Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nikupe mfano rahisi tu Ritz: Atakayefanikiwa kuiingiza CHADEMA, CUF au NCCR ikulu, huyo ndie atakumbukwa daima na milele. Hawa viongozi tulionao na waliowatangulia wa vyama hivi watabaki kutajwatajwa tu kwa sentensi moja hapa na pale. Historia ni katili hivo wakati mwingine.

Hawa akina Sykes, Plantan, Kiyate, Amer, hatuna pa kuwaweka kwenye historia ya nchi hii. Watabaki humo kwenye kitabu cha kijana wao. Kawavisha na UDINI ndio kawamaliza kabisa! Wasubiri NCHI hii itakapokuwa ya KIISLAM.

WildCard,

Mfano wako mbona tofauti sana Chadema, CUF, NCCR Mageuzi, siyo vyama kupigania uhuru ni vyama ambayo vinataka kutawala Tanzania huwezi kuvifananisha na AA, TAA, TANU.

Hao wazee wazalendo wacha waendelee kuwa kwenye kitabu cha Mohamed Said inatosha sana.
 
Asikudanganye mtu Ritz. Kuipata Ikulu kama hii ya Tanzania, kwa namna ilivyokamatwa na CCM, ni zaidi ya kupigania uhuru ule wa 1961. Siku CCM ikiondoka Ikulu, Tanzania haitakuwa hii amin nakwambia!
 
Nani anaujuzi au mamlaka ya kuamua kuwa Abdukarim ni mnafiki na Jaffary sio mnafiki?
Kuhusu hotuba ya Nyerere mwaka 1995 Mohamed Said ameandika:
"The speech was a farce, THE TRUTH is muslims were no better than they were before independence"
Nimemuuliza hiyo "TRUTH" aliipataje hajajibu. Sasa Ritz nisaidie, hao aliowaita "muslims" kwenye hiyo sentence ni waislam wepi? Ni pamoja na akina Kikwete, Bakhresa, wana BAKWATA, Sykes, Salim Ahmed Salim, Salimin Amour, Mustapha Nyang'anyi, Wahindi wa Agha Khan, wenye viwanda na wafanya biashara wa kiarabu, kipemba na kihindi? Give me an honest answer, please.

........

Nanren,

Uislam ni dini inataratibu zake Uislam haufuati umaarufu wa mtu wala utajiri wala rangi.

Mungu anasema Muislam bora ni yule anayemcha Mungu na kufuata kitabu Qur'an na Sunna.

Wewe unadhani mtu yeyote tu hakiwa anaitwa Khamisi, Ally basi anaweza kuwa Muislam Muumini bila kufuata mafundisho ya Uislam.
 
Asikudanganye mtu Ritz. Kuipata Ikulu kama hii ya Tanzania, kwa namna ilivyokamatwa na CCM, ni zaidi ya kupigania uhuru ule wa 1961. Siku CCM ikiondoka Ikulu, Tanzania haitakuwa hii amin nakwambia!

Kuiondoa CCM madarakani rahisi sana tatizo kuna kundi moja ambao ni mabaki ya Nyerere linaojiita wasomi wao ndiyo kikwazo.
 
Nanren,

Uislam ni dini inataratibu zake Uislam haufuati umaarufu wa mtu wala utajiri wala rangi.

Mungu anasema Muislam bora ni yule anayemcha Mungu na kufuata kitabu Qur'an na Sunna.

Wewe unadhani mtu yeyote tu hakiwa anaitwa Khamisi, Ally basi anaweza kuwa Muislam Muumini bila kufuata mafundisho ya Uislam.
Uislam wa Sheikh Ponda, Mzee Mohamed Said, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Ritz, Osama bin Laden, Abdulwahid Sykes, ni sawa?
 
Kuiondoa CCM madarakani rahisi sana tatizo kuna kundi moja ambao ni mabaki ya Nyerere linaojiita wasomi wao ndiyo kikwazo.
Haiwezekani Ritz. Mzee Mohamed alitudokeza humu kuwa ilibidi akina Sheikh Ponda wazunguke nchi nzima kuwaambia Waislam wambakize Jakaya wetu madarakani 2010!
 
Nanren,

Uislam ni dini inataratibu zake Uislam haufuati umaarufu wa mtu wala utajiri wala rangi.

Mungu anasema Muislam bora ni yule anayemcha Mungu na kufuata kitabu Qur'an na Sunna.

Wewe unadhani mtu yeyote tu hakiwa anaitwa Khamisi, Ally basi anaweza kuwa Muislam Muumini bila kufuata mafundisho ya Uislam.

Sawa Nimekusoma.
Naomba basi unisaidie, lile neno "muslims" kwenye ile sentensi ya Moh Said, lilikuwa linamaanisha waislam wepi? na wanatambulikaje? Wanatofautishwa vipi na waislam tulio nao makazini na mitaani kwetu?
 
Uislam wa Sheikh Ponda, Mzee Mohamed Said, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Ritz, Osama bin Laden, Abdulwahid Sykes, ni sawa?

WildCard,

Muislam bora ni yule anayefuata mafundisho ya kitabu Qur'an na Sunna.

Kama utafuata haya mafundisho lazima utajihepusha na maovu yote na kusimama kwenye haki.
 
Haiwezekani Ritz. Mzee Mohamed alitudokeza humu kuwa ilibidi akina Sheikh Ponda wazunguke nchi nzima kuwaambia Waislam wambakize Jakaya wetu madarakani 2010!

Halafu na nyie Makanisani mkaamasishana lazima Dr Slaa tumchague.

Tuliona kule Sumbuwanga waumini walifukuwa Kanisani kwa kuipigia kura CCM.

Sasa hauoni tatizo hapa kama kuna udini Tanzania au udini kwako upo kwa Mohamed Said tu.
 
Ndugu yangu ni ngumu sana kutafuta wapi umweke Mohamed Said.Unatakiwa kumfahamu kabla ya kumchukulia dhamana.

Hakika kama humuopopi MS kuna tatizo. Huyu ni mtu anayeweza kusimama na kuhadithia kuwa maziwa ya ng'ombe yanatoka katika mafenesi na si ngombe hundreds times.

FYI Mohamed is a master mind behind the turmoil seen recently.
He is a gifted story teller with incendiary power.

Ni kwasababu ulizosema tumekuwa na MS mara kadhaa tukitaka kurekebisha pale palipopinda. MS hakubali hilo kwasababu ya madai kuwa anatoa mada Ulaya. Kila tukimtaka ataoe maelezo ya ziada ima anshindwa au anapindisha ukweli na wakati mwingine anakimbia kama si kutoka nje ya swali, hoja au mada.

Hivi ninavyokuambia kuna hoja na maswali lukuki aliyoshindwa kuyajibu, kuyatetea au kutolea maelezo japo kwa fikra. Silaha kubwa ya majaliano aliyo nayo ni kuandika sana na kualikwa ulaya.Mtamwambia nini ninyi wamatumbi!

Badala ya kuwashambulia wanaotaka record ziwe straight ungemshauri MS asimame kidete kutetea hoja zake kwa mantiki. Nadhani umesoma na kuona contradictions nyingi kwa MS mwenyewe na ya mwisho ni hiyo niliyoweka akakana maneno yake achilia mbali wale anaowasemea kumkana bila yeye kujielewaMkuu, Malumbano haya yanatija sana kwasababu moja kubwa. Kuzuia upotoshaji kwa vizazi vijavyo, kuzuia maafa yatokanayo na upotoshaji na kuzuia ongezeko la wapotoshaji duniani.

Niseme kwa nafsi yangu ambayo nina hakika wengi ndipo wanaposimamia. Alichokiandika Mohamed ni historia ya matukio ambayo yalikuwepo. Kleist Syke alikuwepo, Abdul Sykes alikuwepo n.k. Hakuna anayekataa uwepo wa baadhi ya matukio hayo kwasababu historia haiumbwi inajiumba.

Lakini basi hivi tukubali tu kuwa Rais wa kwanza wa AA ni K.Sykes alimyemkabidhi mtoto wake A.Sykes TAA halafu TANU! Kupitia malumbano haya wengi wamejua huo ni uongo, uzushi na uzandiki mzuri tu.

Kwa mfano huo mmoja katika ya mamia unataka tukae chini na kumeza tu! Please tuonee huruma nduguzo.
Akili zetu tutazitumia wapi na lini!!Ndugu yangu kupitia JF na mnakasha huu Mohamed has been brought to his knee by admitting mistakes, accepting facts and most important he has purge and expunge some of his rhetoric and toxic materials.

FYI hii si mara ya kwanza kuwa na mnakasha na MS na kila mara wasomaji wameongezeka. Maana yake si kuwa wanamsoma MS, wapo waliomsoma na sasa wanatazama upya kurasa walizosoma.

Wapo wenye maswali ambayo kupitia mjadala wanapata ufahamu wa sehemu ya pili.
Muhimu sana ajenda, nia na dhamira ya Mohamed sasa vipo wazi kuliko wakati mwingine wowote.

Ngano ni masimulizi matamu ya kusadikika yanayotumia mazingira na yasiyoweza kuthibitika, kuthibitishwa, kutetewa au kujitetea zaidi ya ujumbe wake kumfanya msikiliza ayafurahie.Kwanza tumshukuru sana mzee wako kwa uzalendo wake wa kulitumikia taifa hili hata pale alipoweka maisha ya watoto wake kama wewe on the line.

Huyu ni one too many katika wale tunawaowaongelea na kuwatetea.
Hakika kupitia yeye na wenzake sote tupo huru tena kama taifa.

Maelezo haya yanatusadia kututetea pale tunaposema harakati za uhuru zilizagaa nchi nzima na si Tandamti, Kidogo chekundu au Narung'ombe kama MS anavyouaminisha ulimwengu.

Lakini pia unatutetea ya kuwa wazalendo kama baba yako hawakufanya hayo kama wakristo,waislam au Wanyamwezi.
Hapa ndipo tunapoachana sana na MS kwa kutaka kuibadili hsitoria, kufifisha heshima za watu na kukweza watu bila sababu.

Baba yako alifanya hayo kwa faida yako wewe na sisi sote bila kujali kabila, dini, Umanyema au Unubi.
Ndivyo malefu ya watu walivyofanya kote nchini.Ni tusi kubwa kwa watu kama baba yako pale tunaposikia kuwa kama si wazulu, wamanyema na wanubi tusingepata uhuru.

Baba yako hajaeleza fadhila zake kwa Nyerere, yeye amebaki kuwa rafiki wa Nyerere.
Leo tunaambiwa Nyerere alikwenda sokoni bila kujua kuwa anapaswa kuwa na fedha na wewe unataka tuamini tu kwasababu imeandikwa.

Tunachosem ni kuwa wazalendo wapewe heshima zao kama Watanganyika na si kwasbabu ni Wazulu, Wamanyema au Wanubi. Wazalendo waheshimiwe kwa mchango wao na si kwa imani zao kama ilivyokusudiwa kutugawa kutoka kwa MS.
Na yaandikwe ya kweli si kuficha baadhi, kusingizia, kuzua au kuweka maneno midomoni mwa marehem kwasababu tu hawawezi kujitetea.

Sijui kama baba yako au wewe mnadai nafasi pekee katika taifa hili kwasababu tu mzee ali risk kutoa vifaa vya sauti.
Sijui kama mna madai ya kwanini ninyi hamjapewa uwaziri n.k. kwasababu tu ya historia.
Na wala sijui kuwa mnaonewa na kudhulumiwa kwasababu ya historia ya mzee wako.
Kama sivyo, kwanini MS atake hayo yatokee? Kwamba yeye anapaswa kuwa waziri kwasababu babu yake aliongoza mgomo wa bandari!Nikushukuru kwa kutambua kuwa kuna ya ukweli na ya uongo.
Nadhani mimi na wengine hatuna tatizo na yale ya ukweli, tatizo letu lipo katika yale ya uongo.

Tupo hapa kurekebisha yale yenye mapungufu, but we don't have the right partner.
Sisi tunasimamia ukweli, MS anasimamia agenda yake so we don't have the common ground.

May be it's time you reach MS and convince him to join us regardless of our social differences for the betterment of this nation.Please let him understand that bigotry, hatred, incendiary comments, fallacy and the likes are contrary to Islamic teaching, they're inhumane and ''toxic asset'' we can pass on to next generation.

Huo mstari wa mwisho niliokazia, hapo ndipo MS asipokubaliana nawe.
Agenda yake ni kudhalilisha jamii nyingine na kuleta mifarakano, vipi akubali marekebisho yatokayo huko.

Ameandika kitabu ku-attack wakristo sasa atakubali vipi maoni ya watu wenye imani tofauti na yeye.
Nimalizie kwa kusema tatizo ni MS si wale wanaotaka kuweka record straight!

Unashangaza sana,na unatia kichefu chefu hata kuendelea kukisoma hiko ulichokiandika..

Umeingiza maneno mengi sana katika andiko lako ya uzushi na uzandiki ili uendeleze na harakati zako za kuwatoa wasomaji walio wengi kuupata ujumbe unaostahiki,hivi kama kweli una nia ya kukosoa kwanin sasa ukosoe kwa kutumia uzushi?

wapi katika kitabu cha Mohamed Said aliposema yeye anashikilia maandiko yake na kile anachokieleza eti kwa kuwa wazee wake walikua mstari wa mbele katika kupigana uhuru basi na vizaz vyao vipewe jazaa ya aina fulan?kama vyeo na kadhalika?wapi ilipooneshwa hivyo katika mantik ya kitabu chake..

Na ni wapi alipoandika kitabu ku-attack christians?mbona unapotosha sana?

Kumbe sasa upo hapa ukipigana vita ya msalaba kutetea christians wenzako si ndiyo?

Na siwez kushangaa,kwa kila nimuonaye katika nyie mnaopinga wote ni christians,hakuna hata mmoja ambae kajitambulisha au kujionesha yeye ni mtu wa iman ya uislam,ni waz kbs nyinyi mmeamua kupigana Crusade war,lakini haitosaidia,kwan mliyoelezwa mmeelezwa kwa ushahid uliojitosheleza kabisa..

Hamna lolote mnalosi mamia zaid ya chuki zenu za kidini,wakati hapa kinazungumzwa kitu chenye uhalisia uliotukuka..

Haitawasaidia..
 
Ni Nyerere nasababu ni chuki zake na kutaka wakatoliki wawe juu na ndio sera inayotawala duniani kukuthibitishia haya nijibu swali hili unajua kwanini Nyerere alipambana kumng'oa Idd Amini?
Sio kosa lako bwana mdogo, tatizo lipo kwenye kiwango chako kidogo cha elimu ambacho Mohamed Saidi amekigeuza kuwa uwanja wake wa kufanyia mazoezi ya kupandikiza chuki dhidi ya watu wengine. Sitakulaumu wewe bwana mdogo, nailaumu CCM na sera zake mbovu za elimu zilizo sababisha vijana kama wewe mkose elimu bora mkaishia kupata bora elimu. Namlaumu sana Mohamed Saidi ambaye badala ya kuwasaidia vijana kujiamini na kutafakari kwa kina matatizo yao, yeye anawajengea kuto kujiamini na kufikiri matatizo yanaletwa na ukristo!
 
Halafu na nyie Makanisani mkaamasishana lazima Dr Slaa tumchague.

Tuliona kule Sumbuwanga waumini walifukuwa Kanisani kwa kuipigia kura CCM.

Sasa hauoni tatizo hapa kama kuna udini Tanzania au udini kwako upo kwa Mohamed Said tu.
Kuna mahala aliji-misdirect Kikwete wetu. Juzi kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi aliongea vizuri sana kuhusu UDINI. Akaniunga mkono kwa mimi kuwa na mke wa pili Muislam!
 
Ilianza Ban kwa THE BIG SHOW,ikaja Ban kwa zomba,sasa tunaona imekuja kwa Ritz,,

Wale wote wanaoonekana ni wana jitanabaisha na kuzikubali zile zinazoitwa Ngano na Histohisa za Mohamed Said wameondolewa na kupewa Ban kwa lugha zisizofaa,huku wengine wengi wanaotumia lugha za matusi na kejeli kwa makusudi na kuharibu mjadala huu wanaachwa,Basi ufungwe tu mjadala ieleweke moja,kila mtu ana haki ya kuzungumza uhalisia,kunyimwa haki kwa wengine huku wengine wakiachwa kunazua maswali mengi sana juu ya uhuru ndani ya jukwaa hili..
 
Last edited by a moderator:
Huu mjadala unaonekana umeisha.Hapa nawaonaa akina Ritz na Mohammed Said wakipasha moto misuli katikati ya uwanja.Watu majeruhi kama Mzee Mwanakijii ni wa kuokolewa.Anachofanya Mzee ni udowezi na usanii tu.
Wa kumuokoa hakuna kwa sababu refa na mashabiki bado wana matumaini nao huenda wakajibu au wawe wa mwisho kujibu halafu iwe mwisho.
Nilitamani nirudie kuchangia kule Ukweli kuhusu waasisi lakini nikakuta tayari kumefungwa.
Watetezi wakubwa wa Nyerere wanauliza maswali yaliyojibiwa au kujiuliza na kujijibu wenyewe bila kujua wanachokifanya.Hii ni dalili ya kuchanganyikiwa.

Sehemu nyingi wamesema eti historia ya Mohammed Said watu wameipuuza.hapo chini wanajipinga kwa kusikia kwenye gari
kawaharibusi kidogo jana nipo kwenye bus naelekea mwanza ukazuka mjadala kwenye gari.Vijana walivyokuwa wana'quote MS kana kwamba vitabu vyake ni msaafu

Inaonekana basi wazee wako walikuwa na heshima ya kweli namapenzi kwa Nyerere kuliko nyinyi watoto wao. Lakini kama wazee wako ndio hawawazee wa Kitanganyika ambao walipendana kweli na udugu wa kweli na ndugu zaoWakristu; hawa ambao hawakutaka kumdhuru Nyerere - sababu ya Ukatoliki wake -akikaa katikati yao; hawa wazee ambao walikuwa tayari kwenda kulinda Kanisa iliNyerere asali pale na wakienda naye kwenye kufanya dua na matambiko; hawa wazeehawa huko waliko lazima wakushangae unayoyasema dhidi ya Nyerere na kumdunishambele ya Waislamu watu ambao Nyerere aliwapenda, walimpenda, alisimama nao nayeye akasimama nao hadi mauti. Hii faraka uliyoianzisha wewe wala haina sifa wakujitamba. Unapaswa ufikirie mara mbili unavyotumia majina ya wazee wetu hawakuwagawanya Watanzania na kuchochea fitna kati yetu bila kuchoka.

Leo maskini wa Mungu unafurahia unaposikia vijana wa Kiislamu - pasi ya kujua -wanamlaani Nyerere, leo mzee unafurahia kusikia Nyerere anaitwa Dhalim ukiaminiunafanya jema? Leo Nyerere anatukanwa na kubezwa kwa sababu ya histohisia yamaandishi yako na unasimama kutumia jina la wazee kuhalalisha?

Lahaula! Mzee Said mrudi Mungu, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe madhambi yetuna mwenye kutujalia neema ndogo ndogo na neema kubwa kubwa! Atakupa nafasiusaidia kuliponya taifa lako ambalo kwa kutumia mikuki yako ya maenenoumelijeruhi na sasa damu inamwagika huku ukiwafurahia marafiki zako ambaowametangaza kutaka kuwaua ndugu zao Wakristu pasi ya sababu yoyote ile.Mwenyeewe unajiaminisha kuwa unafanya hivyo kwa jina la Dini..

Mzee Said mwombe toba Mnyezi Mungu!!

hapo ni 410 lakini jibu lilitoka tangu 282.
N,

Nyerere kagombana na Sheikh Suleiman Takadir 1958
Nyerere kagombana na akina Sheikh Hassan bin Amir na Bilal
Waikela 1963 hadi 1968 hali ikawa mbaya kupelekea Sheikh
Hassan kufukuzwa bara na kurejeshwa Unguja.

Hayo magomvi nilisababisha mimi?

Mbona mko kimya na maneno ya Sivalon?
Niyabandike upya?

Mzee Mwanakijiji anapojibiwa tena anakaa kimya kusubiri vumbi litulie aje na swali jengine.Huu ni mjadala wa aina gani jamani?.
Hadi hivi sasa:

Bw. Mohammed Said,

1. Ameshindwa kuthibitisha una dhulma dhidi ya Waislamu na Uislamu - kwani kunaushahidi wa kutosha wa mafanikio makubwa ya Waislamu wa Tanzania tangu kabla yahuru hadi hivi leo. Wasomi, watendaji, wafanyabiashara, walimu, madaktari n.k

2. Ameshindwa kutoa ushahidi hata mmoja wa tendo lolote la Baba wa TaifaMwalimu J. K. Nyerere dhidi ya Uislamu. Ila ametoa ushahidi wa kutosha wa jinsiNyerere alivyowaheshimu Waislamu, alivyojichanganya nao na alivyoyaweka maishayake mikononi mwao. Jinsi walivyomkarimu. Nyerere hata mara moja hajawahikuacha kusema wema huu... ameusema kwenye kitabu chake 1985, amesema kwenye 'WeMust Run While They Walk' na amesema kwenye mahojiano mengine mengi throughouthis years in public service

3. Ameshindwa kutoa uthibitisho wowote kuwa Kanisa la Tanzania limewahikuutangaza Uislamu kama ni adui na kuanza kupunguza kukua kwake. Alipodaiwakutoa ushahidi wa nani aliwahi kutangaza hilo akamtaka Cardinal Levigerie -kutoka Algeria! Ni sawasawa na kusema tutumie maneno ya Sheh mmoja Saudia dhidiya Kanisa halafu tuseme ndio kawaagiza Waislamu wa Tanzania!

4. Ameshindwa kuonesha kuwa lolote ambalo liliwatokea Wazee wa Kiislamuhalikuwatokea wazee wa Kikristu. Kufungwa walifungwa Wakristu na Waislamu, kuwadeported wamewahi kuwa deported hata Wakristu tena Padre! Kuvunjwa kwa EAMWS nakutaifishwa kwa shule na mahospitali za Makanisa kwa Nyerere vyote vilikuwahavijali dini!

5. Ameshindwa kuonesha hata mara moja kuwa Abdulwahid Sykes katika maisha yakeamewahi kumtuhumu Nyerere udini au kuonesha andiko lolote la Abdulwahid kuwaNyerere aliukwa mdini au akiwadhulumu Waislamu.

6. Ameshindwa kuonesha kutoka kwa mlolongo wa wazee wake yeyote ambaye wakatiwote wa utawala wa Nyerere hadi anang'atuka kama kulikuwa na ugomvi kati yaNyerere na Waislamu. Mgogoro pekee ambao Nyerere ulikuwepo kwa muda mrefu marabaada ya uhuru ni makundi ya watu waliokuwa wanajaribu kudhoofisha taifa changa(sabotaging). Katika hili Nyerere hakuangalia sura. Kwa maandiko yake mwenyewehadi katikati ya miaka ya sabini Nyerere alikuwa na mahusiano mazuri tu nawazee wake! Na Nyerere hakusahau kamwe fadhila yao kwake.

Kimsingi, kuamini simulizi la histohisia la Bw. Said ni kuamini kuwa mweziumetengenezwa kwa jibini!

Hiyo ya mwisho inajibiwa na maandishi haya ya Mohammed Said.

"Ilikuwa katika ofisi ya zamani ya TANU tulipokuwa tukisubiri kufanya mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Ghafla tu Sheikh Takadir alisimama wima akishikilia bakora yake ya kutembelea na kumuelekezea Nyerere huku akisema, "Huyu mtu katu hatakuja kutujua ndugu zake. Usipoziba ufa utajenga ukuta." Sheikh Takadir alirudia maneno haya mara mbili. Sisi sote katika kile chumba cha mkutano tulishangazwa sana ama kwa maana ya maneno yale. Nilimwona Nyerere akilia. Nyerere alitugeukia sisi na kutuuliza, "Je, Sheikh Suleiman alisema maneno yale kwa niaba yenu ? Tulijibu kwa kwa pamoja hapana na ule mkutano ulivunjika papo hapo."
Katika maelezo hayo utaona sheikh Suleiman Takadiri akimnyooshea kidole Nyerere ambaye alilia na mkutano ukavunjika
Jee huo ni ugomvi au si ugomvi?.
Yuko wapi Yerico?.Akirudi anauliza viswali vifupi vifupi.Mwenyewe amekubali kuwa Mohammed kaandika historia kutokana na utafiti.Huu si uchochezi bali ndio ukweli wenyewe.
 
Ilianza Ban kwa THE BIG SHOW,ikaja Ban kwa zomba,sasa tunaona imekuja kwa Ritz,,

Wale wote wanaoonekana ni wana jitanabaisha na kuzikubali zile zinazoitwa Ngano na Histohisa za Mohamed Said wameondolewa na kupewa Ban kwa lugha zisizofaa,huku wengine wengi wanaotumia lugha za matusi na kejeli kwa makusudi na kuharibu mjadala huu wanaachwa,Basi ufungwe tu mjadala ieleweke moja,kila mtu ana haki ya kuzungumza uhalisia,kunyimwa haki kwa wengine huku wengine wakiachwa kunazua maswali mengi sana juu ya uhuru ndani ya jukwaa hili..

Ritz, kala ban.
 
Last edited by a moderator:
Sio kosa lako bwana mdogo, tatizo lipo kwenye kiwango chako kidogo cha elimu ambacho Mohamed Saidi amekigeuza kuwa uwanja wake wa kufanyia mazoezi ya kupandikiza chuki dhidi ya watu wengine. Sitakulaumu wewe bwana mdogo, nailaumu CCM na sera zake mbovu za elimu zilizo sababisha vijana kama wewe mkose elimu bora mkaishia kupata bora elimu. Namlaumu sana Mohamed Saidi ambaye badala ya kuwasaidia vijana kujiamini na kutafakari kwa kina matatizo yao, yeye anawajengea kuto kujiamini na kufikiri matatizo yanaletwa na ukristo!

Sawa mkuu elimu yangu ndogo wewe mwenye elimu una nini cha maana? mimi siku fichi nimesoma madrasa sana na ndio kimbilio lenu la kudharau madrasa lakini kwangu madrasa na bora sanaaaa kuliko unavyofikiria wewe ni viongozi wangapi leo hii wamesoma lakini hao hao ndio mafisadi wakutupwa au lusoma sana ndio watu wanafundishwa ufisadi lakini kama kweli unaimani yako ya dini kweli Tanzania isingefika hapa ilipo lakini kwa vile nchi haina dini wacha watu wachote wachape mwendo,uislamu unasema mwizi akatwe mkono,anaezini apigwe fimbo 100 na masuala ya mirathi kitabu chetu kimeeleza yote leo hii ni wanawake wangapi waume zao wamekufa na wamedhulumiwa mtihani mkubwa kwahiyo mkuu usome kwanza uislamu siku force uingie wewe baki huko huko kwenye mambo yako
 
Nikupe mfano rahisi tu Ritz: Atakayefanikiwa kuiingiza CHADEMA, CUF au NCCR ikulu, huyo ndie atakumbukwa daima na milele. Hawa viongozi tulionao na waliowatangulia wa vyama hivi watabaki kutajwatajwa tu kwa sentensi moja hapa na pale. Historia ni katili hivo wakati mwingine.

Hawa akina Sykes, Plantan, Kiyate, Amer, hatuna pa kuwaweka kwenye historia ya nchi hii. Watabaki humo kwenye kitabu cha kijana wao. Kawavisha na UDINI ndio kawamaliza kabisa! Wasubiri NCHI hii itakapokuwa ya KIISLAM.
Tuanze na cdm nani pale anaweza kuingia kwenye historia ukimwangalia katibu mkuu mzi.......z mwenyekiti jd walabda uwapeleke kwenye guinness book ngoja ninyamaze nisije nikala ban kwamaana hali imechafuka kwenye huu uzi sasa hivi utasikia mzee MS kapigwa ban lakini gwalihenzi anatesa kwa raha zake mfumo kristo bwana uko juu!
 
Sawa mkuu elimu yangu ndogo wewe mwenye elimu una nini cha maana? mimi siku fichi nimesoma madrasa sana na ndio kimbilio lenu la kudharau madrasa lakini kwangu madrasa na bora sanaaaa kuliko unavyofikiria wewe ni viongozi wangapi leo hii wamesoma lakini hao hao ndio mafisadi wakutupwa au lusoma sana ndio watu wanafundishwa ufisadi lakini kama kweli unaimani yako ya dini kweli Tanzania isingefika hapa ilipo lakini kwa vile nchi haina dini wacha watu wachote wachape mwendo,uislamu unasema mwizi akatwe mkono,anaezini apigwe fimbo 100 na masuala ya mirathi kitabu chetu kimeeleza yote leo hii ni wanawake wangapi waume zao wamekufa na wamedhulumiwa mtihani mkubwa kwahiyo mkuu usome kwanza uislamu siku force uingie wewe baki huko huko kwenye mambo yako
Pole sana
 
Ha ha haaaaaaaaa....wafia dini wa gerezani wote wamepata Ban. Bado kubwa lao la maadui mzee Mohamed Said.

Lakini mimi niliwaambieni hapa kuwa nyinyi wafia dini wa Gerezani huu mjadala teyari mmeshaangukia pua ila kujiondoa
mkawa mnashindwa kwa kuona aibu, so sasa mlichokuwa mnakifanya hapa ni ushabiki na vijembe tu badala ya hoja.

Sasa mmekosa yote. Kwenye mjadala mmekufa chali na ban juu.....shame on u all.
 
Back
Top Bottom