Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nguruvi3
Inawezekana kabisa hii Al Jamiatul islammiyya never existed, but rather, it is a creation by the brain of the author. Au la kama ilikuwepo, it was not even significant Labda ilikuwa na wanachama hai wasiozidi 20 na wote walikuwa labda DSM na Tanga. Ndio maana Mzee Muddy halalamikii sana kufa kwake, ila analalamika kufa kwa EAMWS ya wahindi ambayo anaamini ingewaletea chuo kikuu. Ukimsoma, utaona kuwa anakumbushiakumbushia, kuwa so and so were members of Al Jamiatul islamiyya, ili tu kujenga msisitizo kuwa wapigania uhuru walisukumwa na uislam wao. He is a very clever old man, in a dangerous way, anyway.
Mohamed Said
Mzee, unaweza ukatusaidia kutuwekea malengo/katiba ya Al Jamiatul islamiyya?

Nanren,

Unailezea Al Jamiatul Islamiya kwa hisia zako pamoja na fikra zako halafu hapo hapo unaomba Mohamed Said, akujibu.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said,

Naomba kukuuliza Mzee Kleist Sykes alikuwa na watoto wangapi.

Halafu Abbas Sykes na Ally Sykes nani mkubwa.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said na kundi lako,

Bado mnaamini kabisa kuwa Hayati Mzee Nyerere alikuwa na chuki kwa Uislamu na Waislamu wa Tanzania?


Kama ndivyo je mnamfahamu Omar Sisko?

Ndugu wanajamvi, kwakuangaza tu uongo na Uchochezi wa Mohamed Said hebu mfahamuni huyu Sisko mtu muhimu sana kwa Mwalimu Nyerere pengine kuzidi hata mke wake kipenzi Mama Maria Nyerere,

Sisko ambae alitokea kuwa bindamu muhimu kwa Mwalimu Nyerere tangu siku ya kwanza Mwalimu alipokalia kiti cha Ikulu takatifu, anatajwa kuwa alikuwa ni muislamu swafi mwenye kutumika kwa swala tano,

Amehudumu Ikulu ya Dar katika kitengo nyeti kabisa cha uhifadhi wa uhai wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,

Huyu asipokuwepo Nyerere alikuwa hawezi kulala wala kula, kumbuka ni muislamu huyo,

Chakula chochote hata kilichopikwa na Mama Maria Nyerere, Mwalimu alikuwa hakigusi mpaka kionjwe kwanza na Sisko, kumbuka ni Muislamu huyo,

Kwaujuma maisha ya Mwalimu Nyerere mpaka anaingia kaburini yalikuwa chini ya Omar Sisko, Kumbuka ni Muislamu huyo!

Jiulize kwanini Mwalimu hakuweka ndugu zake wa damu kama akina Mzee Joseph? Au hata aweke ndugu zake wakurya kwenye kitengo hicho nyeti?

Kikwete leo amemuweka ndugu yake wa damu kabisa kwenye kitengo hicho jiulize kwanini?

Uchochezi unaofanywa na Mohamed Said na kkundi chake wanaojifanya ni waislamu zaidi ya wenzao hauvumiliki na kila mtanzania aukemee!

Mimi nawapatiliza jina jipya lipitalo majina yote ya wachochezi, Mohamed Said na kikundi chake kwa sasa nawaita ni (waislamu mwehu), hawa wanawaona waislamu wenzao wa Tanzania kama vile sio waislamu halisi, wanawadhihaki wenzao vyovyote watakavyo,

Wao wanandoto siku moja wajione wapo pekeyao katika ardhi ya Tanzania!
 
Ritz umemjulia sana mzee wetu huyu. Haya ndio maswali anayotaka aulizwe. Hii ndio historia iliyosahaulika. Keep it up ili kumpumzisha na nondo na misumari ya akina Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, Nanren, Yericko Nyerere, Jasusi,..., actually, mmesababisha tudumu naye humu muda wote huu.

Unajua na mimi huwa najikuta nafurahi mwenyewe wanapomuuliza hivi..Au wakati mwingine watamuuliza "hivi ile nyumba ya tatu mtaa wa Kipata ni ya nani?".

Basi Mzee atatiririka kwa kuremba lugha haswa!
 
Yericko Nyerere,

Naona umekuja na ngano mpya unasema Omar Sisco alikuwa mtu muhimu sana kwa Nyerere zaidi ya Mama Maria Nyerere. Siku Sisco asipokuwepo Nyerere siku hiyo hawezi kula wala kulala...come on...lol.
 
Last edited by a moderator:
Hicho nimekisoma baadhi ya kurasa zake kwenywe mtandao Judith Listoll kajikita sana kuuanzia 1961. Nimeona kawataja watu wa familia ya Sykes, wengi tu waliotajwa na Mohamed Said hawamo.

Kinapatikana wapi hicho kitabu kwa Dar es Salaam. Nipe na vingine.
Hapana. Si kweli kwamba Judith Listowell kajikita kuanzia 1961. Ameanzia 1946 to be exact. Kasimulia vile vile historia ya TAA. Kwa Dar-es- Salaam sijui kama bado kinapatikana. Kuhusu historia ya Uislamu na Ukristo Tanganyika kuanzia 1800-1900 soma kitabu cha Lawrence Mbogoni "The Cross versus the Crescent. Kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers. Hicho kwa hakika utakipata Dar-es-salaam
 
Jasusi,
Hivi wewe unaamini ni kweli waasisi wa TANU ni watu 17 tu. Na hao ndiyo waliongoza mapambano ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Hivi waasisi huwa ni wangapi? Watu wanapoamua kuanzisha kitu kwanza wanakutaka kwa uchache halafu baadaye ndipo kundi linapoongezeka? Sina tatizo na idadi ya watu kumi na saba kuanzisha TANU au watu wanne kuanzisha TAA. It is immaterial.
 
Yericko Nyerere,

Naona umekuja na ngano mpya unasema Omar Sisco alikuwa mtu muhimu sana kwa Nyerere zaidi ya Mama Maria Nyerere. Siku Sisco asipokuwepo Nyerere siku hiyo hawezi kula wala kulala...come on...lol.

Kama hujui protokali za kirais nyamaza,

Hivi unajua Kikwete anamtu ambae ni muhimu kuliko hata mama Salma katika masuala ya uhai wake? Huyo ndie muonjaji wa vyote viliwavyo na Kikwete popote duniani!


Tulia tukufunze ndugu!

Urais sio kama duka la Mpemba tu!
 
Last edited by a moderator:
Ritz umemjulia sana mzee wetu huyu. Haya ndio maswali anayotaka aulizwe. Hii ndio historia iliyosahaulika. Keep it up ili kumpumzisha na nondo na misumari ya akina Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Mag3, Nanren, Yericko Nyerere, Jasusi,..., actually, mmesababisha tudumu naye humu muda wote huu.
WildCard,

Unamjua Omari Sisco alikuwa mtu muhimu kwa Nyerere za zaidi ya Mke wake Mama Maria Nyerere aliyemzalia watoto saba.

CC.. Mzee Mwanakijiji, Jasusi, Mag3, Nguruvi3,
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri ukitaka kupata data nzuri. Jiulize baada ya uhuru wenu Makanisa yeni yaliweza kujenga skuli ngapi, Hospital ngapi?

Jiulize kwanini hizo zote ulizo orodhesha zilijengwa kabla ua uhuru wenu?

Kama hujui kitu uliza. Hata baada ya uhuru makanisa yaliendelea kujenga shule. Musoma College imejengwa na wakatoliki baada ya uhuru na vile vile Musoma Alliance. Makanisa yaliacha kujenga shule baada ya Nyerere kuzitaifisha zile zilizokuwepo. Capice?
 
Kama hujui protokali za kirais nyamaza,

Hivi unajua Kikwete anamtu ambae ni muhimu kuliko hata mama Salma katika masuala ya uhai wake? Huyo ndie muonjaji wa vyote viliwavyo na Kikwete popote duniani!


Tulia tukufunze ndugu!

Urais sio kama duka la Mpemba tu!
Yericko Nyerere,

JF siyo sehemu ya porojo hebu tajie huyo ndugu yake Kikwete. Sasa kejeli na dhihaka kwa Wapemba zimeingiaje.
 
Last edited by a moderator:
Hapana. Si kweli kwamba Judith Listowell kajikita kuanzia 1961. Ameanzia 1946 to be exact. Kasimulia vile vile historia ya TAA. Kwa Dar-es- Salaam sijui kama bado kinapatikana. Kuhusu historia ya Uislamu na Ukristo Tanganyika kuanzia 1800-1900 soma kitabu cha Lawrence Mbogoni "The Cross versus the Crescent. Kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers. Hicho kwa hakika utakipata Dar-es-salaam
Nashukuru tavitafuta ivyo vitabu.
 
Mzee wangu ananidithia kwenye mazishi ya Abdulwahid, Nyerere alitembea kwa miguu kutoka Mtaa wa Lindi, Garezani hadi Msikiti wa Kitumbini, Nyerere alisimama nje ya Msikiti pamoja na Wakristo wengine kungojea maiti.

Mfanyabiashara mmoja wa kiasia kuona rais amesimama wima, kwa ajili ya heshima alileta kiti na kumuwekea Nyerere akae. Nyerere alikataa kukaa na akawa amesima pamoja na watu wengine.

Kutoka Kitumbini msafara uliendelea tena mpaka makaburi ya Kisutu. Wakati wote Nyerere alikuwa nyuma ya jeneza kichwa chake amekiinamisha chini huku akionekana kila wakati akifuta machozi na kitambaa akilia.

Watu walimpenda sana Nyerere zama hizo.

Kuna mtu katika thread hii kasema Nyerere hakuhudhuria mazishi ya Abdulwahid, kwamba aliambiwa juu ya kifo chake baadaye na aliyetokwa machozi ni Mama Maria. Sasa wewe umetoa wapi hii hadithi ya Nyerere kusimama nje ya msikiti kusubiri maiti?
 
Hivi waasisi huwa ni wangapi? Watu wanapoamua kuanzisha kitu kwanza wanakutaka kwa uchache halafu baadaye ndipo kundi linapoongezeka? Sina tatizo na idadi ya watu kumi na saba kuanzisha TANU au watu wanne kuanzisha TAA. It is immaterial.
Kwa Mzee wetu Mohamed historia ya TANU inaanzia mwaka 1929. Jina la TANU lilianzia Burma. TANU yenyewe ikazaliwa Julai 7, 1954. Rais wa KWANZA wa TANU sio miongoni mwa waasisi wake kwa maana hiyo.

Ipo siku atajitokeza mwandishi mwingine wa historia za aina hii, atafanya utafiti, ataongea na wazee wake, atairudisha nyuma tarehe Tanganyika ilipopata uhuru. Wazo la kuwa huru kama nchi lilikuwepo tangu mwaka 1929! Na kama uchaguzi ungefanyika wakati ule bila shaka Kleist Sykes anatakiwa kutambuliwa kama Rais wa KWANZA wa Tanganyika.

Hutaki kuamini hivo, unaacha. Wazee hawadanganyi ebo.
 
Yericko Nyerere,

JF siyo sehemu ya porojo hebu tajie huyo ndugu yake Kikwete.
Usipende kutafuniwa tu ili wewe umeze,

Nenda pale magogoni ikulu mapokezi tu, waulize kuwa unataka mnadhimu wa ikulu na muambata wa Kikwete, watakuitia mtu huyo wa Musoga, ambae ni tester ya JK popote na anaaminiwa kuliko hata mama Salma!
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamedi.
Wewe ni kama baba yangu na napenda nikusalimu kwa salamu ya kiswahili "Shikamoo mzee".
Mzee Mohamed unavyozungumzia upendeleo katika elimu ya Tanzania kwa Wakristo unakuwa hujanitendea haki hata kidogo. Kwanza mimi ni Mkristo lakini majina yangu yote matatu ni ya kiasili, hakuna hata moja la Kiarabu,Kimagharibu au Kiyahudi yote ni majina ya asili yetu.
Mimi nimesoma shule na vijana wa kiisalmu na wa kikristo pia, nilifaulu kusoma sekondari hadi nikamaliza shahada yangu ya kwanza hakuna anayeweza kutambua jina langu kama mimi Mkristo.

Kipindi elimu ikiwa ni bure nchi za Skandnavia nilikuja kusoma shahada ya pili, sikuwa na scholarship yeyote lakini nilikuwa nafanya vibarua kuniwezesha kuishi kwa kua ada ilikuwa bure. Hapo Chuoni tulikuwa karibu vijana 10 hivi toka Tanzania, 7 Wakristo na 3 Waislam. Siku moja ikaja mada na kuwa Tanzania Wakristo wanapata upendeleo toka kwa kijana wa kiislamu, mwingine akakubali. Nikawauliza hivi tupo 10 hapa wote toka Tanzania, je waliokuja na scholarship toka Tanzania ni wangapi?? cha ajabu vijana wa Kiisalam wote 3 toka Tanzania walikuja na scholarship toka Tanzania na kijana 1 kati ya Wakristo 7 ndio pekee aliyekuja na scholarship.
Badae nilipata scholarship ya Phd toka hapo chuoni, serikali yangu ya Tanzania haikuwa inajua nasoma nini au nala nini uku.
Kwa hiyo kuna watu wakiniona na Phd bila kujua nimeipataje, watasema kwa kua mimi ni Mkristo basi nimependelea, hiii si haki na haikubaliki katika jamii zote za waungwana. Sijapata scholarship au msaada wowote ule kwa kua mimi ni Mkristo, naomba uniombe radhi.

Lakini hili unalolalamikia lina madhara kwa upande wa hao unaofikria unawazungumzia.
1.) Unawafanya waamini wao ni VICTIM kwa kua ni waislam hivyo hawana nafasi ya elimu Tanzania.
2.) Unapandikiza chuki na hasira katia ya imani hizi na yanayotokea Geita,Mbagala,Zanzibar ni matokeo.
3.) Unawafanya Wakristo pia kuanza kujihami kwa kua jirani yake ana chuki dhidi yake.

Na fikiri ingekuwa ni vema kama ungesisitizia sana kwenye vitu vya kujenga kuliko vya kubomoa, kubomoa ni rahisi lakini kujenga ni kazi ngumu, utakuja kutambua hili huko mbeleni kama juhudi za maksudi hazitafanywa.
 
Kuna mtu katika thread hii kasema Nyerere hakuhudhuria mazishi ya Abdulwahid, kwamba aliambiwa juu ya kifo chake baadaye na aliyetokwa machozi ni Mama Maria. Sasa wewe umetoa wapi hii hadithi ya Nyerere kusimama nje ya msikiti kusubiri maiti?
Hili hata Mzee wetu Mohamed kalisema. Kasema pia jinsi Mwalimu alivyomwona mke wa marehemu Abdu kando ya barabara akasimamisha msafara wake kwenda kumsalimia yule mama.
 
Back
Top Bottom