Ah, sasa nimekuelewa - mkuu nilisha sema humu kwamba Ndugu Mohamed Said is not some monster; sijui kwa nini baadhi ya wana JF wanamuogopa kupindukia - yeye kaandika kitabu chake baada ya kufanya utafiti kwa madhumuni ya kurekebisha pale palipo pinda, sasa kama baadhi ya wasomaji wanaona kuna vitu ambavyo havijafafanuliwa vizuri, cha kufanya ni kumuomba atoe maelezo ya ziada au wenye kujua mengine ya ziada wamshauri arekebishe vipengere ambavyo vimekaa ndio sivyo alafu msikilizeni anatesema nini, lakini tujikita katika malumbano ambayo hayana tija yoyote au kumsema vibaya, actually ninacho ona mimi ni as if kuna ushindani wa aina fulani vile - kama dunia inakubali kihistoria kwamba Wamerikani ndio walikuwa wa kwanza kutua mwezeni, sasa tatizo liko wapi!! Hata mimi zamani nilikuwa na mawazo kama hayo hayo kwamba ukombozi wa Taifa letu dhidi ya Waingereza alianzia mwaka 1954 na akina Paul Bomani, Rashid Kawawa, Titi Mohamed, Kambona na Nyerere nk - hiyo ndiyo historia tulikuwa tunaisikia tukiwa shule ya msingi!! Nilikuja kushtuliwa kutoka usingizini baada ya kukutana na mzungu mmoja (Mwingereza) nikiwa nje masomoni, ikabidi nifanya kazi ya ziada kuelewa ni kitu gani hasa kilikuwa kinajiri wakati wa ukoloni wa Waingereza ndani ya Tanganyika, hicho ndio kilinifanya kidogo nitofautiane na nyinyi katika misimamo yenu.
Hili la bwana Jericko kusema kwamba ndugu Mohamed Saidi ana uwezo wa kunilisha ngano za masika (hapa sijui unamanisha nini!! Najua kiswahili changu kiko a bit rusty lakini hapo nimetoka kapa)! Mkuu Jericko naweza kuelewa your concern katika hilo, lakini nataka kukuhakikishia kwamba ndugu Moh hana uwezo wa kulisha watu mambo ambayo hawayataki kuyasikia - lakini ukiona wasomaji zaidi ya 8K wamepitia uzi huu so far ujue kuna jambo, kumbuka wengi wao wanasoma tu bila ya ku-comment chochote!
Mkuu labda nikufahimishe kwamba najua mambo mengi kuhusu Taifa letu, kwa kulezwa na baba yangu mzazi ambaye aliwahi kuwa Mwalimu pale Tabora mmoja wa wanafunzi wake alikuwa ni Baba wa Taifa, Mh.Kambarage alipokwenda masomoni Makerere mzee wangu alihamishiwa Sekondary ya Bwiru Mwanza - hapo alikutana na mwalimu mwenzake ambaye alikuwa sijuhi ndugu au mjomba wa Kambarage sikumbuki vizuri (lakini nafikili Andrew anaweza kuwa na kumbukumbu kama aliwahi kuzungumza na baba yake kuhusu huyo mwalimu jamaa yao) sasa Kambarage alipokuwa anakuja likizo kutoka Uganda alikuwa na kawaida ya kupitia Bwiru kwa jamaa/ndugu yake huyo kumtembelea na kukutana na mzee wangu kwa mara nyingine, baadae mzee wangu alibadirisha kazi na kuajiliwa katika mambo ya Public Relations na Serikali ya Kingereza na akawa na access kubwa ya Public Addressing Systems na vifaa vingine, kwa hiyo Kambarage alipokuwa anatembelea mikoani akifika kwetu mzee wangu alikuwa anampatia Nyerere system hizo kutangazia wananchi kinyume cha matakwa ya mwajiri wake i.e Wakoloni hivyo hakujali kupoteza ajira yake pindi Waingereza wangepata tetesi kwamba anamsaidia Kambarage, hivyo mzee wangu alikuwa anamfahamu vizuri Kambarage.
Mkuu kuna mambo mengi ninayo yafahamu lakini siyasemi, nilipata bahati ya kwenda nje na kukutana na na Mzee mmoja Mwingereza ambaye aliwahi kuwa PC wakati wa ukoloni, yeye ndiye aliye nishtua kuhusu harakati za wenzetu Waislaam kuhusu kupinga ukoloni - alisema walikuwa wanawapa wakoloni wakati mgumu kwa kuwa walikuwa well organised na ilikuwa si rahisi kuvunja mikakati yao kwa kuwa walikuwa na mbinu nyingi sana - walijaribu kuwatumia baadhi ya Waislaam
katika mambo ya upelelezi kuhusu nyenendo zao bila mafanikio ya kulidhisha mmoja wao nadhani alikuwa ni mtu Kutoka Kagera - Kweyamba kama sikosei, ndugu Moh anaweza kutusadia katika hilo. Sasa mzungu wa watu alikuwa na maslahi gani katika kunieleza ukweli huo; kwa nini hatutaki kukubali kwamba mambo mengi aliyo andika ndugu Moh yana ukweli ndani yake - ndugu zangu kwani tukikubali tutapoteza nini? Turekebisha pale penye mapungufu au palipo sahaulika bila ya kujali kama mleta marekebisho ni mwislaam, mkristo au mpagani.