Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hakuna jina la Ramadhani Ali katika waasisi wa AA 1929.
Huenda umechanganya majina.

Unaweza kupitia vitabu na paper za John Iliffe kuhusu AA
kujiridhisha.

Cecil Matola ni muasisi wa AA.
Makamu rais wa kwanza wa AA aliitwa nani?
 

Naona umeamia Nigeria...fungua nyuzi tuwajadili marais wa Nigeria kina.

Umunnakwe Aguiyi Ironsi, Abubakar Tawafa Balewa, John Thomas, Murtala Ramat, Shehu Usman Shagari, Ibrahim Babangida, Mohammadu Buhari na wengine.

Unachotakiwa sasa hivi kufanya ni kuthibitisha uchochozi wa Mohamed Said.
 

The beareved begins the wailling latter others join.
 

G,

Wanaukumbi inaelekea tumechoka na dalili ni hii lugha kali.
Mnasemaje kuhusu kulikunja jamvi?
 
Ok! Matola alifariki mara 2! mwaka 1939 kwa mujibu wa Mohamed siku za nyuma na sasa 1933. Anyway hilo si tatizo sana tuendelee

Kwahiyo Mohamed, Cecil Matola hakuwahi kuwa na wadhifa AA kama Mag3 anavyosema?
 
G,

Wanaukumbi inaelekea tumechoka na dalili ni hii lugha kali.
Mnasemaje kuhusu kulikunja jamvi?
Hapana, Mohamed penye wengi pana mengi. Hata wewe page 2 zilizopita umetoka povu hasa baada ya kuona mjadala unaelekea katika Ugaidi.

Mbona kuna mengi ya kujadili, mathalani matokeo ya mitihani, Mauaji ya mapadre na tindikali kwa masheikh, DVD za Ilunga na zako zinaoonyeshwa kwa majenereata vijijini na kadha wa kadha. Bado Mzee Mwekapopo tuendelee na tuvumiliane maana tukiacha njiani tutakuwa hatujaitendea jamii ya JF haki.

Kila jiwe ligeuzwe ili tukianza uzi mwingine hilo liwe tofauti. Usikimbie Mzee Muyukwa
 
Mohamed yanini kubishana? Mimi nakueleza kwa AA ni kikundi/chama kilichoanzishwa na Sir Cameron kwa lengo lakuwajengea weusi chombo chao cha kuratibu mambo ya furaha zao, kwa lugha nyepesi tunaweza kusema kilikuwa kikundi cha walevi,
Kiongozi wao (rais) alikuwa Matola. Hilo halihitaji mjadala, Klest alikuwa chini ya Matola hivyo Matola kwakuweka uafrika wetu mbele ndie muasisi wa AA tangu mwaka 1929 mpaka alipofariki 23/02/1933

Hapo hatamu za AA ndipo zikashikwa na Klest Sykes na kupoka sifa nyingi za uasisi wa AA kuwa zake.

Lakini ukweli tukisimama bila kujali rangi zetu ama ukoloni, basi mwasisi halisi wa AA ni Sir Cameron mkristu na kafiri wa kiingereza.
 
G,

Wanaukumbi inaelekea tumechoka na dalili ni hii lugha kali.
Mnasemaje kuhusu kulikunja jamvi?

Unaweza kuwaita zima moto kwa ajali ya maji ya moto?

Acha woga na uvivu mkuu wangu, mjadala huu bado mbichi sana, kumbuka matokeo kidato cha nne yametoka, mauaji ya padre zanzibar na uchomaji moto kanisa leo hii,

Hayo yote asili yake ni wewe na wenzio
 

Nguruvi3,

Nadhani hilo neno ''usikimbie'' ni pambo katika kuzungumza kwako.
Hukusudii kuniambia mimi kuwa nakimbia.

Nani hapa wakunikimbiza mimi?
Kwa hakika simuoni.

Hayo majina yote unayonipa ni ya watangulizi wangu lakini unaonekana
umeyapenda sana.

Ingawa inaweza kuwa ni ''sacarsm.''

Nimetaka tukunje jamvi nilipoona matusi.

Mimi siogopi hiyo nembo ya ''ugaidi.''
Ningeliogopa nisingetoa ofa ya uzi makhsusi tujadili.

Ngoja nikupe kitu.

Baada ya kukamatwa uwanja wa ndege kumbe pasi yangu ilikuwa imewekewa
alama maalum ya utambulisho.

Popote nitakapoitoa hiyo pasi maofisa wa uhamiaji wanaona ile alama katika
computer zao na wanajua mimi ni mtu wa ''hadhi'' gani.

Baada ya kukamatwa nilisafiri tena na nilipotoa pasi yangu kwa ofisa wa uhamiaji
''he was a bit fascinated with what he saw he had to call a colleague to share
what he had just seen.''

Sasa wakawa wananitazama huku wanacheka.

Nilipowauliza nini kinawachekesha katika pasi yangu wakasema hakuna kitu
wakaigonga nikaendelea na safari.

Hapo ndipo nikajua pasi yangu imewekewa kitu makhususi cha kunitambulisha.

Niko Schipol Amsterdam nishafanya secuity check zote nangoja kuingia katika ndege
inakwenda Detroit Marekani niko katika mstari.

Nikachopolewa kutoka kwenye mstari mimi peke yangu nikawekwa pembeni kwa mahojiano
zaidi.

Huyo askari ana mabastola na kila kitu na nywele zake ni ''crew cut'' nikajua huyu US Army
Marine Corp.

Kuingia Marekani mambo yakawa ni hayo hayo tena na zaidi.
Pasi ilipelekwa mwenye ofisi nyingine kwa uchunguzi zaidi na hii baada ya mahojiano makali...

Nimesimama mstarini kama nusu saa nasubiri.
Nikahofu huenda nikarudishwa Tanzania.

Niko New York nimetia kadi yangu kwenye ATM ya Chase Bank.
Imekataa kusoma chochote...

Kumbe yote hiyo ni security check kutokana na historia yangu...
Siku ya pili ndiyo kadi ikasoma na kutoa fedha.

Walikuwa tayari nishakuwa-cleared...

To me I find all this very amusing.
Wala sitokwi povu na haya yote ila yanazidi kuremba shajara (diary) yangu.

Jana nilitokwa povu kwa kuwa BD alikuwa anacheza shere na marehemu.
Sikuwezi kustahamili upuuzi kama ule.

Na nikasema huo ni upuuzi.

Kwa hiyo hayo mambo ya ugaidi nimeyazoea na ninajua kikitokea nini nifanye nini.

Waamerika ni rafiki zangu.
Humtishi mtu kwa kumsakazia rafiki yake.

BD kaona yeye atanitisha kunambia kuwa natafutwa na CIA/FBI Usalama wa Taifa.
Ndipo nikamjibu wakatafutwa sie mie mimi maarufu sitafutwi.

Najulikana sana.

Hata jiwe linajua nyumba yangu ilipo.
 

Wewe Yericko,

Mimi wewe nimekuwia radhi.
Ikiwa maana hii hujaifahamu muombe Zomba atakufahamisha.
 
Ok! Matola alifariki mara 2! mwaka 1939 kwa mujibu wa Mohamed siku za nyuma na sasa 1933. Anyway hilo si tatizo sana tuendelee

Kwahiyo Mohamed, Cecil Matola hakuwahi kuwa na wadhifa AA kama Mag3 anavyosema?

Nguruvi,

Usiwe hivi utanichosha.

Mimi najua fika ni mwaka gani Matola kafa ni 1933
ikiwa niliandika 1939 itakuwa nimekosea.

Matola kwa hakika si chochote katika siasa za AA
kiasi hata Iliffe hakumtia katika ile project ya kitabu
iliyokuja kuzaa Modern Tanzanians.

Mle katika kitabu yuko:

  1. Kleist Sykes
  2. Martin Kayamba
  3. Columbus Msigala
  4. Hassan Suleiman
  5. Juma Ponda
  6. Na wengineo

Tusonge mbele.
 
Wewe Yericko,

Mimi wewe nimekuwia radhi.
Ikiwa maana hii hujaifahamu muombe Zomba atakufahamisha.

Haya mkuu, twendelee na mjadala wa uasisi wa AA kati ya Sir Cameron, Cecil Matola na Klest Sykes

Unakubaliana na hoja yangu ya awali? Lete sababu
 
Maswali ya kipuuzi kama haya hakuna muda wa kuyajibu peleka kwa wajinga wenzako.

Hata wewe ni mpuuzi achilia mbali maswali ya kipuuzi unayouliza hapa na kudakia maswali ya Mzee Mohamed alaf huna unachojua
 

Dah sidhani kama haya maneno yanaweza kuwa ni ushahidi ambao ni tangible...
 
Mzee Mohamed unabusara sana ningependa hizi busara zako utumie kuwaweka watu wa madhehebu yote pamoja bila mifarakano,tunaihitaji sana amani ya Tanzania yetu
 
Hata wewe ni mpuuzi achilia mbali maswali ya kipuuzi unayouliza hapa na kudakia maswali ya Mzee Mohamed alaf huna unachojua

Multiple ID's at work...ha haa haaa haaaa! Njoo na ID yako ya kawaida unaangaika bure masikini mpaka unatia huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…