Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Chukua hii mbwa koko walikuwa wapo kwenye mapipa wanatafuta chakula mara kwa mbali wanaowaona askari FFU wakipita na mbwa zao wakielekea zao kwenye lindo basi yule mbwa moja pale kwenye mapipa akawambia wenzake mnaona uzuri wa elimu wenzetu wamesoma kila siku wanaletewa chakula.

Turudi kwenye munakasha.
 
Adui wa waislam wa Tanzania ni nani? na kwa nini?
Ni Nyerere nasababu ni chuki zake na kutaka wakatoliki wawe juu na ndio sera inayotawala duniani kukuthibitishia haya nijibu swali hili unajua kwanini Nyerere alipambana kumng'oa Idd Amini?
 
Eeeh ee! Unakosea muungwana. Hakuna anayempinga Mohamed kama ambavyo hakuna anayeweza kupinga Musiba au Hardley chase.
Wapo wanaopinga upotoshaji, uzushi, uenezaji wa chuki, uzandiki na ubabaishaji. Sijui kama hao ndio wanaompinga!

Mwenzetu umejiunga leo na ID mpya, hata hivyo ahadi yetu ni kuwa ''you will run but not find a heaven place to hide''
Kabla sijakuuliza maswali napenda niweke rekodi sawa.

Hii ngano ni historia ya wazee wa Kidongo chekundu, Narung'ombe, Tandamti na Mchikichi. Jambo jema kabisa!
Kwa mshangao imegeuzwa kuwa historia ya Tanganyika.

Huo ni uchochezi wa awali kwasababu uchochezi ni kushadidia jambo usilo na ushahidi nalo au kupigia debe kisichokuwepo au kilichopo lakini kwa kupindua habari.Msingi wa uchochezi ni kuleta farki, husda, inda na hatimaye vurugu katika jamii.

Anapotokea mtu akawagawa watu kwa imani huyo ni mchochezi.
Imani za dini zinaelekeza utangamano miongoni mwa walioamini na wasio amini.
Ndivyo Mitume, Manabii, maswahba na mahalifa walivyosihi tangu enzi za kale.
Anayekwenda kinyume na misingi hiyo ya dini, basi huyo anatumia dini kwa malengo na si kuitumikia kama ilivyoagizwa.

Hatua ya kuwagawa watu imekwenda mbali kiasi cha kuaminisha ulimwengu kuwa kama si Wamanyema ambao asilimia 100 ni waislam, wazulu waliokuja Tanganyika ambao asilimia 99 kasoro mwalimu Thomas ni waislam na Wanubi basi uhuru wa nchi hii ungekuwa matatani.

Nadhani unajua yanayotokea DRC. Watusi walipewa hifadhi kama raia na sasa wanadai nchi isyokuwa yao.
Yaani wamefikia mahali pa kuwaondoa wamanyema katika nchi yao.
Sasa tunapokuwa na wamanyema nao wakaanza na madai ya namna hiyo, hivi hapo huoni hatari ndugu yangu.

Hebu fanya kautafiti kasiko rasmi uangalie nyuma ya vurugu za kidini wapo watu wa aina gani nakutoka eneo gani la nchi hii.

Ndugu yetu, inawezekana kabisa wale wasiokubaliana na Mohamed wamepotoka, na kwa vile umekuja na ID mpya unaweza kutusadia kwa mawazo mapya. Wapi ambapo Mohamed amepingwa au kukoslewa kwa uonevu tu.

Kwanini basi ngano isiwe na ukweli ili kuweka rekodi sawa sawa!
Ni kwanini hotuba maarufu ya Waikela isyokuwepo popote ionekane jambo la uzito sana kuliko nyumba aliyotoa Cameron na kufanyiwa ufisadi na familia ya Sykes?

Kwanini habari ya Mshume Kiyate kumpa Nyerere pesa za kitoweo wakati anakwenda kuomba sokoni iwe habari kubwa kuliko habari za Cecil Matola Rais wa kwanza wa AA ambaye ni babu yake CCM mkubwa(Great grand pa)

Kwanini tuambiwe Nyerere aliua EAMWS na tusiambiwe kule Mombasa ilipoanzia iliuawa na nani?
Kwanini tuambiwe Nyerere alitengeneza dude BAKWATA, tusiambiwe tangazo gani na la lini liliua Jamiatul Isilamia fil Tanganyika.

Kwanini tuambiwe Nyerere na kanisa waliua EAMWS lakini hatuambiwi ni oganaizesheni gani iliua AMNUT!

Kama AMNUT ilikufa kwa matokeo ya family feud, kwanini siwezekane kwa EAMWS.

Sasa tunapofungua na kutumia akili kuhoji haya tunaambiwa tunampinga Mohamed.

Kwanini tuambiwe Nyerere aliwaaga wazee wa Dar es Slaam kwa kusema hamjui Abdul Sykes na tukiomba hotuba kimaandishi au sauti hatupewi? Tumeletewa maandishi ya sehemu ya hotuba hakuna maneno hayo na wala Mohamed hajakanusha kama si kweli, sasa huo kama si uchochezi unaitwa nini kwa lugha nyepesi, maridhawa na mwanana.

Tukiomba maelezo tunaambiwa tuandike vitabu na hata wengine wasiokubaliana na ngano hii kuondolewa katika uumini.
Kwamba tamthilia inaweza kutumika kujua nani mwislam nani asiye. Hadi hapo hujaona tatizo ndugu yangu mpendwa
 
Ni Nyerere nasababu ni chuki zake na kutaka wakatoliki wawe juu na ndio sera inayotawala duniani kukuthibitishia haya nijibu swali hili unajua kwanini Nyerere alipambana kumng'oa Idd Amini?
wee nyambaf hivi unajua Idd amini aliua ndugu zetu kule kagera?
 
Ni Nyerere nasababu ni chuki zake na kutaka wakatoliki wawe juu na ndio sera inayotawala duniani kukuthibitishia haya nijibu swali hili unajua kwanini Nyerere alipambana kumng'oa Idd Amini?

Nyerere alipambana kumng'oa Idi Amin? really? na alipambana kuung'oa utawala wa Ian Smith Rhodesia, wa Makaburu South Africa kwanini? Ooh well.. kwa sababu Idi Amin alikuwa Muislamu na Nyerere alitaka kumuweka Mkristu Obote... ndio simulizi jipya hili.. na alipopambana kupigania haki ya Wapalestina dhidi ya Waisraeli na kukataa kukanyaga Nchi Takatifu kwa sababu gani? Well, alitaka PLO ichukuliwe na Wakatoliki...

Mohammed Said kawaharibu watoto wetu jamani...
 

Kwani PLO ni chama cha Waislam?
 

Mohamed hilo halioni, ila ndoto yake ni kubadili nyeupe kuwa nyeusi na usiku kuwa mchana.

Hilo halitawezekana abadani
 

kawaharibu si kidogo jana nipo kwenye bus naelekea mwanza ukazuka mjadala kwenye gari. Vijana walivyokuwa wana'quote MS kana kwamba vitabu vyake ni msaafu
 
Ni Nyerere nasababu ni chuki zake na kutaka wakatoliki wawe juu na ndio sera inayotawala duniani kukuthibitishia haya nijibu swali hili unajua kwanini Nyerere alipambana kumng'oa Idd Amini?
Hivi kweli umelishwa ngano za aina hiyo?

Kwahiyo mapambano yaukombozi aliyoyaongaza Mwalimu Nyerere kusini mwa jangwa la sahara yalikuwa ni yakidini?

Daaah ikiwa kuna watz wenzetu wanaoamini hivi, sisi tuwasaidiaje?
 
Kwa taarifa yako uzi huu umewafumbua macho wengi kuhusu chuki zinazoenezwa na baadhi yenu hasa kwa hawa vija na waliozaliwa siku za karibuni. Nasema siku za karibuni maana sie wazamani walao tunaelewa nini kilikuwepo wakati huo hata kwa uchache.
 
kawaharibu si kidogo jana nipo kwenye bus naelekea mwanza ukazuka mjadala kwenye gari. Vijana walivyokuwa wana'quote MS kana kwamba vitabu vyake ni msaafu

Mohamed Said kwasasa akitaka kugombea umufti mkuu wa Tanzania atapita bila kupingwa,

Wwjinga wote wamekuwa wafuasi wake watiifu
 
Nimeuliza swali PLO ni chama chama cha Waislam?

Ritz,

Kuna mtu hapa alinitisha na habari za Sheikh Hussein Malik akasema
sheikh ni mtu wa mtandao mbaya duniani nk. nk.

Nikamjibu kuwa nitashukuru kusikia taarifa hizo za kutisha za mwalimu
wangu.

Naona kimya takriban siku zaidi ya nne au tano hivi.
Sijaona taarifa za Sheikh Malik.

Je wewe unamkumbuka mtu huyu?

Halafu video clip ya hotuba.
Bado haijaletwa jamvini.

Katika miaka ya 1980 hivi kulikuwa na soap opera moja inaitwa Dallas.
Ilishika watazamaji dunia nzima hadi Dar es Salaam..

Siku zile kuna maduka ya kukodi zile VHS tape...
Tukifuatilia sana.
 
Hotuba ya maandishi ya rangi ya bluu iliyopo hapo juu unaikubali ama unaipinga?
 

Mohamed Said,

Hata mimi nasubiri kwa hamu habari za Sheikh Malik.

Ndugu yangu hawa jamaa wanachofanya ni kujaribu kung'oa mbuyu kwa bajaji.

Hotuba tuliambiwa inatakiwa pesa TBC watu tukajitolea kuinunua tukaomba namba ya M.PESA watu wakaingia mitini mpaka leo.
 
Nilichoomba mimi ni barua sio "ngano" zako hizi. Si unasema waliandikiana?
 
Hotuba ya maandishi ya rangi ya bluu iliyopo hapo juu unaikubali ama unaipinga?

Naona umeamua kuyakana maneno yako si wewe ndiyo ulikuja humu jamvini na kutuambia umekwenda TBC wamekuambia hotuba inauzwa bahati mbaya hutaki kutaja bei.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…