Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hakuna jina la Ramadhani Ali katika waasisi wa AA 1929.
Huenda umechanganya majina.

Unaweza kupitia vitabu na paper za John Iliffe kuhusu AA
kujiridhisha.

Cecil Matola ni muasisi wa AA.
Makamu rais wa kwanza wa AA aliitwa nani?
 
Hebu tumwangalie kiongozi huyu aliyezaliwa kwenye ukristu na aliyehudumu kwa mafanikio ndani ya ardhi ya mfumo islamu,

Matthew Olusegun Aremu Obasanjo 5 Machi 1937) ni jenerali mstaafu wa Jeshi la Nigeria aliyekuwa rais wa Nigeria mara mbili. Awamu yake ya kwanza ilikuwa kama rais wa kijeshi kati ya 1976 hadi 1979 halafu awamu la pili kama rais aliyechaguliwa na wananchi kati ya 1999 hadi 2007.

Obasanjo alizaliwa katika kabila la Wayoruba akalelewa kama Mkristo wa kibaptisti. 1958 akajiunga na jeshi akapanda ngazi haraka. 1967-1970 alishiriki katika vita dhidi ya Biafra. Baada ya uasi wa jeshi chini ya Murtala Mohammed mwaka 1975 alipewa cheo cha makamu wa rais. 1976 Mohammed aliuawa na wapinzani ndani ya jeshi waliokosa kumwua Obasanjo pia. Obansajo aliweza kukandamiza uasi akateuliwa na halmashauri ya kijeshi kuwa raisi mpya. Alitumia nafasi yake kuandaa uchaguzi wa 1979 akakabidhi madaraka kwa rais aliyechaguliwa Shehu Shagari.

Kati ya 1980 hadi 1995 alikuwa na vyeo mbalimbali vya kimataifa akagombea nafasi ya Katibu Mkuu wa UM halafu alikuwa mwenyekiti wa halmashari ya Transparency International (TI). Dikteta wa kijeshi Sani Abacha alimfunga gerezani kati ya 1995 hadi 1998.

Wakati wa uchaguzi baada ya kifo cha Abacha aligombea uraisi kama mgombea wa chama cha People's Democratic Party akashinda akawa rais tena tangu 1999. Mwaka 2003 alirudishwa madarakani.

Obasanjo alijaribu kubadilisha katiba ili aweze kuwa na nafasi ya tatu lakini hakufaulu kupata wabunge wa kutosha kwa kubadilisha katiba.

Katika kura ya 2007 alisimama upande wa mgombea Umaru Yar'Adua aliyechaguliwa. Kukabidhi kwa madaraka kutoka Obasanjo kwenda Yar'Adua kulikuwa mara ya kwanza katika historia ya Nigeria ya kwamba marais wawili waliochaguliwa na wananchi waliweza kufuatana.

Vuta picha kiongozi huyu aliyezaliwa na kulelewa katika mafundisho ya kikristu anachaguliwa kuwa rais wa nchi inayoaminika kuwa ni ya mfumoislam kaskazini magharibi mwa afrika.

Wale waislamu wa Nigeria wanamtazamo gani juu ya utawala wa nchi?

Naona umeamia Nigeria...fungua nyuzi tuwajadili marais wa Nigeria kina.

Umunnakwe Aguiyi Ironsi, Abubakar Tawafa Balewa, John Thomas, Murtala Ramat, Shehu Usman Shagari, Ibrahim Babangida, Mohammadu Buhari na wengine.

Unachotakiwa sasa hivi kufanya ni kuthibitisha uchochozi wa Mohamed Said.
 
Mkuu Zumbemkuu, hivi vijamaa ni vipuuzi kwelikweli, havina hoja yao zaidi ya kushinda hapa jukwaani vikipika majungu na kelele zisizo na maana kama vyura! na kwa ujinga wao vinaamini watu wanakubaliana navyo! kweli kuwa mjinga ni ajali lakini kuwa mpumbavu kama hivi vijamaa ni maafa.

The beareved begins the wailling latter others join.
 
Mkuu Zumbemkuu, hivi vijamaa ni vipuuzi kwelikweli, havina hoja yao zaidi ya kushinda hapa jukwaani vikipika majungu na kelele zisizo na maana kama vyura! na kwa ujinga wao vinaamini watu wanakubaliana navyo! kweli kuwa mjinga ni ajali lakini kuwa mpumbavu kama hivi vijamaa ni maafa.

G,

Wanaukumbi inaelekea tumechoka na dalili ni hii lugha kali.
Mnasemaje kuhusu kulikunja jamvi?
 
Nimeeleza huko nyuma kuwa hakuna jina la Ramadhani Ali katika waasisi wa AA 1929.
Huenda wamechanganya majina.

Wanaweza kupitia vitabu na paper za John Iliffe kuhusu AA kujiridhisha ikiwa watapenda.

Cecil Matola kuwa ni muasisi mkuu wa AA hapana.

Kleist Sykes alitawala historia ya Dar es Salaam katika miaka ile hadi 1949 alipofariki
kwa sababu ya mambo mengi kubwa likuwa elimu yake na uwezo wake wa fedha.

Unaweza kusoma maisha ya Kleist katika ''Modern Tanzanians'' Iliffe (Ed) ''Kleist Sykes The
Townsman'' na katika kitabu changu ''Kleist Sykes Man of Ideas.''

Kubwa zaidi ni kuwa Iliffe alitumia nyaraka za Kleist Sykes katika kutafiti historia ya AA.
Kabla hajafa Kleist aliandika maisha yake na nyaraka hii imehifadhiwa hadi leo.

Hakuna anaejua habari za Matola ila chache tu na kuwa alifariki 1933 Mzee Bin Sudi akachukua
nafasi ya rais wa AA.

Hakuna mengi ambayo unaweza kuyapata kuhusu mchango wake katika siasa za Dar es Salaam.
Ok! Matola alifariki mara 2! mwaka 1939 kwa mujibu wa Mohamed siku za nyuma na sasa 1933. Anyway hilo si tatizo sana tuendelee

Kwahiyo Mohamed, Cecil Matola hakuwahi kuwa na wadhifa AA kama Mag3 anavyosema?
 
G,

Wanaukumbi inaelekea tumechoka na dalili ni hii lugha kali.
Mnasemaje kuhusu kulikunja jamvi?
Hapana, Mohamed penye wengi pana mengi. Hata wewe page 2 zilizopita umetoka povu hasa baada ya kuona mjadala unaelekea katika Ugaidi.

Mbona kuna mengi ya kujadili, mathalani matokeo ya mitihani, Mauaji ya mapadre na tindikali kwa masheikh, DVD za Ilunga na zako zinaoonyeshwa kwa majenereata vijijini na kadha wa kadha. Bado Mzee Mwekapopo tuendelee na tuvumiliane maana tukiacha njiani tutakuwa hatujaitendea jamii ya JF haki.

Kila jiwe ligeuzwe ili tukianza uzi mwingine hilo liwe tofauti. Usikimbie Mzee Muyukwa
 
Mohamed yanini kubishana? Mimi nakueleza kwa AA ni kikundi/chama kilichoanzishwa na Sir Cameron kwa lengo lakuwajengea weusi chombo chao cha kuratibu mambo ya furaha zao, kwa lugha nyepesi tunaweza kusema kilikuwa kikundi cha walevi,
Kiongozi wao (rais) alikuwa Matola. Hilo halihitaji mjadala, Klest alikuwa chini ya Matola hivyo Matola kwakuweka uafrika wetu mbele ndie muasisi wa AA tangu mwaka 1929 mpaka alipofariki 23/02/1933

Hapo hatamu za AA ndipo zikashikwa na Klest Sykes na kupoka sifa nyingi za uasisi wa AA kuwa zake.

Lakini ukweli tukisimama bila kujali rangi zetu ama ukoloni, basi mwasisi halisi wa AA ni Sir Cameron mkristu na kafiri wa kiingereza.
 
G,

Wanaukumbi inaelekea tumechoka na dalili ni hii lugha kali.
Mnasemaje kuhusu kulikunja jamvi?

Unaweza kuwaita zima moto kwa ajali ya maji ya moto?

Acha woga na uvivu mkuu wangu, mjadala huu bado mbichi sana, kumbuka matokeo kidato cha nne yametoka, mauaji ya padre zanzibar na uchomaji moto kanisa leo hii,

Hayo yote asili yake ni wewe na wenzio
 
Hapana, Mohamed penye wengi pana mengi. Hata wewe page 2 zilizopita umetoka povu hasa baada ya kuona mjadala unaelekea katika Ugaidi.

Mbona kuna mengi ya kujadili, mathalani matokeo ya mitihani, Mauaji ya mapadre na tindikali kwa masheikh, DVD za Ilunga na zako zinaoonyeshwa kwa majenereata vijijini na kadha wa kadha. Bado Mzee Mwekapopo tuendelee na tuvumiliane maana tukiacha njiani tutakuwa hatujaitendea jamii ya JF haki.

Kila jiwe ligeuzwe ili tukianza uzi mwingine hilo liwe tofauti. Usikimbie Mzee Muyukwa

Nguruvi3,

Nadhani hilo neno ''usikimbie'' ni pambo katika kuzungumza kwako.
Hukusudii kuniambia mimi kuwa nakimbia.

Nani hapa wakunikimbiza mimi?
Kwa hakika simuoni.

Hayo majina yote unayonipa ni ya watangulizi wangu lakini unaonekana
umeyapenda sana.

Ingawa inaweza kuwa ni ''sacarsm.''

Nimetaka tukunje jamvi nilipoona matusi.

Mimi siogopi hiyo nembo ya ''ugaidi.''
Ningeliogopa nisingetoa ofa ya uzi makhsusi tujadili.

Ngoja nikupe kitu.

Baada ya kukamatwa uwanja wa ndege kumbe pasi yangu ilikuwa imewekewa
alama maalum ya utambulisho.

Popote nitakapoitoa hiyo pasi maofisa wa uhamiaji wanaona ile alama katika
computer zao na wanajua mimi ni mtu wa ''hadhi'' gani.

Baada ya kukamatwa nilisafiri tena na nilipotoa pasi yangu kwa ofisa wa uhamiaji
''he was a bit fascinated with what he saw he had to call a colleague to share
what he had just seen.''

Sasa wakawa wananitazama huku wanacheka.

Nilipowauliza nini kinawachekesha katika pasi yangu wakasema hakuna kitu
wakaigonga nikaendelea na safari.

Hapo ndipo nikajua pasi yangu imewekewa kitu makhususi cha kunitambulisha.

Niko Schipol Amsterdam nishafanya secuity check zote nangoja kuingia katika ndege
inakwenda Detroit Marekani niko katika mstari.

Nikachopolewa kutoka kwenye mstari mimi peke yangu nikawekwa pembeni kwa mahojiano
zaidi.

Huyo askari ana mabastola na kila kitu na nywele zake ni ''crew cut'' nikajua huyu US Army
Marine Corp.

Kuingia Marekani mambo yakawa ni hayo hayo tena na zaidi.
Pasi ilipelekwa mwenye ofisi nyingine kwa uchunguzi zaidi na hii baada ya mahojiano makali...

Nimesimama mstarini kama nusu saa nasubiri.
Nikahofu huenda nikarudishwa Tanzania.

Niko New York nimetia kadi yangu kwenye ATM ya Chase Bank.
Imekataa kusoma chochote...

Kumbe yote hiyo ni security check kutokana na historia yangu...
Siku ya pili ndiyo kadi ikasoma na kutoa fedha.

Walikuwa tayari nishakuwa-cleared...

To me I find all this very amusing.
Wala sitokwi povu na haya yote ila yanazidi kuremba shajara (diary) yangu.

Jana nilitokwa povu kwa kuwa BD alikuwa anacheza shere na marehemu.
Sikuwezi kustahamili upuuzi kama ule.

Na nikasema huo ni upuuzi.

Kwa hiyo hayo mambo ya ugaidi nimeyazoea na ninajua kikitokea nini nifanye nini.

Waamerika ni rafiki zangu.
Humtishi mtu kwa kumsakazia rafiki yake.

BD kaona yeye atanitisha kunambia kuwa natafutwa na CIA/FBI Usalama wa Taifa.
Ndipo nikamjibu wakatafutwa sie mie mimi maarufu sitafutwi.

Najulikana sana.

Hata jiwe linajua nyumba yangu ilipo.
 
Unaweza kuwaita zima moto kwa ajali ya maji ya moto?

Acha woga na uvivu mkuu wangu, mjadala huu bado mbichi sana, kumbuka matokeo kidato cha nne yametoka, mauaji ya padre zanzibar na uchomaji moto kanisa leo hii,

Hayo yote asili yake ni wewe na wenzio

Wewe Yericko,

Mimi wewe nimekuwia radhi.
Ikiwa maana hii hujaifahamu muombe Zomba atakufahamisha.
 
Ok! Matola alifariki mara 2! mwaka 1939 kwa mujibu wa Mohamed siku za nyuma na sasa 1933. Anyway hilo si tatizo sana tuendelee

Kwahiyo Mohamed, Cecil Matola hakuwahi kuwa na wadhifa AA kama Mag3 anavyosema?

Nguruvi,

Usiwe hivi utanichosha.

Mimi najua fika ni mwaka gani Matola kafa ni 1933
ikiwa niliandika 1939 itakuwa nimekosea.

Matola kwa hakika si chochote katika siasa za AA
kiasi hata Iliffe hakumtia katika ile project ya kitabu
iliyokuja kuzaa Modern Tanzanians.

Mle katika kitabu yuko:

  1. Kleist Sykes
  2. Martin Kayamba
  3. Columbus Msigala
  4. Hassan Suleiman
  5. Juma Ponda
  6. Na wengineo

Tusonge mbele.
 
Wewe Yericko,

Mimi wewe nimekuwia radhi.
Ikiwa maana hii hujaifahamu muombe Zomba atakufahamisha.

Haya mkuu, twendelee na mjadala wa uasisi wa AA kati ya Sir Cameron, Cecil Matola na Klest Sykes

Unakubaliana na hoja yangu ya awali? Lete sababu
 
Maswali ya kipuuzi kama haya hakuna muda wa kuyajibu peleka kwa wajinga wenzako.

Hata wewe ni mpuuzi achilia mbali maswali ya kipuuzi unayouliza hapa na kudakia maswali ya Mzee Mohamed alaf huna unachojua
 
ngoja nichangie hapa kidogo
naona hapa ni tatizo la kumezeshwa maneno
na bila kufanya utafiti,hili lipo kwa watanzania wengi
sakata hili aliyelisema wa kwanza ni slaa wakati wa kampeni 2010
kwamba kuna makontena yameingizwa yakiwa na karatasi za kupigia kura
uchunguzi ulipofanyika ikabainika taarifa iliyotolewa si sahihi
kwanini nimeamua kuweka sawa taarifa hii?
sababu makontena hayo hayakuwa na karatasi za kupigia kura,
bali vipodozi.Muingizaji wa vipodozi hivyo,namjua vizuri sana
na ni mtu wa karibu yangu mno.Familia zetu ni ndugu,
na hata alipotakiwa kuonesha documents zinazothibitisha
uhalali wa umiliki na uingizaji wa vipodozi hivyo tulikuwa pamoja
samahani kwa kuwatoa ktk mada husika

Dah sidhani kama haya maneno yanaweza kuwa ni ushahidi ambao ni tangible...
 
Mzee Mohamed unabusara sana ningependa hizi busara zako utumie kuwaweka watu wa madhehebu yote pamoja bila mifarakano,tunaihitaji sana amani ya Tanzania yetu
 
Hata wewe ni mpuuzi achilia mbali maswali ya kipuuzi unayouliza hapa na kudakia maswali ya Mzee Mohamed alaf huna unachojua

Multiple ID's at work...ha haa haaa haaaa! Njoo na ID yako ya kawaida unaangaika bure masikini mpaka unatia huruma.
 
Back
Top Bottom