Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hapana inawezekana huko alikotoka alifanya makubwa.
Lakini kwa Dar es Salaam ambako ndiko hasa siasa zilikuwa
kali hakuna aliyepata kusikia jina la Nyerere.

Sasa wazee wa Dar kutokusikia jina haina maana Nyerere hakuwa ameanza siasa. Kama wao hawakusikia inawezekana ni kwa sababu walikuwa hawana namna ya kusikia lakini inaonekana kati ya wasomi wa wakati wake wapo waliosikia jina la Nyerere kama unavyoeleza hapa chini.

Mwaka wa 1952 Julius Kambarage alikuja Dar es Salaam kama mwalimu akisomesha St. Francis College, Pugu. Historia ya Nyerere katika siasa inafungamana pakubwa na historia ya Hamza Kibwana Mwapachu. Hamza Mwapachu alisoma na Nyerere Makerere College Uganda na wakawa pamoja Tabora mwaka wa 1945 na baadaye wakawa tena pamoja nchini Uingereza kwa masomo ya juu.

Mwapachu na Nyerere walikaa kati bweni moja walipokuwa wanafunzi Makerere wakati ambapo Kasella Bantu na Nyerere walifundisha pamoja hapo Tabora. Nyerere alitangulia kurudi Tanganyika akitokea Chuo Kikuu Cha Edinburgh, Uskochi akamwacha Mwapachu akiendelea na masomo Chuo Kikuu cha Wales, Cardiff.

Mwapachu alimpa barua Nyererere amfikishie kwa Abdulwahid Sykes.

Yeah inawezekana ilikuwa hivi lakini Nyerere alitumia barua hiyo kujitambulisha kwa Sykes?

Katika hotuba ya kuwaaga wazee wa Dar es Salaam aliyoitoa tarehe 5 Novemba, 1985 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Nyerere aliwaambia waliohudhuria kuwa Kasella Bantu ndiye aliyempeleka nyumbani kwa Abdulwahid na kumtambulisha.

Sijui kama unajaribu kuonesha kuwa Nyerere alisema uongo; lakini sioni contradictions yoyote hapo. Yawezekana alipewa barua na Mwapachu lakini physically ni Kassela Bantu aliyemtambulisha rasmi kwa Sykes?

Barua ya Hamza Mwapachu kwa rafiki yake Abdulwahid Sykes ilikuwa inamtambulisha Nyerere kwa Abdulwahid na ikimueza Nyerere kama mtu mwenye fikra nzuri zinazoweza kuisaidia TAA kufikia malengo yake.

Kwa hiyo ni wazi Sykes hakumpatia Nyerere fikra zozote mpya za kumuingiza katika harakati. Kwa simulizi lako hapo huoni kuwa basi ni Mwapachu ndiye aliyemleta Nyerere TAA na siyo Sykes? Na alimleta kwa sababu Nyerere tayari alikuwa ana fikra za kuweza kuisaidia TAA - hii ilikuwa kabla ya kukutana na Sykes na Sykes alichofanya ni kukubaliana tu na mawazo ya kina Mwapachu na Bantu?

Hotuba hii ya Diamond Jubilee ndiyo ilikuwa mara ya kwanza Nyerere kuzungumza hadharani siku zake za mwanzo Dar es Salaam na ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kuihusisha katika kadamnasi historia yake na TANU na kulitaja jina la Abdulwahid Sykes.

Lakini haiwezekani ikawa ni mara ya kwanza wakati tayari alishasimulia katika mahojiano na mke wa Du Bois na katika simulizi lake la We Must Run While They Walk na masimulizi mengine kadha wa kadha. Vitabu hivi vyote vilikuwa vinapatikana na miye nimeweza kuvipata na kuvisoma.

Nyerere kuelezea siku zake za mwanzo jijin Dar hakufanya mara ya kwanza mwaka 1985. Kihistoria hii si kweli.

Bahati mbaya sana hotuba ile ilivurugika na kitu kidogo sana. Nyerere alipokuwa anaeleza nafasi za uongozi katika TAA alisema hakumbuki marehemu Abdulwahid alikuwa na cheo gani.

Hili kwa hakika lilikuwa jambo lililoshangaza wazee wengi katika hadhira ile kwani wengi wao wasingelimfahamu Nyerere sama na kuletwa Makao Makuu ya TAA pale New Street na marehemu Abdulwahid Sykes.
[/quote]

Lakini hili si zito kivile; hivi kweli mtu baada ya miaka karibu 25 anatakiwa kukumbuka kila kitu wakati wote; hawezi kupitiwa. Leo hii tu kuna watu - mimi mmojawapo - naweza nisikumbuke vizuri watu muhimu katika maisha yangu walikuwa wanafanya nini miaka ishirini iliyopita. Sidhani kama unamaanisha Nyerere alikusudia kumfanya duni Sykes.

Hata hivyo hotuba ya Nyerere ilimpamba sana Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo na Mohamed Jumbe Tambaza. Nyerere alieleza mchango wa wazee hawa kwa maneno na visa vya kupendeza.

Lakini hapa inatatiza kidogo; kwa mtu mwenye chuki na Waislamu na wazee wa Kiislamu iweje awapambe mashehe na hawa wengine? Au alikuwa hajui kuwa ni wazee wa Kiislamu?

Ukimtoa Dossa Aziz aliyekutana na Nyerere kwa muda mfupi katika mkutano mkuu wa TAA Dodoma Aprili 1946, Kasella Bantu mwenyewe na Denis Phombeah, hakuna mtu mwingine aliyewahi kusikia habari za Nyerere.

Ukimaanisha Dar inaweza kuwa kweli lakini serikali ya Mwingereza ilishamgundua Nyerere way kabla ya kuja Dar na wapo watu waliokutana naye miaka mingi kabla ya kuja Dar. Sasa ukisema Dar tu haina maana yoyote kwani kuna watu Mbeya, Kigoma, Iringa, Songea ambao nao walikuwa hawajawahi kumsikia Nyerere. SIdhani kama hii ni hoja nzito kivile. Sidhani kama watu wa Dar walitakiwa wawe wamemjua Nyerere kabla ya kufika Dar.

Katika kukutana huku kati ya Nyerere na Abdulwahid Sykes mapenzi makubwa yalimea kati yao na kwa njia hii Nyerere akatiwa katika kundi la ndani katika TAA, kundi la vijana wasomi waliokuwa wakipanga mikakati ya kumng'oa Muingereza katika ardhi ya Tanganyika.

Nyerere hakuwa ameanzisha tawi la TAA akiwa Tabora kama mwalimu? Ilikuwa ni mwaka gani alipofanya hivi?

Nyerere alimwona Abdulwahid kama mtu mwenye akili sana, kijana aliyejiweza kihali na mtu mwenye moyo mkubwa usiokuwa na hasad wala choyo.

Naomba niulize hapa: Unalipata wapi hili katika hotuba, maelezo au maandishi ya Nyerere kuwa alimuona Sykes kuwa ana "akili sana"? Usinielewe vibaya hapa nataka nijue authority ya kauli hiyo - ama kutoka kwa mtu wa karibu sana na Nyerere kiasi cha kuweza kujua hili.

Abdulwahid alimuona Nyerere, kama mtu aliyeelimika vizuri kati yao na mwenye ustadi katika mijadala. Nyerere alipata nafasi ya kuifahamu dunia vizuri lau kama alikulia kijijini.

Sijui kama ulikusudia kutengeneza 'contrast' kwa makusudi au kwa bahati mbaya; kwamba Nyerere alimuona Sykes mwenye 'akili sana' lakini Sykes alimuona Nyerere 'aliyealimika vizuri' na siyo mwenye akili sana?
Zaidi Nyerere alikuwa amepata uerevu wa siasa kutokana na uhusiano wake na Fabian Society, wakati alipokuwa mwanafunzi Uingereza. Mijadala mizito sana ilijitokeza katika vile vikao vya kila Jumapili wakati akili na ujuzi wa siasa wa Abdulwahid vilipopambana na uhodari wa majadiliano wa Nyerere.

Hii contrast najaribu kuielewa; Nyerere alikuwa hodari wa majadiliano tu - hakuwa na akili sana na Sykes alikuwa na 'akili sana'. Inaburudisha kuona mapenzi yalivyo.

Na unaendelea na contrasts hii ya kiaiana hapa:

Abdulwahid alipata uzoefu mkubwa wa uongozi katika siasa nyumbani kwao kwa baba yake aliyeasisi African Association kisha wakati wa vita Burma na baada ya vita serikali ya kikoloni ilipomteua kuwa katibu wa kwanza wa chama cha wafanyakazi Dockworkers Union akiwa kijana mdogo wa miaka 24.

Sifa kwenda kwa Sykes na uzoefu wake na hapa chini Nyerere unavyomuona weye:
Nyerere hakuwa na wa ujuzi wowote katika siasa ukimlinganisha na Abdulwahid. Wakati African Association Tabora kiliposhiriki katika mgomo wa mwaka 1947 ambao chanzo chake kilikuwa mgomo wa makuli Dar es Salaam, Nyerere hakujihusisha na harakati zile za wafanyakazi ingawa yeye ndiye alikuwa katibu wa African Association pale Tabora.

Lakini unasema Sykes ndio alimwingiza Nyerere kwenye TAA mwaka 1953 lakini hapa unaonesha kuwa mwaka 1947 Nyerere tayari alikuwa Katibu wa AA huko Tabora. Kweli Nyerere hakuwa na uzoefu wa uongozi? Kweli hakuwa anajua siasa lakini akawa katibu kati ya wasomi? Kweli kuna watu wanaweza kuamini hili.

Lakini jambo jingine ambalo sijui kama umewahi kuliangalia kwani Nyerere anazungumzia hili kwenye We Must Run While They Walk ni mgomo ule wa 1947. Umewahi kujiuliza kwanini hakujishughulisha na mgomo ule au kama alijishughulisha kwa namna tofauti?

Kutokana na Nyerere kuingia katika harakati zile pale New Street pakawa na kuheshimiana na mapenzi makubwa baina yake, Abdulwahid, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.

Lakini nikikusoma vizuri hapo juu ni kama kulikuwa na dharau fulani hivi (sijui kama ndio unaita mapenzi) Sykes alimuona Nyerere kama mtu asiye na akili sana kama yeye ni hodari wa majadiliano tu na Nyerere akimuona Sykes mwenye akili sana!

Hivi ndivyo Nyerere alivyokuja kuingia ndani ya TAA Makao Makuu na hatimaye akaja kupendekezwa kugombea cheo cha juu kabisa cha uongozi wa chama mnamo Aprili, 1953.

Lakini kama simulizi lako kuwa Nyerere alikuwa tayari katibu wa AA Tabora mwaka 1947 ni wazi kuwa Nyerere alikuwa anatekeleza mpango wake wa muda mrefu tu wa kujiingiza kwenye siasa na ukiangalia sidhani kama angekuwa mtu mwingine Makao Makuu bado Nyerere angefika tu makao makuu; sidhani kufika kwake makao makuu ni kwa hisani ya Sykes na wale kuinuka kwake katika vyeo ni matokeo ya kuingizwa na Sykes makao makuu.

Nyota ya Nyerere ilikuwa imeshaangaza na ilikuwa muda tu mwanga wake ungefika makao makuu. Katika kitabu chako cha Sykes unaeleza vizuri jinsi habari za Nyerere zilivyoanza kufika kwa watu mbalimbali Dar wakati Nyerere yuko Pugu. Nuru inatabia ya kupenya hata kwenye kipenyo kidogo tu. Watu wa Dar walikuwa hawana namna ya kuikwepa nuru ya Mwalimu.

Uongozi wa TAA ulimpendekeza Julius Nyerere ili kukiimarisha chama kwa kuwa na Waafrika wenye elimu ya juu ndani yake. Ilibakia kwa Nyerere kukubali au kukataa.

Ni wazi asingeweza kukataa kwa sababu tayari alikuwa ameshaamua kuingia katika siasa miaka karibu saba nyuma.

Kujadili siasa haikuwa sawa na kuongoza chama kilichokusudia kunyakua madaraka kutoka kwa serikali ya kikoloni. Hivi vilikuwa ni vita dhidi ya ukoloni na ilibidi mtu ajitayarishe kwa lolote ambalo lingetokea.

Na historia inaonesha kuwa hakukuwa na mtu aliyekuwa amejiandaa kihisia, kifikra na kielemu kufanya kazi hiyo vizuri kama Mwalimu. Siyo Rupia, siyo Tumbo, Siyo Sheh Amir, siyo Mhando isipokuwa Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa.
 
Kitabu changu nimeandika habari za wazee wangu na hili nalisema kila siku.
Siwezi kuandika habari za watu ambao mimi siwafahamu.

Hao wengine nimewataja kama ilivyo ada katika kueleza jambo.
Nisingeweza kueleza habari za watu wote hata wale ambao habari zao
sizijui.

Mimi ni Muislam na katika historia ile ya Kivukoni na mengi yaliyoandikwa
Waislam walitupwa nje.

Hii ndiyo sababu ya kuwarudisha katika historia.
Sasa nyie mngelimjuaje Sheikh Hassan bin Amir kama nisingelimwandika?

Mzee miye wala sina shida kwani nimekuelewa vizuri; tatizo langu ni kuwa watu wanaweza kufikiria unaandika historia ya harakati za Tanganyika za majina ya watu waliosahauliwa. Ni vizuri watu wakusome kama unavyosema unachoandika wewe ni kwa ajili ya kuzipamba harakati za WAislamu na ili hili lifanikiwe ni lazima Wakristu wengine ambao nao walikuwa na mchango mkubwa wawekwe pembeni.

Kimsingi unachomtuhu Nyerere kukifanya kwa Waislamu (au waandishi wa historia ya Nyerere) ndicho wewe unakifanya dhidi ya wazee wa Kikristu walioshiriki harakati zile zile. Kwamba historia ya Waislamu ilifutwa au kuwekwa pembeni na ni muhimu kuirudisha lakini wakati huo huo wewe mwenyewwe unajitahidi kuweka pembeni majina ya wazee Wakristu ili kkupamba wazee wa Kiislamu.

Utakuwa na tofauti gani na wale walioandika historia ya Nyerere basi?
 
MS anaamini kuwa Ditopile anaweza kuwa alitendewa vibaya na magazeti yanayosimamiwa na wakristo lakini yeye na kundi lake wana haki ya kuaminiwa kuwa hakuna upotoshaji hata pale ambapo imedhihirika kuwa kulikuwa na upotoshaji wa hali ya juu. 1. Kuhusu namba za mitihani, 2. Kuhusu kupigwa marufuku kitabu chake UDSM ''by Christian lecturers'' n.k. Anachotaka ni ku-provoke mtafaruku kama alivyowahi kuwataka maaskofu wajibu hoja za kitabu pengine kulenga kuamsha hisia na kuchochea vurugu kwa uwazi kwasababu Ponda si peke yake. Hapa anatupa ushahidi kuwa hana uthibitisho bali hisia zake zinamtuma kusema hivyo. Tena bila haya MS amekua akitumia neno ''huo ni ukweli'' sidhani kama kuna ukweli usiothibitika. Tunaposema historia asemayo imejengwa katika hisia, ushihidi ni kama huo.Hata kama maandishi yake yanaweza kuleta vurugu, MS yupo bize na toleo la tatu, take care of today, tommorrow will take care of itself.

Waliobadili majina ya mitaa ni madiwani wa Dar es salaam. Walioshindwa kuwaenzi wakazi na wanaharakati ni madiwani na wananchi wa Dar es salaam. Kuna nyakati Mwenyekiti wa CCM mkoa, Wilaya, Mkurugenzi, Meya na Madiwani wote walikuwa wazee wake. Anajua fika kuwa kosa si la Nyerere ni la wazee wake kama akina tambalizeni ambao badala ya kufikiria namna ya kuboresha maisha ya wakazi na wenyeji wamebaki kuandika ngonjera kama hizi tunazoziona.

MS hapaswi kutumia muda mwingi kumhukumu Nyerere kwa jina la mtaa mmoja ambao mtendaji wa kata angeweza kukaa na wananchi na madiwani wao wakafanya hivyo.

MS anapaswa aangalie picha kubwa zaidi. Je,kuna kitu gani cha kumbu kumbu ya Mzizima walikoishi wenyeji wetu?
Je, kiwanja cha Chang'ombe kiendelezwe vipi kwa faida ya wakazi wa jiji.
Je, kifanyike nini wakazi wa kariakoo-mzizima wanufaike na ardhi na rasilimali zilizopiganiwa na akina Abdul Sykes na Kiyate. Kwanini wahamishwe kwa kupewa milioni 15 kwa kitu chenye thamani ya milioni 400 n.k.
Kufikiria street moja tu ni tatizo kabla ya tatizo.

Walioifikisha Dar hapo ilipo ni wazee wako, Nyerere anafanywa Bangusilo tena kwasababu tu ya jina Julius.
Anahukumiwa kwa uzembe, ujinga na ututusa usiomhusu.
Nyerere hakuwa diwani Moshi, Mwanza au Mbeya! kimeshindikana nini Dar!
MS warithishe watoto werevu na kujitambua kwasababu dunia ya leo majungu haujawa mtaji wa maana the least to say
Sasa kama unajua hujui na huna majibu, kwanini ujihusishe na kuwa msemaji wa waislam?

Ukweli ni kuwa unaogopa kusema Mwinyi, Mkapa au Kikwete kwasababu kufanya hivyo utagusa wazee wako.
Tunarudi nyuma kuwa tuhuma dhidi ya Nyerere ni za kupikwa kwasababu historia inamsuta MS.
Huwezi ukawa na tukio moja katika historia ukachagua namna ya kulijadili au kuliandika kwa nyakati tofauti.
Chuki dhidi ya Nyerere ni kwasababu tu ya kumhusisha na dini yake.

MS unapaswa kwenda kujadiliana na Kikwete kwanza, kwasababu Nyerere ni marehemu. Kuendelea kumsukumia lawama hakumdhuru bali kunaidhuru jamii yako. Kumzushia yaliyomshinda Mwinyi na Kikwete ni ubaguzi wa ajabu sana.
Ubaguzi ni dhambi mbaya sana na humdhalilisha awayeNyerere aliwahi kulieleza na maandishi yapo. Mkapa kalizungumzia hotuba ipo.
Kikwete hajawahi kulizungumzia. Tatizo lipo lakini si kwa namna unayoielewa wewe na kundi lenu.

Kwanza hamtafuti suluhu mnachotaka ni kuvuruga nchi. Mtu mwenye suluhu hawezi kuwa anapiga mdomo na ikifika mahali anaulizwa tufanye nini anajibu haya
MS anachotaka ni kuita majina na kuwapa watu madaraka. Kuita majina na kuwapa watu kazi za taaluma.
Kwamba kwake Daktari anaweza patikana kwa uwiano au kupiga kura!!!

Kibaya zaidi MS anaamini kuwa mtu anayeitwa Abdallah Husein Bin Suein au John William Walace basi huyo ni muumini wa dini. Tatizo la watu kama akina MS ni kutochukua kioo na kujiangalia!Ni kunajisiwa fikra zao na ukoloni wakidhsni kuwa dini ni jina hata kama awaye ni mzushi, jambazi, muongo.

Hivi unapata wapi mtaalam au kiongozi kutoka Kilwa kama shule zinafungwa kwa kukosa wanafunzi.
Shule ifungwe kwenda kusikiliza kesi ya Ponda!! Hayo si tatizo kwa MS,tatizo ni Nyerere!
MS waambie watu wako ukweli acha kuwadanganya ili uuze nakala za vitabu, unawapotezea muda wa kusonga mbele.

MS hana ushahidi wa maswali yote mawili, bado anasema alichoandika ndio ukweli. Huu ni ushahidi kuwa sehemu kubwa ya ngano hii imejengwa kwa fikra zake binafsi zikichagizwa na uzushi.

Mwanafunzi hawezi kuja kusema na mtafiti akakubali tu kwasababu ni mwanafunzi huyo ni Mwislam.
Hili kama si majungu ni nini. Uliposema ndani ya kitabu kuwa christian lecturers at UDSM... ulichotaka ni kujenga chuki tu.

Huko Ulaya wasikojua hali ya Tanzania hawawezi kukuuliza uwape ushahidi. Ndio maana tunasema MS ni mpotoshaji, mzushi na mjenzi wa historia kwa kutumia majina na matukio huku akichomeka mbegu yake ya chuki miongoni mwa jamii.

Kusema jambo usilo na uhakika nalo ni uzushi na ni uongo. Dini ya kiislam haitaki hivyo na imekataza.
Unapaswa umuogope mwenyezi mungu kwanza kabla ya mauzo ya kitabu.
Muogope mola wako kabla hujazua balaa maana hilo limekatazwa.

Sasa tuna mambo mengi sana ambayo Mohamed ameyaandikia kurasa na kurasa na ameshindwa kuyatetea kwa mantiki,
hoja na hekima. MS nani asiyejua kwanini unakimbia hoja na maswali na umebaki kukata vipande vya kitabu.

Ninafikiria hivi kama kuna mwanafunzi anaandika thesis na amefanyia reference kitabu hiki, atawezaje kuitetea thesis yake kama mwandishi hawezi kutetea maandiko yake. Sad!

Asante sana mkuu kwa kunyumbulisha mjadala huu kwa uchambuzi imara na usanifu wa daraja la juu kabisa!

Watanzania wanatuona na kutusikia, ninawasihi wayatumie mawazo yetu kulinusuru taifa letu na uchochezi wa Mohamed Said.
 
Ninafikiria hivi kama kuna mwanafunzi anaandika thesis na amefanyia reference kitabu hiki, atawezaje kuitetea thesis yake kama mwandishi hawezi kutetea maandiko yake. Sad!

Hili swali la kufikirisha kwa mtu mwenye kutumia chembe zake za Ubongo vizuri. Kama mwandishi wa kitabu anashindwa kutetea kitabu chake mwenyewe na badala yake kutaka watu wengine waandike vya kwao msomi anayeweza kukinukuu atakinukuu vipi?
 
Kwa kuwa mnaojaribu kumuelimisha, kumkosoa Mzee wetu Mohamed Said ni WAKRISTO, hilo tu ni kikwazo tayari kwa Mzee wetu huyu. Mbaya zaidi, tayari keshaandika na tayari anaungwa mkono na wale aliowakusudia. Humu JF atabaki kujitetea na kukwepa kila atakapopata fursa ya kufanya hivo.

Naamini angeshirikisha utafiti wake huu watu wengine ambao bado wako hai na wanaijua vizuri Tanganyika, asingeandika maoni ya upande mmoja tu halafu akayaegesha na kuyaegemeza kwenye DINI yake. Wapo watu wanaojua kwa undani kwa nini familia ya akina Sykes ilijitenga na siasa za nchi hii mara baada ya Abdu kuukosa urais wa TANU. Hili, Mzee wetu Mohamed amelisukumia kwenye udini makusudi kabisa.

Mzee wetu Mohamed hasemi ni kwa nini akina Sykes hawakumuunga mkono Zuberi Mtemvu, Mwislam mwenzao, alipoanzisha chama. Anamtetea sana Abdu na wadogo zake kukaa kimya hadi baadhi yao wakafariki. Anauona ukimya wa Mwalimu juu ya kitabu chake kwamba ni kukiri yote yaliyoko mle ni kweli, kweli tupu!
 
hili swali la kufikirisha kwa mtu mwenye kutumia chembe zake za ubongo vizuri. Kama mwandishi wa kitabu anashindwa kutetea kitabu chake mwenyewe na badala yake kutaka watu wengine waandike vya kwao msomi anayeweza kukinukuu atakinukuu vipi?

ndugu mzee mwanakijiji,huoni jinsi unavojicontradict??alishakuambia ya kwamba yeye anaandika historia ya wale waliosahaulika ama walioufutwa kwa makusudi katika historia ya mapambano ya nchi hii,na kajitahid kuandika ya wale anaowafaham na ambao wengine pia inawafaham ila kwa sababu zao tuh wakaamua kuwaondoa na kuufanya ummah mkubwa kutofaham chochote kuhus wao.anachofanya yeye sasa ni kuihuisha ile historia,
sasa kwanini uje uipinge eti kisa hajaweka majina ya wazee wa kikristu?nyinyi si mnaamin huo mchango wa wazee wa kikristu ambao upo na mnaufaham??sasa kwani yeye ameupinga??yeye alichofanya ni kuandika kwa wale ambao historia imewatenga pasi na sababu za kushibisha njaa ya akili,sasa naona anaandamwa eti kisa wengi wa aliowaandika ni wazee wa kiislam na kwamba anatetea udini,kivipi??sasa kumbe kutetea historia ya wale waliofutwa kunahusiana vipi na dini ya mtu??
Huyu ndugu mohammed said kawafungua wengi sana macho,na juhudi hizo za kuupinga ukweli huu wala hazitazaa matunda,ukweli hupokelewa tuh hata kama ni mchungu.
 
Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji.

Hata siku mmoja hatujawahi kuyasoma mabandiko yenu humu jamvini mkiwaelezea hata kwa chembe ya uzuri ambayo wameyafanywa na hawa wazee wa Dar es Salaam katika harakati za kupigania uhuru.

Mtu makini akiwasoma ataona hata nyie mpo upande wa wazee wa kikiristo ambao walipigania uhuru kwa maana hiyo wote mnaangukia kundi moja. Nyie mnatetea wazee wenu wa kikistu na Mohamed Said anatetea wazee wake wa kiislam.

Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Yericko Nyerere, Mag3, ni wakati wenu sasa kukaa chini na kuunganisha nguvu zenu kuandika kitabu ambacho kije kuboboa kabisa hizo "ngano" za Mohamed Said kama mnavyoziita.

Watanzania watajifunza mengi kupitia nyie.
 
Last edited by a moderator:
kwa kuwa mnaojaribu kumuelimisha, kumkosoa mzee wetu mohamed said ni wakristo, hilo tu ni kikwazo tayari kwa mzee wetu huyu. Mbaya zaidi, tayari keshaandika na tayari anaungwa mkono na wale aliowakusudia. Humu jf atabaki kujitetea na kukwepa kila atakapopata fursa ya kufanya hivo.

Naamini angeshirikisha utafiti wake huu watu wengine ambao bado wako hai na wanaijua vizuri tanganyika, asingeandika maoni ya upande mmoja tu halafu akayaegesha na kuyaegemeza kwenye dini yake. Wapo watu wanaojua kwa undani kwa nini familia ya akina sykes ilijitenga na siasa za nchi hii mara baada ya abdu kuukosa urais wa tanu. Hili, mzee wetu mohamed amelisukumia kwenye udini makusudi kabisa.

Mzee wetu mohamed hasemi ni kwa nini akina sykes hawakumuunga mkono zuberi mtemvu, mwislam mwenzao, alipoanzisha chama. Anamtetea sana abdu na wadogo zake kukaa kimya hadi baadhi yao wakafariki. Anauona ukimya wa mwalimu juu ya kitabu chake kwamba ni kukiri yote yaliyoko mle ni kweli, kweli tupu!

hiyo nayo si hoja ya kuishupalia,na usijaribu kuuchanganya uislam na siasa,uislam ni mfumo timilifu wa maisha na uliojikamilisha katika kila nyanja ya maisha ya mwanadam,

nani asiejua ya kwamba zuberi mtemvu alikuwa anafanya siasa,hadi alipofikia hatua ya kumpinga nyerere wazi wazi na kuanzisha chama chake hoja zake aliziweka hadhwarani,wazi wazi bila kificho,msimamo wa kina sykes na nyerere kisiasa pia ulikuwa unaeleweka na kufahamika wazi wazi,haikuwa sawa kwa kina sykes kumuunga mkono mtemvu eti kisa tuh ni muislam mwenzao,hawakuwa wanapigania dini,au wanafanya jihadi,pale walikuwa wanafanya siasa,na hakuna kipengele katika uislam kinachosema eti uwe bega kwa bega na muislam mwenzako eti kisa mnashare the same political philosophy or idea,si kweli na usijaribu kututoa nje ya mstari,rudi kwenye hoja kuu ya mjadala ili tusiachane achane.
 
Jibu zuri pasi kiasi.
 
ndugu mzee mwanakijiji,huoni jinsi unavojicontradict??alishakuambia ya kwamba yeye anaandika historia ya wale waliosahaulika ama walioufutwa kwa makusudi katika historia ya mapambano ya nchi hii,na kajitahid kuandika ya wale anaowafaham na ambao wengine pia inawafaham ila kwa sababu zao tuh wakaamua kuwaondoa na kuufanya ummah mkubwa kutofaham chochote kuhus wao.anachofanya yeye sasa ni kuihuisha ile historia,
sasa kwanini uje uipinge eti kisa hajaweka majina ya wazee wa kikristu?nyinyi si mnaamin huo mchango wa wazee wa kikristu ambao upo na mnaufaham??sasa kwani yeye ameupinga??yeye alichofanya ni kuandika kwa wale ambao historia imewatenga pasi na sababu za kushibisha njaa ya akili,sasa naona anaandamwa eti kisa wengi wa aliowaandika ni wazee wa kiislam na kwamba anatetea udini,kivipi??sasa kumbe kutetea historia ya wale waliofutwa kunahusiana vipi na dini ya mtu??
Huyu ndugu mohammed said kawafungua wengi sana macho,na juhudi hizo za kuupinga ukweli huu wala hazitazaa matunda,ukweli hupokelewa tuh hata kama ni mchungu.

Usipotoshe ndugu, alichofanya Mohamed ni kuwatenga zaidi, sio kuhuisha historia!

Unadhani waliosahauliwa katika historia ni wazee wakiislamu tu kama alivyofanya?
 
Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji.

Hata siku mmoja hatujawahi kuyasoma mabandiko yenu humu jamvini mkiwaelezea hata kwa chembe ya uzuri ambayo wameyafanywa na hawa wazee wa Dar es Salaam katika harakati za kupigania uhuru.

Mtu makini akiwasoma ataona hata nyie mpo upande wa wazee wa kikiristo ambao walipigania uhuru kwa maana hiyo wote mnaangukia kundi moja. Nyie mnatetea wazee wenu wa kikistu na Mohamed Said anatetea wazee wake wa kiislam.

Mzee Mwanakijiji, Nguruvi3, Yericko Nyerere, Mag3, ni wakati wenu sasa kukaa chini na kuunganisha nguvu zenu kuandika kitabu ambacho kije kuboboa kabisa hizo "ngano" za Mohamed Said kama mnavyoziita.

Watanzania watajifunza mengi kupitia nyie.

Mimi nimewaomba sana hawa ndugu zangu na wao waandike habari za huko kwao
walikotoka ikiwa walikuwapo walioipigania TANU.

Hili hawalitii maanani.

Wameshughulishwa na kupiga vita historia ambayo ishaandikwa na kitabu kinasomwa
sasa mwaka wa 15.
 
ndugu mzee mwanakijiji,huoni jinsi unavojicontradict??alishakuambia ya kwamba yeye anaandika historia ya wale waliosahaulika ama walioufutwa kwa makusudi katika historia ya mapambano ya nchi hii,na kajitahid kuandika ya wale anaowafaham na ambao wengine pia inawafaham ila kwa sababu zao tuh wakaamua kuwaondoa na kuufanya ummah mkubwa kutofaham chochote kuhus wao.anachofanya yeye sasa ni kuihuisha ile historia,
sasa kwanini uje uipinge eti kisa hajaweka majina ya wazee wa kikristu?nyinyi si mnaamin huo mchango wa wazee wa kikristu ambao upo na mnaufaham??sasa kwani yeye ameupinga??yeye alichofanya ni kuandika kwa wale ambao historia imewatenga pasi na sababu za kushibisha njaa ya akili,sasa naona anaandamwa eti kisa wengi wa aliowaandika ni wazee wa kiislam na kwamba anatetea udini,kivipi??sasa kumbe kutetea historia ya wale waliofutwa kunahusiana vipi na dini ya mtu??
Huyu ndugu mohammed said kawafungua wengi sana macho,na juhudi hizo za kuupinga ukweli huu wala hazitazaa matunda,ukweli hupokelewa tuh hata kama ni mchungu.
-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na Mwalimu? Mwalimu amefariki bila kuandika historia ya nchi hii. Hata hiyo ya Kivukoni haina mkono wala baraka za Mwalimu.

-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na DINI yao? Ni watu wa dini hii tu waliosahaulika? Ni kweli Mwalimu aliuchukia UISLAM na WAISLAM?
 
kama mwandishi kaandika na kuirudisha kwa jamii historia ya wale waliotengwa kwa makusudi na kufutwa kwa hila na ghilba,iweje sasa wengine waje wamshutumu ya kwamba kuna wengine wapo tena wa upande mwingine hajawaandika,na ambao hata yeye hawafaham,zaid ya hapo wameandikwa kwenye vitabu vingine na watu wakawafaham,iweje sasa akosolewe eti ooh umeewaacha hawa hujawaandika kisa si wazee wa kiislam ya nini sasa??hao si tayari wameshaandikwa kwenye historia na watu wakawafaham??iweje sasa nayeye anapoandika wengine ambao kwa makusudi walifutwa kwenye historia hiyo aonekane kama ni mdini.,mhaini,ana choko choko,mvunja amani n.k,iweje ahukumiwe hivo??au watu walikuwa wanapenda hii history aliyoihuisha ipotelee kuzimu moja kwa moja??
Tuwe fair,na tusiegemee upande wowote.
 
Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na Mwalimu? Mwalimu amefariki bila kuandika historia ya nchi hii. Hata hiyo ya Kivukoni haina mkono wala baraka za Mwalimu.(KWANI YEYE KAKUAMBIA KUSAHAULIKA UKO KUNA UHUSIANO NA MWALIMU AU YEYE AMEBASE KUELEZEA KUSAHAULIKA KWA WALE WAZEE NA UHUSIANO WA HARAKATI ZA UHURU WA NCHI HII??MANTIKI UMEIPTA LAKINI??

-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na DINI yao? Ni watu wa dini hii tu waliosahaulika? Ni kweli Mwalimu aliuchukia UISLAM na WAISLAM?(LA HASHA,KUSAHAULIKA KWA WALE WAZEE HAKUNA UHUSIANO NA DINI YAO,NDIO MAANA TUNAHOJI WHY WAKASAHAULIKA??AU KWA KUWA WAO NI WAISLAM??KWANIN WENGINE WAMEEANDIKWA NA WAO WAKAACHWA??,HILO SWALI LA KUSEMA MWALIMU ALIWACHUKIA WAISLAM NA UISLAM LINAJIELEZA WAZI WAZI,USITAKE KUNICHOTA HISIA ZANGU UKANIUHUKUMU KAMA MIMI NI MDINI,HOJA YETU HAPA SIO HIYO,ILA UKWELI JUU YA HILO MWENYE MACHO HAAMBIWI ONA,NA MWENYE MASKIO HAAMBIWI TAZAMA.
 
-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na Mwalimu? Mwalimu amefariki bila kuandika historia ya nchi hii. Hata hiyo ya Kivukoni haina mkono wala baraka za Mwalimu.

-Kusahaulika kwa wazee wake hawa kuna uhusiano gani na DINI yao? Ni watu wa dini hii tu waliosahaulika? Ni kweli Mwalimu aliuchukia UISLAM na WAISLAM?

Ingekuwa bora kabla ya kuandika ukafanya utafiti angalau kidogo.
Nani kakuambia kitabu cha historia cha Kivukoni haina mkono wa
Nyerere?

Kasome utangulizi wa kitabu.

Hilo lingine sina haja kulisemea.
 
Kaka Mohamed Said. Nauliza hiyo mitaa ya New Street, Mbaruku Street, Stanley Street, kwa sasa inaitajwe?
 
Usipotoshe ndugu, alichofanya Mohamed ni kuwatenga zaidi, sio kuhuisha historia!

Unadhani waliosahauliwa katika historia ni wazee wakiislamu tu kama alivyofanya?

Fanya utafiti kidogo zungumza na waliokisoma kitabu usikize wanasema nini.
 
hiyo nayo si hoja ya kuishupalia,na usijaribu kuuchanganya uislam na siasa,uislam ni mfumo timilifu wa maisha na uliojikamilisha katika kila nyanja ya maisha ya mwanadam,

nani asiejua ya kwamba zuberi mtemvu alikuwa anafanya siasa,hadi alipofikia hatua ya kumpinga nyerere wazi wazi na kuanzisha chama chake hoja zake aliziweka hadhwarani,wazi wazi bila kificho,msimamo wa kina sykes na nyerere kisiasa pia ulikuwa unaeleweka na kufahamika wazi wazi,haikuwa sawa kwa kina sykes kumuunga mkono mtemvu eti kisa tuh ni muislam mwenzao,hawakuwa wanapigania dini,au wanafanya jihadi,pale walikuwa wanafanya siasa,na hakuna kipengele katika uislam kinachosema eti uwe bega kwa bega na muislam mwenzako eti kisa mnashare the same political philosophy or idea,si kweli na usijaribu kututoa nje ya mstari,rudi kwenye hoja kuu ya mjadala ili tusiachane achane.
Hivi Mzee Mohamed anaposema WAISLAM walitengwa na wakasahauliwa kwenye HISTORIA ya nchi hii anakuwa anamaanisha nini hasa! Hapa Mzee wetu anapigania nini kama sio DINI yake?
 
Hili swali la kufikirisha kwa mtu mwenye kutumia chembe zake za Ubongo vizuri. Kama mwandishi wa kitabu anashindwa kutetea kitabu chake mwenyewe na badala yake kutaka watu wengine waandike vya kwao msomi anayeweza kukinukuu atakinukuu vipi?

Sasa kama mshashinda sasa mnahangaika nini?
 
Back
Top Bottom