Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sasa wewe unelewaa kusoma lakini au ili mradi upinge tu? Mohamed Said kanukuu maandiko ya Sivalon, sasa muulize Sivalon. Au huelewi kilichoandikwa?

Alivyoniwekea lile bandiko ni dhahiri alikuwa anakubaliana na Sivalion sasa si vibaya yeye pia kunipa ufafanuzi au wewe unaonaje?
 
Last edited by a moderator:

Channel Ten na ITV walionyesha video hiyo kwa wale waliokuwa Dar es Salaam waliona hiyo video ITV kabla ya kurusha hewani waliomba msamaha kwa hizo picha ilikuwa kama tukio la kulenga shabaha. Baadae walikatazwa na serikali kuonyesha hilo tukio.
 
Mwandishi alitarajia Nyerere afanye nini na Waislamu baada ya Uhuru kulinganisha na Watanganyika wengine?
Angalau angetekeleza yale aliyoyasema katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakati Tanganyika inakua jamuhuri.
Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislamu na Wakristo. Alsiema kama hivi.: "Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislamu, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa".
Badala yake
Kilichofuata baada ya kupatikana uhuru ilikuwa ni kukamatwa, kuwekwa kizuizini na kuhamishwa kwa masheikh na Waislamu wengine waliodhaniwa kuwa wanapinga utawala wa Nyerere. Mashuhuri miongoni mwao walikuwa: Abdillah Schneider Plantan, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Suleiman Masudi Mnonji, Ali Migeyo, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sharff Hussein Badawiy, Shariff Mwinyibaba, Shariff Adnan, Bilali Rehani Waikela, Sheikh Jumanne Bias, Maalim Matar, Abdalah Mwamba, Sheikh Hashim Haji Abdallah, Sheikh Nurdin Hussein, Salum Abdallah Popo, Sheikh Mzee Ali Comorian, Sheikh Al Amin Maftah, Rajab Kiguu cha Mbuzi na wengine wengi.
Hebu na wewe eleza unafurahia na kuunga mkono kipi Nyerere alichowafanyia waislamu baada ya uhuru.


 

Hawa Masheikh walidhalilishwa walifanyiwa unyama sana.
 
Umeeleza hivyo kwa sababu kuu mbili tatu...kwanza Ramadhani Ali hakuwa uzao wa Wazulu, pili hakuwa Manyema na tatu alikuwa Mtanganyika. Wazulu na Manyema ni makabila mawili ambayo yalitumika sana kama vikaragosi vya Wajerumani katika kuwakandamiza na kuwapiga vita Watanganyika. Tukiacha uhusiano wao kupitia Wajerumani waliowaleta kutoka Congo na Msumbiji, huo uhusiano ulijengeka zaidi kupitia kuoleana...sharti la kwanza kwa mkristo Mzulu kumwoa Manyema Muislaam ilikuwa ni kukubali kubadili dini.

Ramadhani Ali alikuwa ni Mtanganyika, mzaramo na hila zimefanyika kutolihusisha jina lake kama ilivyofanyika kulificha jina la Mtanganyika mwingine Cecil Matola, Myao ambaye ndiye alikuwa Raisi Muasisi wa AA katibu wake akiwa mzulu Kleist Sykes Plantan mwaka 1929.

Hapa chini nanukuu tu sehemu ya kitabu A Modern History of Tanganyika kilichoandikwa na John Iliffe anayependa sana kumwekea mdomoni mambo ya kughushi anayoweza kuyatunga tu mchochezi wa aina yake. Nimemuuliza maswali mengi sana Mohamed Said humu ndani lakini kwa kujua ataumbuka ameshindwa kuyajibu...hiyo ndio ikawa salama yake, alijua akiyajibu amejitia kitanzi shingoni.


Kabla sijaendelea na upuuzi mwingine unaoitwa eti historia ya Tanganyika kama anavyodai Mohamed Said, nitawaomba wasomaji mtafakari tu kidogo imekuwaje huyu mzulu Kleist Sykes akatawala historia ya Dar es Salaam katika miaka ile hadi 1949 alipofariki eti kwa sababu ya mambo mengi kubwa likuwa elimu yake na uwezo wake wa fedha.(sic!)

Je Dar es Salaamwakati huo haikuwa na Watanganyika, wasomi, wenye uwezo wa kifedha hadi aje ex-askari wa Kijerumani kutoka Msumbiji? Kwa nini Sykes?...AA alianzisha Sykes na si Cecil Matola, TAA alianzisha Sykes na si Dr. Kyaruzi na hata TANU alianzisha Sykes na si Mwalimu Nyerere? Leo Mohamed Said anamkana makamu Raisi wa AA Ramadhani Ali, sababu? Alikuwa mzaramo. Yaani Sykes wanapokezana kama vile hakuna Watanganyika, duh!

Karibuni Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Ngongo, Ritz, zomba, sweke na Watanzania wote wanaolitakia mema taifa letu. Tutaendelea...
 

Ahsante mzee M.S kwa kunilielewesha kwa undani sakata hilo na kulikumbuka neno "RUKSA"
 

Wewe ulisha mhukumu MS na kumuita Mchochezi na kila mahali umemuandika! sasa maswali ya nini tena? au ndio mtindo mpya wa kazi zenu za maafisa usalama! we ni mmoja wao bila shaka maana hata Katibu wako wa chama alishatangaza anapata ripoti toka kwa baadhi yenu!
 

Huyo Ramadhan Ali katajwa wapi?

oohh, na Nyerere ali kuwepo Burma kama Askari wa kukodiwa.

Aaah, na Matola, Kyaruzi na Nyerere sijui kwanini walikuwa wanawatafuta kina Sykes kila wanapoanzisha vyama? Au kina Sykes ndio walikuwa wasajili pekee wa vyama wakati huo? Mpaka Nyerere ikambidi akaishi kwa msajili wa vyama mtaa wa Stanley kabla hajaanzisha chama chake, au sio?
 
Hapa huwezi kumsikia Mzee Mwanakijiji, Mag3, nguruvi3, WildCard, wanachagia chochote hawa walikuwa wahuni.

Wewe unaanza kuyazungumzia haya leo; rudi nyuma kanisome... nyinyi mnaangalia waliuawa "Waislamu" wengine wetu tunaangalia waliuawa Watanzania na kwa hilo peke yake tulishasema Mkapa angepelekwa The Hague.. siyo kwa hilo la Mwembechhai tu bali pia la Pemba. Hatuangalii kama ni Mkatoliki au Mkristu... nyinyi angalieni dini ndio muamue kama mtatetea haki ya mtu au la...
 

Mag3,

Hakuna anayekupinga kinachotakiwa utufahamishe vizuri kuhusu Ramadhani All.

Hao unaowaita vikaragosi ndiyo wamempokea Nyerere pamoja na mke wake hebu msome Nyerere kwenye hayo maandishi ya blue.

Nyerere alipelekwa na Kasela Bantu kwa hao unawaita vikaragosi na wakampa hifadhi.
 
Last edited by a moderator:
Huyo Ramadhan Ali katajwa wapi?
zomba, huyo mchochezi angekuwa anajibu maswali, huu mjadala ungeisha zamani...kumbuka njia ya muongo ni fupi. Je unakiri kuwa Cecil Matola ndiye alikuwa Raisi muasisi wa AA mwaka 1929 na si Sykes ili tuweze kuendelea?

Namba nikukumbushe aliyowahi kuyasema ndugu yako FaizaFoxy;
zomba, hayo si maneno yangu, ni ya ndugu yako unayemsaliti leo kwa kumtetea huyu mzushi.
 
Last edited by a moderator:

Mkapa atapelekwaje The Hague wakati ni kipenzi cha unaemwamini K. Pengo
 

Na Nyerere kwa kumpoteza Hanga ashtakiwe wapi? Na wale maelfu kama si mamilioni waliokuwa wanahamishwa makazi yao ya asili na kutupwa maporini, walioliwa na Simba haya, walioumwa na Nyoka haya, waliouguwa mpaka wakafa haya. Jee, huyajuwi? Ulishasema ashtakiwe wapi?

Sasa yuko kwa Hakim wamahakim.
 


Tukuhukumu wewe kwa mauaji ya Nyerere?


Naona umeshindwa kujibu ya Ramadhan Ali na ya Nyerere kuwepo Burma na kuishi kwa wasajili wa vyama mtaa wa Stanley unaleta yasiohusu. Jibu hoja zangu achana na ahli zangu.
 

Wewe hunijui lazima uone nimeanza kuyazungumza leo wakifa Waislam unataka watu waseme wamekufa watanzania lakini akifa Padri unataka Pengo atoe tamko kwani Padri siyo Mtanzania na unataka serikali isichaguliwe tena na wananchi wewe mtu hatari sana katika jamii ya Waislam.
 
Wewe hunijui lazima uone nimeanza kuyazungumza leo wakifa Waislam unataka watu waseme wamekufa watanzania lakini akifa Padri unataka Pengo atoe tamko na unataka serikali isichaguliwe tena na wananchi wewe mtu hatari sana katika jamii ya Waislam.

Duh, hakika RITZ nimekuvulia kofia! yaani wewe ni komesha JF! huyu MM mtu wa ajabu sana! mara anatafsiri Qurani tukufu na sijui alisomea wapi elimu ya tafsiri! mara yuko na Pengo na kumuomba atoe tamko! mara yuko na CHadema anataka nchi isitawalike! duh! hatari mtu huyu kwa usalama wa taifa! na sijui kwa nini mpaka sasa hivi yuko uraiani!
 
Mag3 naona umeshindwa kutuonesha Ramadhan Ali na sasa unatuonesha FaizaFoxy. Muulize your other ID atakukumbusha kisa chake. Ulikaa kimya, fumbo hufumbiwa mjinga.
 
Last edited by a moderator:
Tooba yarabi, Mzee Said mbona umenitia manza kwa vijana wangu! Nilikuwa nawaelezea kuhusu chimbuko la AA nikakunukuu. Mwanzo nikasema Cecil Matola alifairiki 1939 kama nilivyonukuu post yako moja, jana nikawaambia samahani ni 1933, hamadi! leo John Illife anaandika 1931. Jamani nitaweka wapi uso wangu miye!

Anyway, eti Mohamed, Cecil Matola alikuwa Mwalimu na Rais wa AA kabla ya Sykes? Maana Mag3 amenukuu Illife unayependa sana kumnukuu sasa hapo inakuwaje.
 

Huyo ana kila sifa ya ufataani, ni mtu mfupi sana asiyeweza hata kutokeza mbele ya watu, anajificha nyuma ya pazia saa 24 kufitini tu.
 

Ramadhan Ali vipi?

Matola, Kyaruzi na Nyerere walikuwa hawawezi kusajili vyama mpaka wawaone kina Sykes? Na Nyerere ikambidi ahamie kabisa kwa kina Sykes. Khatar kubwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…