Hapana, Mohamed penye wengi pana mengi. Hata wewe page 2 zilizopita umetoka povu hasa baada ya kuona mjadala unaelekea katika Ugaidi.
Mbona kuna mengi ya kujadili, mathalani matokeo ya mitihani, Mauaji ya mapadre na tindikali kwa masheikh, DVD za Ilunga na zako zinaoonyeshwa kwa majenereata vijijini na kadha wa kadha. Bado Mzee Mwekapopo tuendelee na tuvumiliane maana tukiacha njiani tutakuwa hatujaitendea jamii ya JF haki.
Kila jiwe ligeuzwe ili tukianza uzi mwingine hilo liwe tofauti. Usikimbie Mzee Muyukwa
Nguruvi3,
Nadhani hilo neno ''usikimbie'' ni pambo katika kuzungumza kwako.
Hukusudii kuniambia mimi kuwa nakimbia.
Nani hapa wakunikimbiza mimi?
Kwa hakika simuoni.
Hayo majina yote unayonipa ni ya watangulizi wangu lakini unaonekana
umeyapenda sana.
Ingawa inaweza kuwa ni ''sacarsm.''
Nimetaka tukunje jamvi nilipoona matusi.
Mimi siogopi hiyo nembo ya ''ugaidi.''
Ningeliogopa nisingetoa ofa ya uzi makhsusi tujadili.
Ngoja nikupe kitu.
Baada ya kukamatwa uwanja wa ndege kumbe pasi yangu ilikuwa imewekewa
alama maalum ya utambulisho.
Popote nitakapoitoa hiyo pasi maofisa wa uhamiaji wanaona ile alama katika
computer zao na wanajua mimi ni mtu wa ''hadhi'' gani.
Baada ya kukamatwa nilisafiri tena na nilipotoa pasi yangu kwa ofisa wa uhamiaji
''he was a bit fascinated with what he saw he had to call a colleague to share
what he had just seen.''
Sasa wakawa wananitazama huku wanacheka.
Nilipowauliza nini kinawachekesha katika pasi yangu wakasema hakuna kitu
wakaigonga nikaendelea na safari.
Hapo ndipo nikajua pasi yangu imewekewa kitu makhususi cha kunitambulisha.
Niko Schipol Amsterdam nishafanya secuity check zote nangoja kuingia katika ndege
inakwenda Detroit Marekani niko katika mstari.
Nikachopolewa kutoka kwenye mstari mimi peke yangu nikawekwa pembeni kwa mahojiano
zaidi.
Huyo askari ana mabastola na kila kitu na nywele zake ni ''crew cut'' nikajua huyu US Army
Marine Corp.
Kuingia Marekani mambo yakawa ni hayo hayo tena na zaidi.
Pasi ilipelekwa mwenye ofisi nyingine kwa uchunguzi zaidi na hii baada ya mahojiano makali...
Nimesimama mstarini kama nusu saa nasubiri.
Nikahofu huenda nikarudishwa Tanzania.
Niko New York nimetia kadi yangu kwenye ATM ya Chase Bank.
Imekataa kusoma chochote...
Kumbe yote hiyo ni security check kutokana na historia yangu...
Siku ya pili ndiyo kadi ikasoma na kutoa fedha.
Walikuwa tayari nishakuwa-cleared...
To me I find all this very amusing.
Wala sitokwi povu na haya yote ila yanazidi kuremba shajara (diary) yangu.
Jana nilitokwa povu kwa kuwa BD alikuwa anacheza shere na marehemu.
Sikuwezi kustahamili upuuzi kama ule.
Na nikasema huo ni upuuzi.
Kwa hiyo hayo mambo ya ugaidi nimeyazoea na ninajua kikitokea nini nifanye nini.
Waamerika ni rafiki zangu.
Humtishi mtu kwa kumsakazia rafiki yake.
BD kaona yeye atanitisha kunambia kuwa natafutwa na CIA/FBI Usalama wa Taifa.
Ndipo nikamjibu wakatafutwa sie mie mimi maarufu sitafutwi.
Najulikana sana.
Hata jiwe linajua nyumba yangu ilipo.