Jasusi,
Hoja ya Wapagani huletwa kama counter weight dhidi ya Waislam.
Sisi hupuuza.
Tunajua hali ya mambo itakapotakata itakuwa ni hoja zetu na serikali
na labda na kanisa.
Jasusi nadhani Mohamed anachukulia neno upagani kama watu wasio na majina ya kuagiza(imported names). Hili tu kwa kuanzia ni kosa kwasababu hakuna mahali katika vitabu vyote vitakatifu imeelezwa kuwa mtu hakamiliki katika imani ila kwa jina lake. Big confusion across the isle.
In other words ukiitwa Nyachai kamruge wewe hata uwe mcha mungu kiasi gani ufalme na utukufu wa mwenyezi hutauona!
colonial mentality across the board.
Kwakweli huwa natofautiana sana na ahli wangu Baru baru kwa mitazamo lakini kuna jambo moja muhimu sana ameliongea na naomba watu walielewe.
'Baru baru kasema hivi ''kila mtu anaweza kuwa mwislam lakini si kila mwislam ni muumini'' akendelea kusema kuwa muumini wa kiislam ni lazima awe mwislam na si kinyume chake.
Hapa ndipo Mohamed anapochanganya kama si kukanganyikiwa. Ni ukweli usiohitaji kificho kuwa katika miaka hiyo na hata sasa hivi statistic zinaonyesha kuwa watu wengi wa imani zote ni washirikina licha ya majina yao.Shiriki inamuondoa mja katika uumini.
Kwa maneno mengine wote katika dini wanaweza kuwa wakristo au waislam lakini si kila mtu ni muumini wa dini hizo.
Kwanini Bagamoyo iwe maarufu kama wote ni waumini?
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa tukiangalia kwa undani na weledi Mohamed hana ground ya kuorodhesha majina na kusema hawa ni waislam au wale ni wakristo. Kwa mtazamo huo Wapagani ''pagans'' na wasioamini ''atheist'' wapo katika jamii yetu significantly.
Anachojaribu kukifanya ni kuleta simba na Yanga kama mliovyoona sakata la Mwembechai ambapo amejitahidi hadi neno kanisa likaingia hata kama vurugu zile zilizoanzia kwa maandamano kutoka msikiti wa kichangani kupitia Morogoro road hadi Kagera hazikugusa kanisa hata moja.
Anachosahau Mohamed ni kuwa Malecela na Mrema aliowachomeka katika nukuu ya ngano yake inamshtaki leo na sasa hivi.
Vipi vurugu za mbagala na Chang'ombe! Kikwete anahusika! Said Mwema anahusika!Kova nae! Othman Chande je.
Ndio maana siku zote nasema hii strategy ya shoot any moving object eventually it ends up with friendly fire.
Not only friendly fire but adulterate and waterdown every single line and phrase of the infamous ngano.