Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hili swala la udini litawatafuna sana watanzania siku zote na sema the founder is Nyerere yeye kashatangulia huko hii mbegu yake aliyoipanda ndio imeota

Mwalimu Nyerere sio muasisi wa Udini balii ndie muasisi wa VITA dhidi ya Udini Tanganyika/Tanzania,
 
Unasikitishwa na wewe ndio ulioleta huu uzi? maji ukishayavulia nguo uyakoge, Au hujuwi hilo?

Mohamed Said kitabu chake kimetoka Juliasi Nyerere yu hai.

Inawezekana hauelewi maana ya uzi huu mkuu,

Nimeuleta hapa ikiwa ni sehemu ya kumuonya Mohame Said kwa Uchochezi wake!

Na mpaka dakika hii ninaamini nimeokoa watu wengi sana waliokuwa wafuasi wa NGANO za Mchochezi huyu!
 
Mwalimu Nyerere sio muasisi wa Udini balii ndie muasisi wa VITA dhidi ya Udini Tanganyika/Tanzania,

Ungekuwa mtoto wa Julius Kambarage ningekuambia pitia kumbukumbu zake nyumbani uje utuambia kabla ya Nyerere lini Watanzania walipigana vita vya kidini.
 
Wewe ulivyokuja na huu uzi wako kuwa Mohamed Said mchochezi ulidhani watu watakaa kimya.

Si lengo langu watu wakae kimya, bali waujue ukweli nao uwaweke huru dhidi ya minyororo ya Mchochezi Mohamed Said!
 
Mwalimu Nyerere sio muasisi wa Udini balii ndie muasisi wa VITA dhidi ya Udini Tanganyika/Tanzania,
Na katika vita hii Mwalimu alijitengenezea maadui wengi mno ambao wamekuwa wakirithishana visasi hivi hadi leo. Hakujawahi kuundwa Cabinet ya nchi hii ambayo ni "all inclusive" kama ile ya kwanza ya Tanganyika huru na nyingine nyingi zilizofuata baada ya hapo. Bado Mwalimu anaambiwa alikuwa mbaguzi! Kweli akutukanae hakuchagulii tusi.
 
Ungekuwa mtoto wa Julius Kambarage ningekuambia pitia kumbukumbu zake nyumbani uje utuambia kabla ya Nyerere lini Watanzania walipigana vita vya kidini.

Ndugu yangu nilikwambia Historia ya Tanganyika huijui na hutaki kujua kabisaaa!

Hivi unajua DINI hizi mnazozililia wewe na Mohamed Said zimekuja lini?

Unajua ukristu wa RC umekuja lini nchini?

Na uislamu umekuja lini?

Na zaidi Mwalimu Nyerere ameingia lini katika mafundisho ya dini ya Kigeni?
 
Si lengo langu watu wakae kimya, bali waujue ukweli nao uwaweke huru dhidi ya minyororo ya Mchochezi Mohamed Said!

Endelea kujifariji tu kwanza wasomaji hawana chochote wanachopata kutoka kwako labda kejeli na dhihaka.

Wewe ni mtupu za sana kwenye anga za historia.

Umeahidi vitu vingi humu jamvini hakuna hata kimoja ulicholeta watu wameamua kukupuza tu.
 
Kama historia ya Kivukoni kweli siwezi kuijua lakini historia ya Tanganyika unipati kabisa.

Umeshindwa kujua Oscar Kambona alikuwa na cheo gani ndani ya TANU. unasema alikuwa mwanachama wa kawaida tu.

Yericko wewe mchache sana kwenye historia ya Tanganyika.
 
Ungekuwa mtoto wa Julius Kambarage ningekuambia pitia kumbukumbu zake nyumbani uje utuambia kabla ya Nyerere lini Watanzania walipigana vita vya kidini.
Amekuwa madarakani kwa miaka 24 bila vita kama ile ya jana kule Geita kuwepo. Usimamizi wa KATIBA na SHERIA ndio haupo kwa sasa. Mambo haya hayataki nalenale( kama ulipita JKT unalijua neno hili) au kubembelezana.

Tutatwangana kidini bado tutajikuta sio wamoja kwani hata nchi za DINI moja kama Uarabuni na Somalia wanauana. Tutaanza kutwangana KIKABILA, KIUKOO,....
 
Endelea kujifariji tu kwanza wasomaji hawana chochote wanachopata kutoka kwako labda kejeli na dhihaka.

Wewe ni mtupu za sana kwenye anga za historia.

Umeahidi vitu vingi humu jamvini hakuna hata kimoja ulicholeta watu wameamua kukupuza tu.

Mbona unawalisha maneno wasomaji? Wamekwambia kuwa hawajanufaika na chochote kutoka kwangu?

Yaleyale ya Mwalimu wenu Mohamed Said yakulisha watu maneno!

Sema ukweli kuwa wewe ndie hujanufaika na chochote kutoka kwangu, na niukweli huwezi kupendezwa na nilichoandika hapo kwakuwa ninawaharibia mipangu yenu ya uchochezi!
 
Vita vya Kagera vilikuwa siyo vita? Nipe kisa chake tuanze kufungua vitabu upya.
 
"When someone makes a claim, the claim is proven false, and the person makes it again anyway, they’re lying."

Kwi kwi kwi teh teh teh.
 
Ni vema wala sikupingi lakini zingatia unachoulizwa na ukijibu!

Nimeshakwambia Mwalimu Nyerere ameliongoza taifa hili kwa mafanikio makubwa kabisa ya Amani ndani ya miaka 24, pengine hilo ni kwa mfano wa dunia nzima,

Hatukusikia chokochoko za kina Simba Ulanga wala Shehe Farid na wengine

Baada ya yeye kutoka madarakani na hasa baada ya kufariki ndipo tunayashuhudia ya akina Mohamed Said, Illunga, Ponda na wengine wakichochea maasi ya kiroho kwa kasi!
 
Wewe wamekuambia wapi wamenufaika na mchango wako au ndiyo unasema unaamini wanaamini.
 
Inawezekana hauelewi maana ya uzi huu mkuu,

Nimeuleta hapa ikiwa ni sehemu ya kumuonya Mohame Said kwa Uchochezi wake!

Na mpaka dakika hii ninaamini nimeokoa watu wengi sana waliokuwa wafuasi wa NGANO za Mchochezi huyu!

Mpaka sasa wewe ndiye uliyejifunza mengi sana, mpaka unataka kuendelea kujifunza kwa kwenda kutafuta data za kina Mkwawa, mikanda ya hotuba, historia ya Abushiri na mengineyo mengi.

Nna uhakika uzi huu umekuwa na faida kubwa sana kwa jamii. Wengi leo wanamjuwa Mshume Kiate, Mashado Plantan, Iddi Tosiri. Lakini nani kabla ya hapa alikuwa akiwajuwa? na nani alikuwa hamjuwi Nyerere? tulilosoma jipya kuhusu Nyerere ni jinsi alivyowageuka Waislaam na kuwaweka ndani, kuwavunjia jumuia yao ya EAMWS na mambo kadha wa kadha.

Nakupa heko na nakupa hongera. Ni faida kubwa sana huu mjadala. Uzuri ni kwamba umeshindwa mpaka dakika hii kuonesha uchochezi na dhihaka za Mohamed Said kwa wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, tunachokiona ni dhihaka na kejeli mnazowafanyia wewe na wenzako na tunaona Mohamed Said akiwatukuza na kuwaenzi.

Imekula Kwako.
 
Vita vya Kagera vilikuwa siyo vita? Nipe kisa chake tuanze kufungua vitabu upya.
Hiyo vita ndio hatuwezi kuongopeana kabisa uwadanganye hawa vijana waliozaliwa miaka ya '70 kuelekea '80. Uongo mzuri ni kama wa mzee Mohamed aliouficha kwenye kanzu na barghashia za wazee wake wa Kariakoo.
 
Mimi nitamkumbuka zaidi Mshume Kiate kwa maharage, dagaa na mchicha wake alookuwa akipeleka Magomeni kwa Mwalimu.
 
Vita vya Kagera vilikuwa siyo vita? Nipe kisa chake tuanze kufungua vitabu upya.
Haahaa aisee kweli nimeamini wewe na kundi lenu likiongozwa na Mohamed Said ni hatari kwa Taifa,

Vita vya majimaji walivyopigani wa ngoni na wamatengo eti viliongozwa na waislamu!

Hivi wala hamjui kuwa uislamu ulikuwa hauna hata wafuasi zaidi tu pale - Newala enzi hizo za vita vya majimaji?

Wale wanyasa na warodesia wanaoishi kwa miti shamba walikuwa waislamu?

Haya hilo mmekosa ushahidi sasa mmerukia eti vita vya Kagera vilikuwa ni vita vya Kidini, kisa Nduli Amini alikuwa muamini wa Uislamu?

Acheni ujuha nyie ndugu zangu, Watanzania wote tunafahamu na kujua kuwa Uganda iliivamia Tanzania eneo lake la ardhi kule kaskazini katika miji ya Mtukula!

Udini huo umewapofusha, kila jambo nyie mnalitafsiri kidini tu?!
 
Wewe wamekuambia wapi wamenufaika na mchango wako au ndiyo unasema unaamini wanaamini.

Mapokeo nayaona hapahapa kwenye uzi huu kwa macho yangu ya nyama!

Wewe huwezi kuona na siku ukiona umeiasi imani yako!
 
Mimi nitamkumbuka zaidi Mshume Kiate kwa maharage, dagaa na mchicha wake alookuwa akipeleka Magomeni kwa Mwalimu.

Hilo ndilo dhumuni. Jee, ungeyajuwa hayo kabla hujamsoma Mohamed Said?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…