Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

N,

Sikulaumu hata kidogo kwa kufananisha kitabu changu na vitabu vya
riwaya.

Kwa msimamo huo wako wala sitajishughulisha kukueleza lolote katika
matatizo yanayoikabili nchi yetu kwa hivi sasa.

Ila nitakuwekea hapa habari iliyochapwa katika gazeti la An-nuur la siku
ya Ijumaa iliyopita: "Wanafunzi Waislam sasa waikataa NECTA."

Wanafunzi hawa wamefanya mkutano na wameazimia kuandamana hadi
ofisi za NECTA.

Ikiwa hili litafanyika na polisi kama kawaida yao watapambana na hawa
watoto.

Mungu apishie mbali...
Naogopa hata kufikiria nini kitatokea.

Kauliwa mtoto wa Kiislam kwa kuikumbusha serikali kuondoa dhulma dhidi
ya wanafunzi Waislam...

Hapa ndipo tulipofika hivi sasa.
Haisaidii sana kuwapuuza Waislam na shutuma zetu dhidi ya mfumokristo.
 
Brother MS.......maandishi uliyotoa hapo juu hayajibu maswali uliyoulizwa.......rudia kusoma swali la MMKJJ....



....na huo ndio MTEGO wa Brother MS...... uliowanasa vijana wengi....

Njia ya kupinga kitabu changu ni nyie kuandika kitabu.
Hivi hivi itakuwa tabu sana kunishinda.
 
Ndio maana sisi wengine tunamwambia mchochezi Mohamed Said aache kujaza kurasa za JF na ngano na kujinukuu mwenyewe, ajibu maswali anayoulizwa lakini akiamua kuwa muongo ajue kutunza kumbukumbu.

Mag3,

Kujinukuu mwenyewe nitaachaje ilhali mie ndiye niliyetafiti na kuandika?
Utaridhika nikitumia nukuu za nani?

Ikiwa kuna uongo kwangu mimi nyie kinakuzuieni kitu gani kuandika kitabu
kitakachosema kweli?
 

Tukisema lengo lako ni kumdunisha Nyerere mbele ya Waislamu utakataa; simulizi hili ni ushahidi mwingine pia. Inakumbusha kile kisa kingine ulichosimulia miaka ya sitini ambapo Nyerere alikuwa confronted na mmoja wa wazee wako na Nyerere akagwaya; hakujibu kitu.
 
Njia ya kupinga kitabu changu ni nyie kuandika kitabu.
Hivi hivi itakuwa tabu sana kunishinda.

Hili ni chaguo moja lakini siyo chaguo la pekee. Njia nyingine ya kukupinga ni kukupinga kila unapoeneza propaganda zako hizi. Haiitaji kitabu kufanya hivyo.
 

N,

Ndugu yangu amini usiamini.
Yote niliyoandika katika kitabu changu
ni kweli.

Narudia kukueleza tena.

Ilikuwa baada ya Prof. Haroub Othman
kusoma kitabu changu ndipo akaenda kwa
Nyerere.

Matokeo ndiyo haya ya kitabu cha Nyerere
kinachoandikwa hivi sasa.

Kuamini au kutoamini hilo ni chagua lako.
 
Hili ni chaguo moja lakini siyo chaguo la pekee. Njia nyingine ya kukupinga ni kukupinga kila unapoeneza propaganda zako hizi. Haiitaji kitabu kufanya hivyo.

MM,

Unakipinga kitabu kipo kinasomwa mwaka wa 15?
Utawapingaje na hao wanaokisoma?

Kitabu kinakwenda toleo la tatu.
Unasemaje kuhusu hili?
 

MM,

Iikiwa wewe umeona hivyo hiyo ni bahati mbaya sana.
Ila kisa cha Sheikh Mwilima na Nyerere hakijesha.

Ungependa nikieleze hadi mwisho?
 
Mohamed hebu watendee haki watu wanaotufuatilia hapa,

Hivi Mwalimu aahirishe kikao baada ya swali hilo la Abubakar Mwilima?

Je ni kweli Mwalimu hakujibu kitu akabaki kumtazama tu Mwilima kama usemavyo majogoo watazamanavyo?

Y,

Pale haikuwa mwisho.
Nyerere akaahirisha kikao wakenda mapumziko kwa chai.

Sheikh Mwilima anasema katika mapumziko yale wajumbe
wenzake walikuwa wanamkimbia.

Hakuna aliyetaka kumkaribia hata mmoja.

Ikifahamika sana kuwa Uislam lilikuwa suala nyeti na likiepukwa
kuzungumzwa.

Sheikh Mwilima alikuwa amevunja mwiko.

Waliporudi ukumbini kikao kikaendelea bila ya kujadili hoja ya
Sheikh Mwilima.
 

Hizi kweli ngano ni vizuri liwe bandiko lako la mwisho watu wanajadili mambo mazito wewe unaongelea habari za Madj's kina Chogo, Saydou.

Wewe huijui Dar eti unasema miaka ya 80 watu walikuwa hawapendi shule ni kichekesho nakutajia shule za Ilala tu Bunge, Gerezani, Amana, Boma, Ilala, Lumumba, Mnazi Mmoja, Msimbazi, Mtendeni, Muhimbili, Uhuru, Upanga, Zanaki, Olympio, Agha Khan, Tambaza, Kisutu, hizi shule walikuwa wanasoma kina nani hapa sijataja Kinondoni, Temeke.

Halafu darasa la saba kulikuwa hakuna kupasi wanachaguliwa tu bila hata ya kuona matokeo hapa ndiyo mfumo kristu unafanya kazi, umeishajiuliza wale ambao hawajachaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza walikuwa wanaenda wapi au ndiyo hawa hawataki shule.

Unalalamika kuhusu mabaharia wakati Dar kuna bahari hii ingekuwa Moshi, Iringa wangekuwepo mabaharia tu.

Kama Nyerere hakuandika jina lake uwanja wa ndege na chuo kikuu basi hana matatizo mengine.
 
MM,

Unakipinga kitabu kipo kinasomwa mwaka wa 15?
Utawapingaje na hao wanaokisoma?

Kitabu kinakwenda toleo la tatu.
Unasemaje kuhusu hili?

Ni kwa sababu kwa miaka 15 uliweza kuwashawishi kikundi cha Waislamu kuwa unachosema ni kweli, kundi kubwa la wasomi wengi walikuwa hawajakaa chini kusikiliza au kusoma hoja zako. Bahati nzuri mtandao wa net huu umewezesha hoja zako kuwafikia watu wengi zaidi na watu kuzipima kwa ukaribu zaidi kuliko miaka 15 iliyopita. Kusema ukweli naamini muda si mrefu hoja zako zitajibiwa na kwa uzuri zaidi na hatimaye utalazimishwa kujibu hoja ambazo tumezitoa hapa. Hutoweza kuendelea kutoa madai yale yale ambayo hujaweza kuyathibitisha.

Kwa wakati huu furahia miaka kumi na tano ya unchallenged fame.
 
MM,

Wapo wajumbe walio hai kisa hiki ni maarufu
watakikumbuka Insha Allah.

yeah lakini huwaulizi hadi wakifa ndio unatuambia walichokuambia. Si kina Maria Nyerere wapo? Kawawa alikuwepo hadi miaka michache nyuma; Ben Mkapa yupo, na wengine wapo tu lakini unawatuhumu kila kukicha bila kuthubutu kuwahoji.
 
Unasema wazi kuwa uislamu ulikuwa ni mwiko kuuzungumzia, je ukristu ilikuwa ruksa kuuzungumzia?
 
Asante sana mkuu kwa maelezo murua, bado mchango wako nimuhimu sana katika uzi huu mkuu, rudi ndugu uzidi kuwafunza waamini wa Mohamed Said
 
MM,

Iikiwa wewe umeona hivyo hiyo ni bahati mbaya sana.
Ila kisa cha Sheikh Mwilima na Nyerere hakijesha.

Ungependa nikieleze hadi mwisho?

Ilikuwa ni kwenye kikao gani na cha lini? baadhi ya wajumbe wengine waliokuwepo kwenye kikao hicho ni kina nani?
 
By Mohamed Said


MM,

Iikiwa wewe umeona hivyo hiyo ni bahati mbaya sana.
Ila kisa cha Sheikh Mwilima na Nyerere hakijesha.

Ungependa nikieleze hadi mwisho?

Ilikuwa ni kwenye kikao gani na cha lini? baadhi ya wajumbe wengine waliokuwepo kwenye kikao hicho ni kina nani?

Hiyo ndio maana yake ungependa au sio?
 
yeah lakini huwaulizi hadi wakifa ndio unatuambia walichokuambia. Si kina Maria Nyerere wapo? Kawawa alikuwepo hadi miaka michache nyuma; Ben Mkapa yupo, na wengine wapo tu lakini unawatuhumu kila kukicha bila kuthubutu kuwahoji.

Kuwahoji namna gani sasa,kila kitu kipo wazi na wao wenyewe wanakijua na wanakiskia mbona hawakanushi?
yani mtu anaonekana kabisa kavaa shati la kijan kisha umuhoji 'eti hii shati yako ni ya kijani?'
sasa hiyo itakuwa akili ama matope??
maswali yako yanakosa mantiki wakati mwingine..
 
Hili ni chaguo moja lakini siyo chaguo la pekee. Njia nyingine ya kukupinga ni kukupinga kila unapoeneza propaganda zako hizi. Haiitaji kitabu kufanya hivyo.

Unapinga tu kwa sababu upinge lakini ukweli unapingika? hayo ni maradhi yalio ndani ya moyo wako.
 
Unasema wazi kuwa uislamu ulikuwa ni mwiko kuuzungumzia, je ukristu ilikuwa ruksa kuuzungumzia?

hivi mzee mohamed unaweza kutukumbusha vita vya Kagera kwanini tulipigana kwasababu nimesoma gazeti la raia mwema sio annur kwamba Nyerere alikuwa na chuki na IDD AMIN na alikuwa anataka swahiba yake MILTON OBOTE na pia Nyerere alikataa chuo kikuu cha kiislamu kujengwa hapa Tanzania na OIC ndio kikajengwa Uganda hii ni moja wapo hoja za waislamu kwamba kuna mfumo kristo na the founder ni NYERERE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…