Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wanasema ukiwa muongo, unatakiwa uwe na kumbukumbuku kali sana.

Hapana siwezi kusema uongo.
Labda unaninukuu ''out of context.''

Sina sababu ya kusema uongo.

Hebu Insha Allah niwekee hapa hayo maneno yangu.
 

Ndugu yangu Nyerere.

Historia ya Kanisa na harakati za uhuru imekwisha au itaendelea?
Ningependa nami Insha Allah kuchangia katika yale ulotuwekea hapa.
 
Ndugu yangu Nyerere.

Historia ya Kanisa na harakati za uhuru imekwisha au itaendelea?
Ningependa nami Insha Allah kuchangia katika yale ulotuwekea hapa.

Haijaisha mkuu, mimi nimeinyofoa kwa ufupi tu, unaweza kuihuisha tu.

Nakusudia kuwaombeni nyote tunaojadiliana hapa na wengine ili kwapamoja tushirikiane kuandika upya HISTORIA ya nchi yetu na uhuru wake!

Mengi mazuri kutoka kwenye kitabu chako na kile cha Kivukoni tutayanukuu!

Hii iwe kwa maslahi ya taifa letu bila kujali dini, rangi, kabila au vyovyote vile!

Tufanye utafiti pamoja na mwisho wasiku tuje na historia thabiti ya nchi yetu tena yenye kutuunganisha!
 

Kaka Yeriko

Tatizo linakuja sehemu moja tu.

Mtu akishaita utafiti wa mzee Mohamed Said kuwa ni ngano, basi inamaaana kuwa yale yote yalioandikwa ni batili. Sasa kama ni batili, wanashindwa kuwa-acknowledge wazee wa Dar es Salaam, waliompokea babu yako mzee Nyerere, katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika

Inaonyesha dhahir kuwa wazee wa Dar es Salaam hawatambuki katika "historia" waijuayo wao. Hili ndio linalokwamisha mjadala adhwim kwenda mbele.

Ninawasilisha
 

Katika safari yangu ya maisha dunia huwa naamini kuwa, hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu!
 

Unajua Brendon Grimshaw mhariri wa Tanganyika Standard alisema nini katika taazia aliyomwandikia Abdu Sykes?

Grimshaw akijuana na Abdu Sykes kwa miaka mingi.
Huyu alikuwa Mwingereza.
 



Sifanyi utani.
Hakika maneno hayo nimeyatoa kwenye gazeti la Majira.
 
HISTORIA huwa haiandikwi upya wala kuhuishwa. Historia ya nchi hii tayari ipo. Mtaandika nini kipya? Au mnaweza kuyabadili haya:
Rais wa KWANZA wa TANU- Mwalimu;
Mtu aliyetumwa kwenda UN kudai uhuru wetu- Mwalimu;
Waziri Mkuu wa Kwanza Tanganyika- Mwalimu;
Rais wa Kwanza Tanganyika- Mwalimu;
Rais wa Kwanza Tanzania- Mwalimu;
Na mengine meeengi!
 

Hakika lugha imekuchezea.
Nyerere hakufanya.

Umeona kitabu cha maisha yake kimechapwa
toka afariki?

Hiyo ndiyo maana yangu.
Lakini hili si kubwa.

Tuendelee na mengine.
 

Umesema kweli kwa hayo yote.
Hakuna awezae kukupinga katika hayo.
 

Hakuna KIPYA kitachozalishwa katika mpango huo, bali makusanyo yaleyale ya kweli ndio yaunde historia ili kuondoa dhana ya kila mtu/watu kuamini lake katika Historia ya Nchi hii.

Kwaujumla historia huwa inajiandika, tunachofanya sisi nikukusanya tu kumbukumbu hizo nakuhifadhi katika maandishi.
 

Tafadhali iwe nje ya uzi huu. Huu mjadala usipindishwe kwa makosa ya Quran. Sasa hivi ninakwenda Kanisani kufundisha watoto, nikirudi ama kesho asubuhi, nitaku-PM na kukuwekea mada yako special unipe ufafanuzi wa ubishi unaotaka kuanzisha bila sababu za msingi.

By the way nashukuru kuwa tayari umekiri kuwa kuna makosa mengine, ila unakataa ya kimahesabu.
 
By the way nashukuru kuwa tayari umekiri kuwa kuna makosa mengine, ila unakataa ya kimahesabu.
Haya lete hili kosa lolote lile unaloliona lipo kwenye Quran.

Si mimi bali ni Quran yenyewe ndiyo inayowapa changamoto hii zaidi ya miaka 1400 iliyopita ili uingilie na kutafuta kosa kama utaliona
Quran 4:82. Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi"

Mmeshindwa na Mohamed Said wenye Historia ya Tanganyia sasa mnataka kuingilia Quran! haya karibuni.
 

Abdulwahid alipofariki Wizara ya Habari ilitoa taarifa ikieleza kuwa Rais Nyerere
amehudhuria maziko ya Abdulwahid Sykes.

Kingine kinachostaajabisha ni kuwa taarifa ile ilitoa maelezo machache ya uajiriwa
wake katika serikali na kuacha maelezo muhimu ya Abdulwahid katika siasa.

Ilikuwa Mwingereza, Brendon Grimshaw, mhariri wa Tanganyika Standard, ndiye
aliyempa Abdulwahid heshima na hadhi anayostahili baada ya kifo chake kwa
kuchapisha taaízia ambayo ilimweleza Abdulwahid kama: ''mmoja wa wapangaji
wa vuguvugu la kudai uhuru na mmoja wa watu waliomsaidi Nyerere kuingia katika
siasa.''

Taazia ile ilitoa sifa kemkem kwa ukoo wa Sykes katika kuleta maendeleo ya siasa
Tanganyika kwa kusema kuwa, ''msukumo mkubwa wa Waafrika wa Tanganyika kupata
chama cha siasa chenye nguvu ulitokana na juhudi za ukoo wa Sykes.''

Inasemekana taaízia hii iliyompa marehemu Abdulwahid heshima na sifa za uzalendo wa
hali ya juu iliwaudhi baadhi ya viongozi katika TANU.

Viongozi hao wakawa wakisikika wakisema kuwa Ally na Abbas Sykes walikuwa wanajaribu
kumtukuza kaka yao.

(''Tanganyika Standard'' 20th October 1968).

Hali hii ilijitokeza tena wakati CCM ilipokuwa ikitafiti historia yake.

Hassan Upeka,[1]mmoja katika wasaidizi wa utafiti ule alipeleka katika jopo lile la utafiti na
uandishi wa historia ya TANU, mahojiano aliyofanya na Abdulwahid miaka mingi iliyopita
kuhusu historia ya TANU.

Hassan Upeka alifahamishwa kuwa historia inayoandikwa haimhusu Abdulwahid Sykes.
 

hakika
 
Unaweza kutuwekea maelezo hayo kwenye hicho kibao?
Hakika hiyo ni historia muhimu sana.

Ahsante sana.
Nyerere aliitumia gari hiyo 1955-1960,dereva alikuwa Said Tanu,baadaye akaikabidhi kwa Tanu Youth League.Gari inaitwa Austin Morris
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…