Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

umekurupuka kujibu,sikatai kwamba hakuna wakristo walioshiriki harakati za uhuru,la hasha.Ninachopinga ni kanisa kulihusisha na harakati za uhuru

Sasa kama ulikuwa hujui, darasa hili ndio linakujuza rasmi kwa makala hiyo fupi tu.

Unapoisoma tuliza akili kuna maeneo mwishoni nimemalizia kwakuwaunganisha wahusika na itikadi zao (Kasisi Maranta na Shehe Issa)
 
 

Ikiwa imekupitikia kauli yangu ina masimango hiyo ni bahati mbaya sana.
Niwie radhi sana.

Ila ni ukweli kuwa Nyerere hakudhikika ila kwa kipindi kidogo sana.
 
huyohuyo nyerere ndo aliyetoa kibari cha kukamatwa muft wa wakat huo kwa madai anataka kuihuju serikali hali iliyopelekea IGP wa wakat huo akatae na nyerere kuamuru maafisa usalama wamkamate. MFUMO SASA BASI
Maulid Daniel,

..halafu huyo IGP aliyekataa kumkamata mufti akaendelea na wadhifa wake.

..miaka michache baadaye akaua mwananchi kwa kumkanyaga na gari.

..kesi ikapelekwa mahakamani lakini IGP akaachiwa katika mazingira ya ajabu-ajabu.

..Mwalimu akampa IGP "adhabu" ya kwenda kufanya kazi/kupumzika ubalozi wa Tanzania Marekani.

..hivyo ndiyo MFUMO UNAVYOFANYA KAZI!!!

cc: @ Mohamed Said, Jasusi, Yericko Nyerere, Nguruvi3
 
Jana nilikuwa naongea na mzee mmoja Muislam safi akaniambia hali ya ELIMU kwa Waislamu ingekuwa mbaya sana kama Mwalimu asingetaifisha shule za madhehebu ya DINI kwani wazee wa Kiislamu walikuwa wamegoma kupeleka watoto wao kwenye shule hizi kwa kuhofia watoto wao kubadilishwa dini na kulazimishwa kusali kikristo kila asubuhi na jioni.
 

Mbona ndugu yangu umeacha mengi sana kuhusu Hamza Aziz na Nyerere?

Umeliona lile la ajali ya barabarani aliyopata ndiyo kubwa la kuweka humu
kumfedhehesha mzee wangu?

Yapo mengi huyajui.

Ungetaja na Hamza Aziz kuitwa Halmashauri Kuu kushitakiwa kwa kupingana na Leadership Code.
Ungeeleza na mpambano uliotokea mle ndani kati ya Nyerere na Hamza Aziz.

Ungeeleza kuwa katika kikao kile kaka yake Hamza Aziz, Dossa Aziz alipewa safari na alipokuwa
hayupo ndipo kikao kikaitwa kwa haraka ili Hamza Aziz asitetewe na kaka yake.

Ungeeleza na msimamo wa Rashid Kawawa katika sakata ile yote na nini alisema.

Ungeeleza, ungeeleza, ungeeleza na ''bugging'' ya simu zake...

Ungeeleza na vita alokuwa akipigwa ndani ya jeshi la polisi.
Aliyekuwa akiongoza vita vile ni Geoffrey Sawaya aliyetumiwa kuwahonga vibaraka waikubali BAKWATA...

Tunajua mengi.
Na sababu ya kujua hayo yote ni moja tu.

Waliokuwa wakiandamwa ni wazee wetu.
Wameondoka na kutuachia nyuma hazina ya taarifa.

Angalia taarifa zako.
Hamza Aziz hakuenda Marekani bali Canada.

Huko akasoma shahada mbili.
Hivi ndivyo zile fitna zilivyomsaidia.

Kwa kumaliza napenda nikueleze.
Hamza Aziz aliwahi kusomewa dua na Sheikh Hassan bin Amir.

Sheikh Hassan bin Amir alinyanyua mikono yake juu akalia na Allah
amjalie Hamza na amkinge na kila shari.

Hamza Aziz alipokuwa kijana mdogo yuko Morogoro ndiyo kaanza kazi ya polisi
baba yake alimtembelea nyumbani kwake Police Baracks.

Mzee Aziz Ali alimwombea dua akamwambia, ''Hamza mwanagu namuomba Allah
akuhifadhi na akupe kila utakalomuomba.''
 
View attachment 79799Nyerere, Kleist and Dosa

Hii picha ni yangu.
Nilipewa miaka mingi sana iliyopita na Kleist na mimi nikaisambaza.

Hii ilikuwa Arnatouglo Hall 1956.

Nyerere alikuwa anakwenda Umoja wa Mataifa kwa mara ya pili na
TANU walimfanyia tafrija pale ya kumuaga,

Huyo aliyekaa mkono wa kushoto wa Abdu ni Nang'wanda Lawi Sijaona.

Lawi Sijaona aliingizwa katika siasa na Suleiman Masoud Mnonji aliyekuwa
Mwenyekiti wa TANU Lindi.

Hiyo ilikuwa 1955.

Ahsante sana kwa kuleta hii picha hapa.
 
Mohamed Said,

..hayo ya Hamza Aziz kuitwa Halmashauri kuu sikuwa na habari nayo. asante kwa darsa!!

..mimi nilikuwa namjibu Maulid Daniel ambaye alikuwa anajaribu kumchafua Mwalimu Nyerere.

..mwisho, kama utaamua kueleza historia ya Hamza Azizi basi unapaswa kutoa habari zote.
 
Last edited by a moderator:

Mdomo haumkatai bwana wake.

Mzee wangu huyo laiti kama kweli angekuwa ''Muislam safi''
kama unavyosema angelijua kuwa Allah amekataza mtu kusema
kile asichokuwa na ujuzi nacho.
 

Wakuu ili tuweze kujifunza mengi na yenye mafaa, ni lazima tutambue mambo mawili makuu!

1) Kundi la wanaharakati kuhama kutoka uanaharakati kwenda uanasiasa.

2) Filosofia ya TANU na siasa zake za ndani.

Tukiyajua hayo bila shaka tunaweza kuondoa hisia za upande mmoja ama hisia mbaya kwa ujumla.

Bahati nzuri mimi ninaufahamu wa sayansi ya siasa hivyo sifikirii vibaya au mlengo wa kushoto juu ya TAA na TANU na kisha CCM kwakuwa filosofia zao nijua.
 

Pole kaka niwie radhi kama nilishuka ''full speed.''

Hahahahahahaha.
 

Mohamed,'
Sahihisho dogo tu. Hamza Aziz aliahamishiwa hapa Washington D.C. 1974-au 75. Alihamia Canada 1978. Nimemfahamu vizuri tu pamoja na familia yake alipokuwa hapa Washington. Hata masomo alianzia hapa wakati huo balozi Bomani naye akifanya Masters yake.
 

kwani ukikaa pembeni kama mimi kuusikiliza huu mnakasha utaonekana mjinga?.
 
Last edited by a moderator:

Huyo mwislam hajitambui,ndiyo hao hao wanaotupa shida uelewa wao kwa kweli ni mdogo sana,wamezoea kuendeshwa na propaganda.Kwa waislam wa sasa,mpaka ipite suruhu vinginevyo hakuna kitakachoeleweka.
 

Waingereza hawakuondoka kwa khiyari yao.
Inaelekea huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.

Waingereza walifanya mbinu nyingi kupiga vita juhudi
za wazee wetu kujikomboa.

Kuna Government Circular No. 5 na No. 6 walizotoa ili
TAA/TANU ikose viongozi.

Hizo circular zilikataza wafanyakazi serikalini kujiunga na siasa.

Kulikuwa na Speicial Branch iliyokuwa ikiwabughudhi wanasiasa.
Hawa wakiongozwa na Amiri Kweyamba.

Huyu kachero akiwafatafata sana Abdu na Ally Sykes hasa 1953 walipoanza kusambaza
''makaratasi ya uchochezi'' yakihimiza Waafrika kujiunga na TAA.

Ndugu yangu uliza vitu hivi kwa ustaarabu utaelezwa.

Hawa walofanya haya walikuwa wazee wetu na wametueleza mengi sana yaliyopita kipindi
kile hadi uhuru ukapatikana mwaka 1961.
 
Pole kaka niwie radhi kama nilishuka ''full speed.''

Hahahahahahaha.
Mohamed Said,

..hujakosea hata kidogo.

..Waswahili wana msemo wao "penye wengi ..."

..Mimi napenda sana aina yako ya uandishi wa historia, hata kama kuna mambo ambayo sikubaliani nayo.

..I wish tungekuwa na waandishi wengi zaidi wa aina yako, kwasababu nadhani hilo tu ndiyo lingeweza kuitendea haki historia yetu.

NB:

..sasa ngoja na mimi nikupe darsa la "dot com"

..kwenye mtandao hatucheki "hahahahaaa". ukitaka kucheka andika LOL meaning "laughing out loud" au "laughs out loud"

..upooooo!!!??
 
Last edited by a moderator:

Nakubaliana na wewe mkuu!

Huo ni ukweli kuwa muingereza hakutoa nchi kwa urahisi kama wengi wanavyodhani.

Ilikuwa kazi ngumu na ya hatari kuupata uhuru huu tunaouchezea leo!
 
Mohamed, kuna maswali yangu kiporo kule nyuma.

Anyway, labda nikuulize jambo moja.
Huyu AMIR Kweyamba anaangukia katika kundi gani? Wazee wako au kibaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…