Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Dullah, kama kiingereza kinakushinda kwanini unaking'ang'ani? sasa hapo kwenye rangi nyekundu ndio kiingereza gani?

Wewe umeona nimempa likes dullah ukakosoa kithungu chake nilichofanya hapa nikusifu dullah kwasababu ameonyenya kithungu chake ambacho wewe na wagalatia wenzako mumekiponda na kuthibitisha kwamba dullah hacopy na kupaste kama nyinyi wagalatia hapa JF.Cc GWALIHENZI,KABONDE na SWEKE34
 

Ni wapi uliposoma pameandikwa kafa? na huo uongo uko wapi? mbona unaruka-ruka kama kadondo. Unamjuwa kadondo?
 
Nimeongelea matokeo ya kidato cha nne ambayo yapo hapa JF.

Nashukuru sana kuwa unatetea hoja zangu vema sana. Ni kwa sababu hizo naomba uungane nami kumlaani mwandishi wa hiyo makala ambaye amechukua matatizo ya sehemu fulani na kuyafanya matatizo ya waislam.

Kama ulivyosema, huko Bukoba, Mwanza nami naongezea Machame na Mbeya hali ni tofauti sana na kwingineko kama Rufiji Kilwa, Mkuranga na kwingine.

Hivyo basi tatizo kumbe si Uislam wala hujuma kwa Uislam. Tatizo lipo katika jamii accross the board.
Nina maana kama ipo jamii ya wakristo ambayo ipo nyuma basi tatizo si ukristo wao bali maingira waliyopo.

Niliwahi kuandika hapa kuwa nimeishi Peramiho, Magila, Shirati, Bumbuli n.k. huko nimekuta watu ambao hawajakanyaga shule licha ya kwamba ndiko mfumo tuhumiwa''mfumokristo'' ulipo.Kule kwetu Mjasani, Pongwe hadi Pangani nako hakuna tofauti na huko nilikotaja.

Alaa!!! kumbe basi hili ni tatizo la wote na si la jamii fulani.
Tukishaelewa hivyo, sote tusimame na kumkemea mpuuzi yoyote atakayetafuta sababu za kihayawani ili kufanya tatizo la sehemu moja kuwa linasababishwa na upande mwingine hata kama upande husika una tatizo kama hilo pengine kubwa.

Miongoni mwa sababu za kipuuzi ni hizi za kutumia dini.
Kwamba fulani ni John hata kama ni fukara na wala hajaona daftari linakuwaje huyo ana advantage kuliko fulani mwislam.

Kwamba fulani anafanikiwa si kwasababu ya jitihada zake bali dini yake hata kama kichwani hakuna kitu.
Kwamba wale waliofanikiwa kwa kutumia dini wamefanikiwa kwa bahati tu maana majina yao ni kikwazo hata kama ni wataalamu waliobobea.

Tatizo ni kuumba hadithi za kitoto na kijinga za kusema Nyerere alitanguliza wazanzibar wauawe na mwislam Idd Amin.
Kumbe basi leo Talibani wakituvamia wapo wendawazimu watakaosahau Utanzania wao na kujiunga na Taliban hata kama tunajua ni wapuuzi wasioujua uislam.

Haya yanafanywa ili kuleta farki katika jamii. Watanzania bila kujali dini zao wanaumizwa na inflation na wanapigika kikamilifu na maisha. Sasa wanapotokea wapuuzi na kudhani kilo ya siukari inauzwa kwa majina ya dini, hawa hawafai katika jamii yetu, we must denounce them from the very beginning.

Ni kwasababu Somalia iliwappuuza wajinga wa calibre hii ndio maana leo kuna mtoto amezaliwa na ameoa nchini Somalia akiwa anakimbia vita kila siku. Hajui amani ni nini licha ya ukweli kuwa jamii yao ni ya dini moja.

Katika jamii iliyochanganyika kama yetu tukiruhusu tu chuki zikapaliliwa tutauana kwasababu tu wapo wajinga wachache walioamua tuwe hivyo.

Inapofikia mahali Mtanzania anamwita mwenzake adui ujue hapo si kwema.
Lakini Ritz, muhimu si kuficha kichwa katika mchanga huku mwili ukiwa nje. Huko ni kujidanganya.

Unajua wazi kuwa tatizo si Nyerere, Ukristo n.k. kwanini watu waondoe jicho mahali husika na kutafuta simple and stupid reasons to justify their unjustifiable course.

Hivi mtu anaposema Wazanzibar wanachangia elimu ya juu huku tukijua si kweli hawana bajeti hiyo, hapo tunamsitiri mtu huyo kwa heshima gani. Yeye hakutusitiri kutudanganya tunasababu yoyote ya kumsitiri kweli.
Huyu si mpuuzi tu na kama nimekosea tumwiteje!

Mtu anaposimama na kusema commonwelath ni Anglican na Tanzania imejiunga akisahau kuwa Pakistan na Bangladesh kuliko na radicals kweli kweli ni wanachama wa commonwealth anatufikiriaje.

Kwamba mtu anatufanya wajinga wa kuamini kuwa common wealth ni shirika la wakristo huku akijua kuna Francophone na Arab League achilia mbali Latin America.

Huyu mtu anayedhani sisi ni wapumbavu kiasi hicho anahitaji kusetiriwa kweli zaidi ya kumwaga mzima mzima.

Chuki ya mtu binafsi dhidi ya watu wengine iwe yake na ibaki kama yake wala lisiwe suala la kitaifa.
Ni hiari ya mtu kusoma chuki hizo, tusichokivumilia ni kupanda chuki hizo miongoni mwa vijana wetu wadogo wa imani na makabila mbali mbali.

Ritz, fikiria hivi, mtu kapata elimu kutoka shule ya mfumokristo, leo anasimama na kulaani huku akichagiza wenzake wasipeleke watoto kutafuta elimu. Huyu ana heri na waislam kweli. Yeye alikwendaje na kwanini.
 
Zomba,

Kapanda daladala ya kwenda Tabata wakati yeye anakwenda Gongolamboto.


Kama kapandia Buguruni sheli,namshauri asifike mbali sana,ashuke tuh hapo tabata dampo au matumbi asubiri hizo zinazotaka ubungo kwenda gongo la mboto,

kama anang'ang'ania basi mwache aende zake..
 
Kama kapandia Buguruni sheli,namshauri asifike mbali sana,ashuke tuh hapo tabata dampo au matumbi asubiri hizo zinazotaka ubungo kwenda gongo la mboto,

kama anang'ang'ania basi mwache aende zake..

Kwa jinsi ninavyomuona anaweza kushukia magomeni mikumi.
 
G,

Panapo dhulma hayo ndiyo matokeo.
Mzee ms

Unapenda kung'ang'ania dhuluma, je? Ni dhuluma ipi mfano wewe kama wewe ulofanyiwa na mwl nyerere?
Sasa baada ya kupandikiza chuki kwenye hiyo miskiti nini basi faida uipatayo wewe kama wewe.
 
Mzee ms

Unapenda kung'ang'ania dhuluma, je? Ni dhuluma ipi mfano wewe kama wewe ulofanyiwa na mwl nyerere?
Sasa baada ya kupandikiza chuki kwenye hiyo miskiti nini basi faida uipatayo wewe kama wewe.

Hivi uwakamate Masheikh wa Waislaam uwaweke rumande, mmoja baada ya mwingine, wengine uwafukuze nchi, wengine uwahamishe kutoka makazi yao ya asili kuwapeleka kwingine, ufunge jumuia ya Kiislaam iliyokuwa na inaonesha kuleta maendeleo ya haraka haraka kwa Waislaa, Yote hiyo kwako wewe siyo dhulma?
 

Actually nashangaa kwa nini hawa wapumbavu wa UAMSHO bado hawajachukuliwa hatua zozote.
 
Muongo ni wewe pambaf. Do you know the meaning of being out of stock?

Jasusi,

Nakuheshimu lakini nashangaa unaanza matusi sisi wengine uhuni tumeishastaafu kama utataka kunirudisha kwenye uhuni pana shaka tarudi.

Kutokukubaliana mie na wewe kwenye hoja siyo uadui wala ugomvi hakuna haja ya kutukanana hakuna ambaye hawezi kutukana.

Tusifike huko Jasusi nakuheshimu kama mkubwa wangu na wewe niheshimu kama mdogo wako.
 

Hapo Mfumo kristo katika NECTA ulikuwa haufanyi kazi?
Huu ni ushahidi tosha kuwa mafanikio yako yalitokana na kujituma kwako, Huo uchache wa Waislamu ulioukuta Sekondary ulisababishwa na kutojituma kwao tofauti na wewe ulivyokuwa unajituma,
na labda nikwambie tu hilo halikuwa kwa Waislamu tu bali hata Wakristo liliwaathiri, miaka niliyokuwa na Nasoma kulikuwa na Wakristu wachache sana wa kabila la Kigogo, Wasumbwa, Wasukuma, japo yalikuwa ni makabila yenye Wakristo wengi lakini walikuwa ni wachache sana mashuleni na wala hapakuwa na hila ya kuwabeba kuwapelekwa sekondary bila kujituma kwao., na wengi mazingira na culture ndio zilikuwa zinawaathiri same na hayo yanayotokea Lindi na kilwa sasa

Tuna tatizo la Kitamaduni ambalo Waislam wanalinasibisha na DIni, kama maeneo yenye Waislamu wengi hayana maendeleo ya Kielimu basi wajaribu kuangalia ni nini kinachosababisha hilo, ni dini ama ni utamaduni? kuliko kuweka dhana ya uonevu
 
Wewe mtoto umepotea njia, hapa sio kwako, rudi madrasa kwa mzee Mohamed Saidi akakufunze upya, eboo!
 

Nimekusikia. My bad!
 

Umefanya ufafanuzi mzuri lakini mwisho kabisa tumeachana kwa makusudi unataka kutuaminisha tena sehemu kwenye Waislam wengi tatizo linaweza kuwa dini yao ndio maana hawataki kusoma.

Labda tufahamishe nchi kama Dubai, Misri, Saudia Arabia, Qatar, Kuweit, Iran, watu wao hawapendi shule na hawana elimu.
 
Dullah,

Katika maelezo yako umeonyesha ulifanya juhudi binafsi mpaka ulipofikia.
Sasa juhudi zako zote za kusoma kwa bidii kwa nini azikuhujumiwa na mfumo kristo?
Je? Hali iliyopo leo huko lindi na mtwara watoto wamechaguliwa hawalipoti vipi miaka hiyo ya
nyuma hali ilikuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…