Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kwa kweli mimi sina tatizo na fikra zako kama ulizoandika hapo juu.
Yote ni maswali ambayo mtu yoyote anaweza akajiuliza baada ya
kusoma kitabu changu.

Mathalan chuki ya Wazulu Kleist, Plantan dhidi ya utawala wa Kiingereza
hili lilijitokeza wazi kupitia Schneider Abdillah Plantan katika uchaguzi wa
TAA wa 1950.

Kafanya vurugu mbele ya maofisa Waingereza waliohudhuria kikao kile pale
Ukumbi wa Arnautoglo kupelekea hadi uchaguzi ukafanyika.

Mdogo wake Ramadhani Mashado Plantan alikuwa na gazeti Zuhra ambalo ndilo
lilikuwa sauti ya Waafrika wa Tanganyika na gazeti la kwanza kuitangaza TANU
na kumnukuu Nyerere.

Tahariri zake zilikuwa zikiishambulia sana serikali ya kikoloni (nakala za gazeti hili
zipo East Africana, maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam).

Mifano ya chuki hii ipo mingi.

Hilo la Kleist kupinga utawala wa Wajerumani ni kweli hakuna popote katika nyaraka
zake na maisha yake hilo limejitokeza sana sana alikuwa Aide de Camp wa Von Lettow
Vorbeck katika Vita ya Kwanza ya Dunia (1914 - 1918).

Huu ni ukweli hakuna anaeweza kuupinga.

Ni ukweli pia mlezi wake Affande Plantan ndiye aliyekuwa mkuu wa Germany Contabulary
na nafasi hii ndiyo iliyofanya watoto wote wa askari wa Kizulu akina Klest, Mashado, Thomas
nk. wapate elimu ya juu kwa wakati ule.

Huu ni ukweli wa historia na hakuna anaeweza kuukataa.

Lakini hiyo siasa aliyofanya Nyerere Makerere ni ipi basi?

Mimi binafsi nimesoma nyaraka nyingi sana kuhusu Nyerere na sijapata kuvutiwa na yeye mpaka
alipofika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953.

Sasa hapa kuna kitu watu wengi hawakifahamu na yeye mwenyewe kwa kuwa hakupenda kunasibishwa
na harakati za Abdulwahid habari hizi hazikupata kujulikana.

Nyerere alipochukua uongozi wa TAA 1953 chama kilikufa.

Ukipenda na wanaukumbi wakiona kuna haja naweza Insha Allah nikaeleza kwa kirefu nini kilitokea.

Hilo la Nyerere kutotoa jina lake akamwachia Nyerere kupita bila kupingwa vilevile ikiwa ni lazima
naweza nikalieleza hapa.

Iwe itakavyokuwa naheshimu fikra zako.
 
Ushawahi kujiuliza kwanini barabara za lami zipo siku nyingi kutoka dar kwenda Mbeya?nataka arusha Moshi kuja dar?na kwanini hakuna mawasiliano ya kutoka Mtwara lindi kwenda sehemu yoyote kwenye jamhuri hii?


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Napenda kusahihisha jambo dogo.

Mzee Chiume ile historia alokuwa anataka kuandika haikuwa historia ya TANU
bali historia ya vyama vya ukombozi wa Africa pamoja na TANU.

Mimi nilimjua kupitia Ally Sykes.

Mzee Kanyama Chiume alikuwa hana pa kuanzia kuhusu TANU kwa shida ya nyaraka.
Kwa hiyo alikwenda kwa Ally Sykes kumuomba nyaraka ili aanze utafiti.

Hapo ndipo Bwana Ally Sykes akanikutanisha na Mzee Chiume.
 

Kwa hiyo kusema kuwa kina Sykes walikuwa wanaongoza harakati za kupinga ukoloni kama ulivyosema hapo juu kuwa:

Ukoo wa Abdulwahid, mtoto wa Kleist Sykes ulikuwa unafahamika kwa kuongoza mapambano dhidi ya serikali.

Ushahidi wa haya ulikuwa unapatikana katika nyaraka kati ya ukoo huu na serikali ya kikoloni.

Kwa hiyo siyo KWELI kwamba ukoo wa Sykes uliongoza mapambano dhidi ya serikali isipokuwa kama unamaanisha kuwa 'serikali' hapa unaizungumzia ile ya Mwingereza tu.

Je, siyo KWELI kwamba Sykes aligeuka dhidi ya serikali ya Mwingereza kwa sababu walimuondoa Mjerumani na ukoo wake ulifanya hivyo hivyo kwa sababu yule waliyemtumikia kwa maisha yao na ambaye kwake walipata ujira wao aliondolewa na Mwingereza? Kwamba harakati za Sykes dhidi ya Mwingereza hazikuwa kwa sababu ya kutaka uhuru wa Mwafrika zaidi kuliko kumuondoa aliyemwondoa kipenzi chao - Mjerumani?


Lakini hiyo siasa aliyofanya Nyerere Makerere ni ipi basi?

Mimi binafsi nimesoma nyaraka nyingi sana kuhusu Nyerere na sijapata kuvutiea na yeye mpaka


alipofika Dar es Salaam na kuingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953.

Naomba - ikikupendeza - ututajie angalau maandishi au nyaraka tatu tu za Nyerere kabla ya 1953 ambazo umezisoma na ambazo hazikukuvutia hadi alipokuja Dar in 1953. Maana fikra za Nyerere kisiasa hazikuanza kujengwa alipokuja Dar na kujiunga na TAA; zilikuwa zimejengwa miaka mingi nyuma na aliziweka wazi hivyo.

Kwa maana mimi nina maandishi yake akiwa Chuo Kikuu cha Edinburg (1949-1952) hivi ambapo mawazo yake juu ya Ukoloni na Demokrasia yalikuwa tayari yamekomaa. Na yapo maandishi yake wakati akiwa Makerere vile vile ambayo yanaonesha political maturity. Aliyoyafanya Dar baada ya kutoka Uingereza ulikuwa tayari ni mwendelezo wa fikra zake ambazo alikuwa tayari ameanza kuzijenga mapema. Siyo Sykes wala Rupia au mzee mwingine wa Dar waliochangia mabadiliko makubwa ya kifikra hasa dhidi ya Ukoloni ndani ya Mwalimu. Alipokuja Dar alikuwa tayari anajua nini anataka kufanya.

Katika mahojiano yake na jarida la New Internationalist Mwalimu Nyerere mwenyewe anaelezea fikra zake zilivyokua dhidi ya ukoloni na kweli haikutokea Dar. Anasema hivi alipoulizwa juu ya ni jinsi gani alipata mawazo ya kupinga utawala wa kikoloni.



Kutokana na kauli ya Nyerere mwenyewe siyo kusimuliwa na watu anasema kuwa mawazo yake ya kisiasa na kujishughulisha na siasa vilianzia kabla ya Kuja Dar na kuanza kazi na kina Sykes in 1953 kama unavyotaka watu waamini. Tunaweza tukakubali kuwa ilikuwa miaka 10 kabla au angalau miaka minne kabla akiwa Uingereza. Kama hili ni kweli - na sioni unaweza vipi kupingana na kauli yake mwenyewe - basi madai yako kuwa ni kina Sykes waliomuingiza Nyerere kwenye siasa na kuwa ni Dar ndiko alikoanzia siasa hayawezi kuwa kweli. Sivyo?



Miye nitafurahi ukiweka kwani itatupa mwanga wa kuuliza mengi zaidi na kujifunza mengi zaidi. Tafadhali tuwekee hapa mheshimiwa
 
Mzee Mohamed Said, jee huyu Bi Mluguru biti Mussa mama yake Abdu, ndiye huyu aliyekuwa akiiishi pale Upanga, opposite Califonia Dreamer?.

Naomba utuhadithie hicho kisa cha Nyerere "kulishwa sumu!".
Pasco.

Hapana huyo wa pale Upanga ni mama yetu.
Mke wa Abdu Sykes mama yake Daisy, Kleist, Adam na Omar (marehemu).

Bi Mluguru biti Mussa ni mama yake Abdu Sykes.
 
 
 
 
Hapana huyo wa pale Upanga ni mama yetu.
Mke wa Abdu Sykes mama yake Daisy, Kleist, Adam na Omar (marehemu).

Bi Mluguru biti Mussa ni mama yake Abdu Sykes.
Nilipelekwa pale Upanga na Mwamvua, na kuna vitu kuhusu Maria Nyerere, Mama yenu alinihadithia, yeye ndiye aliyempokea na kuishi nao nyumbani kwao mara baada ya Mwalimu kuacha kazi na ikawa ndio kama Mama Maria kaletwa kwa "kungwi", wakamfundisha kila kinachofundishika kuanzia kusukuma chapati, kuokota vifuu na makumbi kwa ajili ya biashara ndogo ndogo, hadi biashara za kuuza vitumbua!. Kwa vile mimi sio mwandishi sikuweza kuandika, ila kwa vile Mama Maria yuu hai, ni busara simulizi yake ikarekodiwa na kuwa documented, vinginevyo itaja siku ya siku, hatakuwepo tena, na ikitokea simulizi kama ya huyo mama yenu, ikasimuliwa upande mmoja, itakuja onekana ni uongo!.
Kwa Watanzania wengi, wanamfahamu Mama Maria kama mama wa nyumbani tuu, simulizi ya mama yenu kuhusu Maisha ya Mwalimu na Mama Maria wakiwa ni wageni wao, wakiishi nyumba moja kabla ya Mwalimu kupatiwa nyumba pale Magomeni, leaves much to be desired!.
Nimewahi kukutana na mama Maria several times na mara ya mwisho ni last December tumesafiri same flight next seat nilitamani kuomba appointment, yule bodyguard wake anakuwa too protective, kumzuia Mama asizungumze hata maongezi ya kawaida tuu!. Nadhani moja ya kazi za hawa ma body guard sio tuu kuzuia asidhurike, bali ni gate keepers kuhakikisha nothing goes out!.
I wish panapo majaaliwa, nitafuata the right channels nimrekodi huyu mama, just for record keeping na sio kusubiri zile simulizi za "..alikuwa".
Pasco.
 
 
 
Mkuu Maalim, Mohamed Said, nimenote katika sumulizi zako, linapotokea jina kama Dr. Kyaruzi na Abdulwahid, hata kama Dr. Kyaruzi ndio aliyekuwa mkuu, wewe utaanza na Abdulwahid na kufuatia Dr. Kyaruzi, hivyo kupelekea kuonekana kana kwamba anaye play the leading role ni Abdulwahid na Dr. Kyaruzi kuonekana kama ni subordinate tuu wakati ukweli halisi unaujua fika kuwa japo ni kweli "the masses" behind harakati za uhuru kwa Dar es Salaam ni "Wazee wa Darisalama", ila the main players, "the brain behind" ni watu kama kina Nyerere, Kyaruzi and the like, na sio Wazee wa Darisalama!.
Pasco.
 
 

anapozungumzia Wazee wa Dar hazungumzii watu kama kina Rupia, Kyaruzi, Mhando n.k... ana maana yake maalum. Tulishaelewa hilo na ukumbuke hataki kuzungumzia ya Wazee waliosahaulika (including hawa kina Rupia, Kyaruzi n.k) yeye ana ndugu yetu anaposema "wazee" ana maana ya Wazee wa Kiislamu na kuwa walikuwa na nafasi ya pekee. Ili kukamilisha hili narrative ni lazima awataje wazee wa Kiislamu kwa namna ya kipekee kuliko wengine ili narrative yake ikamilike. Ni lazima umsome ndugu yetu huyu hivyo.

Ukitaka kuzungumzia mchango wa wazee wengine wasiokuwa Waislamu wakati wa harakati za uhuru na waliokuwa Dar inabidi uandike stori hiyo kuelezea juu ya "wazee wako" kwani yeye kaandika juu ya wazee "wake" a.k.a Wazee wake Waislamu.
 

Inawezekana lakini ndiyo wewe unaniambia sasa.
Haikunipitia kabisa.

Kuhusu ''brains'' baba yangu ananiambia kuwa yeye na Abdu walianza kusomeshwa mashaf
yaani Qur' an siku moja.

Abdu kamaliza kabla ya wenzake wote na akaja kuwa ndiyo mwalimu wao maalim asipofika darasani.

Cambridge alitoka first class.

Kyaruzi alipata kusema kuwa kama si ile mipango ya Mwapachu na Abdu ya 1950 Tanganyika isingepata
uhuru 1961.

Alikuwa mtu wa kipaji sana.
Si ajabu historia ya Nyerere ukimleta Abdu.

Matatizo tayari.

Dar es Salaam ya 1950s ilikuwa nyingine.
Kyaruzi "was playing second fiddle."

Huu ndiyo ukweli wa siasa za miaka ile.
Nani anamjua Kyaruzi?
 
 

Kitabu changu nimeandika habari za wazee wangu na hili nalisema kila siku.
Siwezi kuandika habari za watu ambao mimi siwafahamu.

Hao wengine nimewataja kama ilivyo ada katika kueleza jambo.
Nisingeweza kueleza habari za watu wote hata wale ambao habari zao
sizijui.

Mimi ni Muislam na katika historia ile ya Kivukoni na mengi yaliyoandikwa
Waislam walitupwa nje.

Hii ndiyo sababu ya kuwarudisha katika historia.
Sasa nyie mngelimjuaje Sheikh Hassan bin Amir kama nisingelimwandika?
 
 
MS anaamini kuwa Ditopile anaweza kuwa alitendewa vibaya na magazeti yanayosimamiwa na wakristo lakini yeye na kundi lake wana haki ya kuaminiwa kuwa hakuna upotoshaji hata pale ambapo imedhihirika kuwa kulikuwa na upotoshaji wa hali ya juu. 1. Kuhusu namba za mitihani, 2. Kuhusu kupigwa marufuku kitabu chake UDSM ''by Christian lecturers'' n.k. Anachotaka ni ku-provoke mtafaruku kama alivyowahi kuwataka maaskofu wajibu hoja za kitabu pengine kulenga kuamsha hisia na kuchochea vurugu kwa uwazi kwasababu Ponda si peke yake. Hapa anatupa ushahidi kuwa hana uthibitisho bali hisia zake zinamtuma kusema hivyo. Tena bila haya MS amekua akitumia neno ''huo ni ukweli'' sidhani kama kuna ukweli usiothibitika. Tunaposema historia asemayo imejengwa katika hisia, ushihidi ni kama huo.Hata kama maandishi yake yanaweza kuleta vurugu, MS yupo bize na toleo la tatu, take care of today, tommorrow will take care of itself.

Waliobadili majina ya mitaa ni madiwani wa Dar es salaam. Walioshindwa kuwaenzi wakazi na wanaharakati ni madiwani na wananchi wa Dar es salaam. Kuna nyakati Mwenyekiti wa CCM mkoa, Wilaya, Mkurugenzi, Meya na Madiwani wote walikuwa wazee wake. Anajua fika kuwa kosa si la Nyerere ni la wazee wake kama akina tambalizeni ambao badala ya kufikiria namna ya kuboresha maisha ya wakazi na wenyeji wamebaki kuandika ngonjera kama hizi tunazoziona.

MS hapaswi kutumia muda mwingi kumhukumu Nyerere kwa jina la mtaa mmoja ambao mtendaji wa kata angeweza kukaa na wananchi na madiwani wao wakafanya hivyo.

MS anapaswa aangalie picha kubwa zaidi. Je,kuna kitu gani cha kumbu kumbu ya Mzizima walikoishi wenyeji wetu?
Je, kiwanja cha Chang'ombe kiendelezwe vipi kwa faida ya wakazi wa jiji.
Je, kifanyike nini wakazi wa kariakoo-mzizima wanufaike na ardhi na rasilimali zilizopiganiwa na akina Abdul Sykes na Kiyate. Kwanini wahamishwe kwa kupewa milioni 15 kwa kitu chenye thamani ya milioni 400 n.k.
Kufikiria street moja tu ni tatizo kabla ya tatizo.

Walioifikisha Dar hapo ilipo ni wazee wako, Nyerere anafanywa Bangusilo tena kwasababu tu ya jina Julius.
Anahukumiwa kwa uzembe, ujinga na ututusa usiomhusu.
Nyerere hakuwa diwani Moshi, Mwanza au Mbeya! kimeshindikana nini Dar!
MS warithishe watoto werevu na kujitambua kwasababu dunia ya leo majungu haujawa mtaji wa maana the least to say
Swali 3( a) Kwanini Waislam wasitake kukaa na Mwinyi, Mkapa au Kikwete bali serikali?
b)Mbona yaliyotokea nyuma hayatajwi kama ni matatizo ya serikali yanasemwa ni ya Nyerere na kwanini leo hayasemwi kama ya Kikweteyanasemwa kuwa ni ya serikali?
Mohamed: Sijui hilo swali wanaweza kujibu viongozi wa Waislam (b) Sijui waulizwe viongozi wa Waislam
Sasa kama unajua hujui na huna majibu, kwanini ujihusishe na kuwa msemaji wa waislam?

Ukweli ni kuwa unaogopa kusema Mwinyi, Mkapa au Kikwete kwasababu kufanya hivyo utagusa wazee wako.
Tunarudi nyuma kuwa tuhuma dhidi ya Nyerere ni za kupikwa kwasababu historia inamsuta MS.
Huwezi ukawa na tukio moja katika historia ukachagua namna ya kulijadili au kuliandika kwa nyakati tofauti.
Chuki dhidi ya Nyerere ni kwasababu tu ya kumhusisha na dini yake.

MS unapaswa kwenda kujadiliana na Kikwete kwanza, kwasababu Nyerere ni marehemu. Kuendelea kumsukumia lawama hakumdhuru bali kunaidhuru jamii yako. Kumzushia yaliyomshinda Mwinyi na Kikwete ni ubaguzi wa ajabu sana.
Ubaguzi ni dhambi mbaya sana na humdhalilisha awaye Nyerere aliwahi kulieleza na maandishi yapo. Mkapa kalizungumzia hotuba ipo.
Kikwete hajawahi kulizungumzia. Tatizo lipo lakini si kwa namna unayoielewa wewe na kundi lenu.

Kwanza hamtafuti suluhu mnachotaka ni kuvuruga nchi. Mtu mwenye suluhu hawezi kuwa anapiga mdomo na ikifika mahali anaulizwa tufanye nini anajibu haya
Hayo mengine matatu ni Waislam wanyewe waseme uwiano nk
MS anachotaka ni kuita majina na kuwapa watu madaraka. Kuita majina na kuwapa watu kazi za taaluma.
Kwamba kwake Daktari anaweza patikana kwa uwiano au kupiga kura!!!

Kibaya zaidi MS anaamini kuwa mtu anayeitwa Abdallah Husein Bin Suein au John William Walace basi huyo ni muumini wa dini. Tatizo la watu kama akina MS ni kutochukua kioo na kujiangalia!Ni kunajisiwa fikra zao na ukoloni wakidhsni kuwa dini ni jina hata kama awaye ni mzushi, jambazi, muongo.

Hivi unapata wapi mtaalam au kiongozi kutoka Kilwa kama shule zinafungwa kwa kukosa wanafunzi.
Shule ifungwe kwenda kusikiliza kesi ya Ponda!! Hayo si tatizo kwa MS,tatizo ni Nyerere!
MS waambie watu wako ukweli acha kuwadanganya ili uuze nakala za vitabu, unawapotezea muda wa kusonga mbele.
Swali 4 (a)Kitabu cha Bergen Kimepigwa marufuku kwa tamko la nani na lini!
b) Kitabu cha Mohamed kilichozuiliwa kuwa reference UDSM, ni kwa tamko la nani na lilitoka lini
Mohamed :Kitabu kuzuiwa hilo haliwekwi dhahir ila wanafunzi wa historia wanaambiwa hivyo
MS hana ushahidi wa maswali yote mawili, bado anasema alichoandika ndio ukweli. Huu ni ushahidi kuwa sehemu kubwa ya ngano hii imejengwa kwa fikra zake binafsi zikichagizwa na uzushi.

Mwanafunzi hawezi kuja kusema na mtafiti akakubali tu kwasababu ni mwanafunzi huyo ni Mwislam.
Hili kama si majungu ni nini. Uliposema ndani ya kitabu kuwa christian lecturers at UDSM... ulichotaka ni kujenga chuki tu.

Huko Ulaya wasikojua hali ya Tanzania hawawezi kukuuliza uwape ushahidi. Ndio maana tunasema MS ni mpotoshaji, mzushi na mjenzi wa historia kwa kutumia majina na matukio huku akichomeka mbegu yake ya chuki miongoni mwa jamii.

Kusema jambo usilo na uhakika nalo ni uzushi na ni uongo. Dini ya kiislam haitaki hivyo na imekataza.
Unapaswa umuogope mwenyezi mungu kwanza kabla ya mauzo ya kitabu.
Muogope mola wako kabla hujazua balaa maana hilo limekatazwa.

Sasa tuna mambo mengi sana ambayo Mohamed ameyaandikia kurasa na kurasa na ameshindwa kuyatetea kwa mantiki,
hoja na hekima. MS nani asiyejua kwanini unakimbia hoja na maswali na umebaki kukata vipande vya kitabu.

Ninafikiria hivi kama kuna mwanafunzi anaandika thesis na amefanyia reference kitabu hiki, atawezaje kuitetea thesis yake kama mwandishi hawezi kutetea maandiko yake. Sad!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…