MM,
Labda unipe jibu.
Ilikuwaje historia hii niliyoandika mimi ikawa haifahamiki
na mashujaa hao niliowataja hadi leo hawajaadhimishwa?
Napenda kujibu swali la mheshimiwa Mzee Said kama ifuatavyo. Kwa vile swali lake linadhania mambo kadha wa kadha naomba niainieshe mambo ambayo ni ya msingi na ya tofauti baina yetu kuhusiana na maandishi yake (points of contention)
a. Ulichoandika wewe kwanza siyo historia; ni histohisia. Umetumia matukio ya historia kuelezea hisia zako. Sasa kila mwanadamu ana hisia zake na hivyo hakuna mtu mwingine anayeweza kuwaangalia watu wale wale wa kihistoria (historical figures) na akatoa tafsiri ile ile hasa kama kuna tofauti kubwa ya hisia baina ya watu.
b. Kwa vile hukufuata kanuni za uandishi wa kihistoria (historical method) basi uandishi wako wa aina ya simulizi, vijembe, na kukisia hauwezi kuandikwa na mtu mwingine yeyote. Ukisoma John Illife aliyeandika kwa kufuata kanuni za historia na uandishi wako wewe tofauti ni kama bahari na mlima. Yeye aliandika kitabu cha historia kweli kweli.
c. Kwa vile umeamua kutumia dini kuangalia historia na kuilezea ni wazikuwa mtu mwingine asiyetumia dini anaweza kuangalia matkio yale yale unaoyaona wewe na akayapa tafsiri nyingine kabisa. Mimi niliposoma kitabu chako cha Sykes kwa kweli nilivutiwa na masimulizi ya majina ya watu mbalimbali. Lakini sikuvutiwa kabisa na ushawishi wa hoja. Katika kujenga hoja kwa kweli una udhaifu mkubwa mno kwani badala ya kutumia reason kujenga hoja unatumia 'emotional appeal' na ndio maana umewapata wengi kwa kugusa dini, imani yao.
d. Kwa vile matukio mengi unayoyasimulia yanatokana na yale unayodai ni mang'amuzi yako binafsi (personal experience) au ya kuambiwa (hearsay) na hivyo vyanzo unavyotumia haviwezi kuhojiwa na wanataaluma wengine ni wazi kuwa hicho unachodai ni historia kitabakia cha kwako peke yako. NInaamini udhaifu wako mkubwa kabisa katika uandishi wako ni hili - the failure to make it possible for other scholars to access the sources you claim to have used to get some information - for either these sources are dead, hidden or exclusively known to you.
Kutokana na hayo basi ni vigumu na haiwezekani mtu mwingine kuandika kuhusu wazee wako namna hiyo. Hata hivyo, inawezekana kabisa mtu kuandika historia ya Tanganyika kwa umakini mkubwa na kutaja baadhi ya majina uliyonayo vizuri zaidi.
Pamoja na hayo ni ukweli pia kuwa umejitahidi kuweka kumbukumbu ya wazee wako na kuyaacha majina yao yatajwe katika historia. Haya ni mafanikio yako makubwa - hata kama ndani yake umeweka limau, pilipili, mdalasini, tangawizi na pilipili manga.
0