Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kwa Mzee wetu Mohamed historia ya TANU inaanzia mwaka 1929. Jina la TANU lilianzia Burma. TANU yenyewe ikazaliwa Julai 7, 1954. Rais wa KWANZA wa TANU sio miongoni mwa waasisi wake kwa maana hiyo.

Ipo siku atajitokeza mwandishi mwingine wa historia za aina hii, atafanya utafiti, ataongea na wazee wake, atairudisha nyuma tarehe Tanganyika ilipopata uhuru. Wazo la kuwa huru kama nchi lilikuwepo tangu mwaka 1929! Na kama uchaguzi ungefanyika wakati ule bila shaka Kleist Sykes anatakiwa kutambuliwa kama Rais wa KWANZA wa Tanganyika.

Hutaki kuamini hivo, unaacha. Wazee hawadanganyi ebo.
Na usisahau kuwa hotuba aliyoisoma Nyerere UN iliandikwa wakati chama kikiitwa TAA!!

Na pia Nyerere hakuwa rais wa kwanza wa TANU yeye aliingia kila kitu kikiwa tayari.

Tena, Nyerere alifundishwa siasa na Sykes ''kwa mara ya kwanza alipokanyaga Dar es slaam mwa 1950..''

Nyerere hakuwahi kufika Dar es salaam kabla ya hapo, inasemekana mwaka 1946 kuna mtu akiitwa Nyerireh ndiye alikuja katika mkutano mkuu wa AA, shajara zangu zina jina hilo

Nyerere pia alikuwa mwakilishi wa kanisa kama katibu wa AA kule Tabora. Inasemekana alikuwa ni pandikizi la kuua jitihada za kupigania Uhuru.

Hili la nyumba aliyotoa D.Cameron sina ujuzi nalo.

Hili la Jamiyatul Islamiya fir Tanganyika kuuawa inasemekana liliambatanishwa na EAMWS ingawa gazeti halikutoa jina hilo. Wakati huo mhariri alikuwa Mkapa mkatoliki na (mkristo). Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Ali Maswanya( ) alishinikizwa atangaze kuvunjwa kwa EAMWS.

Kama kuna asiykubaliana na yangu aandike kitabu chake.
 
Mag3,

Unakumbukwa mswada wa Abdu Sykes na Dk.Klerruu?
Si ulipotea?

Tena ulipotea palepale TANU HQ, Dar es Salaam.
Unajua kujaza jigsaw puzzle?

Fananisha Ulotu na kile cha Kivukoni.

Mohamed Said
Swali dogo nje ya mnakasha.
Huyu Abubakar Ulotu mwandishi wa historia ya TANU ndiye yule Abubakar Ulotu aliyeanzisha NRA kilichopigwa marufuku 1995 kwa kuwa na mwelekeo wa udini?
 
Last edited by a moderator:
Joka Kuu,

Hata mie nazikumbuka siku hizo.
Kimetokea kitu gani?

Nani kasababisha fitna hii?
nyeje tujikwamue na dhahama hii?

Haiwezekani kuwa ni Nyerere kwani hizo ndizo siku za Nyerere akiwa madarakani wengi tunakumbmuka. Uliza wale walioenda jeshini jinsi gani dini ilikuwa so irrelevant..
 
Usipende kutafuniwa tu ili wewe umeze,

Nenda pale magogoni ikulu mapokezi tu, waulize kuwa unataka mnadhimu wa ikulu na muambata wa Kikwete, watakuitia mtu huyo wa Musoga, ambae ni tester ya JK popote na anaaminiwa kuliko hata mama Salma!

Wewe ulipoenda TBC kuomba hotuba ya Baba ako ulipewa? seuze Ikulu!
 
Na usisahau kuwa hotuba aliyoisoma Nyerere UN iliandikwa wakati chama kikiitwa TAA!!

Na pia Nyerere hakuwa rais wa kwanza wa TANU yeye aliingia kila kitu kikiwa tayari.

Tena, Nyerere alifundishwa siasa na Sykes ''kwa mara ya kwanza alipokanyaga Dar es slaam mwa 1950..''

Nyerere hakuwahi kufika Dar es salaam kabla ya hapo, inasemekana mwaka 1946 kuna mtu akiitwa Nyerireh ndiye alikuja katika mkutano mkuu wa AA, shajara zangu zina jina hilo

Nyerere pia alikuwa mwakilishi wa kanisa kama katibu wa AA kule Tabora. Inasemekana alikuwa ni pandikizi la kuua jitihada za kupigania Uhuru.

Hili la nyumba aliyotoa D.Cameron sina ujuzi nalo.

Hili la Jamiyatul Islamiya fir Tanganyika kuuawa inasemekana liliambatanishwa na EAMWS ingawa gazeti halikutoa jina hilo. Wakati huo mhariri alikuwa Mkapa mkatoliki na (mkristo). Aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani bw Ali Maswanya( ) alishinikizwa atangaze kuvunjwa kwa EAMWS.

Kama kuna asiykubaliana na yangu aandike kitabu chake.

Nguruvi3,

Ikiwa hapa ndipo tulipofika basi tuko karibu ya kumaliza safari yetu.
 
Mzee Mohamed ni msemaji wa Waislam wepi? Mnaweza kuishusha hadhi na heshima ya Mwalimu? Hadhi yake ni Rais wa KWANZA Tanganyika na baadae Tanzania. Mtaishushaje hadhi hii? Siwashangai. Waislam wenzenu kungineko duniani wamewafanyia mazito zaidi marais wao akina Gadafi, Hosni Mubarak,...

WC,

Mimi naeleza lile ambalo naliona katika jamii ya Waislam hivi sasa.
Wala sina haja ya kulazimisha mtu kuniamini.

Lakini atakae kujua ukweli na afanye utafiti wake atapata jibu.
 
Nguruvi3
Inawezekana kabisa hii Al Jamiatul islammiyya never existed, but rather, it is a creation by the brain of the author. Au la kama ilikuwepo, it was not even significant Labda ilikuwa na wanachama hai wasiozidi 20 na wote walikuwa labda DSM na Tanga. Ndio maana Mzee Muddy halalamikii sana kufa kwake, ila analalamika kufa kwa EAMWS ya wahindi ambayo anaamini ingewaletea chuo kikuu. Ukimsoma, utaona kuwa anakumbushiakumbushia, kuwa so and so were members of Al Jamiatul islamiyya, ili tu kujenga msisitizo kuwa wapigania uhuru walisukumwa na uislam wao. He is a very clever old man, in a dangerous way, anyway.
Mohamed Said
Mzee, unaweza ukatusaidia kutuwekea malengo/katiba ya Al Jamiatul islamiyya?
Mkuu Nanren, mzee Mohamed Saidi huwa hana kawaida ya kusoma katiba yoyote, yeye huleta simulizi za wazee wake tu. Kama wazee wake hawakumsimlia juu ya katiba hiyo basi hatakuwa na jibu!
 
Joka Kuu,

Hata mie nazikumbuka siku hizo.
Kimetokea kitu gani?

Nani kasababisha fitna hii?
nyeje tujikwamue na dhahama hii?
Mohamed, wewe unayeleta madai unapaswa kuainisha kwa ukamilifu nini kimetokea na wala si kwa kudhania tu.

Unauliza nini kifanyike? Mbona tumekuuliza swali hilo mara nyingi na jibu ulilo nalo ni kuwa unasubiri serikali itolee majibu malalamiko ya waislam, sasa iweje utuulize tena nini kifanyike.

Kwa vile wewe una mashtaka na ambayo kwa mujibu wako una ushahidi basi tungekuomba utupe na suluhu.
Kinyume chake utakuwa unauliza swali kama sisi tunavyouliza na kwa msingi huo hakuna ajuaye kama yapo madai au la.

cc Jokakuu
 
Hawa ndiyo wasomi wetu wa Tanzania tena unasema una PhD endelea kuwadanganya kina Mag3, Nguruvi3, Jasusi, lakini watu makini huwezi kuwadanganya.

Acha uongo nani kakuambia Oman wana utajiri wa mafuta sijui umeipata wapi hii.

Acha uongo eti Oman mwaka huu ndiyo wamejenga chuo kuu sijui umeipata wapi hii.

Oman wana vyuo vikuu zaidi ya 30 nakutajia vichache tu.


1) Uraimi University

2) Dhofar University

3) Sultan Qaboos University

4) The University of Nizwa

5) Oman Medical College

Angalia sana usipende kuokota maneno vijiweni kuleta JF.


Nami naongezea listi yote halafu Oman yenyewe wanaishi watu Milioni 3 na nusu tu!

[h=5]List of Universities of Oman[/h]
  1. Bayan University College
  2. Buraimi University College
  3. Caledonian College of Engineering Oman
  4. College of Banking and Financial Studies
  5. Dhofar University
  6. Fire and Safety Engineering College
  7. German University of Technology in Oman
  8. Gulf College
  9. Majan University College
  10. Mazoon College for Management and Applied Sciences
  11. Middle East College of Information Technology
  12. Modern College of Business & Science
  13. Muscat College
  14. Nizwa College of Technology
  15. Oman Dental College
  16. Oman Medical College
  17. Salalah College of Technology
  18. Sohar University
  19. Sultan Qaboos University
  20. Sur University College
  21. University of Nizwa
  22. Waljat Colleges of Applied Sciences
Kwa taarifa Reali 1 ya Oman=dola 2.5 USA! na ni sawa ni shilingi 4000 za TZ!

Hapo sasa imekuwaje nchi inayodaiwa haina Elimu kuwa na uchumi kihivyo!
 
MM,

Kwa muda mrefu ikidhaniwa hivyo.

ooh ya mahusiano mazuri hayakuwepo wakati wa Nyerere? Mbona miye nakumbuka wakati naishi Tanga (predominantly Muslim town) tulikuwa tukitaka kuchinja kuku tunamtafuta Bw. Said au Muislmu yeyote kuja "kutuchinjia" just incase kwamba akija mgeni ambaye ni Muislamu tusije kumlisha kitu kisicho halali? Nimesoma elimu yangu yote ya sekondari wakati wa Nyerere tena bweni na ninakumbuka vizuri tu jinsi ambavyo wakati wa Maulid au wakati wa Mfungo wa Mwezi wa Ramadhani Wakristu hawakulalamika hata kidogo kuona kila jioni Waislamu wanaandaliwa futari ns marafiki zetu wengine wakituletea futari hiyo na sisi wengine... nakumbuka tukitoka Prep kwenda kujibanza kwenye cubicle ya mtu kujipongeza.

Nakumbuka na hawa hawa marafiki zetu Waislamu siku ya Jumapili tukitaka kwenda Mjini na wenyewe wanatag along kama vile wao wakiamua kwenda Kuswali Msikiti wa Mjini Ijumaa na sisi vijana wakikristu tukidandia kwwenda nao mjini. Kwetu sisi tumeoa kwa Waislamu na Waislamu wameoa kwetu hata leo hii watoto wangu (wa kaka yangu) nusu wamechagua kuwa Waislamu na wanaishi vizuri tu.

Unaposema "ilidhaniwa hivyo" manake nini? kuwa haikuwa hivyo? kwamba wakati wa Nyerere kulikuwa na animosity ambayo tunaiona leo kati ya Wakristu na Waislamu?
 
Kwa hiyo huu moto wa waislam ambao Waikela alitishia 1963 ndio huu Nyerere aliojaribu kuuzima 1968 na ndio huu uliouwasha tena na unaendelea kuukoleza?
Kwa hiyo kimsingi, ni kwamba hizi elements za radicalism pamoja na malalamiko haviwezi kuisha regardless ya serikali inawafanyia nini.

Huyu Waikela was very irrational in my opinion. Yaani only two years in independece akawa anataka mabadiliko makubwa kwa maisha ya waislam na waislam pekee, hivi ingewezekanaje? Sasa cha kushangaza ni kuwa wewe mwenyewe ni kama vile unawaza kama Waikela. Au nakosea?

Na hii Muslim association of Tanganyika, ambayo umeikuza na kuitumia kuunganisha juhudi za wapigania uhuru na uislam, ilianzishwa lini na ilikuwa na wanachama wapi na wapi na wa aina gani? Na ilikuwaje ikawa "imefulia" mpaka waislam wakaanza kuitegemea EAMWS badala yake? What were their sources of funds, considering that non-asian muslims were not that well off by then?

N,

Angalia na chunguza mambo yanavyokwenda.

Usifanye mzaha wala kejeli.

Chukulia kama mtu aliyekuja usiku akakugongea
dirisha kukuambia kuwa nyumba yako imeshika moto.
 
Mohamed, wewe unayeleta madai unapaswa kuainisha kwa ukamilifu nini kimetokea na wala si kwa kudhania tu.

Unauliza nini kifanyike? Mbona tumekuuliza swali hilo mara nyingi na jibu ulilo nalo ni kuwa unasubiri serikali itolee majibu malalamiko ya waislam, sasa iweje utuulize tena nini kifanyike.

Kwa vile wewe una mashtaka na ambayo kwa mujibu wako una ushahidi basi tungekuomba utupe na suluhu.
Kinyume chake utakuwa unauliza swali kama sisi tunavyouliza na kwa msingi huo hakuna ajuaye kama yapo madai au la.

cc Jokakuu

Nguruvi,

Unanipa madaraka yasiyo yangu.
 
WC,

Mimi naeleza lile ambalo naliona katika jamii ya Waislam hivi sasa.
Wala sina haja ya kulazimisha mtu kuniamini.

Lakini atakae kujua ukweli na afanye utafiti wake atapata jibu.

Unafikiri Wakristu wote Tanzania wanapata maisha mazuri, elimu nzuri, hawana umaskini, na hawana manung'uniko dhidi ya serikali yao?
 

Mbona unataka kumuumbua msomi mwenye PhD amesema mwaka huu Oman ndiyo wanajenga Chuo Kikuu, msomi kaishasema Oman wana utajiri mkubwa wa mafuta usibishe wewe siyo msomi.
 
N,

Angalia na chunguza mambo yanavyokwenda.

Usifanye mzaha wala kejeli.

Chukulia kama mtu aliyekuja usiku akakugongea
dirisha kukuambia kuwa nyumba yako imeshika moto.


yeah lakini kama mtu huyo anasema hivyo halafu mkononi ameshika galoni la petroli sijui kama nitaanza kumshukuru kwanza...
 
Mkuu Nanren, mzee Mohamed Saidi huwa hana kawaida ya kusoma katiba yoyote, yeye huleta simulizi za wazee wake tu. Kama wazee wake hawakumsimlia juu ya katiba hiyo basi hatakuwa na jibu!

G,

Umesema kweli.
Sikuwa na haja ya katiba hilo halikuwa lengo langu.
 
Mag3, Unakumbukwa mswada wa Abdu Sykes na Dk.Klerruu? Si ulipotea? Tena ulipotea palepale TANU HQ, Dar es Salaam. Unajua kujaza jigsaw puzzle? Fananisha Ulotu na kile cha Kivukoni.
Mohamed Said, lengo langu la kumpa Ritz jina la hicho kitabu (Historia ya TANU) na mwandishi wake Ulotu Abubakar Ulotu haikuwa kuonesha kuwa nakubaliana na yaliyomo bali ni kukuumbua kwa madai yako kwamba hakuna mtu mwingine aliyewahi kuandika historia ya TANU. Naomba pia nikufahamishe kwamba mimi si kijana mdogo, mengi yanayoongelewa nimeyaishi na katu si porojo za kusimuliwa na wazee mitaani, naomba utilie maanani hilo unapojadiliana na mimi. Wakati harakati za kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954 zimeshika kazi, mimi tayari nilikuwa kijana nikisikiliza na kuona yaliyokuwa yakitendeka nje ya Dar es Salaam.

Kama unavyodai kuwa bingwa wa kujaza jigsaw puzzle, hivyo hivyo historia unayodai kuiandika kuhusu harakati za UHURU Tanganyika ni za kuungaunga kwa vipande vya kuokoteza hapa na pale mitaani. Historia ni historia, historia si histohisia, inabaki na itaendelea kubaki historia kwa sababu hakuna mtu anayeweza kupambana na historia, kama unavyothubutu, akafaulu. Historia tayari ipo na huwezi kuibadili, yaliyofanyika yalifanyika na hata ukijaribu kuipinda kwa kuegemea hisani ya uelewa finyu wa wafuasi wako, hautafanikiwa, utazidi kuonekana mpuuzi tu.

You cant change history "unless by misremembering"

African Association (AA) ilizaliwa 1929 na kuzinduliwa nyumbani kwa muasisi na Raisi wake wa kwanza Cecil Matola, na ikafa mwaka 1948 baada ya vijana wasomi wenye mawazo mapya kujitokezana na kuzaliwa TAA, muasisi na Raisi wake wa kwanza akiwa Dr. Vedasto Kyaruzi. Mwaka 1954 TAA nayo ikafa na Chama cha kwanza cha siasa Tanganyika TANU ikazaliwa muasisi na Raisi wake wa kwanza akiwa Julius Kambarage Nyerere. Mohamed Said huo ndio ukweli na hata ukitumia hila gani kujaribu kuupindisha huwezi, ni kama kusukuma tu ukuta, chutama JF inakuumbua.

Mengi yamesemwa humu, hadithi kibao zimetolewa humu, porojo nyingi zimesimuliwa, madai ya kipuuzi mengi tu yametolewa humu lakini historia, kama ilivyo kawaida yake inabaki pale pale. Hisia haiwezi kuibadili historia, chuki haiwezi kuibadili historia, uwongo hauwezi kuibadili historia...historia haitishiki wala kufutika! Nina hakika wananchi wote, bila kujali dini wala kabila, Waislaam kwa Wakristo, watafanya kama Watanganyika walivyofanya miaka mingi kabla hujazaliwa, kuungana pamoja kupambana na adui huyu mpya ambaye hata hajui madhara ya anayoyahubiri wala mbegu za chuki anazozipanda.
 
Mohamed,
Umemdisqualify Ulotu kama si mwandishi. What was he? Did he just copy and paste in his book? Unfortunately sijakisoma kitabu chake kwa hivyo sina uamuzi wa yaliyomo.
 
Back
Top Bottom