Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kiswahili fasaha hilo ni tusi.
 
Kiswahili cha wapi hicho mkuu?

Usiingize kiarabu ukafanya kiwe kiswahili mkuu!

Nadhani Kiswahili si lugha mama kwako. Soma post yangu tena imefafanuwa.

Vipi, umetimiza ule msururu wako wa ahadi au ndio tukuweke kwenye kundi la wanafik? maana mafundisho yetu yanasema alama za mnafik ni tatu, moja wapo ni hiyo ya kutotimiza ahadi.
 

Sawa sawa Mkuu,
hao ni wale wale..
 

Hiyo ndio historia uliyoiandika wewe? au ni copy and paste? hata reference basi?
 
Haya yanauhusiano gani na mnakasha uliopo?
 
Hiyo ndio historia uliyoiandika wewe? au ni copy and paste? hata reference basi?

Wapi hujaelewa mpaka uombe vielelezo?

Nimekupeni historia ya Tanganyika isome na uihifadhi ndugu!
 
Muhammad Ally,kakuambia and "back then",,black people didn't talk o boast like that,umemuelewa?
au wewe unaweka substitution zako tuh..!
ukweli unajiongea wenyewe..


Kuna biography ya Ali ''The Greatest My Own Story.''
Ni katika biography mimi nizipendazo kama ''Long Walk
to Freedom'' Nelson Mandela, ''Ghandi'' Robert Payne,
of course ''The Biography of Malcolm X'' Alex Hailey na
Booker T Washington ''Up From Slavery.''
 
Mojamed,hujamuelewa Zumbemkuu. Yeye anasema page 200+ lakini hujaweza kujibu hoja kwa mashiko na pengine matarajio ya wengi. Hajasema serikali haijibu.

Pili, hivi kwanini unasema serikali haina majibu? Huko nyuma tatizo lilikuwa ''muovu, mhalifu Nyerere'' aliyeua EAMWS na kuwakawandamiza waislam. Haikuwa serikali alikuwa Nyerere.

Hata pale tangazo la kuua EAMWS lilipotolewa na Maswanya na Kawawa akiwa waziri mkuu na makamu wa rais bado tuhuma zinamwendea Mwalimu huko alipo mbele ya haki. Sasa hizi double standard zinakujaje? kwamba kuna Nyerere na kuna serikali!

Kwanini sasa hivi isiwe Kikwete, Mkapa au Mwinyi?

Hapa hatupo kujibu kwa niaba ya serikali kama unavyosema. Kikubwa ni kuusadia umma kuona kile kilicho nyuma ya fikra zako. Hakuna chembe ya nia ya historia bali nia ya mashambulizi dhidi ya Nyerere na Wakristo.

Ni kwa mamshambulizi hayo ndipo kinatokea kitu hicho rise of religious tension.
Ni ukweli usio na kificho kuwa tension inayojengeka ni matokeo ya kazi yako kwahiyo hiyo ni faraja kwako na wala si hatari.

Watanzania wameishi kama taifa moja kwa kupendana na kuheshimiana kwa miaka mingi sana. Leo kuna mzozo wa kuchinja ng'ombe. Hilo halikuwepo kwasababu katika mitaa siku za sikukuu watu waimani nyingine kwa kuelewa imani nyingine walifanya the right thing in right way. Kuku alipelekwa kwa mwislam kuchinjwa ili wageni wote wajisikie amani na furaha.

Kupitia kazi yako ''nzuri'' ya kupandikiza chuki ambayo ni kinyume na mafundisho ya Uisla na Uislam sasa chuki imetamalaki. Haionekani kama umejifunza kuwa tatizo likitokea si wewe, mimi au awaye atakayekuwa na amani.
Hutauza DVD kwa watu wanaotafuta ukimbizi kusalimisha roho zao na wala hutakuwa na hadhira ukakaa kinarani.

Tumeyaona Somalia, Rwanda na Nigeria, Bosnia na Crotia n.k na inashangaza, kusikitisha na kutisha kuona kuwa kuna watu hawaoni yote hayo bado wakijinasibu ni wasomi, waadilifu na waumini.
Tena wanayafanya hayo wakiwa wamebeba ''label'' ya kufanya kazi ya mwenyezi mungu. Hakuna woga hata mbele ya Allah!

Labda kuthibitisha chuki za muungwana bin Samtungo, ameulizwa swali na Mwankijiji kama walivyouliza wengine na hajaweza kulijibu. Swali ni kuwa wapi na kwa ushahidi gani wa Nyerere kuwatukana, kashifu Waislam hadharani au kwa siri.
Hakuna mahali popote ambapo Nyerere amekaririwa akiushaumbilia uislam na waislam ( labda kwa ''inasemekana'')

Hii maana yake ni kuwa dhana nzima ni ya kupanda na kuchomeka na haina mahali inaposimama yenyewe.
 

Eti ilikuwa nyerere haikuwa serikali. Hivi wewe unajuwa unachokiandika au mradi ujaze mistari tu?
 
Mkuu Nguruvi3

Jambo linaloshangaza ni kuwa madai mengi ya sijui mfumo kristu, dhulma nk bado hawana ushahidi wakututhibitishia hapa au kokote kule!

Ngano zao kila leo zimejaa maneno ya "inasemekana, tulisikia, inajulikana tu, tunadhani nk"

Wakishasema hayo sasa sentensi hiyo wanaiita ni jibu halisi la wanaemtuhumu!

Leo wanasema tatizo lipo NECTA, lakini mtuhumiwa ni Nyerere huku wanaomba kukutana na serikali,

Kumbuka hapo kati hawatamki neno Mwinyi ama Kikwete, wakijisahau kidogo watamtaja Mkapa kwaajili ya maumivi ya Mwembe chai na Zanzibar basi!

Wananishangaza sana hawa ndugu sijui wanaathiriwa na nini???????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…