Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said, haya dnakujuza tu kuwa nduguyo mchochezi mwenzio wa maasi ya kiroho Shehe Ilunga yasemekana kashatiwa korokoroni na FBI, bado wewe na wenzio wengine,

Yericko,

Umesahau mara hii kuhusu hotuba ya muago ya Nyerere.

Nilikuasa nikakuambia usishangilie goli kabla mpira haujagusa
nyavu.

Una haraka gani?
Subiri nikamatwe ndiyo ushangilie.

Unadhani mie kuwekwa korokoroni nakuhofia?
Hiyo ni sunna kwa kila asimamiae haki.

Nikiwekwa korokoroni nitakuwa nimewekwa kwa ajili
ya Allah, Mfalme wa Wafalme, Hakimu Muadilifu.
Yeye ambae hakalifu miadi.

Umesahau Nyerere na kesi ya Mzungu wa Geita?
Nyerere kawaita Waingereza ''wanyonya damu.''

Akafunguliwa kesi na hukumu ikawa kifungo au faini.

Nakudokezea.

Sunna ya kufungwa Muislam ni hii.
Akitoka jela heshma na hadhi yake hupanda.

Mimi siogopi kwenda jela kwa kusema kweli kuwa serikali inatudhulumu
Waislamu.

Itakuwa kazi ya mahakama kunitia hatiani kuwa nisemayo si kweli.

Tusubiri.
 

WildCard,

Hebu pitia maneno ya Nyerere hapo juu kwenye maandishi ya blue.
 

Unakubaliana nami nikisema wewe ni mpigania dini na siobmpigania historia ya uhuru?
 
Hawa wazee wazalendo leo hii watu wanawakejeli na kuwadhiaki kuwa hawakufanya chochote katika harakati za kugombania uhuru wa Tanganyika.

Mwaka 1951 Ally Sykes akiwa katibu wa TAGSA alitoa maneno makali dhidi ya serikali ya Uingereza kama mtawala wa Tanganyika.

Ally Sykes aliandikia barua serikali ya kikoloni na kuiomba ijitoe katika utawala wa Tanganyika. Mkutano ulisisitaza kuwa waafrika wa Tanganyika hawakuwa raia wa Uingereza.

Kwa hiyo Malkia hakuwa na mamlaka juu yao. TANU ilieleza kuwa ilimtambua Malkia kama kiongozi wa serikali ya kikoloni inayoongozwa na Gavana Edward Twining.

TANU ilidai bendera ya UNO ipandishwe sawasawa na bendera ya Uingereza ili kuonyesha kuwa mamlaka hizo zote mbili ndizo zinatawala.
 

MM,

Sijafahamu ni vipi CCM inaingia hapa.

Kama uantaka kujua naionaje CCM weka uzi mpya.
Nina mengi na nina hakika tutakuwa na mjadala mzuri.

Ngoja nikuonjeshe kutoka ''In Search of Justice...'' huu bado mswada naupiga msasa.

''The second attempt was more daring as the activists registered their own party the United Peoples’ Congress (UPC).

UPC received its preliminary registration pending full registration upon completion of the laid down regulations as specified by the law.

The party began membership drive but these efforts were bogged down by the secrecy, which was surrounding the party.

The membership drive could not come out into the open because the law establishing political parties barred religious as well as regional based parties.

Despite of all these obstacles UPC leadership believed the party had a special mission to create a political platform for Muslims and would try to have the party registered...''

Mwanakijiji fungua uzi nikushushie vitu hiyo hapo juu inaitwa ''pati gazeti.''
Zomba angekuwa hewani angekupa maana yake.

Ukitaka mimi nikupe maana nipe hela kwanza.
Ukitaka kupambana na Mohamed Said ule ushibe na uage kwenu.
 
Hahaaaa wewe mzee umelaaniwa,
Mbona mjadala huu tu umepwaya je utauweza huo mwingine tena wakisiasa bila udini?
 
Mwalimu ametumia neno "wakatuunga mkono", bila shaka kama chama sio yeye kama Mwalimu.

WildCard,

Msome Nyerere hapa chini.

"Shukran kwa wazee, jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam."
 
Mwalimu ametumia neno "wakatuunga mkono", bila shaka kama chama sio yeye kama Mwalimu.

WC,

Unataka kushinda hoja kwa semantics?
Mjanja sana wewe halafu unanilaumu mimi.

Ehe Mzee Mohamed unakwepa hiki.
Ehe Mzee Mohamed hivi na hivi.

Au WC unafata nyayo za mzee wako na kisha wewe sasa unaboresha
zaidi?

''Wild Card'' hii nikiitumia wakati huo kijana mwanafunzi Ughaibuni najifunza
computer nasoma Dos.

Nyie mmekuta windows.
Dos Command ni wazimu tosha.

Computer Room nikiona kama ''mortuary.''

We umetoka Africa hujaigusa PC hata siku moja sasa Wazungu wanakukabidhi
hilo dude unapoteza spread sheet ya kurasa 10 hujui kuwa ipo command ya
kurejesha hizo figure!

Home Work inatakiwa na mwalimu asubuhi.
Kimbembe.
 
Hahaaaa wewe mzee umelaaniwa,
Mbona mjadala huu tu umepwaya je utauweza huo mwingine tena wakisiasa bila udini?

Yerichko Kambarage Nyerere.
Ahalan Wasaalan sahib wangu.

Bila ya wewe nani angenipa darsa kusomesha.
Kesho Ijumaa nakualika Mandi mchana.

Tutashushia na juice bardiiiiii ya matunda mchanganyiko
Insha Allah.
 
Kwa maneno haya akawa amepigania uhuru kwelikweli! Ally Sykes bado yupo. Mwalimu alimpeleka Italia akawa Balozi wetu mzuri tu huko. Akastaafu, akarudi hapa. Akawa Mwenyekiti wa bodi ya ATC,..., hakusahaulika sana mzee huyu.
 
Yerichko Kambarage Nyerere.
Ahalan Wasaalan sahib wangu.

Bila ya wewe nani angenipa darsa kusomesha.
Kesho Ijumaa nakualika Mandi mchana.

Tutashushia na juice bardiiiiii ya matunda mchanganyiko
Insha Allah.

ha haa haaa! Mandi ya nini ya mbuzi au kuku? na unashushia sheki tende juice "Mujarabu"
 
Kwa maneno haya akawa amepigania uhuru kwelikweli! Ally Sykes bado yupo. Mwalimu alimpeleka Italia akawa Balozi wetu mzuri tu huko. Akastaafu, akarudi hapa. Akawa Mwenyekiti wa bodi ya ATC,..., hakusahaulika sana mzee huyu.
Uhuru alipangania Nyerere peke yake hao wengine wote walikuwa wasaidizi.
 


Mohamed Said ni bwana mkubwa,huyo Mzee Mwanakijiji,sisi tushampuuza mda mrefu sana..

Wala asikughulishe akili,dawa ya watu sampuli hiyo ni kumpuuza tuh..
Bwana mdogo inaonekana maandishi ya mwanakijiji yanakukosesha usingizi kabisa toka huko nyuma umekazana, tumempuuza, tumpuuze..... lakini kinachoonekana wewe ndiye uliyepuuzwa, maana mwanakijiji hajibishani na wwewe lakini kila akitundika post yake umesharukia sasa nani aliyepuuzwa hapa inaonekana kabisa huna hoja yoyote ya kuchangia zaidi ya upambe kwa Mohamed Said. Man up toa hoja ujibiwe hoja sio kukurupukia tu maandiko ya wenzio. Nakunong'oneza tu kama ulikuwa hujui Mwanakijiji amekupuuza....
 

Hujanielewa! siongelei maradhi aliyonayo bali alitaka kuwa Rais wa nchi hii kwa udi na uvumba lakini matokeo yake viti vinawaka moto havikaliki! kila chama kinamtema! sasa kabaki peke yake! yeye ndie Mwenyekiti, mwanachama, na kama sio Kikwete kumnusuru na kumwachia Ubunge, tungekuwa tunaongea mengine! Yaani Mrema amebaki kuwa mtu wa kuchunga ubunge na uenyekiti wa chama kama hicho?

Bila shaka Waislamu hawakumuombea dua ili apate kisukari na mbalanga au kupepesuka! hayo kayapata tokana na stress za misukosuko ya kugombea madaraka lakini dua za Waislamu zinajikita ktk kupoteza madaraka aliyokuwa nayo kuanzia Naibu Waziri Mkuu. Waziri mambo ya ndani, waziri wa kazi, Mwenyekiti NCCR, Rais mtarajiwa hewa, na kuishia uenyekiti na ubunge wa kuonewa huruma!
 
ha haa haaa! Mandi ya nini ya mbuzi au kuku? na unashushia sheki tende juice "Mujarabu"

Ritz,

Hebu acha hatari.
Sheki ya tende imetiwa na njugu na kidogo abasoda.

Huyu sahib wangu nachelea asije pindukwa na tumbo!
 
Uhuru alipangania Nyerere peke yake hao wengine wote walikuwa wasaidizi.
Wewe wasema. Uhuru wa Tanganyika tulifanya kurudishiwa tu na Waingereza. Hakukuwa na mikutano kule Lancaster House au vita kama ile ya MAUMAU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…