Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kusema ukweli binafsi nasikitika kuona vijana wa Kiislamu ambao wana nia njema kwelii na wanataka kujua sana wanaamini habari za Mohammed Said bila kuzihoji. Wanaamini si kwa sabbau wanajua ni kweli bali kwa sababu mzee anaonekana anautetea Uislamu na hivyo kumuuliza au kumkatalia kunawafanya wajihisi kama hawautendei haki Uislamu. Hii si sahihi kwa sababu ni mbinu ya 'sympathy' ambayo kwa kweli kwenye ukweli haina nafasi.

Maandishi ya mzee Said yanahitaji kuangaliwa kwa mwanga wa kisomi tu; hoja zake hata zingetolewa na mpagani bado zingeangaliwa kisomi. Ni jukumu la mtu yeyote mwenye akili kuuliza maswali mbele ya mtu anayetoa madai. Lengo si kumdhalilisha mtoa hoja bali kumsaidia mtoa hoja kuelezea vizuri hoja zake, kuzisahihisha na hata kuzitetea vizuri. Binafsi naamini Waislamu na hasa wale mashabiki wa Bw. Said waanze kumuuliza maswali ya akili ili kuupata ukweli vizuri.
Tatizo ni kuweka kitu kinachowatisha watu ''tunapigania dini''. Mohamed ameweka tuhuma dhdi ya kanisa makusudi kabisa ili ima mtu awe mwislam au awe kafir. Ili kuwa mwislam unapaswa kumeza kila unachoambiwa. Ukitaka kutoka katika Uislam kama BAKWATA hoji jambo kinyume na lengo tarajiwa.

Kwa jinsi mjadala ulivyo na yanavyozuka tuyajuayo na tusiyoyajua, jinsi watu wanavyo flip flop position na kutengeneza conducieve environment, kuna vijana wengi wa kiislam watasoma makala za Mohamed kwa jicho tofauti kabisa na awali.
Wengine watakuwa chumbani ima wakiugulia maumivu ya kupigwa changa au wakilaani upotoshwaji n.k.

Hii ni changamoto kwa wanahabari hasa wale wachanga. Pitieni uzi huu na nyingine chagueni yale mnaona yana walakini, fanyieni tafiti kidogo kujiridhisha na majibu yaliyo wazi kabisa, waiteni wahusika wayatetee.

Kwa mwandishi makini Mohamed can hardly speak for 20 minute!
Kwanza hana uwezo wa kutetea hoja zake na hoja zake hazisimami zenyewe bila 'self quotation''.
Kitu kizuri sana, hoja zake zina ji contradict na akipelekwa kwenye kona hatoki! flat!
 
Naomba nikuulize swali moja je wewe ni muislamu na kama si muislamu hebu katafute wanachuoni wa kiislamu kuna mtu alikuwa anaitwa ABUU JAHAL(BABA WA WAJINGA) historia yake haitofautiani na mawazo yako mgando
Akili zako za kushikiwa pole sana mjinga sana wewe. Nilisha kuambia mimi ni adent ATHEIST, au hujui ni kitu gani hicho. Baki ukiburuza makalio ukimuabu Mohamed Saidi, maana huna mchangao mwingine zaidi ya huo.
 
E,

Unajua mie huwa sijibu maswali kwa sababu nyingi sana.

Una shaka kuwa simfahamu huyu marehemu?

Namjua vizuri sana pamoja na jina la mumewa na laiti
ningelitaja jina la mume wake hata wewe ungemtambua.

Haya mambo ni ya zamani na yanahusu ihsani walotendeana
watu.

Wazee waliponihadithia haya walinieleza kwa mapenzi kudhihiridha
ule udugu wao.

Inataka ujuzi mkubwa sana unapozihadithia ili isionekane kuwa
sasa unasimanga.

Ndiyo maana hujikinga kama hivyo kwa kuficha majina ambayo si
lazima yatajwe.

Nadhani umeelewa na utaheshimu msimamo wangu.

Sasa kama unataka mtu amuelewe huyo mtu unayetumia kwenye kupasha habari zako ni kwanini usimtaje ili wanaomjua watuthibitishie. Lazima utakuwa una la zaidi ya hili unalolisema angalizo la kutotaja jina. Umeamua kufunguka unemaliza tusiojua tujue
 
Son...

Sijapata kuthubutu kushusha uwezo wa Nyerere hata siku moja.

Ninachosema ni kuwa katika hili la kuasisi TANU...panahitaji
maelezo.

Hili la EAMWS na Sheikh Hassan Bin Amir pana hitaji maelezo.

Mchango wa Waislam katika uhuru wa Tanganyika ipo historia
nyingine ya wazee wangu.

Ni hayo tu ndugu yangu.

Umesoma taazia niliyomwandikia Nyerere ilichapwa na Mtanzania.
Itafute Insha Allah.

mbona umefanya mara nyingi kwenye maandishi yako? simulizi moja umeliweka ambapo umefanya contrast kati ya Abdul - mwenye akili sana na Nyerere mwenye ujuzi wa kuzungumza (ukimaanisha hakuwa na akili sana); umeonesha katika lile simulizi maarufu la Mshume Kiyate (ambalo tunalijua kwa sababu inadaiwa Nyerere kalisimulia) Nyerere kaondoka kwake bila hela mfukoni kwenda sokoni akitegemea kuna mtu angemsave... sijui asingekutana na Kiyate angeenda kumuomba nani hela ya kuwanunulia watoto chakula.. mtu asiye na akili tu anaweza kuamua kwenda sokoni bila hela na kutegemea nasibu.
 
Naona umezidi ngoja nikueleze kisa kimoja kilichonifanya nikufananishe na ABUU JAHAL huyu bwana skumoja walikuwawanapanga njama ya kumuua mtume muhamad (s.a.w) akawa anawaambia makafiri wenzake tuongeeni taratibu mungu wa muhamad asisikie mipango yetu kabla ya hapo makafiri walikuwa wanamuita ABUL HAKAM(BABA WA HEKIMA) mtume kuanzia sku hiyo akamuita ABUU JAHAL na wewe nilikua nakuona unaakili sana sasa hivi nakuona ni IGNORANT
Wapelekee upuuzi wako waumini wenzako! "to me that sounds as buzzing and annoying sound!"
 
kitu kimoja nakusifu-you have got a way with words,you always cunningly wriggle out of tight corners

Son...

Hapana.

Baba yake Abdu Sykes ni katibu muasisi wa African Association 1929.

Family yake siku zote kwa miaka 25 wamekuwa wakishughilika na TAA.

Mwaka 1950 Abdu anachukua nafasi ya baba yake akiwa katibu wa TAA
na anaunda TAA Political Sub Committee.

Mwaka wa 1952 Abdu anakutana na Nyerere na mikakati ya kumchagua
Nyerere kama rais wa TAA inaanza.

Mwaka 1953 Nyerere anachaguliwa kuwa rais wa TAA.
Mwaka 1954 TANU inaasisiwa Nyerere akiwa rais wake.

Kuanzia 1929 -1954 kuna mengi sana mtafiti atakutananayo katika nyaraka
za akina Sykes na katika maelezo ya wazee wangu.

Tutoke hapo sasa tuingie katika kuijenga TANU.

Kuna haja ya mie kujirudia tena?

Ndiyo nikasema itakuwa kauli ya Nyerere na ya Abdu Sykes.

Wala huku si ''wriggling from a tight corner as there is no corner after all let
alone the corner being tight as you have put it.''
 
MM,

Nimekuchoka.
Hata kukunyamazia pia huelewi.

Nimekuchoka.

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Nimeweka hapa paper ya Islam and Terrorism huna la kusema
nami nimeichambua Sheria ya Ugaidi na Kanisa?

Wewe umekuwa kichwa cha gramafoni na santuri yenye shimo?

Nyerere, Nyerere, Nyerere...

maneno mazito sana mzee wangu umenisikitisha
 
mbona umefanya mara nyingi kwenye maandishi yako? simulizi moja umeliweka ambapo umefanya contrast kati ya Abdul - mwenye akili sana na Nyerere mwenye ujuzi wa kuzungumza (ukimaanisha hakuwa na akili sana); umeonesha katika lile simulizi maarufu la Mshume Kiyate (ambalo tunalijua kwa sababu inadaiwa Nyerere kalisimulia) Nyerere kaondoka kwake bila hela mfukoni kwenda sokoni akitegemea kuna mtu angemsave... sijui asingekutana na Kiyate angeenda kumuomba nani hela ya kuwanunulia watoto chakula.. mtu asiye na akili tu anaweza kuamua kwenda sokoni bila hela na kutegemea nasibu.

MM,

Ngoja nikuambie kitu.

Niamini.

Nyerere wakati ule angeingia pale sokoni na angepewa kila kitu
bila ya kutoa senti hata moja.

Tena hata bila ya msaada wa Abdu aliyekuwa pale kama Market
Master.

Ikifanyika...
Unajua siye kwetu ni mwiko kuhadithia ihsani.

Humfanyii mtu wema ukaanza kuhadithia.

Utosheke na maelezo haya nakuomba.
 
maneno mazito sana mzee wangu umenisikitisha

Wewe naweka hapa post nzito za kujadiliwa.

Nimeweka paper ya Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience mada niliyowasilisha
Chuo Kikuu Cha Ibadan.

Chanzo ni Nguruvi kuniwekea Sheria ya Ugaidi.

Nikaeleza kuwa niliwasilisha mada kuhusu Sheria ya Ugaidi na nikawakanyaga Waamerika na
wao wapo pale wananisikiliza.

Taarifa zikaja Dar es Salaam.

Natoka safari nje ya nchi nikakamatwa na kufanyiwa mahojiano usiku kucha Uwanja wa Ndege
nk. nk. nk.

Paper nimebandika jamvini inaeleza ile sheria ya ugaidi imepita kwa kuwa Kanisa walipata silaha ya
kuupiga vita Uislam.

Yote hukuona unaniuliza mambo ambayo kwangu mimi naona hayana maana yoyote.
Maana kuhusu Nyerere nimejibu mengi pamoja na hilo swali lako.
 
Paper nimebadika jamvini inaeleza ile sheria ya ugaidi imepita kwa kuwa Kanisa walipata silaha ya
kuupiga vita Uislam.

Yote hukuona unaniuliza mambo ambayo kwangu mimi naona hayana maana yoyote.
Maana kuhusu Nyerere nimejibu mengi pamoja na hilo swali lako.
Taratibu Mohamed! sijaweka sheria hiyo nadhani una hamaki angalia vizuri uzi na quotation.
 
mbona umefanya mara nyingi kwenye maandishi yako? simulizi moja umeliweka ambapo umefanya contrast kati ya Abdul - mwenye akili sana na Nyerere mwenye ujuzi wa kuzungumza (ukimaanisha hakuwa na akili sana); umeonesha katika lile simulizi maarufu la Mshume Kiyate (ambalo tunalijua kwa sababu inadaiwa Nyerere kalisimulia) Nyerere kaondoka kwake bila hela mfukoni kwenda sokoni akitegemea kuna mtu angemsave... sijui asingekutana na Kiyate angeenda kumuomba nani hela ya kuwanunulia watoto chakula.. mtu asiye na akili tu anaweza kuamua kwenda sokoni bila hela na kutegemea nasibu.

MM,

Ni bahati mbaya umefanya tafsiri hiyo.

Maana yangu iko mbali sana na hilo.
 
maneno mazito sana mzee wangu umenisikitisha

Wewe naweka hapa post nzito za kujadiliwa.

Nimeweka paper ya Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience mada niliyowasilisha
Chuo Kikuu Cha Ibadan.

Chanzo ni Nguruvi kuniwekea Sheria ya Ugaidi.

Nikaeleza kuwa niliwasilisha mada kuhusu Sheria ya Ugaidi na nikawakanyaga Waamerika na
wao wapo pale wananisikiliza.

Taarifa zikaja Dar es Salaam.

Natoka safari nje ya nchi nikakamatwa na kufanyiwa mahojiano usiku kucha Uwanja wa Ndege
nk. nk. nk.

Paper nimebandika jamvini inaeleza ile sheria ya ugaidi imepita kwa kuwa Kanisa walipata silaha ya
kuupiga vita Uislam.

Yote hukuona unaniuliza mambo ambayo kwangu mimi naona hayana maana yoyote.
Maana kuhusu Nyerere nimejibu mengi pamoja na hilo swali lako.
 
Taratibu Mohamed! sijaweka sheria hiyo nadhani una hamaki angalia vizuri uzi na quotation.

N,

Niwie radhi ndugu yangu.

Kuna mtu kaweka Patriot Act 2002 kama attach.

Nami nikamwambia nimezungumza Chuo Kikuu Cha
Ibadan, Nigeria kuhusu hayo.

Mkuu samahani sana.
 
Kama ni hicho na washarika ni hao, sina neno kwakuwa taarifa ninayo,

Nilidhani ni wakujitegemea kama ulivyofanya wewe na ngano/simulizi za wazee wako!

Y,

Unajua Abdu Sykes unaesema maelezo yake ni ''ngano''
alikuwa kipenzi cha baba yako?

Walifanya mengi pamoja katika TANU...

Usiwe mwizi wa fadhila.

Mtaa wa Swahili na Tandamiti kwenye kona ya Soko
la Kariakoo pale kama unatazama Mtaa wa Mkunguni
ndipo ilipokuwa ofisi ya Market Master Abdu Sykes.

Nyerere akienda pale sana baada ya kujiuzulu kazi
ya ualimu.

Ni sehemu ya kihistoria ile na mzee wako ni muhusika
mkuu katika historia hii.

Haikupata kuwa ''ngano.''
 
Mzee mimi nanyamaza mimi nakuheshimu sana huyu jamaa ameniudhi kukutukana wewe hana adabu na nimeachana nae kwasababu wewe umesema niko tayari kupigwa ban lakini awe na adabu

BH,

Nimeshukuru kuwa umenisikiliza.
 
G,

Hapa jamvini mie ndiyo mzee wenu.

Nakuombeni hebu samehaneni tuweke
heshima ya hii barza yetu.

Najua nyote ni vijana na ujana unafananishwa
na wazimu.

Basi yamekwisha tuanzeni upya.
Tusisubiri ban ya MOD tutakuwa tumechelewa.

asante kwa busara wamekuelewa
 
Busara zako zidumu!

G,

Hapa jamvini mie ndiyo mzee wenu.

Nakuombeni hebu samehaneni tuweke
heshima ya hii barza yetu.

Najua nyote ni vijana na ujana unafananishwa
na wazimu.

Basi yamekwisha tuanzeni upya.
Tusisubiri ban ya MOD tutakuwa tumechelewa.
 
MM,

Ni bahati mbaya umefanya tafsiri hiyo.

Maana yangu iko mbali sana na hilo.

sidhani kama mtu yeyote anaweza akasoma ulichoandika na kushindwa kuona maana iliyofichika; mara kadhaa umefanya hivvyo kumdunisha Nyerere mbele ya hadhara na matokeo yake wanafunzi wako hapa wamefuata cue yako...
 
Back
Top Bottom