Abdulwahid Sykes alikuwa Rais wa Tanganyika African Association mpe heshima yake.
Ritz,
Abdu alikuwa zaidi ya hayo.
Yeye ndie alikuwa kiungo kati ya "the intelligentsia"
akina Hamza Mwapachu, Nyerere, Steven Mhando,
Michael Lugazia na wengineo na wazee watu wazima
walounda Baraza la Wazee wa TANU?
Kitu kingine yeye ndiye aliyekuwa na nyumba yenye
nafasi kufanyia mikutano ya siri na zile lunch zao na
diner wakitumia kuweka mipango ya TANU.
Makachero walikuwa hawapungui nje ya ofisi yake pale
Kariakoo Market na mtaani kwake Stanley wakinusa na
kuangalia nani kaingia nani katoka nk.
Kubwa zaidi siku zile uongozi ni kutoa fedha kuendesha
mambo na Abdu wanaomjua wanasema alikuwa mtu karim
sana.
Kuna taarifa za kikachero zimefunguliwa Uingereza baada ya
miaka 50 nazisaka katika archive yangu nikizipata nitaziweka
hapa Insha Allah.
Taarifa hizo zimuunganisha hata na barua za siri akiandika
Tanganyika Standard zilizokuwa zikikera serikali na wakati
ule alikuwa kijana wa miaka 26.
Waingereza walipokuja kufafananisha baadae na uandishi
wake akiwa kiongozi wa TAA wakajiridhisha ni yeye ndiye
mwandishi.
Ingekuwa leo tungemwita "Abdu Sykes Mchochezi."
Yapo mengi sana...