Ritz
Hivi wewe umepofushwa na ufuasi wako kwa Moh Said mpaka unafikiri kuwa tunampinga kila kitu?
Yeye akiandika Mshume Kiyate na Nyerere na Abdu walikuwa wanakula mara tano kwa siku au walikuwa wanacheza bao au mpira, sisi hatuwezi kupinga. Mbona ni stori nzuri tu, tena zipo
entertaining..
Uchochezi wake ni ule unao-emanate kwenye hisia zake. Na hisia hizo kaziweka makusudi ili kuamsha chuki kwa waislam. Ni hisia hizo ndizo tunazopinga.
Kwa mfano atakwambai:
"Nyerere hakupenda historia ya TANU ihusishwe na waislam"-
"church lobby did this or that against muslims"
"Nyerere na kanisa waliua EAMWS ambayo ingejenga chuo kikuu cha waislam"
Hayo na mengine mengi ya kihisia, ukimuuliza ushahidi anaji-quote mwenyewe, na mara nyingine anarudia kwa ku-
paste ka-
passage kale kale ka Sivalon. Tukimbana sana, anasema
"sijibu kila post",
"mdomo haumkatai bwana wake"
Na mara nyingine anatusemea hisia zetu
"Ritz/Zomba hawa ndugu zetu wamestushwa na historia niliyoandika mimi"
"Hawapendi niliyoandika, wanataka historia ianzie na kuishia kwa nyerere"
Stori zake ni nzuri na hata kama kaamua kuandika kuhusu wazee waliosahaulika, it is well and good. Hatuna shida na hilo. Ambacho hatukubaliani nacho ni hizo hisia alizoziingiza kwa makusudi ili kulazimisha CHUKI YAKE BINAFSI KWA NYERERE igeuke kuwa chuki ya Waislam dhidi ya Wakristo. Hizo hisia ndizo tunazipinga na tutazipinga, hata kama kitabu chake kitakuwepo kwa miaka mia moja.