Waaaaaaooo asante sana ndugu!
Niliambiwa ilikuwa mwaka 1956 pale mnazimmoja Ukumbi wa Anatoglo
Ukumbi huo una historia kubwa sana.
Mkutano wa uchaguzi wa TAA 1953 ulifanywa hapo na ndipo ule uchaguzi maarufu
wa Abdu Sykes na Julius Nyerere ulikofanyika.
Vilevile hapo ndipo Schneider Abdillah Plantan alipofanya vurugu kubwa 1950 kwenye mkutano
wa dharura wa TAA ulipofanyika kutafuta viongozi wapya wa TAA baada ya mapinduzi ya kumng'oa
Mwalimu Thomas Plantan aliyekuwa rais na katibu wake Clement Mtamila.
Waingereza walihudhuria mkutano ule kuja kuwatisha Waafrika.
Schneider, mtoto wa Chief wa Kizulu Mohosh, askari katika jeshi la Kijerumani na askari aliyepigana
dhidi ya Waingereza katika Vita Vya Kwanza alikuwa anawasubiri kwa hamu maofisa wale wa Kiingereza.
Akawaambia hapa hapakaliki hadi uchaguzi umefanyika.
Huyu mtu ana mengi sana...
Kapata kumtukana Nyerere uso kwa uso nyumbani kwake Msasani baada ya kutolewa na Nyerere kizuizini
alipomfunga.
Alikuwa akitembea huku anavuta mguu mmoja kutokana na risasi alopigwa vitani.
Yeye na Kleist walikuwa kwenye battalion moja walipopambana na Waingereza kwa silaha Mwele Juu, Tanga.
Schneider ndiye alikuwa katibu wa Daawati Islamiyya (Wito kwa Waislam) rais wake akiwa Sheikh Hassan
bin Amir.
Uchaguzi huu ndiyo uliowaingiza madarakani Dk. Vedasto Kyaruzi kama rais na Abdu Sykes katibu.
Meneja wa Arnatouglo wakati ule alikuwa Denis Phombeah Mnyasa huyu bwana.
Baadae meneja akaja kuwa Mzee Chihota ambaye alikufa Uingereza katika miaka hiyo hiyo ya 1950.
Huyu Mzee Chihota alikuwa Mzimbabwe.
Hadi leo kuna mtaa Temeke unaitwa ''Chihota.''
Huyu ndiye baba yao Raymond Chihota (marehemu), Norman, Deborah Mwenda na Gershom.