Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kama huu ndio upeo wa mchango wako basi pole sana.
Umekanusha nini?.Kumbe umekubali kuwa Prof.Haroub Othman alimfuata Nyerere kumshauri aandike historia yake.Kitu hicho hicho ndicho alichosema Mohammed.
Sisi watu wa mantiq na balagha huwezi kutubabaisha na makeke ya aina hiyo.
Angalia Nyambala!.Wewe hakuna sehemu uliyosema unafahamiana au uliwahi kuzungumza na prof.Haroub Othman tofauti na Mohammed aliyekuwa na usuhuba nae.Kitendo cha hao maprofesa kumfuata Nyerere kilifanyika baada ya kitabu cha Mohammed kutoka na mwishoni mwa maisha ya Nyerere.Kati ya utakayosema wewe na Mohammed ni nani atakayekuamini wewe akawacha aliyosema Mohammed kuhusiana na profesa Haroub ?..
 
Siyo ya kidini wala ya kikabila, kama hujui omba msaada tukufunze hapahapa bila malipo, gharama yako kuu ni intaneti tu.
Spike Lee,'
Kony hana tofauti na Osama bin Laden. Hawa ni watu wanaotumia dini kuendeleza ajenda zao. Dini gani inakushauri ukamate kwa nguvu binti za watu, kuwaingiza msituni na kuwabaka? Labda ungesema IRA kule Northern Ireland yale yalikuwa mapigano ya kidini ingawa tofauti zao zilikuwa za kisiasa zaidi.
 

Kama huu ndio upeo wa mchango wako basi pole sana.
Umekanusha nini?.Kumbe umekubali kuwa Prof.Haroub Othman alimfuata Nyerere kumshauri aandike historia yake.Kitu hicho hicho ndicho alichosema Mohammed.


Ami,

Asichojua Nyambala ni kuwa Prof. Haroub mimi ni ndugu yangu na
mazungumzo yetu hayakuwa na pazia hata kidogo.

Alipokuja kufahamu mchango wa Abdu Sykes katika kuunda TANU
alikuwa kama mtu aliyepagawa kwa kuwa alikuwa anajua hatari ya
habari ile na uzito wake.

Alikwenda kwa Ahmed Rashad Ali kuuliza zaidi.
Huko ndiko alipopata wazimu.

Mzee Rashad akamwambia mimi na Abdu tulikwenda pamoja kumuona
Kenyatta mwaka 1950.

Lakini kubwa lililomshtusha ni zile siasa za Nyerere, Kanisa na Waislam.
Vitu hivi vilimnyima raha sana.

Kuna mengi Ami mimi siwezi kuyasema kwani unasema na kubakiza.

Katika msiba wa Abdu Sykes watu wa protocal walimkalisha Nyerere jamvi
moja na Ahmed Rashad Ali na wakati wa kutoa sadaka ulipowadia Rashad
alikula pilau sinia moja na Nyerere mkono kwa mkono.
 
Darwin, zomba, Boko haram, Shijaf, Isalia, DULLAH MSAVIVOR, Achahasira, Tanzania Kwanza, Ritz, Ami, Spike Lee...ninayo matumaini kwamba mpaka sasa mtakuwa tayari mmepata majibu ya maswali yangu kutoka kwa Mwalimu wenu mtoa darsa Mohamed Said, tafadhalini yawekeni hapa wasomaji wafaidike nayo. Kwa faida ya wengi inanibidi nirudie ombi langu kama nilivolitoa kwenye posti No. 8591;

Kulingana na maelezo ya mtoa darsa Mohamed Said, Mwalimu Nyerere alikaribishwa Dar es Salaam na wazee wake mwaka 1953 na kuikuta TAA ikidunda chini ya uongozi shupavu wa Abdulwahid Sykes Raisi wake. Ingawa hana hakika ilichukua muda gani lakini katika muda mfupi baada ya kumfunda Mwalimu Nyerere na kumfundisha ustaarabu wakamkabidhi uongozi wa juu kabisa wa TAA! Miezi kumi na tano baadaye wazee hao hao wa Mohamed Said wakaiasisi TANU na kwa mara nyingine tena wakamkabidhi Mwalimu Nyerere awe Raisi wake wa kwanza...sasa nawaombeni akawape na darsa kuhusu maswali mawili tu;


  1. Kwa nini ilibidi iasisiwe TANU huku TAA tayari ilikuwepo?
  2. Kwa nini ilibidi Mwalimu Nyerere ndiye akabidhiwe uongozi?

Kwa mara nyingine nawaombeni twende tu taratibu tufaidike na ilmu kutoka kwa mwana historia, mtoa darsa na gwiji Mohamed Said
 

Mag3,

Ningekaa kimya lakini kwa kuwa umenitaja nitakujibu.

Huyo Abdu Sykes wala hakuwa mali kitu.
Si lolote si chochote na hiyo TAA yake.

TAA kilikuwa chama cha starehe cha wanywa kahawa
pale New Street.

Hatuna haja ya kupoteza muda wetu na wanywa kahawa.
 
Exactly!
 
Kitabu uandike wewe, mjadala uhusu kitabu hichohicho, mtuhumiwa ni wewe, kisha utetezi uutoe kwenye kitabu hichohicho halafu useme hujinukuu?

Inaingia akilini kweli mzee wangu wewe?
Sasa ulitaka iweje?.Kichwa cha habari ni Uchochezi wa Mohammed Said.................kuhusua kitabu alichoandika.Hiyo mada nayo yeye kakumbana nayo hapa JF wala hakukuomba uianzishe kama imekushinda sema.Yeye anachofanya ni kujitetea kwamba hicho kitabu hakina uchochezi.Itakuwaje umepewa paper ya Chemistry lakini majawabu yako yote ni BIology?.
Mohammed endelea kama hivyo sisi tunakusoma na tunawaona walivyopwaya.Eti wanakufundisha majibu!.
 
punguza jazba mzee wetu, tupe darsa kidogo kwenye hayo maswali mawili tu ya babu Mag3
 
Last edited by a moderator:
Wewe wanena, kumbuka 80,000 wanakusoma! Asante kwa majibu yako ila nina maswali mawili tu ya nyongeza;

  1. Kwa nini mtaa ule uliitwa New Street na ni mwaka gani ulipewa jina hilo?
  2. Je wakati huo wazulu, wanubi na manyema walikuwa wakiishi mtaa gani?
Nakuachia uwanja, endelea kutoa darsa...
 

Mag3,

Kuhusu darsa.
Angalia hizo post nilizoweka leo.
 

Ami,

Wanasoma na wanafaidika hilo nina hakika.
Alhamdulilah.
 

mbona tayari hayo maswali umeshajibiwa au hukuyapenda kupewa uongozi nyerere sio tatizo, tatizo limekuja baada kupata uhuru akijitoa mshipa wa fahamu na kuwadharau wale waliomsaidi na kumpokea na kuwafanya maadui wake,kwa ustadi mkubwa mzee ms akaelezea ukweli ambao msioutaka nyinyi upande wa pili.
 
Mimi nimependa hiyo darsa uliyotoa kwangu.Najua wengi watafaidika.Endelea kufanya kama hivyo kwa kila atakayenasa kuingia mjadala huu.Allah azidi kukupa afya njema ya kufanya kazi hii.Hata hivyo wale wajinga sana wasikuchoshe.Achana nao.
Huo mshangao alioupata profesa Haroub naufananisha na ule nilioupata mwenyewe nyumbani kijijini.Bibi yangu aliyekuwa akinilea na kufuatana naye kila pahala nilipokua kidogo nikaelezwa kuwa ni mchawi nilishtuka sana.Nilishtuka kwa sababu aliyenieleza hivyo alinipa na alama ambazo zote nilimkuta bibi anazo pale ndani.
 
HAPA mtu mzima Mohamed Said ana "smell rat" anaogopa kujipiga kitanzi-swali limeenda shule,majibu yake hapa yanaweza kuja pangua mengi,heri akae kimya-kwa lugha ya chandimu hapa tunasema kawekwa "mtu kati"



  1. Kwa nini mtaa ule uliitwa New Street na ni mwaka gani ulipewa jina hilo?
  2. Je wakati huo wazulu, wanubi na manyema walikuwa wakiishi mtaa gani?
 
Last edited by a moderator:

Son...

Una maana ''smell a rat.''
Yaani nimegutuka.

Kaka hunijui.
 
Son of Alaska, huyu mwalimu wa Spike Lee na wenzake angekuwa hakwepi maswali huu mjadala haungefika hapa ulipofikia ila subiri atakavyojaribu kukwepa au "spin" atakazozileta! Hata hivyo nampa hint kidogo tu kuhusu miaka hiyo;

  • Wazaramo ambao idadi yao ilikuwa kubwa, makazi yao ya nyumba za makuti yalikuwa nje kidogo ya City Center kama Buguruni, Tabata na Ubungo.
  • Washomvi waliweka makazi yao Kunduchi na Msasani.
  • Wasukuma waliweka makazi Msasani na Magogoni.
  • Wanyamwezi (idadi yao pia haikuwa ndogo) makazi yao yalikuwa Kindondoni na Bonde la Msimbazi.
  • Wangoni walijikita Keko na Kijitonyama.
Swali langu kwa Mohamed Said ni kuwa wazee wake (wazulu na Manyema) makazi yao yalikuwa wapi? Hapa naongelea mara tu baada ya Tanganyika kutwaliwa na Uingereza kwenye 1920s. Sasa namwomba asiwanyime wanafunzi wake akina Spike Lee fursa ya kufyonza ilmu, awaambie wazee wake waliishi mitaa ipi...hilo tu. Tukumbuke kuwa idadi ya wakaazi wote wa Dar es Salaam wakati huo ilikuwa haifiki 20,000!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…