwa TANU wazee wangu wamekuishi maisha yao kuanzia 1929 hadi 1954 walipounda TANU. Katika maisha yao hayo ya siasa nimeandika kitabu chenye kurasa takriban 400. Vipi katika hali kama hii nijiingize katika mjadala na wewe? Mtu ambae hukuwajua wazee wangu mpaka pale nilopowaeleza katika kitabu changu? Endelea na kejeli lakini historia hii ya wazee wangu ipo na kama unapenda kuamini kuwa Nyerere kaja Dar es Salaam na fikra ya kuunda TANU na akafanikiwa kuiunda peke yake ni sawa kwangu.
Wewe mwenyewe unaziita habari za Mohamed Said ni simulizi za hadithi hadithi. Leo tena unapinda mgongo unataka darsa. Achana na hizo ngano muulize Yericko Nyerere na Mag3, wajuvi wa historia ya Tanganyika.
Unaongopa mzee Mohamed. hakuna KATIBA ulioiona wala kuisoma. Ulijuaje katiba haikubadilishwa? Historia ya TANU na TANGANYIKA nisioifahamu ni hii yenye DINI za watu.WC,
Mimi nakusihi kitu kimoja.
Lete maswali uniulize hivi tutakwenda vyema na utafaidika na jamvi.
Usinijie na sura kuwa wewe ni mjuzi wa historia hii.
Sitazungumza TANU na ASP baada ya 1977 sina ujuzi mkubwa wa
vyama hivyo.
Nitazungumza kuhusu African Association (AA) na TAA.
Mwaka 1948 AA ilibadili jina na kuwa Tanganyika African Association.
Katiba haikubadilishwa katika kubadili jina.
Kutokana na haya maswali yako najua kuwa huijui historia ya uhuru
wa Tanganyika.
sasa si tulikubaliana tena hakuna kejeli za namna hii? sijawahi kusema unayoandika ni ngano... unless wewe mwenyewe unaamini hivyo. Swali langu kwa kweli ni genuine. Nani alishinda baina ya hawa wawili na ilikuwa ni katika mazingira gani?
Ukishaandika au ukisema kitu kwa kuegemea DINI au KABILA utapata wafuasi wa dini yako au kabila yako! Siamini watu kama Ritz, zomba, hawajaona kasoro, dosari, uongo wowote kwenye historia ya Mzee Mohamed. Watakuwa hawazitendei haki nyoyo na nafsi zao!Ni kweli anachotoa ni simulizi ambapo ndani yake kuna utamu na ukweli.. na manjonjo..
Tatizo ndiyo lipo hapo. Hata kichaa anajiona ana akili timamu. Hata mtu aliyeshikiwa akili anajiona ana akili timamu. Haya mambo inabidi uzifungue fikra zako na siyo kuyapokea tu na kuyaamini kama maandiko matakatifu.Kama ni malumbano ya hoja na facts za uhakika,basi Mohamed Said kawafisha kifo kibaya sana,
Yan amefafanua kwa kila mwenye akili zake timamu hawezi kuona wapi kwenye uchochezi zaid ya kuelezwa kwa uhalisia ulivyo,
Kawafisha kifo kibaya sana cha hoja na ushahid wazi wazi kama hiki..
View attachment 82154
Pole mzee mwezangu; tatizo la msingi hapa ni kuwa hubishani na mimi hata kidogo. Ninaijua historia ya Tanganyika kwa kiasi kikubwa sana kuliko historia ya wazee wa Dar. Katika hilo la wazee wa Kiislamu wa Dar sidhani kama kuna mtu anakupita. Lakini kwenye historia ya Tanganyika nzima tunaweza kuzungumza hadi mtondogoo. Lakini hili hapa wala sikuwa nakukejeli au kudharau mchango wa wazee wetu.
Miye naipenda historia sana na nimeisoma vizuri tu na ninaendelea kujifunza. Wewe ulisema ulimwambia mwalimu wako chuuoni kuwa ni Abdul Sykes aliyeanzisha TANU na yeye akapigwa na mshangao. Sasa hilo ni dai (claim). In argumentation sir, once you make a claim you need to give evidence of it to make it valid. You just don't make a claim and leave it hanging there na watu wapokee tu.
Vinginevyo you need to learn qualifying claims - don't give generalized claims which can me misconstrued as attempts at deception. Labda niulize swali ambalo jibu lake siyo simulizi refu na unaruhusiwa kuqualify: Unaamini Abdul Sykes ndiye aliyeanzisha TANU?
Jibu ni 'ndiyo' au 'hapana' au ukipenda unaweza kuqualify statement yako ya awali na itakuwa vyema tu.
WildCard,Ukishaandika au ukisema kitu kwa kuegemea DINI au KABILA utapata wafuasi wa dini yako au kabila yako! Siamini watu kama Ritz, zomba, hawajaona kasoro, dosari, uongo wowote kwenye historia ya Mzee Mohamed. Watakuwa hawazitendei haki nyoyo na nafsi zao!
Sisi tunaomkosoa Mzee Mohamed hatupingi kila kitu alichokiandika. Tunapinga UDINI wake na udini anaowapakazia wazee wake na Mwalimu. Mchango wa kuanzisha TANU na kudai uhuru wa Tanganyika wa wazee wake hawa ulianzia Kipata na kuishia New Street. Mwalimu ndie aliyekwenda bara. Mwalimu ndie aliyekwenda UNO. Wazee wake hawa walitafuta nauli, wengine wakamhifadhi majumbani mwao. Wengine wakampelekea chakula Magomeni. Wengine wakamfanyia tambiko.
Kuna elimu kubwa sana kwenye huu mjadala.
ila kuwa makini kuna "histohisia" na "ngano" uwe mwerevu wa kupembua mambo; mwezako nilishatekwa kupitia hicho kitabu na upembuzi wa radio imaani mnamo tarehe 14/10/12 ila nashukuru Mungu mnakasha umenipa ilmu kubwa
Hakuna mzee wa Kiislam anayepondwa humu. Infact, baadhi yetu tunajaribu kuwaepusha na UDINI wa Mzee Mohamed anaowapakazia. Wazee wenye UDINI walikuwepo. Wengi wao walijiunga na AMNUT ilipoanzishwa.WildCard,
Hivi umeshajiuliza kwa nini wewe Mwanakiji, Nguruvi, Mag3, Sweke, na Wakiristo wengine kwa nini mnawaponda wazee wa Kiislam na kumsifia Nyerere kwa kila kitu mnasukumwa na nini kama siyo Ukiristu.
Bahati nzuri tunajuana kwa maandiko yetu labda hayo maneno uwambie mtu mgeni JF.
Tatizo ndiyo lipo hapo. Hata kichaa anajiona ana akili timamu. Hata mtu aliyeshikiwa akili anajiona ana akili timamu. Haya mambo inabidi uzifungue fikra zako na siyo kuyapokea tu na kuyaamini kama maandiko matakatifu.
Mwanahistoria Shekh Mohamed Said, kaka naomba unijuze kuhusu mgogoro kati ya Al marhum Shekh Kassim bin Jumaa aliyekuwa Imamu wa Msikiti maarufu wa Mtoro Dar na Serikali hususan John Malecela! Jee, Shekh Kassim ana uhusiano wowote na harakati za kupigania uhuru?
Na jee, Almarhum Shekh Mohamed Ali Al Burhi aliyekuwa katibu Mkuu wa Bakwata nini kilisababisha ajiuzulu Ukatibu Mkuu? na Kuna Mtu aliyeitwa Adam Nasibu kiongozi mkubwa Bakwata! huyu Mzee yuko hai au ameshatangulia? na Jee, Al marhum Tewa Saidi Tewa alifariki lini? maana mara ya mwisho kumuona Mpigania uhuru huyu ilikuwa mwaka 1991 ktk ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu dar ktk harakati za kuleta mabadiliko Bakwata!
Jee, Mohamed, ktk vitabu vyako umewakumbuka wapigania uhuru wetu wa huku Moshi kama akina Mzee Yusuf Olotu, Osman Farah, Mariam baiskeli, Mama Halima Selengia (bado yu hai), Liwali Musa Mwinyijanga na wengine? hawa Wazee ni watu muhimu sana hasa kwa huku Moshi walishiriki kikamilifu ktk kuchangishana fedha Misikitini na fedha hizo kupewa Tanu ili ijiimarishe! lakini wote wamesahaulika na hakuna mtu anaewakumbuka hata kwa dua!
Unaongopa mzee Mohamed. hakuna KATIBA ulioiona wala kuisoma. Ulijuaje katiba haikubadilishwa? Historia ya TANU na TANGANYIKA nisioifahamu ni hii yenye DINI za watu.
Wewe uwezi kuona sababu wewe na wenzako ndiyo mnaponda, wewe Uislam hujui ndiyo maana unasema mwanamke wa kiislam akiolewa na mkiristu au mwanaume wa kiislam akioa mwanamke wa kiristu wewe unamuta muislam safi ndiyo maana hata kejeli na dhihaka dhidi ya uislam na waislam huwezi kuziona.Hakuna mzee wa Kiislam anayepondwa humu. Infact, baadhi yetu tunajaribu kuwaepusha na UDINI wa Mzee Mohamed anaowapakazia. Wazee wenye UDINI walikuwepo. Wengi wao walijiunga na AMNUT ilipoanzishwa.
Mwalimu hakuwa MDINI. Ndio maana hakupata taabu kujiunga na TAA ya Kariakoo iliyokuwa na Waislam watupu na kuipatia sura ya KITAIFA zaidi.
TANU imeanzishwa na WATANGANYIKA wengi. Wale wazee 17 akiwemo Abdu na Mwalimu walitusaidia kuiasisi bila kutumwa na DINI zao.