Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

hivi waislam J.K., MWINYI, SALIMIN na wengine walioongoza katika nchi hii, wameifanyia nini Tanzania?

"If you're not careful, the newspapers will have you hating the people who are being oppressed, and loving the people who are doing the oppressing
 
Ritz, ungekuwa umeuweka ushabiki pembeni na kuziangalia hoja za Nguruzi3 kwa jicho la kisoma hakika ungejua kwamba mzee Mohamed Saidi ameziddiwa kabisa na sasa amebaki na turufu ya uislam na mashabiki wa uislam tu.


As long as you are convinced you have never done anything, you can never do anything
 
Ritz,
Kwanza nikuulize. Ulichobandika hapa ni kutoka kitabu cha van Bergen au kutoka kwa mwandishi mwingine anayemnukuu? Kama ni mwandishi mwingine naomba uweke jina lake. Mimi nimeomba nukuu kutoka "horse's mouth" yaani kitabu cha van Bergen chenyewe na si third party. Asante
 
Huuoni wewe na nani? mara ngapi umeuulizwa maswali "very genuine" ukayakimbia kwa visingizio visivyo hata na maana. Mohamed, kitu gani kinakupa imani kwamba hawa watu wanaofutilia mnakasha huu wanaamini hii HISTOHISIA yako?
 
Wacha hizo wewe mzee ametoa ushauri mzuri kwasababu sio watu wote walokisoma kitabu cha mzee mohamed said wako hapa jf kwahiyo nyinyi mnaodai ni uchochezi wazindueni kwa kuandika kitabu chenu sawa bwana mdogo?
Wewe nilisha kwambia upo chini ya kiwango, funga domo lako, hii ngoma mwachie huyo mzee wako
Mohamed Saidi a.k.a mzee chauchochezi!
 
Hicho kitabu cha Bergen Jan Pvan nimemletea Jasusi,

Hata wewe ni rafiki yangu kipenzi hakuna audui wazee wetu wametufundisha ivyo.
Lakini bado nina swali. Ulichoweka hapo juu ni kitabu cha van Bergen au ni mtu anajaribu kutuelezea aliyoyaandika van Bergen? Kwa nini? Kwa sababu sijawahi kusoma kitabu cha van Bergen lakini hizo nukuu nimewahi kuzisoma elsewhere.
 
Mohamed Saidi, umeona jinsi wazee wako walivyoona mbali na walivyotumia busara kuweka pembeni "religious prejudices" na kufungamana na wasio waislam kupambana na ukoloni! Sasa wewe kinakushinda nini kuwaiga hao wazee? Mbona wewe huishi kutafuta visingizio vya kuuvunja umoja wetu na amani tunayofurahia nchini mwetu. Adui wa watanzania sio imani zao ila viongozi waliokosa "vision" , umaskini, ujinga, maradhi na ufisadi. Tuunganishe nguvu kupambana na maadui hao kama vile wazee wetu walivyounganisha nguvu zao kupambana na ukoloni wa muingereza.
 

G,

Nakuuliza baada ya haya yote walifanya wazee wetu nini
ilikuwa ijaza yao?

Nyerere na Kanisa Katoliki wakala njama dhidi ya Uislam
na Waislam.

Sehemu ya tatu ya kitabu changu nimeeleza kwa kina
njama hizo na athari zake.

Unataka tuweke ushahidi hapa?
 
Lakini bado nina swali. Ulichoweka hapo juu ni kitabu cha van Bergen au ni mtu anajaribu kutuelezea aliyoyaandika van Bergen? Kwa nini? Kwa sababu sijawahi kusoma kitabu cha van Bergen lakini hizo nukuu nimewahi kuzisoma elsewhere.

Jasusi,

Kitabu ujawahi kukisoma lakini unapinga kilichandikwa.
 
Wewe nilisha kwambia upo chini ya kiwango, funga domo lako, hii ngoma mwachie huyo mzee wako
Mohamed Saidi a.k.a mzee chauchochezi!

Gwalihenzi,

Mbona tena unaghadhibika?

Kuandika historia ya kweli ndiyo
kuchochea?

Bergen ni mchochezi?
Sivalon je?

Au Njozi na ''Mwembechai Kiliings...''
nae ni mchochezi?

Kwa hiyo kuandika kitabu kama
kile cha Kivukoni College ndiyo sawa?

Kwa kuwa kimewaweka nje Waislam
waliopiganiauhuru na kumtaja Nyerere
peke yake ndiyokimekuwa kitabu cha
maana cha kupigiwa mfano?
 
Jasusi,

Kitabu ujawahi kukisoma lakini unapinga kilichandikwa.
Kitabu cha van Bergen sijawahi kukisoma. Lakini hizo quotes zinazozungumzia kitabu cha van Bergen nimeshawahi kuzisoma. Umezitoa wapi?
 
Huuoni wewe na nani? mara ngapi umeuulizwa maswali "very genuine" ukayakimbia kwa visingizio visivyo hata na maana. Mohamed, kitu gani kinakupa imani kwamba hawa watu wanaofutilia mnakasha huu wanaamini hii HISTOHISIA yako?

G,

Mbona hili nishasema mara elfu?

Siko humu kuaminiwa kwa kile ninachooleza.

Niko hapa kueleza tu kile ambacho wengi hawakuwa
wanakijua.

Wangapi walikuwa wanjua maisha ya Abdu Sykes na
uhusiano wake na harakati za uhuru na kuasisi TANU?

Wangapi walikuwa wanamjua Sheikh Hassan bin Amir?
Au Mshume Kiyate au Sheikh Suleiman Takadir.

Au wangapi walikuwa wanajua ule moyo wa TANU miaka
ya 1950 ilivyokuwa unawatuma wazalendo kujitolea hadi
nafsi zao ili uhuru upatikane?

Nani alikuwa anakijua kisa cha Rashid Ali Meli bwana fedha
wa Dar es Salaam Municipal Council aliyekwenda kuchota
fedha za serikali akamletea mweka hazina wa TANU Idd
Faiz atunishe mfuko wa safari ya Nyerere UNO 1955?

Kama ninsingeandika historia hii leo hazina hii ingepotea.

Najua historia hii nzuri inakuchomeni.
Lakini nina khiyari?
 
Hapo kwenye rangi nyekundu ndipo penye mzizi wa HISTOHISIA yako! tangu ulipoanza kuimba hizo nyimbo zako za uchochezi hujawahi kutoa ushahidi thabiti kuthibitisha madai yako haya zaidi ya kujenga hoja kupitia hisia na dini ya kislam kuungwa mkono.
 
Unaonesha huu mjadala umeuvamia bila kusoma posts za mwanzo, kwa faida yako nakurudisha page ya kwanza yenye majibu, jisomee kidogo upate faida:
Zomba.
Mengi uliyoyanukuu hayana ukweli wowote.
Punguzeni chuki na ukristo.
Hivi inashindikana nini kwa kikwete kuupngua huo mfumo kristo kama kweli upo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…