Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

 

Mzee miye wala sina shida kwani nimekuelewa vizuri; tatizo langu ni kuwa watu wanaweza kufikiria unaandika historia ya harakati za Tanganyika za majina ya watu waliosahauliwa. Ni vizuri watu wakusome kama unavyosema unachoandika wewe ni kwa ajili ya kuzipamba harakati za WAislamu na ili hili lifanikiwe ni lazima Wakristu wengine ambao nao walikuwa na mchango mkubwa wawekwe pembeni.

Kimsingi unachomtuhu Nyerere kukifanya kwa Waislamu (au waandishi wa historia ya Nyerere) ndicho wewe unakifanya dhidi ya wazee wa Kikristu walioshiriki harakati zile zile. Kwamba historia ya Waislamu ilifutwa au kuwekwa pembeni na ni muhimu kuirudisha lakini wakati huo huo wewe mwenyewwe unajitahidi kuweka pembeni majina ya wazee Wakristu ili kkupamba wazee wa Kiislamu.

Utakuwa na tofauti gani na wale walioandika historia ya Nyerere basi?
 

Asante sana mkuu kwa kunyumbulisha mjadala huu kwa uchambuzi imara na usanifu wa daraja la juu kabisa!

Watanzania wanatuona na kutusikia, ninawasihi wayatumie mawazo yetu kulinusuru taifa letu na uchochezi wa Mohamed Said.
 
Ninafikiria hivi kama kuna mwanafunzi anaandika thesis na amefanyia reference kitabu hiki, atawezaje kuitetea thesis yake kama mwandishi hawezi kutetea maandiko yake. Sad!

Hili swali la kufikirisha kwa mtu mwenye kutumia chembe zake za Ubongo vizuri. Kama mwandishi wa kitabu anashindwa kutetea kitabu chake mwenyewe na badala yake kutaka watu wengine waandike vya kwao msomi anayeweza kukinukuu atakinukuu vipi?
 
Kwa kuwa mnaojaribu kumuelimisha, kumkosoa Mzee wetu Mohamed Said ni WAKRISTO, hilo tu ni kikwazo tayari kwa Mzee wetu huyu. Mbaya zaidi, tayari keshaandika na tayari anaungwa mkono na wale aliowakusudia. Humu JF atabaki kujitetea na kukwepa kila atakapopata fursa ya kufanya hivo.

Naamini angeshirikisha utafiti wake huu watu wengine ambao bado wako hai na wanaijua vizuri Tanganyika, asingeandika maoni ya upande mmoja tu halafu akayaegesha na kuyaegemeza kwenye DINI yake. Wapo watu wanaojua kwa undani kwa nini familia ya akina Sykes ilijitenga na siasa za nchi hii mara baada ya Abdu kuukosa urais wa TANU. Hili, Mzee wetu Mohamed amelisukumia kwenye udini makusudi kabisa.


Mzee wetu Mohamed hasemi ni kwa nini akina Sykes hawakumuunga mkono Zuberi Mtemvu, Mwislam mwenzao, alipoanzisha chama. Anamtetea sana Abdu na wadogo zake kukaa kimya hadi baadhi yao wakafariki. Anauona ukimya wa Mwalimu juu ya kitabu chake kwamba ni kukiri yote yaliyoko mle ni kweli, kweli tupu!
 
hili swali la kufikirisha kwa mtu mwenye kutumia chembe zake za ubongo vizuri. Kama mwandishi wa kitabu anashindwa kutetea kitabu chake mwenyewe na badala yake kutaka watu wengine waandike vya kwao msomi anayeweza kukinukuu atakinukuu vipi?


ndugu mzee mwanakijiji,huoni jinsi unavojicontradict??alishakuambia ya kwamba yeye anaandika historia ya wale waliosahaulika ama walioufutwa kwa makusudi katika historia ya mapambano ya nchi hii,na kajitahid kuandika ya wale anaowafaham na ambao wengine pia inawafaham ila kwa sababu zao tuh wakaamua kuwaondoa na kuufanya ummah mkubwa kutofaham chochote kuhus wao.anachofanya yeye sasa ni kuihuisha ile historia,
sasa kwanini uje uipinge eti kisa hajaweka majina ya wazee wa kikristu?nyinyi si mnaamin huo mchango wa wazee wa kikristu ambao upo na mnaufaham??sasa kwani yeye ameupinga??yeye alichofanya ni kuandika kwa wale ambao historia imewatenga pasi na sababu za kushibisha njaa ya akili,sasa naona anaandamwa eti kisa wengi wa aliowaandika ni wazee wa kiislam na kwamba anatetea udini,kivipi??sasa kumbe kutetea historia ya wale waliofutwa kunahusiana vipi na dini ya mtu??
Huyu ndugu mohammed said kawafungua wengi sana macho,na juhudi hizo za kuupinga ukweli huu wala hazitazaa matunda,ukweli hupokelewa tuh hata kama ni mchungu.
 
Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji.

Hata siku mmoja hatujawahi kuyasoma mabandiko yenu humu jamvini mkiwaelezea hata kwa chembe ya uzuri ambayo wameyafanywa na hawa wazee wa Dar es Salaam katika harakati za kupigania uhuru.

Mtu makini akiwasoma ataona hata nyie mpo upande wa wazee wa kikiristo ambao walipigania uhuru kwa maana hiyo wote mnaangukia kundi moja. Nyie mnatetea wazee wenu wa kikistu na Mohamed Said anatetea wazee wake wa kiislam.

Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Yericko Nyerere, Mag3, ni wakati wenu sasa kukaa chini na kuunganisha nguvu zenu kuandika kitabu ambacho kije kuboboa kabisa hizo "ngano" za Mohamed Said kama mnavyoziita.

Watanzania watajifunza mengi kupitia nyie.
 
Last edited by a moderator:


hiyo nayo si hoja ya kuishupalia,na usijaribu kuuchanganya uislam na siasa,uislam ni mfumo timilifu wa maisha na uliojikamilisha katika kila nyanja ya maisha ya mwanadam,

nani asiejua ya kwamba zuberi mtemvu alikuwa anafanya siasa,hadi alipofikia hatua ya kumpinga nyerere wazi wazi na kuanzisha chama chake hoja zake aliziweka hadhwarani,wazi wazi bila kificho,msimamo wa kina sykes na nyerere kisiasa pia ulikuwa unaeleweka na kufahamika wazi wazi,haikuwa sawa kwa kina sykes kumuunga mkono mtemvu eti kisa tuh ni muislam mwenzao,hawakuwa wanapigania dini,au wanafanya jihadi,pale walikuwa wanafanya siasa,na hakuna kipengele katika uislam kinachosema eti uwe bega kwa bega na muislam mwenzako eti kisa mnashare the same political philosophy or idea,si kweli na usijaribu kututoa nje ya mstari,rudi kwenye hoja kuu ya mjadala ili tusiachane achane.
 

Jibu zuri pasi kiasi.
 

Usipotoshe ndugu, alichofanya Mohamed ni kuwatenga zaidi, sio kuhuisha historia!

Unadhani waliosahauliwa katika historia ni wazee wakiislamu tu kama alivyofanya?
 

Mimi nimewaomba sana hawa ndugu zangu na wao waandike habari za huko kwao
walikotoka ikiwa walikuwapo walioipigania TANU.

Hili hawalitii maanani.

Wameshughulishwa na kupiga vita historia ambayo ishaandikwa na kitabu kinasomwa
sasa mwaka wa 15.
 
-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na Mwalimu? Mwalimu amefariki bila kuandika historia ya nchi hii. Hata hiyo ya Kivukoni haina mkono wala baraka za Mwalimu.

-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na DINI yao? Ni watu wa dini hii tu waliosahaulika? Ni kweli Mwalimu aliuchukia UISLAM na WAISLAM?
 
kama mwandishi kaandika na kuirudisha kwa jamii historia ya wale waliotengwa kwa makusudi na kufutwa kwa hila na ghilba,iweje sasa wengine waje wamshutumu ya kwamba kuna wengine wapo tena wa upande mwingine hajawaandika,na ambao hata yeye hawafaham,zaid ya hapo wameandikwa kwenye vitabu vingine na watu wakawafaham,iweje sasa akosolewe eti ooh umeewaacha hawa hujawaandika kisa si wazee wa kiislam ya nini sasa??hao si tayari wameshaandikwa kwenye historia na watu wakawafaham??iweje sasa nayeye anapoandika wengine ambao kwa makusudi walifutwa kwenye historia hiyo aonekane kama ni mdini.,mhaini,ana choko choko,mvunja amani n.k,iweje ahukumiwe hivo??au watu walikuwa wanapenda hii history aliyoihuisha ipotelee kuzimu moja kwa moja??
Tuwe fair,na tusiegemee upande wowote.
 
Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na Mwalimu? Mwalimu amefariki bila kuandika historia ya nchi hii. Hata hiyo ya Kivukoni haina mkono wala baraka za Mwalimu.(KWANI YEYE KAKUAMBIA KUSAHAULIKA UKO KUNA UHUSIANO NA MWALIMU AU YEYE AMEBASE KUELEZEA KUSAHAULIKA KWA WALE WAZEE NA UHUSIANO WA HARAKATI ZA UHURU WA NCHI HII??MANTIKI UMEIPTA LAKINI??

-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na DINI yao? Ni watu wa dini hii tu waliosahaulika? Ni kweli Mwalimu aliuchukia UISLAM na WAISLAM?(LA HASHA,KUSAHAULIKA KWA WALE WAZEE HAKUNA UHUSIANO NA DINI YAO,NDIO MAANA TUNAHOJI WHY WAKASAHAULIKA??AU KWA KUWA WAO NI WAISLAM??KWANIN WENGINE WAMEEANDIKWA NA WAO WAKAACHWA??,HILO SWALI LA KUSEMA MWALIMU ALIWACHUKIA WAISLAM NA UISLAM LINAJIELEZA WAZI WAZI,USITAKE KUNICHOTA HISIA ZANGU UKANIUHUKUMU KAMA MIMI NI MDINI,HOJA YETU HAPA SIO HIYO,ILA UKWELI JUU YA HILO MWENYE MACHO HAAMBIWI ONA,NA MWENYE MASKIO HAAMBIWI TAZAMA.
 

Ingekuwa bora kabla ya kuandika ukafanya utafiti angalau kidogo.
Nani kakuambia kitabu cha historia cha Kivukoni haina mkono wa
Nyerere?

Kasome utangulizi wa kitabu.

Hilo lingine sina haja kulisemea.
 
Kaka Mohamed Said. Nauliza hiyo mitaa ya New Street, Mbaruku Street, Stanley Street, kwa sasa inaitajwe?
 
Usipotoshe ndugu, alichofanya Mohamed ni kuwatenga zaidi, sio kuhuisha historia!

Unadhani waliosahauliwa katika historia ni wazee wakiislamu tu kama alivyofanya?

Fanya utafiti kidogo zungumza na waliokisoma kitabu usikize wanasema nini.
 
Hivi Mzee Mohamed anaposema WAISLAM walitengwa na wakasahauliwa kwenye HISTORIA ya nchi hii anakuwa anamaanisha nini hasa! Hapa Mzee wetu anapigania nini kama sio DINI yake?
 
Kaka Mohamed Said. Nauliza hiyo mitaa ya New Street, Mbaruku Street, Stanley Street, kwa sasa inaitajwe?

Spike the cool one.

New Street ni Lumumba.

Mbaruku umebakia hivyo hivyo.

Stanley ni Aggrey
 
Hili swali la kufikirisha kwa mtu mwenye kutumia chembe zake za Ubongo vizuri. Kama mwandishi wa kitabu anashindwa kutetea kitabu chake mwenyewe na badala yake kutaka watu wengine waandike vya kwao msomi anayeweza kukinukuu atakinukuu vipi?

Sasa kama mshashinda sasa mnahangaika nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…