Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kumbe historia ya nchi hii ilipotoshwa kiasi hiki??

Tunashukuru sana leo kuja kuufahm ukweli,sasa hao wanaosema chuki za MOHAMED SAID,,

Chuki ziko wapi??
 
Ritz,
Mimi sivuti bangi, lakini nampenda Bob Marley. It is the message in his song and not his lifestyle that moves me. Kilevi changu ni wine, basi. Hata bia ya safari siku hizi sinywi baada ya makaburu kuichakachuwa.
Sifa za kijinga! kunywa wine umeona issue eti ndio ma great thinkers upumbavu mtupu saa nyingine muwe munaficha upumbavu sio kilakitu ni cha kuleta hapa
 
Jasusi,

Naamini unajua kuwa sijawahi kugusia ustaarabu wa Nyerere katika
mjadala huu.

Huwa sifurahishwi na maneno yanayoweza kumvunjia adabu mtu mzima.

Katika mihadhara yako hujawahi kusahihisha hili au hata kuonekana kulikemea... na hivyo kwa mtu ambaye anazungumzia heshima kwa wazee wake inaonekana ni kukubaliana nalo... hasa unapoleta stori za Mtu mzima kwenda sokoni bila senti hata moja mfukoni akitumaini kuokota njiani...
 
Kumbe historia ya nchi hii ilipotoshwa kiasi hiki??

Tunashukuru sana leo kuja kuufahm ukweli,sasa hao wanaosema chuki za MOHAMED SAID,,

Chuki ziko wapi??

KI,

Wakati mwingine mie hujisemea huenda hawa jamaa wanabisha kwa kutokujua.

Nimeeleza kuwa Abdu Sykes akifahamiana na Jomo Kenyatta katika miaka ya 1950
mdogo wake Ally akimjua Kenyatta Nairobi katika miaka ya 1940s mwishoni.

Nawaambia Ally Sykes akiandikiana na Kenneth Kaunda 1953.
Imepita taharuki nzito.

Jamaa wamekuwa kama wamepigwa na radi ya saa saba mchana jua kali.

Ndugu zangu wananishika uongo.

Kote ninakopita ulimwenguni nikieleza haya maswali huwa yanalenga kutaka taarifa zaidi.

Hapa nyumbani naitwa "mwongo," "mzandiki," "mchochezi."
Wanatamani kuwa historia hii ingeanza na Nyerere.

Tujalie tuikatae historia hii...
Ndiyo tutakuwa tumejenga au tunabomoa muruwa wetu?
 

MM,

Hili jambo ni la kweli na wala nikilihadithia ikiwa utanisikiza wewe
kwa masikio yako hutakereka utaona ule umoja na mapenzi ya TANU.

Wewe ni mgeni Dar es Salaam wala hujui mila na tamaduni zetu.

Mimi babu yangu Shariff Mwamedi akiuuza kuku pale sokoni.
Alikuwapo Shariff Attas, Shariff Mbayamtu na Mkuu wa Soko
Abdu.

Mimi wajomba zangu wawili walikuwa na ubao wa biashara pale.
Najua ninachosema.

Wala hicho kikapu asingeingia nacho ndani.
Kingedakwa nje na yeye kurudishiwa kimejaa.

Lakini wewe una nini na wazee wangu wewe?
Ati "ataokota."

Kaka hukuwepo.
Sisi wazee wetu ndio walofanya haya kwa mapenzi na udugu.

Usiifananishe TANU ile ya Sheikh Suleiman Takadir 1950s na
hii CHADEMA yako...

TANU ilikuwa na historia ya pekee Afrika nzima.
Uliza akina Mzee Ngombale watakuambia.

Ngombale anasema yeye kaingizwa TANU na Ally Sykes 1954.
 


Wewe usiwe na shaka,wengi tunaosoma na kupima tumeyaelewa na Insha allah tutakuwa mabalozi wa kuwafikishia wengine walio mbali na wasio na uwezo wa kupatikana katika vyanzo kama hivi vya habari na elimu..
Waache waendelee kukejeli wewe endelea kutoa elimu na insha allah jazaa yako ni kubwa sana kwa mola..
 

Ahsante kwa kuweka mambo sawa.
Ubarikiwe.
 
Ahsante kwa kuweka mambo sawa.
Ubarikiwe.

MK,

Amin.

Sasa mambo yalipotulia na serikali ikajatambua kuwa Padri Lwambano
ni mwongo na uongo wake ndiyo uliosababisha mauaji ya Waislam serikali
ikawa haijui ifanye nini.

Ndiyo maana ikakataa kufanya uchunguzi na kufanya Inquest kama sheria
za nchi zinavyoelekeza.

Waislam wakabaki kuelekeza kilio chao kwa Allah wakifata maneno ya Mtume
SAW aliposema dua ya aliyedhulumiwa haina pazia iogopeni.
 
Hivi, kule Scotland na baridi yote ile Nyerere alikuwa akivaa kaptura tu mpaka alipofika Dar?
Jasusi swali la msingi kabisa hilo. Humu kuna michango inayoonyesha chuki za wazi kwa Hayati mwalimu Nyerere na kutaka kumdhalilisha kuwa Ustaarabu na ujanja alikuja kuufahamia kwa wazee wa Kariakoo jambo ambalo si kweli.
Hata hivyo,kama alivyosema Mag3 hapo juu bado Nyerere atabaki ndani ya 5 bora ya viongozi mashuhuri na wazalendo kupata kutokea barani Afrika. Hilo hata watu waandike vitabu vyao hawawezi kulifuta kwa sasa.
 
Lakini wewe una nini na wazee wangu wewe?
Ati "ataokota."

Inaonekana basi wazee wako walikuwa na heshima ya kweli na mapenzi kwa Nyerere kuliko nyinyi watoto wao. Lakini kama wazee wako ndio hawa wazee wa Kitanganyika ambao walipendana kweli na udugu wa kweli na ndugu zao Wakristu; hawa ambao hawakutaka kumdhuru Nyerere - sababu ya Ukatoliki wake - akikaa katikati yao; hawa wazee ambao walikuwa tayari kwenda kulinda Kanisa ili Nyerere asali pale na wakienda naye kwenye kufanya dua na matambiko; hawa wazee hawa huko waliko lazima wakushangae unayoyasema dhidi ya Nyerere na kumdunisha mbele ya Waislamu watu ambao Nyerere aliwapenda, walimpenda, alisimama nao na yeye akasimama nao hadi mauti. Hii faraka uliyoianzisha wewe wala haina sifa wa kujitamba. Unapaswa ufikirie mara mbili unavyotumia majina ya wazee wetu hawa kuwagawanya Watanzania na kuchochea fitna kati yetu bila kuchoka.

Leo maskini wa Mungu unafurahia unaposikia vijana wa Kiislamu - pasi ya kujua - wanamlaani Nyerere, leo mzee unafurahia kusikia Nyerere anaitwa Dhalim ukiamini unafanya jema? Leo Nyerere anatukanwa na kubezwa kwa sababu ya histohisia ya maandishi yako na unasimama kutumia jina la wazee kuhalalisha?

Lahaula! Mzee Said mrudi Mungu, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe madhambi yetu na mwenye kutujalia neema ndogo ndogo na neema kubwa kubwa! Atakupa nafasi usaidia kuliponya taifa lako ambalo kwa kutumia mikuki yako ya maeneno umelijeruhi na sasa damu inamwagika huku ukiwafurahia marafiki zako ambao wametangaza kutaka kuwaua ndugu zao Wakristu pasi ya sababu yoyote ile. Mwenyeewe unajiaminisha kuwa unafanya hivyo kwa jina la Dini..

Mzee Said mwombe toba Mnyezi Mungu!!
 

Chakaza,

Unajitia hofu pasi na sababu hakuna mwenye uwezo wa kufuta historia
ya Nyerere wala hakuna njama na ujanja wa kumfifilisha.

Wala ukubwa wake hakuna atakaethubutu kuupinga kwani atashindwa
vibaya.

Mimi ninachosema katika kitabu changu ni kuwa historia ya uhuru wa
Tanganyika ina mashujaa wengi ambao wamefutwa.

Kitabu changu kimewarudisha katika historia.
 

MM,

Matatizo yalianza baada ya uhuru kupatikana.
Nimeeleza kwa kirefu yote katika kitabu changu.

Mpaka inaingia 1980s TANU inaandika historia
yake hawa wazee wangu wakafutwa kabisa.

Tusijirudie tutawachosha wasikilizaji.
Insha Alla watafika 100,000.
 

Wewe mbona utajakusikia ukimkemea mwenzako Mag3 ambaye mnashirikiana humu kupambana na Mohamed Said amesema ni matusi makubwa kuwataja Abdalwahid Sykes na Mshume Kiyate.

Kwako wewe unaona kawaida sababu wametajwa wazee wa Kiislam.

Hapa ndiyo jamaa ya Kiislam inapowaona nyie ni maadui wao wakubwa.
 

Lakini Mzee Said, ni wewe uliyesema hadi mwaka 1975 hhivi Nyerere alikuwa anawakumbuka wazee waliomkaribisha Dar tena kwa heshima kubwa. Ni lini baada ya Uhuru matatizo yalipoanza?
 
Ndugu yangu ni ngumu sana kutafuta wapi umweke Mohamed Said.Unatakiwa kumfahamu kabla ya kumchukulia dhamana.

Hakika kama humuopopi MS kuna tatizo. Huyu ni mtu anayeweza kusimama na kuhadithia kuwa maziwa ya ng'ombe yanatoka katika mafenesi na si ngombe hundreds times.

FYI Mohamed is a master mind behind the turmoil seen recently.
He is a gifted story teller with incendiary power.

Ni kwasababu ulizosema tumekuwa na MS mara kadhaa tukitaka kurekebisha pale palipopinda. MS hakubali hilo kwasababu ya madai kuwa anatoa mada Ulaya. Kila tukimtaka ataoe maelezo ya ziada ima anshindwa au anapindisha ukweli na wakati mwingine anakimbia kama si kutoka nje ya swali, hoja au mada.

Hivi ninavyokuambia kuna hoja na maswali lukuki aliyoshindwa kuyajibu, kuyatetea au kutolea maelezo japo kwa fikra. Silaha kubwa ya majaliano aliyo nayo ni kuandika sana na kualikwa ulaya.Mtamwambia nini ninyi wamatumbi!

Badala ya kuwashambulia wanaotaka record ziwe straight ungemshauri MS asimame kidete kutetea hoja zake kwa mantiki. Nadhani umesoma na kuona contradictions nyingi kwa MS mwenyewe na ya mwisho ni hiyo niliyoweka akakana maneno yake achilia mbali wale anaowasemea kumkana bila yeye kujielewa Mkuu, Malumbano haya yanatija sana kwasababu moja kubwa. Kuzuia upotoshaji kwa vizazi vijavyo, kuzuia maafa yatokanayo na upotoshaji na kuzuia ongezeko la wapotoshaji duniani.

Niseme kwa nafsi yangu ambayo nina hakika wengi ndipo wanaposimamia. Alichokiandika Mohamed ni historia ya matukio ambayo yalikuwepo. Kleist Syke alikuwepo, Abdul Sykes alikuwepo n.k. Hakuna anayekataa uwepo wa baadhi ya matukio hayo kwasababu historia haiumbwi inajiumba.

Lakini basi hivi tukubali tu kuwa Rais wa kwanza wa AA ni K.Sykes alimyemkabidhi mtoto wake A.Sykes TAA halafu TANU! Kupitia malumbano haya wengi wamejua huo ni uongo, uzushi na uzandiki mzuri tu.

Kwa mfano huo mmoja katika ya mamia unataka tukae chini na kumeza tu! Please tuonee huruma nduguzo.
Akili zetu tutazitumia wapi na lini!! Ndugu yangu kupitia JF na mnakasha huu Mohamed has been brought to his knee by admitting mistakes, accepting facts and most important he has purge and expunge some of his rhetoric and toxic materials.

FYI hii si mara ya kwanza kuwa na mnakasha na MS na kila mara wasomaji wameongezeka. Maana yake si kuwa wanamsoma MS, wapo waliomsoma na sasa wanatazama upya kurasa walizosoma.

Wapo wenye maswali ambayo kupitia mjadala wanapata ufahamu wa sehemu ya pili.
Muhimu sana ajenda, nia na dhamira ya Mohamed sasa vipo wazi kuliko wakati mwingine wowote.

Ngano ni masimulizi matamu ya kusadikika yanayotumia mazingira na yasiyoweza kuthibitika, kuthibitishwa, kutetewa au kujitetea zaidi ya ujumbe wake kumfanya msikiliza ayafurahie. Kwanza tumshukuru sana mzee wako kwa uzalendo wake wa kulitumikia taifa hili hata pale alipoweka maisha ya watoto wake kama wewe on the line.

Huyu ni one too many katika wale tunawaowaongelea na kuwatetea.
Hakika kupitia yeye na wenzake sote tupo huru tena kama taifa.

Maelezo haya yanatusadia kututetea pale tunaposema harakati za uhuru zilizagaa nchi nzima na si Tandamti, Kidogo chekundu au Narung'ombe kama MS anavyouaminisha ulimwengu.

Lakini pia unatutetea ya kuwa wazalendo kama baba yako hawakufanya hayo kama wakristo,waislam au Wanyamwezi.
Hapa ndipo tunapoachana sana na MS kwa kutaka kuibadili hsitoria, kufifisha heshima za watu na kukweza watu bila sababu.

Baba yako alifanya hayo kwa faida yako wewe na sisi sote bila kujali kabila, dini, Umanyema au Unubi.
Ndivyo malefu ya watu walivyofanya kote nchini.Ni tusi kubwa kwa watu kama baba yako pale tunaposikia kuwa kama si wazulu, wamanyema na wanubi tusingepata uhuru.

Baba yako hajaeleza fadhila zake kwa Nyerere, yeye amebaki kuwa rafiki wa Nyerere.
Leo tunaambiwa Nyerere alikwenda sokoni bila kujua kuwa anapaswa kuwa na fedha na wewe unataka tuamini tu kwasababu imeandikwa.

Tunachosem ni kuwa wazalendo wapewe heshima zao kama Watanganyika na si kwasbabu ni Wazulu, Wamanyema au Wanubi. Wazalendo waheshimiwe kwa mchango wao na si kwa imani zao kama ilivyokusudiwa kutugawa kutoka kwa MS.
Na yaandikwe ya kweli si kuficha baadhi, kusingizia, kuzua au kuweka maneno midomoni mwa marehem kwasababu tu hawawezi kujitetea.

Sijui kama baba yako au wewe mnadai nafasi pekee katika taifa hili kwasababu tu mzee ali risk kutoa vifaa vya sauti.
Sijui kama mna madai ya kwanini ninyi hamjapewa uwaziri n.k. kwasababu tu ya historia.
Na wala sijui kuwa mnaonewa na kudhulumiwa kwasababu ya historia ya mzee wako.
Kama sivyo, kwanini MS atake hayo yatokee? Kwamba yeye anapaswa kuwa waziri kwasababu babu yake aliongoza mgomo wa bandari! Nikushukuru kwa kutambua kuwa kuna ya ukweli na ya uongo.
Nadhani mimi na wengine hatuna tatizo na yale ya ukweli, tatizo letu lipo katika yale ya uongo.

Tupo hapa kurekebisha yale yenye mapungufu, but we don't have the right partner.
Sisi tunasimamia ukweli, MS anasimamia agenda yake so we don't have the common ground.

May be it's time you reach MS and convince him to join us regardless of our social differences for the betterment of this nation.Please let him understand that bigotry, hatred, incendiary comments, fallacy and the likes are contrary to Islamic teaching, they're inhumane and ''toxic asset'' we can pass on to next generation.

Huo mstari wa mwisho niliokazia, hapo ndipo MS asipokubaliana nawe.
Agenda yake ni kudhalilisha jamii nyingine na kuleta mifarakano, vipi akubali marekebisho yatokayo huko.

Ameandika kitabu ku-attack wakristo sasa atakubali vipi maoni ya watu wenye imani tofauti na yeye.
Nimalizie kwa kusema tatizo ni MS si wale wanaotaka kuweka record straight!
 

Nguruvi,

Ndugu yangu wakati mwingine unaniudhi pasi kiasi.
Sikiza kisa hiki.

Katika Battle of Alamein mabingwa wa vita vya matanki walikutana uso kwa uso
hapo Alamein, Misri wakati wa Vita Vya Pili Vya Dunia.

Upande wa Allied Forces yuko George Patton na upande wa Axis yuko Erwin Rommel
maarufu ''The Desert Fox.''

Patton akaomba askari wake wamwonyeshe tanki alokuwa kapanda Rommel.
Akaonyeshwa.

Patton akasema yeye alitaka kujua Rommel yuko wapi ili apiganenae kwa kuwa yeye
hapendi kupigana na mtu dhaifu.

Nami halikadhalika Yericko na mfano wake sitaki kupambananao.

Nguruvi ikiwa husomi vizuri utakuwa dhaifu katika hoja zako.
Naamini umenipata.

Sijapata kusema Kleist alikuwa rais wa AA.
Wapi nimesema kama si Wamanyema, Wazulu nk uhuru usingekuja?

Unaweza kuweka hizo post hapa au hata kusema wapi maneno hayo yapo katika kitabu
changu?

Ndiyo kila mara nachagiza jamani someni kwanza kabla ya kuandika.

Kleist katika jumuia zote aloanzisha hiyo AA na Al Jamitul Islamiyya alikuwa katibu
kwa kuwa alikuwa na ujuzi mkubwa wa kuandika na akijua kupiga type writer, akisema
Kijerumani na Kiingereza.

Ujuzi adimu sana kwa Mwafrika wakati ule.

Sasa kuhusu Abdu kuchukua uongozi wa TAA 1950 chama alichoanzisha baba yake kama
wewe unaona ni uongo ni sawa kwangu wala povu halinivuji.

Lakini nimeweka hapa TAA Political Subcommittee ya 1950 pamoja na rejea zake kutoka kwa
Cranford Pratt na kutoka Sykes' papers Abdu akiwa katibu wa kamati hiyo.

Nguruvi najua una mshtuko ni tabu kuamini haya.
Prof. Haroub kama wewe alitaabika sana na kitabu changu.

Sheikh Ali Muhsin Barwani yeye baada ya kusoma kitabu changu alinialika kabisa Oman anione
kwa jicho lake nikenda tukaonana.

Halikadhalika University of Ohio na Northwestern US na Zentrum Moderner Orient (ZMO) Berlin
na kwengine Afrika.

Siku zote namshukuru Allah kwa kunipa hii hidaya.
Hii ya mie kwenda Ulaya isikukere.

Nimekwenda Ulaya hata kabla sijaandika kitabu na kwa mara nyingi.
 
Unaambiwa marehem Miriam Makeba hakuwa anatumia hiyo bange yako.
 

Ritz,

Unajua leo nimekuwa mtu mzima hukaa nikarudi nyuma kuangalia nilikotoka na
niliyojifunza katika maisha yangu.

Nilipokuwa mtoto hamu yangu ilikuwa kuja kuwa star footballer nicheze Sunderland
kisha timu ya taifa.

Lakini nadhani sikuwa na ile ''what it takes'' kipaji changu kilikuwa chini kwa kuwa wako
wenzangu walifanikiwa na kuweka majina katika vilabu vikubwa vya Dar es Salaam ya
1960/70s.

Kuna kitu nilijifunza katika mpira.
Nilikuwa nikikabwa na watu wawili ilikuwa ni wepesi kuwatoka kuliko mmoja.

Mimi Mag3 na Ngurivi34 wananipa raha sana wanapokuja kujaribu kupambana na mimi
najiona niko Tua Tugawe 1960s beki mkali Atika Kombo na mwenzake Mandemla wananikamia
kunikomesha hiki ''kitoto cha magorofani'' kinajidai kijanja sana...

Naingia na mpira kwa kuwafata uso kwa uso na wao huwa na hofu ya kuogopa kupigwa chenga
na kitoto itakuwa aibu kila mmoja anamtegea aende mwenzake.

Ikiwa uko kidogo nje ya 18 na kuna ule upigaji wa mkono wa kulia nje pembeni more often than not
goli huingia.

Basi huwa hivi ndivyo fikra zangu huzitoa kule leo nikazileta kwa hawa ndugu zangu.
Wakinichangia ndiyo wanavyonidhihirishia maneno ya maalim wangu Sheikh Haruna.

Akisema, ''Na hayo mabuku ya skuli unatalii vizuri naukiyatalii vyema utakuwa mjuzi na hapo wewe
utakuwa rais katika mnakasha wowote... utatawala.''

Allah amlipe pepo.
Amin.
 
Hampo wengi, upo wewe, Dullah, Zomba na Ritz!
 
Hampo wengi, upo wewe, Dullah, Zomba na Ritz!

G,

Hakika sisi ni wachache.
Tumekuja kukfanyieni vita kwenye uwanja wenu juu ya uchache wetu.

Lakini usisahau kuna wasikilizaji 80,000 plus wametega masikio wanatusikiza.
Hawa ndiyo muhimu kwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…