Bukyanagandi;5816766]Ndugu Mohamed Said is not some monster; sijui kwa nini baadhi ya wana JF wanamuogopa kupindukia - yeye kaandika kitabu chake baada ya kufanya utafiti kwa madhumuni ya kurekebisha pale palipo pinda, sasa kama baadhi ya wasomaji wanaona kuna vitu ambavyo havijafafanuliwa vizuri, cha kufanya ni kumuomba atoe maelezo ya ziada au wenye kujua mengine ya ziada wamshauri arekebishe vipengere ambavyo vimekaa ndio sivyo alafu msikilizeni anatesema nini
Ndugu yangu ni ngumu sana kutafuta wapi umweke Mohamed Said.Unatakiwa kumfahamu kabla ya kumchukulia dhamana.
Hakika kama humuopopi MS kuna tatizo. Huyu ni mtu anayeweza kusimama na kuhadithia kuwa maziwa ya ng'ombe yanatoka katika mafenesi na si ngombe hundreds times.
FYI Mohamed is a master mind behind the turmoil seen recently.
He is a gifted story teller with incendiary power.
Ni kwasababu ulizosema tumekuwa na MS mara kadhaa tukitaka kurekebisha pale palipopinda. MS hakubali hilo kwasababu ya madai kuwa anatoa mada Ulaya. Kila tukimtaka ataoe maelezo ya ziada ima anshindwa au anapindisha ukweli na wakati mwingine anakimbia kama si kutoka nje ya swali, hoja au mada.
Hivi ninavyokuambia kuna hoja na maswali lukuki aliyoshindwa kuyajibu, kuyatetea au kutolea maelezo japo kwa fikra. Silaha kubwa ya majaliano aliyo nayo ni kuandika sana na kualikwa ulaya.Mtamwambia nini ninyi wamatumbi!
Badala ya kuwashambulia wanaotaka record ziwe straight ungemshauri MS asimame kidete kutetea hoja zake kwa mantiki. Nadhani umesoma na kuona contradictions nyingi kwa MS mwenyewe na ya mwisho ni hiyo niliyoweka akakana maneno yake achilia mbali wale anaowasemea kumkana bila yeye kujielewa
lakini tujikita katika malumbano ambayo hayana tija yoyote au kumsema vibaya, actually ninacho ona mimi ni as if kuna ushindani wa aina fulani vile - kama dunia inakubali kihistoria kwamba Wamerikani ndio walikuwa wa kwanza kutua mwezeni, sasa tatizo liko wapi!! Hata mimi zamani nilikuwa na mawazo kama hayo hayo kwamba ukombozi wa Taifa letu dhidi ya Waingereza alianzia mwaka 1954 na akina Paul Bomani, Rashid Kawawa, Titi Mohamed, Kambona na Nyerere nk - hiyo ndiyo historia tulikuwa tunaisikia tukiwa shule ya msingi!! Nilikuja kushtuliwa kutoka usingizini baada ya kukutana na mzungu mmoja (Mwingereza) nikiwa nje masomoni, ikabidi nifanya kazi ya ziada kuelewa ni kitu gani hasa kilikuwa kinajiri wakati wa ukoloni wa Waingereza ndani ya Tanganyika, hicho ndio kilinifanya kidogo nitofautiane na nyinyi katika misimamo yenu.
Mkuu, Malumbano haya yanatija sana kwasababu moja kubwa. Kuzuia upotoshaji kwa vizazi vijavyo, kuzuia maafa yatokanayo na upotoshaji na kuzuia ongezeko la wapotoshaji duniani.
Niseme kwa nafsi yangu ambayo nina hakika wengi ndipo wanaposimamia. Alichokiandika Mohamed ni historia ya matukio ambayo yalikuwepo. Kleist Syke alikuwepo, Abdul Sykes alikuwepo n.k. Hakuna anayekataa uwepo wa baadhi ya matukio hayo kwasababu historia haiumbwi inajiumba.
Lakini basi hivi tukubali tu kuwa Rais wa kwanza wa AA ni K.Sykes alimyemkabidhi mtoto wake A.Sykes TAA halafu TANU! Kupitia malumbano haya wengi wamejua huo ni uongo, uzushi na uzandiki mzuri tu.
Kwa mfano huo mmoja katika ya mamia unataka tukae chini na kumeza tu! Please tuonee huruma nduguzo.
Akili zetu tutazitumia wapi na lini!!
Hili la bwana Jericko kusema kwamba ndugu Mohamed Saidi ana uwezo wa kunilisha ngano za masika (hapa sijui unamanisha nini!! Najua kiswahili changu kiko a bit rusty lakini hapo nimetoka kapa)! Mkuu Jericko naweza kuelewa your concern katika hilo, lakini nataka kukuhakikishia kwamba ndugu Moh hana uwezo wa kulisha watu mambo ambayo hawayataki kuyasikia - lakini ukiona wasomaji zaidi ya 8K wamepitia uzi huu so far ujue kuna jambo, kumbuka wengi wao wanasoma tu bila ya ku-comment chochote!
Ndugu yangu kupitia JF na mnakasha huu Mohamed has been brought to his knee by admitting mistakes, accepting facts and most important he has purge and expunge some of his rhetoric and toxic materials.
FYI hii si mara ya kwanza kuwa na mnakasha na MS na kila mara wasomaji wameongezeka. Maana yake si kuwa wanamsoma MS, wapo waliomsoma na sasa wanatazama upya kurasa walizosoma.
Wapo wenye maswali ambayo kupitia mjadala wanapata ufahamu wa sehemu ya pili.
Muhimu sana ajenda, nia na dhamira ya Mohamed sasa vipo wazi kuliko wakati mwingine wowote.
Ngano ni masimulizi matamu ya kusadikika yanayotumia mazingira na yasiyoweza kuthibitika, kuthibitishwa, kutetewa au kujitetea zaidi ya ujumbe wake kumfanya msikiliza ayafurahie.
Mkuu labda nikufahimishe kwamba najua mambo mengi kuhusu Taifa letu, kwa kulezwa na baba yangu mzazi ambaye aliwahi kuwa Mwalimu pale Tabora mmoja wa wanafunzi wake alikuwa ni Baba wa Taifa, Mh.Kambarage alipokwenda masomoni Makerere mzee wangu alihamishiwa Sekondary ya Bwiru Mwanza - hapo alikutana na mwalimu mwenzake ambaye alikuwa sijuhi ndugu au mjomba wa Kambarage sikumbuki vizuri (lakini nafikili Andrew anaweza kuwa na kumbukumbu kama aliwahi kuzungumza na baba yake kuhusu huyo mwalimu jamaa yao) sasa Kambarage alipokuwa anakuja likizo kutoka Uganda alikuwa na kawaida ya kupitia Bwiru kwa jamaa/ndugu yake huyo kumtembelea na kukutana na mzee wangu kwa mara nyingine, baadae mzee wangu alibadirisha kazi na kuajiliwa katika mambo ya Public Relations na Serikali ya Kingereza na akawa na access kubwa ya Public Addressing Systems na vifaa vingine, kwa hiyo Kambarage alipokuwa anatembelea mikoani akifika kwetu mzee wangu alikuwa anampatia Nyerere system hizo kutangazia wananchi kinyume cha matakwa ya mwajiri wake i.e Wakoloni hivyo hakujali kupoteza ajira yake pindi Waingereza wangepata tetesi kwamba anamsaidia Kambarage, hivyo mzee wangu alikuwa anamfahamu vizuri Kambarage.
Kwanza tumshukuru sana mzee wako kwa uzalendo wake wa kulitumikia taifa hili hata pale alipoweka maisha ya watoto wake kama wewe on the line.
Huyu ni one too many katika wale tunawaowaongelea na kuwatetea.
Hakika kupitia yeye na wenzake sote tupo huru tena kama taifa.
Maelezo haya yanatusadia kututetea pale tunaposema harakati za uhuru zilizagaa nchi nzima na si Tandamti, Kidogo chekundu au Narung'ombe kama MS anavyouaminisha ulimwengu.
Lakini pia unatutetea ya kuwa wazalendo kama baba yako hawakufanya hayo kama wakristo,waislam au Wanyamwezi.
Hapa ndipo tunapoachana sana na MS kwa kutaka kuibadili hsitoria, kufifisha heshima za watu na kukweza watu bila sababu.
Baba yako alifanya hayo kwa faida yako wewe na sisi sote bila kujali kabila, dini, Umanyema au Unubi.
Ndivyo malefu ya watu walivyofanya kote nchini.Ni tusi kubwa kwa watu kama baba yako pale tunaposikia kuwa kama si wazulu, wamanyema na wanubi tusingepata uhuru.
Baba yako hajaeleza fadhila zake kwa Nyerere, yeye amebaki kuwa rafiki wa Nyerere.
Leo tunaambiwa Nyerere alikwenda sokoni bila kujua kuwa anapaswa kuwa na fedha na wewe unataka tuamini tu kwasababu imeandikwa.
Tunachosem ni kuwa wazalendo wapewe heshima zao kama Watanganyika na si kwasbabu ni Wazulu, Wamanyema au Wanubi. Wazalendo waheshimiwe kwa mchango wao na si kwa imani zao kama ilivyokusudiwa kutugawa kutoka kwa MS.
Na yaandikwe ya kweli si kuficha baadhi, kusingizia, kuzua au kuweka maneno midomoni mwa marehem kwasababu tu hawawezi kujitetea.
Sijui kama baba yako au wewe mnadai nafasi pekee katika taifa hili kwasababu tu mzee ali risk kutoa vifaa vya sauti.
Sijui kama mna madai ya kwanini ninyi hamjapewa uwaziri n.k. kwasababu tu ya historia.
Na wala sijui kuwa mnaonewa na kudhulumiwa kwasababu ya historia ya mzee wako.
Kama sivyo, kwanini MS atake hayo yatokee? Kwamba yeye anapaswa kuwa waziri kwasababu babu yake aliongoza mgomo wa bandari!
Sasa mzungu wa watu alikuwa na maslahi gani katika kunieleza ukweli huo; kwa nini hatutaki kukubali kwamba mambo mengi aliyo andika ndugu Moh yana ukweli ndani yake - ndugu zangu kwani tukikubali tutapoteza nini? Turekebisha pale penye mapungufu au palipo sahaulika bila ya kujali kama mleta marekebisho ni mwislaam, mkristo au mpagani.
Nikushukuru kwa kutambua kuwa kuna ya ukweli na ya uongo.
Nadhani mimi na wengine hatuna tatizo na yale ya ukweli, tatizo letu lipo katika yale ya uongo.
Tupo hapa kurekebisha yale yenye mapungufu, but we don't have the right partner.
Sisi tunasimamia ukweli, MS anasimamia agenda yake so we don't have the common ground.
May be it's time you reach MS and convince him to join us regardless of our social differences for the betterment of this nation.Please let him understand that bigotry, hatred, incendiary comments, fallacy and the likes are contrary to Islamic teaching, they're inhumane and ''toxic asset'' we can pass on to next generation.
Huo mstari wa mwisho niliokazia, hapo ndipo MS asipokubaliana nawe.
Agenda yake ni kudhalilisha jamii nyingine na kuleta mifarakano, vipi akubali marekebisho yatokayo huko.
Ameandika kitabu ku-attack wakristo sasa atakubali vipi maoni ya watu wenye imani tofauti na yeye.
Nimalizie kwa kusema tatizo ni MS si wale wanaotaka kuweka record straight!