Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

sikubaliani na mohamad said katika mambo mengi.

Kusingizia Nyerere hakuiambua na kuitamini familia ya SYKES ni uongo uliopindukia. Nakumbuka mwaka 2008 nikiwa udsm, kwenye maadhimisho ya miaka ya uhuru, sijui ilikuwa 49, Mzee Syke alijumuika na wanazuoni, katika malezo yake, alisifia wazee na viongozi chini ya uongozi wa Nyerere, akaelezea walivyokuwa na uchungu na nchi hii.

Nakumbuka mzee yule kwa uchungu alitoa machozi akasema watawala wa kipindi hiki ni wezi na hakuna aliye na azma ya kutuvusha kama wao walivyomaanisha. Na kwa hasira alitueleza kuwa yeye kama balozi mstaafu wa tanzania Italy, alipewa kadi/mwaliko kuhudhuria maadhimisho yale uwanja wa taifa, lakini kwa kuona unafiki wa viongozi wa CCM, alikataa mwaliko na kuja kujumuika na wanafunzi ili atoe chanhamoto hiyo.

Na kama Nyerere aliipuuza familia ya Syke, ni wazi mzee yule asingefanya kazi ubalozini kama balozi. Amestaafu na wanae wapo wengi wanafanya kazi balozi mbalimbali za nchi yetuu ughaibuni.
 

Unajua nimefanya uamuzi wa kuanza kumjjibu na kuwajulisha Watanzania wengine juu ya maandishi ya huyu bwana na kwa kiasi gani yamechangia katika hili linaloendelea leo hii. Tumwombe Mungu atusaidie.
 
ukisoma principle of physics utakutana na akina newtons, Faraday, albert Eintein n.k.,natabiri kuna siku kule uarabuni watasema wazungu waliwakandamiza, kwa kutokuweka majina ya wataalam wa kiarabu katika uvumbuzi wa magari, ndege, na vitu vya kisayansi, na wapo watakaoamini pia. tukiachana na utabiri wangu huu, tujiulize hivi tulikuwa tulipigania uhuru wa mwaafrika au dini.je hao waafrika walikuwa ma-founder wa dini au wakoloni wa waliwapa? kimsingi kitabu chochote chenye kuleta uchochezi dhidi ya tabaka lolote hakina weledi wa kutosha.
 

Ntamaholo,
Umemtaja mzee Abbas Sykes na kunikumbusha jambo moja ambalo ningependa wana JF walifahamu. Aliporudi kutoka kazi ya ubalozi nchini aliwekwa kwenye bodi ya Air Tanzania. Huu ulikuwa wakati wa ubinafsishaji wa kila kitu wakati wa utawala wa Mwinyi. Mzee Sykes alipinga kwa kinagaubaga kuigawa Air Tanzania kwa Afrika kusini. Leo sote tunajua kilichotokea kwa shirika hilo la umma. Tulikuwa na ndege 13 wakati huo leo tunakodisha ndege mitumba kufufua shirika tuliloliua wenyewe. Hawa wazee walikuwa wa calibre ya kipekee.
 
Unajua nimefanya uamuzi wa kuanza kumjjibu na kuwajulisha Watanzania wengine juu ya maandishi ya huyu bwana na kwa kiasi gani yamechangia katika hili linaloendelea leo hii. Tumwombe Mungu atusaidie.
Mzee Mwanakijiji, kwa kweli huyu bwana ni mchochezi na anazo chuki zilizoanzia mbali...kwa babu zikahamia kwa baba na sasa ziko kwa mwana. Miaka michache kabla ya uhuru tayari manung'uniko yalishaanza dhidi ya Nyerere na idadi kubwa ya Wakristo ndani ya TANU kutoka sehemu mbali mbali. Malalamiko yalitoka hasa kwa wazee wa Dar es Salaam ambao walidhani Tanganyika ni Dar es Salaam, hawakujua kuwa idadi kubwa ya Watanganyika waliishi nje ya Dar es Salaam. Ghafla kama vile wazee wake Mohamed Said wanaamka usingizini wakakuta TANU waliyodhani ni mali yao kumbe ni ya Watanganyika wote watu milioni nane na si wa Dar es Salaam tu watu laki moja.
Swali nililomuuliza mohamed Said ni hili hawa viongozi wengi wakristo kiasi cha kuwatisha Wazee wa Dar es Salaam hadi waanzishe chama kipya (AMNUT) kumpinga Nyerere kabla ya uhuru walipatikanaje? Je TANU kabla ya uhuru haikuwa na namna ya viongozi wake kupatikana? Kama waliteuliwa, je uteuzi huo ulifanywa na nani na kwa utaratibu upi kwani kulingana na hadithi za Mohamed Said wengi wa waliojiunga na TANU mwanzoni walikuwa Waislaam. AU anatuambia kuwa Nyerere aliteua tu watu hawa alivyotaka yeye mwenyewe bila kuhusisha uongozi wa TANU? Jibu ni kwamba hawa wengi walikuwa tayari ni viongozi huko majimboni kwao.

Hata hivyo AMNUT pamoja na kukubalika kwa baadhi ya Waislaam wa Dar es Salaam, haikuungwa mkono na Waislaam walio wengi na hasa majimboni na hivyo mwaka 1963 ikafa.
Hapa tunaona masalia ya AMNUT yanaivamia Jumuiya ya Wahindi (Agakhan) na kutaka kuyaendeleza yale yale yaliyokataliwa hata na Waislaam wenzao hapo nyuma. EAMWS ya Wahindi ambayo hapo kabla ya uhuru haikujiingiza hata kidogo kwenye mambo ya siasa hadi ilipovamiwa na ex-AMNUT na ambayo shule zake nyingi ilizozijenga sana sana zilikuwa zikiwasomesha watoto wa kihindi, sasa leo zinadaiwa zilikuwa za wazee wa Gerezani. Halafu leo hii na bila aibu Mohamed Said analaumu serikali ya wakati huo kuipiga marufuku EAMWS baada ya kuanza kutumika kama chama cha kuipinga serikali nje ya madhumuni na malengo ya kuanzishwa kwake.
 

Mzee mwenzangu hapa umetoa jibu la swali ambalo limekuwa likiulizwa sana (kwa namna ya shutma); kwanini Nyerere aliivunja EAMWS (kama kweli aliivunja)? Jibu liko wazi: Masalia ya Wadini wa AMNUT na wale waliokuwepo kwenye jaribio la kumng'oa Nyerere sababu ya Ukristo wake.
 

Kwa hiyo nyerere alibaguwa wahindi? Au Mnataka kusema nini?
 

tatizo lako huelewi unachokisema. Kwa hiyo nyerere alibaguwa wahindi? Au Mnataka kusema nini?
 
Mzee Mwanakijiji, EAMWS baada ya kuvamiwa na masalia ya AMNUT ukorofi wake haukuwa na tofauti yoyote na UAMUSHO kama tunavyoshuhudia hivi leo...je Kikwete alaumiwe kwa viongozi wa UAMUSHO kuswekwa ndani? Ndivyo ilivyokuwa kwa EAMWS...la ajabu shirika la Aga Khan liliendelea na shughuli zake kama kawaida bila bugdha.
 
Last edited by a moderator:

Hapa ndipo patamu, enhee, endelea kutupa darsa hili zuri kabisa la matusiria.
 

Mag3,

Hapa ndipo ilipo hatari.

Msimamo wenu ndiyo huo wa kufananisha EAMWS na ''vurugu'' za Waislam.

Huku mtaani Waislam wanaelewa EAMWS imevunjwa kwa fitna za Nyerere
na Kanisa.

EAMWS haikuwa na uhusiano wowote na AMNUT na kwa ukweli AMNUT haikupata
kuwa na nguvu yoyote kwa Waislam.

Naelewa ni kiasi gani taarifa hizi zinavyo kuchomeni lakini mimi dhima yangu ni kueleza
ukweli kwa faida ya nchi yetu.

Mnayo khiyari ya kuamini unachotaka:

The second book is by Dr John C. Sivalon, who in his expose, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, [1] unmasks a conspiracy in the government to subvert Islam.

Sivalon revealed that the Catholic Church as far back as 1961 was worried by two prospects.

First, was the unity between the Muslim madhheb (sect) of Sunni, Bohora, Ismailia and Ithnasheri in Tanganyika; and the second, was the transfer of the headquarters of the East African Muslim Welfare Society (EAMWS) from Mombasa to Dar es Salaam.

The Church was worried that the resources in the hands of rich Asian Muslim community in East Africa, coupled with the political power of African Muslims, particularly in Tanganyika, would endanger Christian interests in East Africa.

The Church therefore declared Islam as its enemy in the country and plotted to thwart its progress.[2]


[1] John C. Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985, (Ndanda, 1992).
[2]Ibid. p 37.

Ilikuwa wazi kuwa wale waliokuwa wanadai utengano katika EAMWS hawakuwa watu wajinga kiasi cha kukosa kujua kuwa hayo waliyokuwa wakidai yalikuwa kinyume na Uislam.

Kwa kuwa walikuwa wanangíangíania kujitoa katika EAMWS, ilikuwa sasa kitu dhahiri kuwa hiki kikundi cha Waislam waliojawa na ''hamasa za kizalendo'' walikuwa na mpango maalum uliokuwa ukisaidiwa na serikali wa kuvunja umoja wa umma wa Kiislam ili Waislam wadhoofike na wawe hawana nguvu tena katika siasa.


Baada ya kukamatwa kwa Sheikh Hassan Bin Amir Tewa Said Tewa gazeti moja la Kiingereza lilimfuata ili afanye mazungumzo nalo.

Tewa alimfahamisha mwandishi kuwa kulikuwa na hofu juu ya maendeleo yanayofanywa na Waislam na mikutano mikubwa ya Waislam iliyokuwa ikifanyika nchi nzima.[1]

Waislam waliokuwa na vyeo katika serikali walikataa kabisa kuisaidia Tume ya Kikwima kwa njia yeyote wakidai kuwa kufanya hivyo ni sawasawa na kuchanganya dini na siasa.

Waislam hawa walikaa pembeni kama watazamaji huku Nyerere kwa taratibu akivunja uongozi wa EAMWS na kutayarisha watu wake kuwaongoza Waislam.

Kundi la Adam Nasibu lilikataa kukutana na Tume ya Kwikima.

Maulamaa wa Kiislam ambao walikuwa na hadhi na uwezo wa kuleta sulhu katika sakata ile hawakuweza kufanya hivyo kwa kuwa walikuwa wanajua fika kuwa aliyekuwa akivunja EAMWS hakuwa Adam Nasibu, yeye na wenzake walikuwa wakitumiwa tu.


Kundi la Adam Nasibu lilikuwa halitaki chochote ila EAMWS ivunjwe na badala yake iundwe jumuiya itakayokuwa chini ya kivuli cha serikali. [1]

Vilevile kukawa na uvumi kuwa Muislam yeyote ambae atakaejejihusisha na shughuli za EAMWS atawekwa kizuizini na serekali.

Tume ya Kikwima haukuweza kupuuza vitisho hivyo kwa sababu serekali ilishawahi kuwaweka vizuizini masheikh.


Huu ndiyo ukweli ulio vifuani kwa Waislam hivi sasa.
 

Mag3,

Tatizo lako una chuki sana na hawa wazee wazalendo wa Dar es Salaam uwezi kuwatoa hawa wazee kwenye historia ya Tanganyika.

Cecil Matola siyo rais wa kwanza AA. Rais wa kwanza wa AA ni Thomas Plantan mwaka 1949.

Wewe huwezi na wala una uwezo wa kumtoa Abdulwahid Sykes katika kuasisi TANU. Nyerere mwenyewe kamtaja soma hiyo hotuba yake mtu aliyetoa jina la TANU halafu asiwe muasisi TANU.

Kwa hiyo Nyerere ameasisi kitu ambacho kakikuta wewe roho yako ya hasad na husda ndiyo vinakusumbua. Hata siku moja hawa wazee kwako hawana jema lolote.
 
Last edited by a moderator:
Hapa ndipo patamu, enhee, endelea kutupa darsa hili zuri kabisa la matusiria.

zomba,
Huyo saizi ni mwalimu wa matusi kwenye huu uzi cha kuchekesha naye anataka kuandika kitabu.
 
Last edited by a moderator:

N,

Nisingeweza kukaa kuandika kitu kama hicho.

Nakuwekea hapa chini nilichoandika katika kitabu changu
ili uwe mwongozo wa fikra zako na upate kujua nilichosema:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Table of Contents
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 1. Dedication[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 2. Acknowledgements[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 3. Table of Contents[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] 4. Introduction[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Part One
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Abdulwahid Sykes 1924-1968
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 1. The Sykes: Origins 1894-1929[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Old Town of Dar es Salaam and its Elites[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Kleist Sykes, Pioneer and Man of Ideas: 1894-1949[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · World War One 1914-1918[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Founding of the African Association and Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Association of Tanganyika), 1929-1933[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 2.The Second World War and Tanganyika's Political Foundation, 1938-1945
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Burma Infantry, 1942[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 3. Dar es SalaamDockworkers Movement 1947-1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Dar es Salaam Port, 1947[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Erika Fiah[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Dockworkers' Union, 1948[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 4. The Genesis of Open Politics in Tanganyika 1950 -1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Tanganyika African Association, 1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · TAA Political Subcommittee, 1951[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Tanganyika as a Mandate Territory[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Kenyan Nationalists in the Struggle of Tanganyika,1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · TAA and KAU: Attempts at Linkage and Solidarity, 1950 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Meru Land Evictions, 1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 5. Julius Kambarage Nyerere [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Story of Julius Nyerere, 1952[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Tanganyika African National Union (TANU)-The Party of Independence, 1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 6. The Pan African Congress of Northern Rhodesia, 1953[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Ally Kleist Sykes[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Part Two
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Mass Mobilisation and Independence 1954-1961
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 7. Mass Mobilisation 1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Elders' Council and Nyerere's Visit to the United Nations, New York, 1954[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Idd Faiz Mafongo [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The African Press-Ramadhani Mashado Plantan, 1950[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Ahmed Rashad Ali-Radio Free Africa (Radio ya Afrika Huru), 1952 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Propagandists-The Bantu Group,1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Incorporation of Swahili Women's Societies into the Struggle, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Football As a Political Weapon[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 8. The Formation of the Party in the Provinces[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Central Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Southern Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Western Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Tanga Province, 1956[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · TANU in Mombasa, Kenya, 1957[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 9. The Tabora Conference-The Road to Independence, 1958[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Tanga Strategy, 1958[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Debate for Tripartite Voting[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Pan-African Movement of East and Central Africa (PAFMECA), 1958[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Independence, 1961[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Part Three
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Conspiracy Against Islam 1961-1970
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 10. The Muslim Factor in Post-Independence Tanzania 1961-1970[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Islam: The Ideology of Colonial Resistance[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The First Muslim Congress, 1962[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Resistance to Change[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Second Muslim Congress, 1963[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Proposal for an Islamic University, 1964[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Politics of Islam, Church, State and the African Christian[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Chapter 11. The East African Muslim Welfare Society (EAMWS) ‘Crisis'[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Fomentation of the BAKWATA ‘Crisis'[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Nyerere, Tewa, Bibi Titi Encounter, 1968[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · The Islamic National Conference, 1968[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Omissions Analysed[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Betrayal of Ideals[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Conspiracy Theory[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Epilogue [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] · Bibliography[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Mohamed,
Umemdisqualify Ulotu kama si mwandishi. What was he? Did he just copy and paste in his book? Unfortunately sijakisoma kitabu chake kwa hivyo sina uamuzi wa yaliyomo.

.......

J,

Ngoja nikupe kitu.
Soma hapa chini na unganisha:

Kwa mara ya kwanza historia ya TANU ilitaka kuandikwa na Abdulwahid mwenyewe.

Baada ya kupatikana kwa uhuru mwaka 1961 na TANU ilipokuwa sasa inataka kujiimarisha kama chama cha umma, inasemekana Nyerere wakati ule Waziri Mkuu alimuomba Abdulwahid aandike historia ya harakati ya Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni wa Waingereza.

Hii kwa hakika ndiyo historia ya TANU.

Dr Wilbert Kleruu ambae ndiyo kwanza alikuwa ametoka masomoni Marekani alichaguliwa na TANU asaidiane na Abdulwahid katika utafiti na uandishi wa historia ile.


Abdulwahid alirudi kwenye ofisi za TANU makao makuu; kwenye ofisi yake ya zamani aliyokuwa akiitumia kama rais wa TAA.

Nyaraka zake binafsi, za baba yake nyingine kuanzia mwaka wa 1929 wakati wa enzi za African Association zililetwa pale kwa utafiti kama ushahidi wa yale yaliyopitika zama hizo.

Maelezo ya Abdulwahid katika kuanzishwa kwa Africa Association inasemekana hayakumpendeza Nyerere, kwa kuwa mwanzo wa harakati dhidi ya ukoloni jina la baba yake Abdulwahid, Kleist Sykes, lilikuwa likitawala.

Halikadhalika ilipofika kueleza namna TAA ilivyokujabadilishwa kuwa TANU watoto wake wote watatu Abdulwahid, Ally na Abbas wakiongozwa na kaka yao mkubwa Abdulwahid halikadhalika likawa linatawala harakati zile.

Historia hii inasemekana haikumpendeza Nyerere na baadhi ya viongozi wa TANU.

Haukupita muda Abdulwahid akatambua kuwa viongozi wapya walioshika nafasi katika TANU kwa kweli hawakuwa na nia hasa ya kutafiti na kuandika historia ya Tanganyika bali nia na azma yao ilikuwa na kumjenga Nyerere na kumkuza kwa sifa ambazo hazikumstahili.

Abdulwahid alipong'amua hili haraka akajitoa katika kazi ile. Hata hivyo Dr Kleruu aliendelea na utafiti na akaandika historia ya TANU. Historia hii inasemekana ilifuta mchango mzima wa akina Sykes katika kuunda TAA na baadae TANU.

Hata hivyo baada ya kazi hii kukamilika haikuchapishwa na ikabaki katika maktaba ya TANU, Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam.

Lakini baadae kazi ile ilitoweka na ikachapishwa baada ya ''mwandishi'' kufanya mabadiliko kadhaa katika mswada ule ili usitambulike chanzo chake.

Hata hivyo TANU iligundua kuwa ile ilikuwa historia yao iliyoandikwa na Dr. Kleruu na wakafanya bidii kuzuia isichapishwe.

Kimya kimya TANU ikafanya juhudi ya kuzuia kitabu hicho kisitoke toleo la pili. Lakini hili halikuwezekana na kitabu hicho kimechapishwa sasa mara kadhaa.

Uandishi wa kitabu kile haukutofautiana sana na kitabu cha TANU kilichotoka mwaka 1981 kilichoandikwa na Chuo cha TANU cha Kivukoni.
 

Kwa kuwa walikuwa wanangíangíania kujitoa katika EAMWS, ilikuwa sasa kitu dhahiri kuwa hiki kikundi cha Waislam waliojawa na ''hamasa za kizalendo'' walikuwa na mpango maalum uliokuwa ukisaidiwa na serikali wa kuvunja umoja wa umma wa Kiislam ili Waislam wadhoofike na wawe hawana nguvu tena katika siasa.

Hapa Mohamed naomba ufafanuzi kidogo kwani sijakuelewa. Unamaanisha kwamba Waislamu waliojawa na "hamasa za kizalendo" walikuwa na mpango wa kuvunja umoja wa Waislamu na kuwadhoofisha waislamu wenzao kisiasa? Inaingia akilini kweli? Wakati huo huo unasema kulikuwepo na umoja miongoni mwa waislamu ambao ulitishia kanisa la katoliki?
Which is which? Na hapo bado tunamlaumu Nyerere kwa kuwabagua/kuwapuuza waislamu?
 
Mohamed,
Hata ingekuwa ni mimi naandika historia ya TANU, yaliyofanywa na AA kupelekea kuundwa kwa TAA ningeyaweka tu katika footnotes. AA ilizaa TAA na ni TAA iliyozaa TANU. Mimi ningeanzia hapo. Halafu ningemulika zaidi juhudi zilizofanywa na TANU na jinsi TANU ilivyosambaa katika kila kona za nchi mpaka kupatikana uhuru. Hiyo ndiyo historia ya kweli. Ile kwamba Kleist Sykes baba yake Abdulwahid alianzisha AA, ingebaki tu kwenye footnotes, kwa nini? Kwa sababu AA ilifanya nini? Kuna chochote kilichofanywa na AA ambacho kilisaidia mwamko wa kudai uhuru Tanganyika? Na kama utasema hivyo basi kwa nini tusirudi nyuma hadi juhudi za maji-maji? Tuanzie hapo basi. Lakini kama ni historia ya TANU kama modern nationalist movement, ningejikita zaidi kuanzia 1954 hadi 1961. Hiyo ndiyo historia sahihi ya TANU.
 

Jasusi,

Nimekusoma.
Hapo pa kuanzia ndipo pakawa tatizo kati ya Abdu na rafiki yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…