- a. Kejeli kwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere (hawawezi kamwe kujenga hoja bila kumdunisha Nyerere)
- b. Chuki dhahiri dhidi ya Wakristu (hata kama ni ndugu zao wa damu)
- c. A revisionist outlook ya historia yetu (Sykes ndiye muasisi wa taifa, Waislamu ndio wapigania uhuru pekee, na Dar-es-Salaam ndio mahali pekee walikotaka uhuru; na Wakristu hawakutaka Uhuru isipokuwa baada ya kukaribishwa na Waislamu wa Dar)
- d. Wengi (kama siyo wote) bado ni watu wa CCM; chama kile kile kinachodaiwa kuendesha dhulma dhidi ya Waislamu ndicho hicho hicho kinakumbatiwa; serikali ile ile 'iliyounda BAKWATA' ndio hiyo hiyo inatarajia itatue matatizo ya "Waislamu". Utaona pamoja na malalamiko yao yote hutawasikia wanataka kuiondoa CCM madarakani!
Hayo usemayo si kweli.
Kitabu changu kipo na atakae ukweli atakisoma.
Post zangu zimo humu ndani.
Atakae kujua msimamo wangu Insha Allah anaweza kuzisoma.
Mohamed, mimi naujua msimamo wako na hapa naainisha hoja za MM kwa uchache sana kwa kutumia hoja zako ili kukutendea haki.
A.Kejeli kwa baba wa taifa
- Kwamba alianza siasa alipokutana na Sykes na alikuja Dar kuanza siasa huku watu wa mjini tayari wana mapambano.
-Kwamba alipewa hotuba akaisome UN, yeye hakushiriki kuandika wala ku-review, alikuwa kipaza sauti tu.
-Kwamba alikwenda sokoni bila kujua bidhaa zinanunuliwa, aliyemuokoa ni mshume Kiyate
- Kwamba, alinyooshewa bakora Anatouglo na Rehani Waikela.
-Kwamba alikuwa mdini na alidhalilisha wazee wa kipata, mkunguni na Gerezani
-Kwamba alifika Dar mara ya kwanza 1950 na kabla ya hapo hakujua Dar ilikuwa nchi gani
-Kwamba hakushiriki kuanzisha TANU,Chama kilianzia Burma na wala hakuwa rais wa kwanza wa TANU
-Kwamba alitoa hotuba ya kuaga wazee na kusema hamjui Sykes ni nani
-Kwamba aliua EAMWS kwa maagizo ya kanisa ili kuuhujumu Uislam
-Kwama aliwaweka kizuzini na magereza masheikh bila sababu na hivyo kuwa mwendawazimu
kwa uchache wa kuorodhesha. Twende hoja namba 2
B.- Kutothamini mchango wa wakristu kama akina Lugazia, Cecil Matola, Dr Kyaruzi, Mhando, Dunstan, Kirlo n.k na kuwaondoa katika orodha ya wazee wako kwasababu tu ya dini yao.
- Kuwasingizia wakristo kuwa hawkushiriki shughuli za Uhuru asilani kwa kuogopa vinbarua na kanisa
-Kwa kuficha ukweli kuwa shirika la Maryknoll lilitoa ticket ya Nyerere kwenda New York
-Kumshambulia Mkapa kama Mhariri na kumwacha Ali Maswanya kama waziri wa mambo ya ndani
-Kuweka dhana ya mfumokristo ulioshindwa kuthibitisha kwa mantiki na ushahidi uwepo wake.
-Kusingizia Malima alivunja mfumokristo wizara ya elimu kwa kuanzisha namba za mitihani
-Kuita baraza la mitihani NECTA kama kigango cha kanisa bila kuwa na ushahidi
-Kudai kuwa jeshi la polisi ni mkono wa kanisa hata kama viongozi waliosimamia operesheni hizo ni waislam
- Kudai kuwa EAMWS iliuawa na kanisa bila kuwa na ushahidi wa maneno, nukuu, karatasi au kiwacho.
-Kusingizia kanisa kuwa kuawa kwa EAMWS ili kumaliza ndoto za chuo kikuu ni mkono wa kanisa
-Kusingizia kuwa BAKWATA ilundwa kwa mkono wa kanisa bila ushahidi.
-Kukubali jaribio la Nyerere kuondoshwa uongozini na radicals wa TANU kwasababu tu ni mkristo
--Tukio la awamu ya kwanza lilimhusu Mkatoliki Nyerere, awamu ya pili Mzee wetu, awamu ya tatu Mkatoliki Mkapa na awamu ya nne serikali.
C.''Revistionist outlook ya history''
-Kwamba mapinduzi ya ZNZ ni kazi ya Nyerere na wala sio Wazanzibar ili kuua Uislam
- Kwamba Nyerere alikuja Dar mwaka 1950 wakati huo ni uongo dhahiri shahiri
-Kwamba Nyerere alianza siasa baada ya kukutana na Sykes huo nao ni uongo dhahiri shahiri
-Kwamba Nyerere hakuwa katibu wa AA na wala hakujulikana makao makuu
- Kwamba AA ilianza na Sykes na kuishia kwa Sykes kama TAA
-Kufuta ukweli kuwa Nyerere ni miongoni mwa waanzilishi wa TANU
-Kwamba ni Dar peke ndipo uhuru wa Tanganyika ulipopiganiwa
- Kuficha ukweli wa wapigania uhuru wengine ambao mchango wao kwa taifa hili ni mkubwa sana.
-Kuficha ufisadi wa nyumba ya D.Cameron uliofanywa na familia ya Sykes
-Kuficha ukweli kuhusu kufukuzwa kwa sheik Amir
D: Wengi wa waislam ni CCM
- Umesema mlinong'oneza misikitini msimchague Mkatoliki na mkafanyikiwa
- Ulisema mtoto wa CCM, TANU ndiye aliyeua EAMWS ili kuua uislam
-Kwamba CCM a.k.a TANU iliyoua EAMWS, Baraza la wazee wa TANU ndio hiyo mlionong'onezana kuichagua misikitini
-Kwamba mwaka 2000 hadi 2005 Masheikh mliichukia CCM kwa dhulma katika elimu, mkahamasishana kuiunga mkono CUF.
Leo dhulma ile ile ipo mnahamasishana misikitini kuitetea CCM.
Haya ni kwa uchache tu na haraka haraka, nikiwa na muda nitachimba hadi yale uliohimiza suluhu ama sivyo UN,AU watatia timu kusuluhisha vita.
Msimamo wako kumuunga mkono Ilunga dhidi ya mauaji ya maaskofu upo hapa.
Msimamo wako kuhusu historia ya Tanganyika iliyopiganiwa na wazee wako tu ipo hapa.
Msimamo wako kuhusu Christian Hegemony upo hapa.
Msimamo wako kutetea utafiti wa Warsha ambayo wewe ulikuwa mshiriki upo hapa.
Msimamo wako juu ya fikra za Malik ambaye ni mkufunzi wako upo hapa na kwamba ndiye aliyeongoza utafiti.
Msimamo wa ushiriki katika kuandika kitabu cha Ghessany ambacho umekinukuu mara nyingi upo hapa.
Msimamo wako kuhusu uzushi wa namba za mitihani upo hapa.
Msimamo wako kuhusu hotuba ya Nyerere kumkana Sykes upo hapa jamvini Yarabi!
Lakini muhimu zaidi msimamo wako wa kukataa hoja zinazokinzana na zako upo hapa.
Msimamo wako kukimbia maswali yatakayo ibua ukweli uliofichika upo hapa.
Na msimamo wako kukiri kuwa haya ni mawazo yako na wala si ukweli wa kuaminiwa na kila mtu tunao hapa.
Msimamo wako kuhusu kutoktokuwa na hotuba ya Rehani waikela upo hapa.
Katika hayo kama lipo nililokuonea liseme, sitajibu kwa maneno yangu nitavuta uzi na quotation.
Khairi inshallah wasalimie maswahib wote hapa Kariakoo panapo majaaliwa tutawatembelea karibuni.
Masalam