Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Jumamosi tarehe 12 Oktoba, mwaka 1968 Mama Maria Nyerere alizimia aliposikia habari za msiba wa Abdulwahid Sykes kwa kukumbuka fadhira zake alizowafanyia walipokuwa wanakaa kwake yeye na mume wake Nyerere.
Halafu kuna jamaa humu anasema alikuwa anafuatilia sana siasa mpaka za Marekani mwaka 1961 lakini hawa wazee tumewasikia leo.
Sasa sijuhi huyo jamaa na Mama Maria tumuamini nani.
Ritz,
Nyerere alikuwa na dada yake anaitwa Sophia.
Bi. Sophia na mumewe walikuwa wakimpenda sana Bwana Abdu.
Abdu akiwafanyia party hadi watoto wao.
Huyu mama ni marehemu sasa.
Yericko atamjua maana ni shangazi lake.
Unajua the ''Tanu spirit ...'' wazee wanasema mpaka uwe umieshi
zama zile ndiyo utaijua.
Mtu anatoa chumba cha mbele nyumbani kwake kuwa ofisi ya TANU.
Hadai kodi.
Chamwenyewe anapanda baiskeli kutoka Dar es Salaam hadi Rufiji
njia nzima anawakatisha watu kadi za TANU.
Akifika Dar es Salaam anamtafuta Idd Faiz kumkabidhi hela za kadi
na yeye wala hachukui hata masurufu kwa ajili ya kujikimu.
Hawa ndugu zetu wanakejeli haya kwa kuwa hawayajui.
Hapana haja ya kuwalaumu sie tuwafahamishe tu wajue kuwa watu hawa walikuwepo
katika historia ya Tanganyika.
Rashidi Ali Meli alikuwa mhasibu wa Dar es Salaam Municipal Council.
Kachukua fedha za ofisi kampa Idd Faiz kutunisha mfuko wa safari ya Nyerere UNO.
Rashid Ali Meli alihudhuria ule mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnautoglo.
Baada ya kutoa zile fedha asubuhi wakaguzi wamemvamia kufanya ukaguzi...
Pazuri hapa....
Inaelekea makachero walinusa wakapeleka taarifa kwa Waingereza kuwa TANU
wamechota katika hazina ya serikali na Rashid Ali Meli ndiyo mbaya wao.
Huyu kachero katika TANU Wazungu watu kama hawa wanawaita ''mole.''
Huyu ''mole'' mzee wangu mmoja kanitajia alikuwa ndani kabisa katika uongozi
wa juu wa TANU.
Mbona nilitaka kuzimia?
Rashid Ali Meli akikaa Ilala.
Wazee walikesha wakimlilia Allah amnusuru Rashid Ali Meli...
Visomo kuanzia Isha hadi Salat Fajr.
Siku nilipompelekea kitabu cha Abdu Sykes (English Version) Mama Daisy (Mke
wa Abdu Sykes)alinambia, ''Nilikuwa nikimwambia baba yako Bwana Abdu taratibu
na mambo haya. Maana alikuwa na kabati lake la fedha. Yeye akiletewa taarifa kuwa
TANU ofisi kuna tatizo hili haulizi zaidi anaingia ndani anatoka na fedha anakabidhi
basi ilikwenda vile hadi ile biashara yake ya Petrol Station pale Ilala Boma ikafilisika.
Nazerali ndiyo akamkopesha fedha na dhamana akaweka ile nyumba yake ya Stanley.
Uhuru umepatikana baba yako anaambiwa si yeye aliyeasisi TANU...''
Kwa muda mama yangu akajiinamia...
''Ahsante mwanangu Mohamed leo watu watamsoma baba yako na watamjua Abdu
kafanya nini. Nilikutana na Maria baada ya miaka mingi sana pale Diamond Jubilee siku
Nyerere anaaga tulikukaanae wanawake wa Dar es Salaam. Maria akasimama akasema,
''Mimi nafika Dar es Salaam kanipokea Mama Daisy na mumewe marehemu Abdu Sykes...''
Mama Daisy anasema, ''Tulikuwa tukienda sokoni namwambia Maria jitande kanga kichwani
maana yeye hawezi kuvaa baibui namwambia huku kwetu wanawake hawatembei kichwa
wazi anacheka ananambia Mwamvua unataka kunifanya niwe Mswahili?''
Haya ndiyo yalikuwa maisha pale Stanley Street kwa Bwana Abdu au Kirk Street kwa Bi.
Mluguru pale kwenye ile nyumba ilipoingia hofu kuwa Nyerere kalishwa ''sumu.''
Yericko kakikumbuka kisa hiki.
Mie sikusema yote kwa maana kwa kweli Abdu na TANU nzima walipata pigo na mtihani
mkubwa kupambana na propaganda za Waingereza.
Hivi Abdu anaweza kumtilia rafiki yake kipenzi sumu...
Au nani, au nani, au Bi Mluguru nk. nk. nk.
Hawa watu wametoka mbali sana.
Sishangai kama anatoka mtu akasema yeye wazee wangu hakupata kuwasikia hata siku
moja wala mambo haya hayajui.
Na ni kweli hajapatapo kuwasikia.
Atawasikiaje?
Na sisi yeye peke yake wengi humu hawayajui haya ndiyo maana wanasema ''hadithi''
na ''ngano'' za Mohamed Said.
Laiti Nyerere angeliwaadhimisha wazee wangu dunia nzima ingewajua na kuwathamini.
Panatosha.