Nguruvi3,
Tuendelee na mjadala:
Mapema mwaka wa 1930 katika juhudi za kuikiimarisha chama,
Kleist akawa anasimamia ujenzi wa jengo la makao makuu ya
African Association, New Street (sasa Mtaa wa Lumumba) ambalo
wananchi walikuwa wakijenga ofisi yao kwa kujitolea nguvu zao
wenyewe.
Hili ndilo jengo ambalo TANU ilikuja kuzaliwa tarehe 7 Julai, 1954.
Nyumba hii ipo hadi leo ingawa si kama ilivyojengwa hapo hapo
mwanzo.
Hivi sasa jengo hilo ni katika majengo ya hapo mwanzo makao
makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hivi sasa ni ofisi yake
ndogo.
Ile nyumba ya zamani ilikuwa imejengwa kwa chokaa, udongo na
mawe kama ilivyokuwa desturi ya ujenzi wa wakati ule.
Chokaa ndiyo iliyokuwa ikitumika badala ya sementi.
Akiwa bado mtoto mdogo, Abdulwahid anakumbuka kumuona
baba yake na wenzake wakijenga nyumba hiyo kwa kujitolea
siku za Jumapili.
Vilevile alimuona baba yake akifanya mikutano na akishughulika na
uongozi wa harakati za Kiislam na vyama vya wafanyakazi.
(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
Kuna picha ndani ya kitabu ya ufunguzi wa jengo hilo iliyopigwa 1933
Gavana Cameron yupo pamoja na Kleist, Mashado Plantan, Mwalimu
Mdachi Shariff na wanachama wengine wa African Association.
Cecil Mtola alikufa mwaka 1933 na Mzee bin Sudi akachaguliwa kushika
nafasi yake.