Views 84164 si haba,ujumbe umewafikia wengi sana,na wengi wanazidi nufaika kwa Elimu hii kubwa kupata kutokea katika historia ya nchi yetu,sisi na walio wengi wanaofuatlia mjadala huu hatuoni uchochez uko wapi,
Na hawa wanaopinga na kukejeli hawaeleweki hasa hoja zao za msingi ni zipi..
Eeeh ee! Unakosea muungwana. Hakuna anayempinga Mohamed kama ambavyo hakuna anayeweza kupinga Musiba au Hardley chase.
Wapo wanaopinga upotoshaji, uzushi, uenezaji wa chuki, uzandiki na ubabaishaji. Sijui kama hao ndio wanaompinga!
Mwenzetu umejiunga leo na ID mpya, hata hivyo ahadi yetu ni kuwa ''you will run but not find a heaven place to hide''
Kabla sijakuuliza maswali napenda niweke rekodi sawa.
Hii ngano ni historia ya wazee wa Kidongo chekundu, Narung'ombe, Tandamti na Mchikichi. Jambo jema kabisa!
Kwa mshangao imegeuzwa kuwa historia ya Tanganyika.
Huo ni uchochezi wa awali kwasababu uchochezi ni kushadidia jambo usilo na ushahidi nalo au kupigia debe kisichokuwepo au kilichopo lakini kwa kupindua habari.Msingi wa uchochezi ni kuleta farki, husda, inda na hatimaye vurugu katika jamii.
Anapotokea mtu akawagawa watu kwa imani huyo ni mchochezi.
Imani za dini zinaelekeza utangamano miongoni mwa walioamini na wasio amini.
Ndivyo Mitume, Manabii, maswahba na mahalifa walivyosihi tangu enzi za kale.
Anayekwenda kinyume na misingi hiyo ya dini, basi huyo anatumia dini kwa malengo na si kuitumikia kama ilivyoagizwa.
Hatua ya kuwagawa watu imekwenda mbali kiasi cha kuaminisha ulimwengu kuwa kama si Wamanyema ambao asilimia 100 ni waislam, wazulu waliokuja Tanganyika ambao asilimia 99 kasoro mwalimu Thomas ni waislam na Wanubi basi uhuru wa nchi hii ungekuwa matatani.
Nadhani unajua yanayotokea DRC. Watusi walipewa hifadhi kama raia na sasa wanadai nchi isyokuwa yao.
Yaani wamefikia mahali pa kuwaondoa wamanyema katika nchi yao.
Sasa tunapokuwa na wamanyema nao wakaanza na madai ya namna hiyo, hivi hapo huoni hatari ndugu yangu.
Hebu fanya kautafiti kasiko rasmi uangalie nyuma ya vurugu za kidini wapo watu wa aina gani nakutoka eneo gani la nchi hii.
Ndugu yetu, inawezekana kabisa wale wasiokubaliana na Mohamed wamepotoka, na kwa vile umekuja na ID mpya unaweza kutusadia kwa mawazo mapya. Wapi ambapo Mohamed amepingwa au kukoslewa kwa uonevu tu.
Kwanini basi ngano isiwe na ukweli ili kuweka rekodi sawa sawa!
Ni kwanini hotuba maarufu ya Waikela isyokuwepo popote ionekane jambo la uzito sana kuliko nyumba aliyotoa Cameron na kufanyiwa ufisadi na familia ya Sykes?
Kwanini habari ya Mshume Kiyate kumpa Nyerere pesa za kitoweo wakati anakwenda kuomba sokoni iwe habari kubwa kuliko habari za Cecil Matola Rais wa kwanza wa AA ambaye ni babu yake CCM mkubwa(Great grand pa)
Kwanini tuambiwe Nyerere aliua EAMWS na tusiambiwe kule Mombasa ilipoanzia iliuawa na nani?
Kwanini tuambiwe Nyerere alitengeneza dude BAKWATA, tusiambiwe tangazo gani na la lini liliua Jamiatul Isilamia fil Tanganyika.
Kwanini tuambiwe Nyerere na kanisa waliua EAMWS lakini hatuambiwi ni oganaizesheni gani iliua AMNUT!
Kama AMNUT ilikufa kwa matokeo ya family feud, kwanini siwezekane kwa EAMWS.
Sasa tunapofungua na kutumia akili kuhoji haya tunaambiwa tunampinga Mohamed.
Kwanini tuambiwe Nyerere aliwaaga wazee wa Dar es Slaam kwa kusema hamjui Abdul Sykes na tukiomba hotuba kimaandishi au sauti hatupewi? Tumeletewa maandishi ya sehemu ya hotuba hakuna maneno hayo na wala Mohamed hajakanusha kama si kweli, sasa huo kama si uchochezi unaitwa nini kwa lugha nyepesi, maridhawa na mwanana.
Tukiomba maelezo tunaambiwa tuandike vitabu na hata wengine wasiokubaliana na ngano hii kuondolewa katika uumini.
Kwamba tamthilia inaweza kutumika kujua nani mwislam nani asiye. Hadi hapo hujaona tatizo ndugu yangu mpendwa