Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Na usisahau kuwa hotuba aliyoisoma Nyerere UN iliandikwa wakati chama kikiitwa TAA!!Kwa Mzee wetu Mohamed historia ya TANU inaanzia mwaka 1929. Jina la TANU lilianzia Burma. TANU yenyewe ikazaliwa Julai 7, 1954. Rais wa KWANZA wa TANU sio miongoni mwa waasisi wake kwa maana hiyo.
Ipo siku atajitokeza mwandishi mwingine wa historia za aina hii, atafanya utafiti, ataongea na wazee wake, atairudisha nyuma tarehe Tanganyika ilipopata uhuru. Wazo la kuwa huru kama nchi lilikuwepo tangu mwaka 1929! Na kama uchaguzi ungefanyika wakati ule bila shaka Kleist Sykes anatakiwa kutambuliwa kama Rais wa KWANZA wa Tanganyika.
Hutaki kuamini hivo, unaacha. Wazee hawadanganyi ebo.
Na pia Nyerere hakuwa rais wa kwanza wa TANU yeye aliingia kila kitu kikiwa tayari.
Tena, Nyerere alifundishwa siasa na Sykes ''kwa mara ya kwanza alipokanyaga Dar es slaam mwa 1950..''
Nyerere hakuwahi kufika Dar es salaam kabla ya hapo, inasemekana mwaka 1946 kuna mtu akiitwa Nyerireh ndiye alikuja katika mkutano mkuu wa AA, shajara zangu zina jina hilo
Nyerere pia alikuwa mwakilishi wa kanisa kama katibu wa AA kule Tabora. Inasemekana alikuwa ni pandikizi la kuua jitihada za kupigania Uhuru.
Hili la nyumba aliyotoa D.Cameron sina ujuzi nalo.
Hili la Jamiyatul Islamiya fir Tanganyika kuuawa inasemekana liliambatanishwa na EAMWS ingawa gazeti halikutoa jina hilo. Wakati huo mhariri alikuwa Mkapa mkatoliki na (mkristo). Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Ali Maswanya( ) alishinikizwa atangaze kuvunjwa kwa EAMWS.
Kama kuna asiykubaliana na yangu aandike kitabu chake.