Umeeleza hivyo kwa sababu kuu mbili tatu...kwanza Ramadhani Ali hakuwa uzao wa Wazulu, pili hakuwa Manyema na tatu alikuwa Mtanganyika. Wazulu na Manyema ni makabila mawili ambayo yalitumika sana kama vikaragosi vya Wajerumani katika kuwakandamiza na kuwapiga vita Watanganyika. Tukiacha uhusiano wao kupitia Wajerumani waliowaleta kutoka Congo na Msumbiji, huo uhusiano ulijengeka zaidi kupitia kuoleana...sharti la kwanza kwa
mkristo Mzulu kumwoa
Manyema Muislaam ilikuwa ni kukubali kubadili dini.
Ramadhani Ali alikuwa ni Mtanganyika, mzaramo na hila zimefanyika kutolihusisha jina lake kama ilivyofanyika kulificha jina la Mtanganyika mwingine
Cecil Matola, Myao ambaye ndiye alikuwa Raisi Muasisi wa
AA katibu wake akiwa mzulu Kleist Sykes Plantan mwaka
1929.
Hapa chini nanukuu tu sehemu ya kitabu
A Modern History of Tanganyika kilichoandikwa na
John Iliffe anayependa sana kumwekea mdomoni mambo ya kughushi anayoweza kuyatunga tu mchochezi wa aina yake. Nimemuuliza maswali mengi sana
Mohamed Said humu ndani lakini kwa kujua ataumbuka ameshindwa kuyajibu...hiyo ndio ikawa salama yake, alijua akiyajibu amejitia kitanzi shingoni.
Kabla sijaendelea na upuuzi mwingine unaoitwa eti historia ya Tanganyika kama anavyodai
Mohamed Said, nitawaomba wasomaji mtafakari tu kidogo imekuwaje huyu mzulu
Kleist Sykes akatawala historia ya Dar es Salaam katika miaka ile hadi 1949 alipofariki eti kwa sababu ya mambo mengi kubwa likuwa
elimu yake na uwezo wake wa fedha.(sic!)
Je Dar es Salaamwakati huo haikuwa na Watanganyika, wasomi, wenye uwezo wa kifedha hadi aje ex-askari wa Kijerumani kutoka Msumbiji? Kwa nini Sykes?...AA alianzisha Sykes na si
Cecil Matola, TAA alianzisha Sykes na si
Dr. Kyaruzi na hata TANU alianzisha Sykes na si
Mwalimu Nyerere? Leo Mohamed Said anamkana makamu Raisi wa AA
Ramadhani Ali, sababu? Alikuwa mzaramo. Yaani Sykes wanapokezana kama vile hakuna Watanganyika, duh!
Karibuni
Mzee Mwanakijiji,
Nguruvi3,
Ngongo,
Ritz,
zomba,
sweke na
Watanzania wote wanaolitakia mema taifa letu. Tutaendelea...