Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wanajamvi,
Mara nyingi tumemsikia Mohamed akimtuhumu Mkapa wakati akiwa mhariri wa magazeti.
Hivi karibuni alimtuhumu Mkapa kama mshabiki wa kifo cha EAMWS akiwa na Martin K.
Alimtuhumu kwa kushindwa kuelezea kifo cha Sykes, mtu muhimu sana katika taifa.
Nimemuuliza kuwa Amir Kweyamba anaaungikia wapi katika makundi yake (wazee wake au vibaraka).
Mohamed amesema hilo hana haja ya kulijibu. Japo kaonyesha uungwana kidogo wa kusema hivyo na si dharau na kejeli.
Mantiki ya hapo juu ni kuwa Mkapa anatuhumiwa si kwasababu ya utendaji wake(uwe mzuri au mbaya) bali njia mojawapo ya kumhusisha yeye na Nyerere na Kanisa ili kukidhi matakwa ya kila siku ya ya kujenga historia kwa kutanguliza maoni yake yakifuatiwa na majina na mikasa.
Mohamed ameshindwa kusema Amir Kweyamba ni wa kundi gani kwasababu huyu ni miongoni mwa waliokuwa wanafuatilia nyendo za Sheikh na wenzake. Mohamed anatatizika kusema ni kibaraka kwasababu hizi
1. Ni mwislam na historia yake watatajwa tu lakini si kueleza uovu wao kwa kushirikiana na ''dhalimu''
Kuwasema kutaondoa maana nzima ya waislam kuwa bega kwa bega na Nyerere na kwamba hakukuwa na hujuma zilizofanywa na kundi jingine isipokuwa waislam wenyewe kwa wenyewe.
2. Kumsema Amir Kweyemba kutaondoa dhana ya Nyerere kupandikiza vibaraka BAKWATA kwasababu zama hizo BAKWATA haikuwepo. Anachokikwepa ni kusema ukweli kwamba failure na sucess za waislam hazikuwa na mkono wa kundi analotuhumu bali wao wenyewe.
3. Kutandoa dhana kuwa wakristo walipinga uhuru kwasababu Amir Kweyamba naye si alifanya kazi special unit ya kuwapiga vita wazee wake, sasa hoja kuwa wapo waliopinga itatoka wapi.
Historia ilipaswa umwangalie Amir Kweyamba aliyezuaia harakati mapema kabisa zaidi kuliko mhariri wa gazeti bw. Mkapa aliyefuata baada ya uhuru na ambaye nafasi yake ni finyu kwa nyakati hizo.
Kwa vile lengo ni kupandikiza fikra za chuki hasa dhidi ya ukristo, Mohamed anachagua maovu na waovu wa kuwasema na hapa Mkapa si mwandishi bali Mkristo.Kwa mantiki hiyo hata pale alipofanya vizuri, Mohamed hatathubutu kuandika ili kutokinzana na simulizi yake.
Historia ni ''dead subject'' kwamba imekamilika kama ilivyo na haina nafasi ya evolution.
Anachokihadithia Mohamed ni kweli kilitokea kwa maana ya kuwa watu anaowataja walikuwepo, harakati zilikuwepo n.k. Ni ukweli Sykes walikuwepo, kama Mshume, Kyaruzi, Boman, Rupia, Chaurembo, Sheikh Amir n.k.
Historia yake inageuga kuwa ngano kwasababu, kwanza amejenga hisia halafu akaweka matukio juu ya hisia zake.
Hapo ndipo historia inakuwa hisia. Kwa vile anashindana na nguvu ya historia isiyohitaji ''evolution'' amekwama sana katika kujibu hoja, amejikita katika kukimbia hoja na kujiingiza katika trivial things za spelling ili mradi kujisitiri.
Kwa vile historia yake imejengwa katika hisia, Mohamed amejikuta anashambulia wakristo kwa majina na dini zao.
Hilo halikutokea kwa wazee wake hata kama walikuwa ''wahalifu'' kama Amir Kweyamba.
Huyu angekuwa mkristo hicho kingekuwa kiambata cha jina lake.
Hisia zake ndizo zimepelekea kusahau makundi mengine hasa wasio na dini walioshiriki uhuru.
Lengo lake la kuushambulia ukristo kwa hisia na si kwa historia iliyokuwepo limepelekea Mohamed kuwa katika wakati mgumu sana na Wazanzibar na Wanazuoni wengine.
Anamshambulia Nyerere kwa kuandaa mapinduzi huku Ali Hassan, Nosor Moyo, Jumbe na wengine wapo hai na anakutana nao kila mara bila kuwahoji.
Juzi WZNZ waliadhimisha mapinduzi, nikamuuliza Mohamed,je angewambia nini kuhusiana na hilo.
Hakuwa na jibu kwasababu historia ya mapinduzi ya ZNZ inamsuta na wanamapainduzi wanamsuta, waandishi kama Ahmed Rajab wanamsuta hadharani. Hii ni kwanini? Jibu ni rahisi alipokuwa anaandika alitafuta namna ya kumhusisha Nyerere na mapinduzi ili kudhihirisha chuki ya Nyerere dhidi ya Waislam na ushiriki wa kanisa katika dhulma ya waislam.
Hadi hapo kilichobaki ni nini kama si ngano na tamthilia.
Mohamed hakuna swali hapo, hii ni kwa wasomaji.
Nimekusoma na naheshimu fikra zako.