Mpaka sasa wewe ndiye uliyejifunza mengi sana, mpaka unataka kuendelea kujifunza kwa kwenda kutafuta data za kina Mkwawa, mikanda ya hotuba, historia ya Abushiri na mengineyi mengi.
Nna uhakika uzi huu umekuwa na faida kubwa sana kwa jamii. Wengi leo wanamjuwa Mshume Kiate, Mashado Plantan, Iddi Tosiri. Lakini nani kabla ya hapa alikuwa akiwajuwa? na nani alikuwa hamjuwi Nyerere? tulilosoma jipya kuhusu Nyerere ni jinsi alivyowageuka Waislaam na kuwaweka ndani, kuwavunjia jumuia yao ya EAMWS na mambo kadha wa kadha.
Nakupa heko na nakupa hongera. Ni faida kubwa sana huu mjadala. Uzuri ni kwamba umeshindwa mpaka dakika hii kuonesha uchochezi na dhihaka za Mohamed Said kwa wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar, tunachokiona ni dhihaka na kejeli mnazowafanyia wewe na wenzako na tunaona Mohamed Said akiwatukuza na kuwaenzi.
Imekula Kwako.