Maulid Daniel,
..halafu huyo IGP aliyekataa kumkamata mufti akaendelea na wadhifa wake.
..miaka michache baadaye akaua mwananchi kwa kumkanyaga na gari.
..kesi ikapelekwa mahakamani lakini IGP akaachiwa katika mazingira ya ajabu-ajabu.
..Mwalimu akampa IGP "adhabu" ya kwenda kufanya kazi/kupumzika ubalozi wa Tanzania Marekani.
..hivyo ndiyo MFUMO UNAVYOFANYA KAZI!!!
cc: @ Mohamed Said,
Jasusi,
Yericko Nyerere,
Nguruvi3
Mbona ndugu yangu umeacha mengi sana kuhusu Hamza Aziz na Nyerere?
Umeliona lile la ajali ya barabarani aliyopata ndiyo kubwa la kuweka humu
kumfedhehesha mzee wangu?
Yapo mengi huyajui.
Ungetaja na Hamza Aziz kuitwa Halmashauri Kuu kushitakiwa kwa kupingana na Leadership Code.
Ungeeleza na mpambano uliotokea mle ndani kati ya Nyerere na Hamza Aziz.
Ungeeleza kuwa katika kikao kile kaka yake Hamza Aziz, Dossa Aziz alipewa safari na alipokuwa
hayupo ndipo kikao kikaitwa kwa haraka ili Hamza Aziz asitetewe na kaka yake.
Ungeeleza na msimamo wa Rashid Kawawa katika sakata ile yote na nini alisema.
Ungeeleza, ungeeleza, ungeeleza na ''bugging'' ya simu zake...
Ungeeleza na vita alokuwa akipigwa ndani ya jeshi la polisi.
Aliyekuwa akiongoza vita vile ni Geoffrey Sawaya aliyetumiwa kuwahonga vibaraka waikubali BAKWATA...
Tunajua mengi.
Na sababu ya kujua hayo yote ni moja tu.
Waliokuwa wakiandamwa ni wazee wetu.
Wameondoka na kutuachia nyuma hazina ya taarifa.
Angalia taarifa zako.
Hamza Aziz hakuenda Marekani bali Canada.
Huko akasoma shahada mbili.
Hivi ndivyo zile fitna zilivyomsaidia.
Kwa kumaliza napenda nikueleze.
Hamza Aziz aliwahi kusomewa dua na Sheikh Hassan bin Amir.
Sheikh Hassan bin Amir alinyanyua mikono yake juu akalia na Allah
amjalie Hamza na amkinge na kila shari.
Hamza Aziz alipokuwa kijana mdogo yuko Morogoro ndiyo kaanza kazi ya polisi
baba yake alimtembelea nyumbani kwake Police Baracks.
Mzee Aziz Ali alimwombea dua akamwambia, ''Hamza mwanagu namuomba Allah
akuhifadhi na akupe kila utakalomuomba.''