Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Ahsante sana kwa taarifa.
 
Haahaa mkuu unamitego hatari!

Nashukuru kwa kunikumbusha maswali yako.

Nimekusoma lakini umeeandika mengi hadi ya Saigon, Meya Kleist, madiwani nk.

Nakuomba kitu kimoja kwa kuwa ''passage'' ni ''full loaded'' nakuomba niwekee
maswali yako kwa lugha fupi mathalan Kleist alikuwa Meya mbona hakufanya kadha
wa kadha nk. kisha unaandika swali jingine.

Kama maswali ya mtihani vile.

Mimi nitajibu moja baada ya moja Insha Allah.
Imeniwia taabu kuyatafuta maswali mle ndani.
 
Mohamed, kuna maswali yangu kiporo kule nyuma.

Anyway, labda nikuulize jambo moja.
Huyu AMIR Kweyamba anaangukia katika kundi gani? Wazee wako au kibaraka

Nashukuru kwa kunikumbusha maswali yako.

Nimekusoma lakini umeeandika mengi hadi ya Saigon, Meya Kleist, madiwani nk.

Nakuomba kitu kimoja kwa kuwa ''passage'' ni ''full loaded'' nakuomba niwekee
maswali yako kwa lugha fupi mathalan Kleist alikuwa Meya mbona hakufanya kadha
wa kadha nk. kisha unaandika swali jingine.

Kama maswali ya mtihani vile.

Mimi nitajibu moja baada ya moja Insha Allah.
Imeniwia taabu kuyatafuta maswali mle ndani.

Kuhusu Amiri Kweyamba.
Kuna umuhimu kuna tija itapatikana kwa kukueleza kama alikuwa mzee wangu au vipi?
 

LOL Mkuu....
JK kijana wangu ahsante sana kwa kunitia mjini.
 
Mohamed, hivi nimeanza kujadilina na wewe leo kweli!
Mohamed kuuliza maswali kama mtoto wa shule hilo halisaidii wasomaji. Kuna maswali na maswali yanayotokana na hoja.

Kwa kawaida najenga hoja ya msingi wa swali langu halafu ndipo maswali yanajitokeza.
Kuuliza maswali kama mtoto wa shule ya msingi huko nimeshapita niwie radhi.

Ingawa unasema hukuona maswali, ni mara tatu nimeyaweka na unayakimbia. Imekuwa hivyo si leo ni kila mara tunapokuwa na mnakasha.Umeanza kutoa visingizio vya ''ngano'' nikaviondoa, sasa unataka niulize maswali kwa mtindo wa chekechea

As much as unapenda kuheshimiwa unapaswa kuheshimu watu wengine. I could read between the lines unaonyesha dharau ya hali ya juu. Hilo halinisumbui kwasababu najua fika kama ungekuwa na uwezo ungenipiga Ban nisikuhoji au nisijenge hoja zangu.
Nafahamu wazi hupendi, midhali upo hapa jamvini hilo hutalikwepa, ndio JF.

Unahiari ya kujibu au kukimbia kama ilivyo kawaida.

Swali la mwisho nililouliza kwa mtindo unaoutaka ni hili.

Je, AMRI Kweyamba anaangukia katika kundi gani, Wazee wako au kibaraka.
Tuendelee kuanzia hapa huko nyuma tuache maana kila mtu anafahamu utaratibu wako wa kukwepa hoja na maswali.
Haiwezekani wanajamvi wanielewe wewe usione swali, sasa hapo tatizo litakuwa kwangu au kwako!

Inshallah tuendelee na swali hili
AMRI Kweyamba anaangukia katika kundi gani, Wazee wako au kibaraka
 

Ni bahati mbaya hatufamihani vyema ila kwa maandishi.
Siwezi kukutusi ''in between lines.''

Sithubutu ndugu yangu niamini.
Hiyo chekechea umeweka wewe.

Ninalokusudia ni kuniwekea kwa mtindo wa moja, mbili, tatu...

Mimi sikimbii swali lolote kama sitaki kujibu nitakuambia tu kuwa sina haja ya kulijibu
kama hilo la Amir Kweyamba.

Sasa tutoke kwenye huu mkwamo tusongee mbele na mengine.
 
Waaaaaaooo asante sana ndugu!

Niliambiwa ilikuwa mwaka 1956 pale mnazimmoja Ukumbi wa Anatoglo

Ukumbi huo una historia kubwa sana.

Mkutano wa uchaguzi wa TAA 1953 ulifanywa hapo na ndipo ule uchaguzi maarufu
wa Abdu Sykes na Julius Nyerere ulikofanyika.

Vilevile hapo ndipo Schneider Abdillah Plantan alipofanya vurugu kubwa 1950 kwenye mkutano
wa dharura wa TAA ulipofanyika kutafuta viongozi wapya wa TAA baada ya mapinduzi ya kumng'oa
Mwalimu Thomas Plantan aliyekuwa rais na katibu wake Clement Mtamila.

Waingereza walihudhuria mkutano ule kuja kuwatisha Waafrika.

Schneider, mtoto wa Chief wa Kizulu Mohosh, askari katika jeshi la Kijerumani na askari aliyepigana
dhidi ya Waingereza katika Vita Vya Kwanza alikuwa anawasubiri kwa hamu maofisa wale wa Kiingereza.
Akawaambia hapa hapakaliki hadi uchaguzi umefanyika.

Huyu mtu ana mengi sana...

Kapata kumtukana Nyerere uso kwa uso nyumbani kwake Msasani baada ya kutolewa na Nyerere kizuizini
alipomfunga.

Alikuwa akitembea huku anavuta mguu mmoja kutokana na risasi alopigwa vitani.
Yeye na Kleist walikuwa kwenye battalion moja walipopambana na Waingereza kwa silaha Mwele Juu, Tanga.

Schneider ndiye alikuwa katibu wa Daawati Islamiyya (Wito kwa Waislam) rais wake akiwa Sheikh Hassan
bin Amir.

Uchaguzi huu ndiyo uliowaingiza madarakani Dk. Vedasto Kyaruzi kama rais na Abdu Sykes katibu.

Meneja wa Arnatouglo wakati ule alikuwa Denis Phombeah Mnyasa huyu bwana.
Baadae meneja akaja kuwa Mzee Chihota ambaye alikufa Uingereza katika miaka hiyo hiyo ya 1950.

Huyu Mzee Chihota alikuwa Mzimbabwe.
Hadi leo kuna mtaa Temeke unaitwa ''Chihota.''

Huyu ndiye baba yao Raymond Chihota (marehemu), Norman, Deborah Mwenda na Gershom.
 

Haya wadau tuendelee na mjadala wetu huku maswali na hoja zote zikijibiwa!
 
Hapana Mzee Mohammed Said hututendei haki wanajamvi kwa kukwepa hoja za msingi za nguruvi 3 na Sweke 34 Wameyaondoa yote uliyoita kejeli lakini bado unakwepa.

Hizi habari za historia ni muhimu sana hasa kwa kuwa unalaumiwa kwa kuwa "biased" ni vyema pia kujibu hoja za msingi......Nchi yetu sote hii.

 

Hebu fafanua kidogo ilikuwa vita ya kwanza ya dunia au ya pili?

Nijuavyo ilikuwa ni vita ya pili ya dunia ambayo ilizaa makutano ya berlin,
 
Hebu fafanua kidogo ilikuwa vita ya kwanza ya dunia au ya pili?

Nijuavyo ilikuwa ni vita ya pili ya dunia ambayo ilizaa makutano ya berlin,

Vita ya kwanza 1914 - 1918 ndiyo walipigana Kleist na Schneider dhidi ya Waingereza.

Vita ya pili 1938 - 1945 Schneider aliwekwa kizuizini Mwanza na Waingereza kwa kuwa alikuwa
akipita mitaa ya Dar es Salaam akimsifia Hitler.
 

Kama nijibu kwa kuwa nalaumiwa hilo siwezi kuliepuka.
Mwenye kulaumu atalaumu tu hata iweje.

Mimi nitajibu lakini hebu nipangieni basi hayo maswali katika njia yajitokeze
kama maswali.

Hiyo niliyowekewa ni passage ngumu kwangu kunyanyambua maswali.
Ikiwe wewe unaweza hebu ifanye hiyo kazi mimi Insha Allah nitajibu.
 
Asanteni sana kwa kuja ila mjue kizazi kijacho kitautaka ukweli historia ya tanganyika ni butu na sijui kwa nn kwa maksudi mazima imefanywa iwe butu ila ipo siku mtakimbiana tu hilo mlitambue lipo tatizo
 
Vita ya kwanza 1914 - 1918 ndiyo walipigana Kleist na Schneider dhidi ya Waingereza.

Vita ya pili 1938 - 1945 Schneider aliwekwa kizuizini Mwanza na Waingereza kwa kuwa alikuwa
akipita mitaa ya Dar es Salaam akimsifia Hitler.

Asante kwa ufafanuzi, tusonge mbele!
 
Waaaaaaooo asante sana ndugu!

Niliambiwa ilikuwa mwaka 1956 pale mnazimmoja Ukumbi wa Anatoglo

Sahihisho dogo.

Kwenye picha imeandikwa ''Kleist.''

Abdu akijulikana kama Abdu Kleist au Abdu Sykes.

Watu wa Dar es Salaam wakimwita Abdu Kleist wenzake maofisini TAA/TANU
wakimwita Abdu Sykes.
 
Wanajamvi,
Mara nyingi tumemsikia Mohamed akimtuhumu Mkapa wakati akiwa mhariri wa magazeti.
Hivi karibuni alimtuhumu Mkapa kama mshabiki wa kifo cha EAMWS akiwa na Martin K.
Alimtuhumu kwa kushindwa kuelezea kifo cha Sykes, mtu muhimu sana katika taifa.

Nimemuuliza kuwa Amir Kweyamba anaaungikia wapi katika makundi yake (wazee wake au vibaraka).
Mohamed amesema hilo hana haja ya kulijibu. Japo kaonyesha uungwana kidogo wa kusema hivyo na si dharau na kejeli.

Mantiki ya hapo juu ni kuwa Mkapa anatuhumiwa si kwasababu ya utendaji wake(uwe mzuri au mbaya) bali njia mojawapo ya kumhusisha yeye na Nyerere na Kanisa ili kukidhi matakwa ya kila siku ya ya kujenga historia kwa kutanguliza maoni yake yakifuatiwa na majina na mikasa.

Mohamed ameshindwa kusema Amir Kweyamba ni wa kundi gani kwasababu huyu ni miongoni mwa waliokuwa wanafuatilia nyendo za Sheikh na wenzake. Mohamed anatatizika kusema ni kibaraka kwasababu hizi

1. Ni mwislam na historia yake watatajwa tu lakini si kueleza uovu wao kwa kushirikiana na ''dhalimu''
Kuwasema kutaondoa maana nzima ya waislam kuwa bega kwa bega na Nyerere na kwamba hakukuwa na hujuma zilizofanywa na kundi jingine isipokuwa waislam wenyewe kwa wenyewe.

2. Kumsema Amir Kweyemba kutaondoa dhana ya Nyerere kupandikiza vibaraka BAKWATA kwasababu zama hizo BAKWATA haikuwepo. Anachokikwepa ni kusema ukweli kwamba failure na sucess za waislam hazikuwa na mkono wa kundi analotuhumu bali wao wenyewe.

3. Kutandoa dhana kuwa wakristo walipinga uhuru kwasababu Amir Kweyamba naye si alifanya kazi special unit ya kuwapiga vita wazee wake, sasa hoja kuwa wapo waliopinga itatoka wapi.

Historia ilipaswa umwangalie Amir Kweyamba aliyezuaia harakati mapema kabisa zaidi kuliko mhariri wa gazeti bw. Mkapa aliyefuata baada ya uhuru na ambaye nafasi yake ni finyu kwa nyakati hizo.

Kwa vile lengo ni kupandikiza fikra za chuki hasa dhidi ya ukristo, Mohamed anachagua maovu na waovu wa kuwasema na hapa Mkapa si mwandishi bali Mkristo.Kwa mantiki hiyo hata pale alipofanya vizuri, Mohamed hatathubutu kuandika ili kutokinzana na simulizi yake.

Historia ni ''dead subject'' kwamba imekamilika kama ilivyo na haina nafasi ya evolution.
Anachokihadithia Mohamed ni kweli kilitokea kwa maana ya kuwa watu anaowataja walikuwepo, harakati zilikuwepo n.k. Ni ukweli Sykes walikuwepo, kama Mshume, Kyaruzi, Boman, Rupia, Chaurembo, Sheikh Amir n.k.

Historia yake inageuga kuwa ngano kwasababu, kwanza amejenga hisia halafu akaweka matukio juu ya hisia zake.
Hapo ndipo historia inakuwa hisia. Kwa vile anashindana na nguvu ya historia isiyohitaji ''evolution'' amekwama sana katika kujibu hoja, amejikita katika kukimbia hoja na kujiingiza katika trivial things za spelling ili mradi kujisitiri.

Kwa vile historia yake imejengwa katika hisia, Mohamed amejikuta anashambulia wakristo kwa majina na dini zao.
Hilo halikutokea kwa wazee wake hata kama walikuwa ''wahalifu'' kama Amir Kweyamba.
Huyu angekuwa mkristo hicho kingekuwa kiambata cha jina lake.
Hisia zake ndizo zimepelekea kusahau makundi mengine hasa wasio na dini walioshiriki uhuru.

Lengo lake la kuushambulia ukristo kwa hisia na si kwa historia iliyokuwepo limepelekea Mohamed kuwa katika wakati mgumu sana na Wazanzibar na Wanazuoni wengine.

Anamshambulia Nyerere kwa kuandaa mapinduzi huku Ali Hassan, Nosor Moyo, Jumbe na wengine wapo hai na anakutana nao kila mara bila kuwahoji.

Juzi WZNZ waliadhimisha mapinduzi, nikamuuliza Mohamed,je angewambia nini kuhusiana na hilo.
Hakuwa na jibu kwasababu historia ya mapinduzi ya ZNZ inamsuta na wanamapainduzi wanamsuta, waandishi kama Ahmed Rajab wanamsuta hadharani. Hii ni kwanini? Jibu ni rahisi alipokuwa anaandika alitafuta namna ya kumhusisha Nyerere na mapinduzi ili kudhihirisha chuki ya Nyerere dhidi ya Waislam na ushiriki wa kanisa katika dhulma ya waislam.

Hadi hapo kilichobaki ni nini kama si ngano na tamthilia.
Mohamed hakuna swali hapo, hii ni kwa wasomaji.
 
Asanteni sana kwa kuja ila mjue kizazi kijacho kitautaka ukweli historia ya tanganyika ni butu na sijui kwa nn kwa maksudi mazima imefanywa iwe butu ila ipo siku mtakimbiana tu hilo mlitambue lipo tatizo

Kwanini tukimbiane?

Wenye kuiandika historia ya nchi ni mimi, wewe na yule.

Hakuna mjomba kutoka ughaibuni atakaekuja kutuandikia historia ya nchi hii.
 

Ina maana humo huoni hoja ya kujibu!
Kwa nini udhani siye ni wanafunzi wako na wewe Mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…