Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Duh! yaani wazee wote walikuwa Waislamu! sasa wenzao walikuwa wapi jamani? au walikuwa hawataki uhuru?
 

Heheehee haya bwana!
 

Z,

Maskahara ni kitu kizuri kinaburudisha.

Yericko haluwa wala kahawa haipiti nimemshushia vitu vya 1950
mzee wake hajaingia Dar es Salaam.

Yeye anasema mzee wake alikuwa na chama hata jina lake silijui.

Tuendelee na kisa cha Sheikh Mwilima na Nyerere...

Sasa waliporudi ukumbini ile aganda Nyerere hakuileta kikaoni.
Mkutano ukaendelea hadi mwisho.

Lakini kuanzia pale Sheikh Mwilima akawa sasa anatafutwa ili
atolewe katika Halmashauri Kuu.

Lile neno aliloleta pale katika kikao lilikuwa jambo nyeti.
Nyerere akiogopa vitu viwili kuhusishwa navyo.

Kitu cha kwanza kuwa historia ya kudai uhuru ni historia ya
Waislam na pili akiogopa kuhusishwa akina Sykes.

Sheikh Mwilima alikuwa kamletea moja ya vitu vinavyomtisha.
Suala la Waislam.

Sasa ukileta katika kikao swala la dhulma dhidi ya Uislam lazima
itabidi mrudi nyuma kwenye kudai uhuru...

Haikupita muda Sheikh Mwilima akatuhumiwa kuwa anafanya biashara
ya kuuza fedha za kigeni kwa njia za haramu na akaitwa Halmashauri
Kuu ajieleze.

Akamkuta Nyerere kwenye kiti anamsubiri.
Huo ndiyo ukawa mwisho wa Sheikh Mwilima katika siasa.
 
Duh! yaani wazee wote walikuwa Waislamu! sasa wenzao walikuwa wapi jamani? au walikuwa hawataki uhuru?

Z,

Nitakuwekea hapa Government Circular No. 5 na No. 6 hizi ndizo
zilikuwa zinawatisha Wakristo kuingia katika siasa.

Hizi circular zilikuwa zinapiga marufuku watumishi wa serikali kujihusisha
na siasa.

Ukikamatwa adhabu ni kufukuzwa kazi.

Abdu ilikuwa kidogo afukuzwe kazi.

Iko siku pale ofisini kwake Kariakoo afisa wa Kiingereza kamwingilia ofisini
anamwambia kuwa ana taarifa Abdu anauza kadi za TANU pale sokoni.

Uzuri wa Abdu Sykes ni kuwa kwanza alikuwa na hela hivyo ule woga kuwa
akifukuzwa kazi atapata tabu haukuweko.

Abdu alikuwa na ulimi mzuri sana wa Kiingereza.

Watu wanasema siku ile tuliona senema ya bure pale sokoni Abdu na Mzungu
walivyokuwa wanapeana maneno.

Kimombo kilivyokuwa kikimtoka Abdu ilikuwa burudani ya aina yake.
Mzungu aliondoka akamwacha Abdu ofisini kwake.

Nina hazina wazee wameniachia kuhusu uhuru wa nchi yetu.
 
Nikukosoe kidogo ndugu yangu, miaka hiyo hakukuwa na siasa Tanganyika bali harakati!

Siasa zilianza rasmi baada ya mwanzoni mwa 1953 hadi 1961

Baada ya filosofia ya TAA kubadilika hasa kwa ujio wa Nyerere aliyekuja na filosofia yake kutoka TAWA

Yericko Nyerere,

Unapishana na historia ya Tanganyika nilichogundua wasomi wengi wa Tanzania hawana ufahamu wowote wa siasa za Tanganyika. Wanafahamu kuanzia mwaka 1961 baada ya Nyerere kuwa rais kupitia historia ya Kivukoni.

Hujui kama wakati wa TAA kulikuwa na mpambano mkubwa wa kisiasa kati ya wanasiasa vijana na wanasiasa wazee katika kushika madaraka na hatimaye wanasiasa vijana wakachukuwa madaraka.

Ngoja nikutajie wa hawa wachache Abdulwahid, Stephen Mhando, Dossa Aziz, James Mkande, Tewa Said Tewa, Ally Sykes, pamoja na wale madaktari watano.

Unataka kutuambia hawa wote walikuwa wanaharakati.
 
Last edited by a moderator:

Ritz,

Msamehe Yericko,

Ana maradhi ya ''uoga wa historia.''
Mtie kundi moja na wanahistoria wa Kivukoni.

We uandike historia ya TANU umuache Abdu Sykes...

Umeona vitu nimekuwekea hapa kutoka ''Under the
Shadow of British Colonialism...''

Inawezekanaje tuache historia yote ile?
 
hivi na kakwambia somali wako nyuma kwa eleimu? kwa ufupi wasomali wamesoma zaidi kuliko watanganyika wapo dunia nzima na ni watafiti , wa madaktari wazuri..japo nchi yao imedhulumiwa na mataifa ya kikiristo kuweka vibaraka na kiuishambulia kuivuruga lakini ....hatuwezi kuwafika ..wasomali.....hebu nambie haswa kuna msomi gani ....unemuona huku Tanzania ukamlinganisha na wasomali ambao wamesoma zamani na kustaarabika kabla watanganyika hwajajua kuvaa nguo....nao hawa wasomali hawajawahi kuwa watumwa na sababu kubwa ni kwa sababu wao wamesoma ..watumwa walifanywa zaidi wale walikua wajinga hawakusoma...chukua mfano wa historia hii hapa ya baadhi ya wasomi na personality za kisomali kabla hamjamtoa ngombe bandani alale nje
Important Islamic figures

kwa ufupi Tanzania hakuna nchi katika nchi za kiislam au zenye chembe ya waislam....mnayo ipita kwa elemu...labda zanzibar nao kwa sababu ya ujinga wao kuungana
 

Mbona kawataja kwingi tu.

Joseph Mutahangarwa, James Mkande, Stephen Mhando, Vedasto Kyaruzi, John Rupia, Oscar Kambona, Wilbard Mwanjisi. Denis Phombeah, Alexander Tobias, Michael Lugazia.

Hawa wote bila Mohamed Said tusingewafahamu.
 

Ndugu yangu kuna kitu kikubwa sana lazima ukielewe katika siasa,Harakati nk, kitu hicho huitwa SHABAHA/Filosofia/ideology

Huo ndio muongozo wa chama ama kikundi chochote kile,

AA ilikuwa na SHABAHA yake, na TAA ilikuwa na yake mpaka ilipobadilika kuanzi 1953 baada ya Mwalimu kushika urais wa TAA,

Hao vijana ni sawa waligombea uongozi wa chama lakini chama kilichokuwa na filosofia yenye kujikita kudai HAKI na sio UHURU
 
Last edited by a moderator:

Ok lets talk about the facts if you will...

a. Kuna wakati wowote ambapo Wakristu hawakushiriki katika harakati za Uhuru au katika vyama mbalimbali vya kupigania haki za Wakristu?

b. Kuna wakati ambapo Wakristu hawakuwa viongozi wa juu katika vyama hivyo mbalimbali na hivyo kuwa aktika "centre stage" ya shughuli za vyama hivyo?

It is absolutely absurd and silly to suggest - even remotely - that the names such of those of John Rupia, Dr. Mwanjisi, Dr. Kyaruzi, Stephen Mhando, Clement, na wengine wengi only appear in 'dramatis personae' sijui hata kama ulimaanisha hivyo maana "dramatis personae' ni characters wa mchezo - na haihusishi watu ambao hawakuwa na centre role. Hivyo kina Dossa Aziz, Abdulwahid, Nyerere, Titi Mohammed wote wako kwenye orodha ya characters tu na katika hao walioshika nafasi kuu of course ni Nyerere (star of the show) akiwa na supporting cast kama kina Abdul, Rupia na wengine.

Mchango wa Wakristu katika harakati za uhuru na nafasi zao haiwezekani kupuuzwa, kubezwa au kudunishwa. Kama walivyofanya ndugu zao ndivyo hivyo Wakristu nao walishiriki bega kwa bega na kulipia gharama ile ile ambayo wengine walilipia katika kupigania uhuru. HIstoria inatufundisha jinsi wazee wetu walivyoshirikiana kumpinga ukoloni licha ya tofauti zao za mahali, dini, kabila, na hata hali (status).

Those my dear one are the indisputable facts. You DO NOT have any facts to the contrary. No you don't.
 
Mohamed Said kumbe prophets of doom mko wengi
"
"Church affiliated writers also advance the idea that Nyerere's efforts to cultivate mutual relationships with and between Christians and Muslims religious leaders ensured religious tolerance in Tanzania since independence. However, authors like Fairoz, al-Zinjibari and Said Mohammed, see Nyerere as a serious bulwark against the flourishing of Islam in Tanzania. Foremost they take issue with close association between Islam and slavery in the persona of the Arab in the country's political rhetoric and condemn the elevation of the role of the missionary and its institutions in Tanganyika's liberation
 
Last edited by a moderator:
Mbona kawataja kwingi tu.

Joseph Mutahangarwa, James Mkande, Stephen Mhando, Vedasto Kyaruzi, John Rupia, Oscar Kambona, Wilbard Mwanjisi.

Hawa wote bila Mohamed Said tusingewafahamu.

Are you really serious? Kweli M Said kawaweza; kawaaminisha kuwa watu hawa wote yeye ndio kawataja kwa mara ya kwanza katika historia. Na la kusikitisha zaidi ni kuwa mpo mnaoamini kabisa kuwa Mohammed Said ndiye mtu wa kwanza kuwataja watu hawa na nafasi yao katika historia. That is really sad. Ukiondoa majina machache ambayo labda yanahusiana na watu wa Gerezani na Kariakoo majina ya washirika wa harakati za Uhuru kutoka sehemu mbalimbali nchini yanajulikana kwa muda mrefu yameandikwa kwa kiasi kikubwa tu.

Alichofanya Mohammed Said katika kujaribu kuiandika upya historia hiyo ni kuwagawa wazee wetu kwa misingi ya dini (Waislamu Vs. Wakristu). Anafanya kile ambacho baadhi ya wazee wake wa Kariakoo walijaribu kukifanya mwaka 1958 walipojaribu kuzigawanya harakati hizo za uhuru kwa misingi hiyo ya dini na matokeo yake wakatimuliwa miaka michache baadaye.

Kama unaamini kuwa Mohammed Said ndiye anawataja hawa - tena kwa dharau kuwa hawakuwa na central role kwenye harakati hizo ila wanatajwa tu kama waigizaji kwenye mchezo wa kuigiza - it is in itself tragic.
 

Notable individuals of the somali....Tanzania yupo Nyerere tu...na yeye ndio mfumo...akikosolewa basi wenye mfumo wote....wanakuja juu...lakini tunamshukuru mzee wetu Ali Hassan Mwinyi...aliupindua kwa kiasi mfumo.......

Abdi YusufHassan – Somali politician, diplomat and journalist. Former Director of IRIN and UNHCR Head ofExternal and Media Relations in Southwestand Central Asia



 
Na kwa taarifa yako Mohamed Said,kwenda kwa Nyerere twice UNO,bulk kubwa ya nauli ilitolewa na Maryknoll sisters
 
Last edited by a moderator:

MM,

Ndugu yangu mimi huniwezi katika historia hii.
Mimi hawa watu wazee wangu nimewaona na nimewasikia wakizungumza.

Mimi hawa ni watu wangu.
Vipi wewe uwajue hawa na historia yao unishinde mie?

We si unaona nilivyokubadilishia dawa?
Sasa nakupa vidonge vipya.

Unasikia mzee anavyosema katika ''Under the Shadow of British Colonialism...''

We hayo utayapata Kivukoni College?
Kutokujua mambo si ujinga.

Shughulilka na wengine.
 

Kibaya zaidi hasemi ukweli wakilicho wasibu hapo wazee wake mpaka wakafukuzwa na wengune kufungwa jela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…